Zitto: Mabilioni ya Uswisi – Tusigeuzwe Mazezeta

Kinachoshangaza marehemu takukuru wanalipwa kwa ajili ya kuchunguza wala rushwa, iweje huyu hosea anaongea kama punguani? umesha pata taarifa tumieni mbinu kupata hizo data.
We unakaa ofcn eti m2 akuletee majina? Hivi huyu ni zezeta? Kikwete ondoa hili jamaa make halijui kazi yake. linakula hela za walipa kodi linashindwa kufatilia kazi zake linasuburi watu walipelekee majina! kweli Takukuru ni marehemu!
 
Kweli kabisa tusifanywe Mazezeta!

Nilimsikiliza jana Osea wa takukuru ana sema watawashughulikia lakini nikaona ni nyimbo zilezile!
Hosea ana limitation ndugu yangu tena anaogopa kufa si aliishasema, yeye kawekwa kama figure ili Watanzania tuamini kuna TAKUKURU hana ubavu wa kuleta hizo fedha, mpaka apewe amri ya kufanya hivyo!!!

 
Jana nilimwona Mkuchika akiongelea issue hii,
Serikali yenye vyombo vyote, kuanzia polisi, CID, Usalama wa Taifa, Marehemu Takukuru, leo hii wanataka mtu binafsi ndiye awaelekeze jinsi ya kufanya kazi! Mwisho watamwomba Zitto akawakamate, maana ni hawa hawa waliokwishawahi kutuambia kwamba Wezi wa fedha za EPA(zilizoibwa kwa vimemo vya akina Mangula) wakikamatwa, eti nchi italipuka!
Hata mimi niliona kwenye taarifa ya ITV saa tano usiku, kali ni pale Hosea alipomalizia kuwa "wenye ushahidi walete si wanajifanya wana uchungu na nchi hii, walete"
 
Nadhani kinachokuja kutokea ni kilekile cha Richmond. Kati ya maazimio ya Bunge 23 kuhusu kashfa ya Richmond yaliyotekelezwa hata 10 hayafiki, bunge limefyata mkia. Anachokifanya Mkuchika na Serikali yake ni mwendelezo tu wa Serikali ya CCM kulipuuza Bunge na kuligeuza kama mdoli unaochezewa na mtoto kitandani. Wengi wamesema na watazidi kusema kilio cha mabilioni haya kitaenda na maji tu as far as Serikali ni hii hii kiburi dhidi ya bunge na wananchi kwa ujumla.

Labda bunge (hili hili la Makinda na CCM yake?) waseme watamfanya nini JK na Serikali kama watapuuza maazimio hayo maana tayari dalili zote zinaonesha bunge (wananchi) litapuuzwa tu.I think we need new approach to this scam
Mkuu kinacho wapa shida ni majibu kwa wananchi maana wanajua kuwa CHADEMA itapeleka hii hoja kwa wananchii nA KIPINDI HIKI NI CHA LALA SALAMA bila majibu mazuri wananchi wataelewa na watatoa majibu wao wenyewe nini la kufanya!!!

 
Inasikitisha pale MKURUGENZI ANAPORUDIARUDIA kukosa ushahidi ya matukio ya RUSHWA KUBWAKUBWA MARA KWA MARA. JE INAMAANISHA NINI? AMESHINDWA KAMA KIONGOZI AU IMESHINSHINDWA KAMA TAASISI au TUMESHINDWA KAMA NCHI? JE WALE AKINA JULIAN ASSANGE (WENGINE WANAMWITA JULIAN ASENGA UKITAKA) WANAWEZAJE?!!

INASIKITISHA SANA KAMA NCHI INAWEZA KUTOA MAJIBU KAMA YALE. SERIKALI IKISHINDWA KWENYE MAMBO MUHIMU KAMA YA RUSHWA KUBWA KAMA HIZI NI BORA KUKAA KIMYA!! KULIKO KUKATISHA TAAMAA!

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

katika Vitu FBI wanajitahidi kiwe sawa ni kutochafua ushahidi ,kuulinda ushahidi ili ushahidi uwe na vigezo vyote vya kimahakama.Ndio maana wameajiri si tuu wanasjeria bali pia watu waliowahi kuwa mahakamani.HUwatumia wtau hawa kw aumakini na kuangalia kila angle ili kesi iwe cha chance kubwa ya kushinda kabla ya kuingia mahakamani

Sijui hawa Takukuru kwanini wasiende extra miles, watoke jasho ili kupata taairfa zote muhimu, wapata ushahid wote unaohitajika kwa kila kosa.
 
