Zitto: "Majibu ya Sumari ni 'ovyo ovyo'"; atakiwa kufuta kauli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto: "Majibu ya Sumari ni 'ovyo ovyo'"; atakiwa kufuta kauli!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdau, Jun 24, 2009.

 1. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2009
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  A controvesial CHADEMA MP from Kigoma North constituency has once again tested the wrath of Union Parliament today, after refusing to detract his ownstatement that " majibu aliyotoa waziri Sumari kwa Mh. Slaa ni ya HOVYOHOVYO..." pamoja na pressure ya wazi toka kwa two CCM MPs wakiomba mwongozo wa Mwenyekiti, Zitto aligoma katakata kufuta kauli yake na kudai kwamba wabunge kadhaa (nadhani akimaanisha wa CCM), wameshaongea kauli za kutatanisha katika bunge hili lakini hakuna hatua zilizochukuliwa..alimalizia kwa kusema "NIPO TAYARI KWA LOLOTE" kabla hajendelea kuchangia mjadala wa budget..


  =============================

  MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia katika hotuba hii ya Waziri Mkuu, Ofisi ambayo inashughulikia uendeshaji mzima wa Serikali. Kabla sijaendelea nichukue fursa hii kutambua mchango mkubwa sana unaofanywa na viongozi wa Mkoa wa Kigoma katika kuleta maendeleo ya Mkoa wa Kigoma. Ningependa kumpongeza sana Mkuu wetu wa Mkoa Kanali Simbakalia kwa mabadiliko makubwa sana, barabara sasa zinajengwa, lakini nashukuru zaidi kwamba barabara zote zinazojengwa zipo jimbo la Kigoma Kaskazini kwa hiyo inadhihirisha kabisa kwamba hata wananchi wakiamua kuchagua Upinzani maendeleo watapata kwa sababu wanalipa kodi. (Makofi)

  Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Mwandiga/Manyovu Kigoma Kaskazini, barabara ya Kigoma/Kidawe iko Kigoma Kaskazini na Kigoma ina majimbo 7 ya uchaguzi ni jimbo moja tu ndilo liko Upinzani Mheshimiwa Waziri Mkuu nakupongeza kwenda kufungua barabara ile, naomba radhi sikuwepo siku ile kwa sababu nilikuwa Biharamulo. Unajua tupo wachache Bungeni humu inabidi kuongeza idadi ya Wabunge wa Upinzani ili tuendelee kuwabana. (Makofi/Kicheko)

  Mheshimiwa Mwenyekiti, mazingira ya michango ya Wabunge katika hotuba hii ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni ya kiuchaguzi uchaguzi na mimi nitakwenda kiuchaguzi uchaguzi. Sasa hivi tumejenga mazingira ya kujenga Taifa lenye mgawanyiko mkubwa sana. Mwaka jana wakati nachangia hotuba ya bajeti nilisema kwamba tunajenga Mataifa mawili ndani ya nchi moja kwa sababu ya mgawanyiko mkubwa na tofauti kubwa sana za kipato kati ya wananchi mbalimbali na nitazungumza kwa takwimu.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2005 Chama cha Mapinduzi kiliahidi kupunguza idadi ya watu maskini Tanzania kwa nusu. Kwa mujibu wa Ilani na MKUKUTA pia ulionyesha hivyo hivyo. Taarifa ya Household Budget Survey ambayo imetoka mwezi Novemba, 2008 inaonyesha idadi ya watu maskini kati ya mwaka 2001 na mwaka 2007 imeongezeka kutoka watu 11,000,000 mpaka 12,700,000. Kwa hiyo badala ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Kimapinduzi kupunguza idadi ya watu maskini kutoka 11,000,000 mpaka 5,000,000 watu maskini 1,700,000 zaidi wameongezeka Tanzania na hii ni taarifa ya Serikali sio taarifa zangu Household Budget Survey ni ya Serikali.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, katika idadi ya watu 12,700,000 maskini Tanzania ambayo ni asilimia 33.5 ya Watanzania wote asilimia 74 ya watu hao ni wakulima wa vijijini. 74% of poor people Watanzania ni wakulima wa vijijini, kwa hiyo hali inaonyesha kwamba umaskini umejikita zaidi vijijini. Chama cha Mapinduzi kiliahidi kwenye Ilani ya Uchaguzi mwaka 2005 kwamba watahakikisha sekta ya kilimo inakua kati ya asilimia 8 na 10 ili kufikia hilo lengo la kupunguza idadi ya watu maskini. Toka Serikali ya Awamu ya Nne iingie madarakani sekta ya kilimo imekua kwa asilimia 4 mpaka asilimia 4.1, tunaposema sekta ya kilimo maana yake tunazungumzia rural economy, rural growth. Leo tunaambiwa kilimo kwanza watu wanakumbuka shuka wakati alfajiri imefika malengo mliojiwekea hamjayatekeleza hamuelezi sababu zilizowafanya mshindwe kutekeleza malengo hayo na watu wanasema Ilani

