kinepi_nepi
JF-Expert Member
- Aug 16, 2007
- 869
- 235
Kuna kila haja ya kuongeza idadi ya wabunge mahiri Bungeni kutoka kambi ya upinzani. Zitto I salute you on this.Pale inahitaji kila mbunge mwenye mapenzi akisimama anamkoma nyani bila huruma, na anamwaga point mwishowe wangeachia, ila bunge bado ni butu sana, kwani wanaomkoma nyani ki ukweli ni wawili tu Dr. Slaa na Zitto. wengine ni wa msimu na kutegemea upepo wa chama chao ukoje.
Maendeleo ya Tanzania na kushughulikia maswala ya ufisadi hususani wa Meremeta , tanggold, Deep green nk na wizi mwingie na ufisadi unaibuka kila siku kama hii EPA mpya ya Jk kunahitaji wabunge wa upinzani wasomi, werevu wajasiri na wenye mapenzi ya kweli na nchi. Sasa upinzani kwa kuanzia inabidi hata wabunge wa kuteuliwa ambao vyama vinapewa nafasi ya kufanya hivyo wachaguliwe wenye mapenzi na nchi na uelewa wa kutosha na elimu pambanishi. Sioni sababu ya mbunge wa upinzani anamaliza miaka mitano hakuna alilofanya zaidi ya kupiga makofi, najua uchache wetu lakini lazima wabunge wetu wawe ndio chachu ya maendeleo na mijadala ya kitaifa na ukombozi kutoka mikononi mwa chama chenye mafisadi na kinachozalisha ufisadi.
Zitto kwenye hansard yako umeweka point ya msingi sana kwamba asilimia 44 ni vijana chini ya miaka 20. Hawa ndio wapiga kura wa 2010/2015. Ni Kazi ya wabunge vijana wa upinzani kuanza kufikia hiki kizazi kipya cha dot.com kuhusisha maisha yao na utawala dhalimu wa CCM. Miundo mbinu mibovu, elimu duni ukosefu wa ajira vifo vya wapenzi wao wakijifungua, na watoto wao wachanga, ajali za barabarani zinazouwa kila kukicha kwa mfumo mbaya wa polisi na barabara mbovu, magari mabovu ni mengi sana yanaruhusiwa kubeba abiria na mizigo, hayana takwimu za matengenezo, matairi ya kanjanja kutoka china, break pads na drums mbovu, chasiss zilizopinda nk. Polisi wa usalama barabarani hawafanyi kazi kwani magari ni ya wahemiwa. haya yote taratibu yakiingia akilini nchi itakuwa nchi. 2010 tutakuwa na wabunge 100+ na 2015 tutakuwa na majority, hapo tutamkoma nyani kwa kwenda mbele.