Kabwe zinawahusu hao wakishikwa hao watawataja wenzao ndo ugumu unapoanzia hao. faamu hili pande la nyama wote wamelishika na wote wana damu mikononi isipokua hawa wa sasa ndo tumewaona na damu ila wote wadamu hiyo.
 
Kama change ya Rada imeishia kwenye matumbo yao, hela za EPA nazo tuliambiwa zilirudishwa na hatuna uhakika, hata hizo za Uswis zitakuwa vile vile, kwanini motion isichenji tukasema serikali ijiuzuru kwa makashfa yote haya! Hata wakisema zimerejeshwa tutajuaje?
MI NAONA TUANZE KASHIKASHI ZA SERIKALI IJIUZURU KWA HUU UFISADI!
 
Kuna mambo yanafanyika kana kwamba nchi hii haina mwenyewe au watawala wapo likizo,
1.Meno ya tembo
2.Kashfa za rushwa
3.Mabilioni ya uswis nk
Mbona hatuoni hatua zikichukuliwa?Kila jambo linakuja na kupita na hakuna hatua stahili zinazochukuliwa.
Ni vyema sasa tukaacha siasa na tuwe watendaji.
 
Kwa serikali hii ya Magamba,sitarijii jipya hata kidogo,hakuna wa kumatwa wala wa kuhojiwa juu ya mabilioni yaliyopatikana kwa njia za kifisadi.mifano hai ni mingi,leo wako wapi kina Kagoda,Meremeta,Deep green,Je leo nani alihusika na ufisadi wa Richmond?ni vipi leo mtarajie jambo jipya?hamkumbuki kuwa List of shame ilitajwa hadharani pale Mwembe yanga?na je hamkumbuki ni bunge hili hili la jamhuri ya Muungano liliweka maazimio na kuitaka serikali iyatekeleze kuhusu sakata la Richmond?je kimefanyika nini?hata hili sakata la mabilioni ya Uswis hakuna kitakachofanywa na serikali ya CCM,amini amini nawaambieni hakuna kitu kama hicho,ni bora kulileta suala hili kwa wananchi linaweza kusaidia kupata wananchi kadhaa wakaichukia serikali ya kifisadi,wakawachukia walificha mabilioni ya pesa ambayo yanasaidia kuinua na kuimarisha uchumi wa waswis,mabilioni hayo yanayosaidia kutoa ajira kwa vijana nchini Uswis,mimi napendekeza Mh Zitto atoke na hiyo list awataje hadharani na kisha awaelimishe wananchi hasa vijana jinsi yanavyowanyima fursa za ajira katika skta binafsi,yanavyowanyima huduma za kijamii nk.maana tukisema bunge liunde kamati au serikali ichunguze hakuna kitakachotokea.ni vema tukaongeza idadi ya watu watakaochukizwa na mafisadi hao kwa kuwajua majina yao,mwisho wa siku tutaongeza idadi ya wapinga ufisadi na wapenda mabadiliko. naomba kuwasilisha
 
Serikali haiwezi kushughulikia suala hilo. Fuatilieni maazimio ya bunge si kitu kwa serikali. Tunasahau haraka Azimio la Richmond bunge liliamua kufunga mjadala wakati serikali ilishindwa kutekeleza maazimio ya bunge. Zitto acha njia ya bunge haiwezi kuzaa lolote la maana. Ipelekeni hoja hii kwa wananchi na wote watajwe kwa majina katika mikutano ya hadhara. Kutegemea serikali kujichukulia hatua na kijichunguza hizo ni ndoto za utopia, na mimi simo.
 
Mkuu, Bornagain huo ndo utaratibu. Mimi sijui ZZK anachopinga ni nini.