  [MHE. KABWE Z. ZITTO]

  imetekelezwa kwa asilimia 100, nashangaa sana, takwimu za Serikali zinaonyesha tofauti.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Serikali ya Awamu ya Nne inachukua nchi hii inaongoza nchi, asilimia 11 ya watoto waliokuwa wanazaliwa walikuwa wanakufa kabla hawajatimiza umri wa miaka 5. Leo ninavyozungumza nanyi kwa mujibu wa taarifa ya hali ya uchumi katika kila watoto 1,000 wanaozaliwa Tanzania watoto 134 wanafariki kabla hawajatimiza umri wa miaka 5, tunapoteza watoto 800,000 kila mwaka. Mkoa wa Lindi ina idadi ya watu 800,000. Ukitaka kujua idadi ya watoto wanaofariki dunia kabla hawajatimiza miaka 5 Tanzania angalia population yote ya Mkoa wa Lindi, mnasema mnatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, Maternal Mortality Rate kina mama wajawazito wanaofariki dunia kwa matatizo ya uzazi. Katika kila wanawake 100,000 wanaopata ujauzito Tanzania wanawake 578 wanafariki dunia kwa matatizo ya uzazi. Kila saa takwimu hizi zinaonyesha kila saa inayopita katika nchi yetu kuna mwanamke mmoja amefariki kwa sababu ya matatizo ya uzazi katika Taifa letu, kila saa inayopita. Miaka 48 ya uhuru tunashindwa kulinda afya za mama zetu na ni takwimu za Serikali, mnatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

  WABUNGE FULANI: Ndio!!!!!!!

  MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, idadi ya watu wa Tanzania asilimia 44 ya Watanzania ni watoto walio chini ya umri wa miaka 15. Medium age kwa mujibu wa population yetu 17 yaani half ya Watanzania wako chini ya umri wa miaka 17, asilimia 44 ya Watanzania wako chini ya umri 15, kwa hiyo hii a very young population. Lakini takwimu za Serikali kwenye vitabu vya Serikali zinaonyesha kwamba asilimia 38 ya hao watoto ni stunted, wamedumaa, kudumaa masuala ya Lishe. 38% katika kila watoto 10 wa Tanzania, watoto 4 ni stunted, tunajenga Taifa la namna gani?

  Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba ya Waziri Mkuu sijaiona hatua yoyote inayochukuliwa ku-address matatizo hayo ya kitakwimu, lakini haiwezekani kukawa na hizi measures kwa sababu tunapotunga sera, tunapotunga mikakati tunajiangalia sisi ambao hatupo katika lile kundi la 74% of the poorest katika Taifa letu ambalo ni wakulima, mnasema mnatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi. Mwaka 2005 Ilani ya Uchaguzi iliahidi kuongeza ajira takwimu za Serikali zimeonyesha Watanzania 2,300,000 hawana ajira kabisa sio informal sio formal, Mkoa wa Kagera una watu 2,300,000. Ukitaka kujua idadi ya Watanzania ambao hawana kazi nenda uwanja wa Kaitaba kusanya watu wote wa Mkoa wa Kagera ndio Watanzania ambao hawana kazi 2.3 million mnatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ndio mambo ambayo tunategemea in the run up to the election, tunapoelekea uchaguzi watu waliopewa nafasi ya kuongoza dola wajibu

  [MHE. KABWE Z. ZITTO]

  kwa wananchi. Hatujibu kwa kelele tu za kulalamika, lalamika, tunajibu kwa takwimu na takwimu ni za Serikali kwa sababu Idara ya Takwimu iko chini ya Serikali, iko chini ya Wizara ya Fedha, kwa hiyo tunataka majibu haya mikakati gani inayofanyika kuliokoa hili Taifa tunakoelekea ni kubaya sana, Mheshimiwa Mwenyekiti.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na hali hii mwaka jana nilizungumza hapa taarifa ya poverty and human development report inaonyesha 78% ya Watanzania hawaaminiani. Katika kila Watanzania 10 ni 2 tu ambao wanaaminiana, Watanzania 8 hawaaminiani. Ndiyo maana watu hawalipi mikopo, ndiyo maana watu wakisikia vi-scheme vya ovyo ovyo kama DECI wanakimbilia kwa sababu they don’t trust the systems. Wanasiasa hawaaminiani ndio kumekuwa na makundi makundi ya kusemanasemana ya kulanianalaniana maana yake nimesikia juzi kuna Wabunge wanawalaani Mawaziri, Mawaziri wanakasirika, watu wanaambiwa kwamba wanapeleka miradi ya maendeleo kwenye majimbo yao ni kwa sababu ya lack of trust. Tunajenga Taifa ambalo social fabrics limekwisha kabisa, hivi ndio vitu ambavyo ningetegemea kwamba hotuba ya Waziri Mkuu iweze kuvi-address, tuna tatizo kubwa sana.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi nilikuwa natoka Biharamulo nikapita Igunga pale gari yangu iliharibika nikakutana na walimu wanalalamika wakaniletea Mkataba ambao walimu wameingia na nimeupeleka kwa Mawaziri hapa waushughulikie na Kampuni moja inaitwa Blue Finance siwezi kuwahukumu hawa kwa sababu sijapata nafasi ya kuwasikiliza na mimi ni mtu wa haki sana. Wamewakopesha walimu shilingi 400,000/= riba asilimia 231, sababu wanachotakiwa kulipa ni shilingi 1,300,000. Nimempatia Mheshimiwa Waziri Mkuu aweze kuona jinsi gani ambavyo Watanzania wanyonge kwa sababu ya ukosefu wa mfumo mzuri wa fedha walimu wanavyonyanyasika. Mwaka jana hapa Mheshimiwa Erasto Zambi alizungumzia kuhusu Kampuni moja ya Bayport na akaweka ushahidi. Leo nimepita tu Igunga kwa watu walivyo desperate na nimempelekea Mheshimiwa Waziri na Mama Kombani ndio yuko anaisoma pale aweze kuona jinsi gani ambavyo hali ambayo tumeifikia.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, nitazungumzia kuhusu ufisadi. Kamati ya Bomani nitaiomba kuinukuu katika masuala ambayo alisumbuliwa sumbuliwa Dr. Slaa juzi hapa. Alisema hivi Kamati ya Bomani ilipendekeza hivi “Kwa kuwa malipo ya Dola za Marekani 132,000,000 yaliyofanywa na Benki Kuu kwa Netbank ya South Africa hayana uwiano dhahiri na mkopo wa Dola za Marekani 10,000,000 zilizokuwa zimekopwa na Kampuni ya Meremeta kutoka Netbank Serikali ifanye uchunguzi kuhusu malipo hayo. Hii ni taarifa ya utekelezaji wa ahadi za Serikali ambao Waziri Mkuu aliitoa mwaka jana, taarifa hiyo inasema ukurasa 23. Taarifa ya Serikali inasema “Uchunguzi unaendelea, uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha za Serikali kupitia Benki Kuu kwa Kampuni ya Meremeta na Tangold unaendelea, Julai mwaka 2008, Taarifa ya Serikali ambayo Waziri Mkuu ameitoa hapa. Juzi Waziri Sumari anamjibu ovyo ovyo tu Mbunge hapa, tena Katibu Mkuu wa Chama kinachokua kuliko vyama vyote Tanzania anamjibujibu tu.
  [MHE. KABWE Z. ZITTO]