Tuanzeni kuwataja kama tunawajua. Switzerland inahitaji list ya politically exposed persons. Akina Mkuchika hawawezi kumfunga paka kengele. Mimi naanzisha

1.ZZK
2.
3.
Jazia list hiyo. ZZK kwa kigezo kwamba ukiwa POAC kama ambavyo alishakuwa Cheyo michongo kama hiyo you must get your cut. If you think ZZK is squeaky clean, you had better think again

naona unajitahidi kuifanya hoja hii ififie! sisi si mazezeta tena! kama unataka inchi iingie kwenye "anarchy" endelea na ujinga wako huo. zitto! wakileta utani leta kwa raia tutawahukumu kwa ile torati yetu. hili si swala la chama ni swala la watanzania na mstakabali wa taifa lao dhidi ya wabadhirifu, wezi na mafisadi wanaoangamiza taifa lao walilojaliwa na mola wao. zitto songa mbele tupo na wewe. nadhani hiyop thread kaandika mkuchika kwa kujiita "azpa" chunguzeni maana hata hawa mawaziri wamo jf kwa acount zisizo eleweka.
 
Jamaa waliopo serikalini hawawezi kuukata mti walioukalia. Tumefikishwa hapa tulipo kwa makusudi kabisa na hao tunaowathamini sana, yaani wahisani. Akina Mkuchika na wenzake wanafuata upepo tu, ... Jumping to the masters voice. Yes, massa! Ndio maana akina Sokoine waliondolewa mwanzo kabisa ili kusafisha njia. ASIBAKI kiongozi wa aina ile ya akina Mwalimu (RIP) baba. Uongozi mbovu, putrid for that, tulio nao leo hii ni matokeo ya hujuma iliyonza pale yalipotimizwa malengo ya kufyagia njia. Usishangae tukabaki utumwani for another 1000 years licha ya massive plunder ya rasilimali zetu ikiendelea. Tumeridhia na kuwakabidhi utajiri wetu kwa mikono yetu wenyewe on a silver platter. Sasa hao hao watusaidie kurejesha?

Aspect moja inayojitokeza katika kutimiza strategy zao ni kuwarithisha uongozi ndugu wa waliopo madarakani. Wataendeleza yale yale. ANAEBISHA atazama trend hii ilivyo barani kote Africa. That aint no coincidence! Its very strategic and makes a whole lots of sense pale majority ya walalalahoi wanavyoendeleza ujinga na kukubali kujazwa ujinga ili mradi wasiibukie nje ya cycle hiyo ya ujinga.
 
Kama mwanasiasa ZZK hajawatendea haki waathirika wa haki waathirika na familia za watu wenye hali ya uzezeta au down syndrome ktk kauli zake.kwa kauli hiyo anaonyesha dharau ya kimaumbile na ulemavu mbalimbali.
Tukiacha hapo yawezekana yeye ni zezeta zaidi kwa kukurupuka na tuhuma za uswizi.ilimpasa atambue utendaji wa mabenki ya uswizi na usiri mkubwa walionao,maana akaunti nyingi ni numbered na ni siri kubwa kati ya mteja na personal banker kwa maana hiyo urejeshwaji wa pesa chafu utawezekana kwa kuiridhisha benki hiyo fedha zimeibiwa wapi?za umma?mlolongo mzima mpaka kufika uswizi,pesa nyingi hupitia off shore banks,companies baada ya kuhalalishwa.
Sasa swali;ameangalia haya kabla ya kutuita watanzania wapiga kura zezeta?

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Tukikubali ujinga huu wa watu kuchukua mafedha yetu hovyo hovyo tutakuwa si mazezeta tu bali Misukule!!!
 
Serikali yetu inageuka kichekesho kila siku, nilisikiliza matamshi ya Mkuchika na mkulu wa TaKUKURU yakanishangaza sana, eti wapelekewe majina, this is rubbish wao wana vyombo vya uchunguzi halafu wanaanza longolongo.
 
Mimi ndo nashangaa maajabu ya dunia yapo Tanzania, inakuweje serikali ya Uswisi yenye account number na majina ya walioweka fedha then iulizie tena majina Tanzania kama sio usanii ni nini hapo

Kwa upeo wangu mdogo sheria za benki akaunti za watu hazitolewi kienyeji. Lazima kuwe na sababu zinazotosheleza taarifa hizo unazitakia nini. Lazima useme ni fedha chafu zimepatikana isivyo halali na usalama lazima watoe historia inayokubalika kuwa mtu huyu kweli alipata huo mshiko visivyo. Na useme hiyo hela ukipewa utaiyumia kwa manufaa ya nani! Hapo utapewa ripoti kamili.
 
Wengine ni:

1. Lowa.............
2. Hussein Mwi......

Malizia na wewe.
 
Back
Top Bottom