  What is a contradiction kati ya taarifa ya Serikali na majibu ambayo Mawaziri wanayatoa. CAG anafanya uchunguzi kuhusu Meremeta na nilichokiomba ni kwamba Serikali isiingilie Sheria ya Ukaguzi inasema kwamba CAG ana uhuru wa kufanya uchunguzi wowote, CAG ame-confirm kwamba anafanya uchunguzi kuhusu Meremeta na tunaiomba Serikali isingilie mpaka taarifa hiyo inapokuja, lakini hapo hapo Serikali……

  MWONGOZO WA SPIKA

  MHE. PONSIANO D. NYAMI: Kanuni 68 na pia ningepata utaratibu. Katika kuongea kwa Mheshimiwa aliyekuwa anachangia sasa hivi sidhani kama ni uungwana. Ukiacha heshima aliyonayo na umri unavyokwenda kitendo cha kusema Waziri anajibu ovyoovyo, maana yake Serikali inajibu ovyoovyo na kwa maana hiyo ni kutokufikiria majibu wanayoyajibu. Lugha hiyo ni ya kuudhi sana na haipaswi kuwa ni lugha ya Bunge na haipaswi kukaa ndani ya Hansard.

  Ninaomba maneno hayo ayafute na aombe radhi. (Makofi)

  MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa, nitamruhusu Mheshimiwa aendelee bila ya kuyatumia hayo maneno kwa sababu hayapendezi.

  WABUNGE FULANI: Asiendelee

  MWENYEKITI: Naomba niendelee kuongea asiendelee kuyatumia na yafutwe kwenye Hansard, naomba uyafute hayo maneno ovyoovyo halafu uendelee kuchangia.

  MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Mbunge hapa alitaka Mawaziri walaaniwe hakufuta kauli yake. Kuna Mbunge hapa leo asubuhi amemshambulia waziwazi Waziri wa Utumishi Mheshimiwa Hawa Ghasia hakuna mtu aliyesimama kuweza…

  MWENYEKITI: Mheshimiwa Kabwe Zitto naomba ukae.

  MHE KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, maneno haya sitayafuta.

  MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge usibishane na Kiti, nilichotaka ufanye ni kwamba ufute maneno yako halafu uendelee kuchangia, usianze kubishana na kuanza kutoa reference ya mambo yaliyopita, naomba ufute hiyo tu hiyo ovyoovyo halafu uendelee kuchangia. Tafadhali sana.

  MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, majibu ambayo Waziri alimpatia Mbunge wa Karatu yalikuwa ni ya ovyoovyo nasimamia maneno yangu na niko tayari kwa lolote ambalo Meza itakayoamua. (Makofi)

  MWENYEKITI: Naomba uendelee sasa na mchango wako na hatua zaidi zitafuata kuhusiana na hiyo kauli yako. (Makofi)

  MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho.

  MWONGOZO WA SPIKA

  MHE. DR. ZAINAB A. GAMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Waziri Kivuli wa Wizara hii alipokuwa anazungumza alikatazwa kuzungumza baadhi ya mambo pamoja na Meremeta, leo inaruhusiwa tena lile lile alilokataza Naibu Spika, linazungumzwa, naomba Mwongozo wako.

  MWENYEKITI: Ahsante nadhani ni sahihi katika kumbukumbu kwamba Mheshimiwa Waziri Kivuli alipokuwa akiongea masuala yote yaliyohusiana na Meremeta alitakiwa ayafute na yaondolewe kwanye Hansard. Kwa hiyo Mheshimiwa Zitto Kabwe utamalizia bila ya kuyazungumza tena masuala hayo kwa sababu uamuzi ulikwishakutoka wakati ule kwamba hayo masuala hayatazungumzwa humu ndani.

  Mheshimiwa Kabwe endelea.

  MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nitamalizia kwa mambo mawili ya mwisho kwamba lazima ifikie wakati tuhuma mbalimbali za rushwa kubwa zinapotoka Serikali iweze kuchukua hatua kuhakikisha kama mambo haya yanakwisha kwa sababu mnapokuwa mnazungumza zungumza kila wakati mambo haya hasa kwa kuzingatia kwamba Taifa letu lina watoto wengi sana tunarithisha vitu vibaya sana kwa watoto na matokeo yake badala ya kujenga Tanzania imara iliyo moja tunajenga Taifa ambalo tutakuja kuitwa fisadistan, Republic of fisadis kitu ambacho mimi nisingependa tujenge Taifa la namna hiyo, kwa hiyo nilikuwa naomba Serikali iweze kuchukua hatua muafaka kuhakikisha kwamba hoja zote ambazo Wabunge wanazitoa kuhusiana na masuala ya rushwa kubwa kubwa zinashughulikiwa ili tufike mwisho na tuweze kufanya mambo mengine ya kimaendeleo.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa nilikuwa nasoma kitabu cha Mwalimu Nyerere ukurasa 94 na sijui ni kitu ambacho tunaweza tukakijadili namna gani kwa sababu imekuwa ni tendency ambayo hata imepelekea Serikali kuweza kushindwa kuchukua baadhi ya maamuzi. Tendency ya kuwasema Watendaji wa Serikali yaani (Civil Servants). Tarehe 12 Oktoba, Mwalimu alikuwa anafungua Bunge la kwanza la Tanganyika alisema hivi nanukuu. “Most important of all Members must not under any circumstances attack a Member of Civil Service in this House. If they believe a Civil Servant is acting wrongly and that in justice is inconsequence being done it is the Minister whom Members must call to account then it’s task to investigate and if necessary to evoke the displinary procedures against the government Servant”

  Sasa kumekuwa na utamaduni toka Bunge hili la Tisa limeanza kwamba tumekuwa tuki-attack sana Civil Servants watu ambao hawana fursa ya kujitetea humu ndani na hata imepelekea baadhi ya Maazimio ya Bunge ambayo yalikuwa yanawataja
  [MHE. KABWE Z. ZITTO]

  moja kwa moja Civil Servants kushindwa kutekelezwa kwa sababu ya taratibu za uendeshaji wa Civil Servants Service jinsi ulivyo. Nilikuwa naomba tujaribu kuangalia kama Bunge kama hotuba hii ya Mwalimu hasa kipengele hiki ambacho nimekinukuu wakati anazindua Bunge kinaweza kikawa ni sehemu ya kanuni za Bunge ili kuhakikisha kwamba wale ambao ndio front bench wanakuwa responsible kwa matendo yote ambayo watu wao wanakuwa wanayafanya ili iwe rahisi zaidi utekelezaji wa masuala mbalimbali ya Kiserikali kuweza kutumika.

  MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge muda wako ume-expire.

  MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia.
   
  Last edited by a moderator: Jun 24, 2009
 2. M

  Magehema JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Pls keep us posted with the updates
   
 3. M

  Masatu JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni Zitto Zubeir Kabwe sio Kwabe!

  Just for records.....
   
 4. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kawaambia wasicho taka kusikia....japo kuwa ndio ukweli wenyewe.Bravo zitto.
   
 5. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  enhee...naona mambo yameanza tena, tafadhali wadau mliopo on the ground tujulisheni kinachoendelea
   
 6. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Yaah....tena kuna mmoja kaongea juzi tu maneno ya ajabu ajabu....Mudhihir...mbona walibanisha tu?
   
 7. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Bunge lenyewe ubabaishaji tu. Kama mtu huwezi kusema mchango wa waziri ni hovyo hovyo, wanataka utumie neno gani? Michango mingine sio tu kwamba ni ya hovyo hivyo bali pia ni ya kijinga.

  Zitto usiombe msamaha, wakaitaka wakufungie tena na upate umaarufu zaidi.

  Huyo Mudhihir kaongea pumba nyingi sana hapo juzi na hawakusema kitu; huo ndio unafiki tunaopinga wengine.
   
 8. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Ukweli ni kwamba Waziri Sumari aliongea ovyo. Mimi namuunga mkono Zitto Kabwe.

  Zitto endelea na msimamo wako huo huo.
   
 9. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Na mwingine jana alisema watu wanaomsema Mkapa ni sawa na NGIRI kwani ngiri huwa hakumbuki kitu chochote. Watu wa! wa! wa! wanashangilia.
   
 10. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ...they better be prepaired and get used to it....thats just the calm before the storm!
   
 11. M

  Msharika JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mh. Zitto Zuberi Kabwe, Usiombe msamaha, hawa watu wanadhihaka sana! aswa wabunge wa CCM. Mbona Selelii akuonywa, Mbona Mudhihiri na matusi yake ya kishahiri hakuonywa? Wewe kusema ukweli umegusa kichwa cha jipu. Wewe bonyeza jipu lipasuke tupo wote. Kwanini wakuandame wewe unayetetea wananchi na wasiandame wanaokataa kujadili Tangold na meremeta? Au wasitumie hiyo nguvu nyingi kumsaka KAGODA?
  BRAVO Zitto kaza buti.
   
 12. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hivi wabunge wa ccm wao kwao masilahi ya nchii hii ni yapiiiii???

  wanaboa sana kwa tabia zao hizo za KINAFIKIIIIIII....

  TUWAPUMZISHEEE JAMANIIII...
   
 13. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Big up Zitto
   
 14. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mbona selelii aliwaombea laana mawaziri wote na hakuambiwa afute kauli? uonevu
   
 15. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #15
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  he he nafikiri hichi ndio kikao chake cha mwisho kuropoka
   
 16. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Tumekusikia mzee wa "IT".
   
 17. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  nabata ushungu mie...!! hawa wendawazimu wa Sio Sio Mimi wana shida gani? msema ukweli aitwa ngiri........nayo ni Sawa machoni pao, asemaye uwongo tena usiokuwa umepangiliwa akiambiwa amechemka.........oooh! hapana!!
   
 18. M

  Mulugwanza Member

  #18
  Jun 24, 2009
  Joined: Feb 3, 2008
  Messages: 89
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Mkuu SHY una maana gani?? we nadhani utakuwa kada wa chama cha mafisadi (CCM)
   
 19. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #19
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  wewe zitto amesema uwongo mara nyingi siku moja hata nilikutana nae katika live debate kwenye ishu ya madini pale soma book cafe akashindwa kutetea matamshi yake hawa ni watu wa kuogopwa sana katika taifa hili
   
 20. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #20
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  mimi sina chama wala dini lakini huyo kijana asidanganye jamii na ummah asifikiri vitisho vyake vitamtingisha yeyote , ninahamu angetaka kugombea jimbo la ubungo nisimame nae kama mgombea binafsi nimwonyeshe vijana walivyo si maneno matupu na vijitu vinatoa support kupumbazwa na kulaghaiwa tu
   
Loading...