Zitto: Mabilioni ya Uswisi – Tusigeuzwe Mazezeta

."The World suffer a lot.Not because of Violence of bad People.But because of the silence of good People" Big up our next coming President.
 
naona unajitahidi kuifanya hoja hii ififie! sisi si mazezeta tena! kama unataka inchi iingie kwenye "anarchy" endelea na ujinga wako huo.
Ikija kuthibitika ZZK naye ana pesa Uswiss utaona aibu kwa kuniita mjinga
. Worst case scenario hutajiita tena Buberwa
 
Namsifu sana Zitto kusimamia hoja yake.Ila mkuu,unaowataka watekeleze hiyo hoja naona ndo miongoni mwa watuhumiwa,je itawezekana?.
 
wacha wabwabwanye ndio zao ila mwisho unakaribia. nawasihi watanzania kuwa makini na swala hili na si ushabiki bali ni kwa maslahi ya nchi.
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto
(CHADEMA), amepinga kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika kuwa
Serikali ya Uswisi inataka majina ya Watanzania
walioficha fedha huko ndio waweze kusaidia
uchunguzi. Zitto ambaye hivi karibuni aliwasilisha bungeni
hoja binafsi ya kulitaka Bunge liazimie kuunda
kamati teule ya kuchunguza vigogo hao
wanaotuhumiwa, alisema kauli ya Mkuchika ni
wazi serikali inajihami kwa kuona kuwa itashindwa
kutekeleza azimio la Bunge. Katika taarifa yake aliyoiandika kwenye ukurasa wake wa mtandao
wa kijamii wa Twitter jana, Zitto aliwaonya
Watanzania wasikubali propaganda hiyo ya
serikali. “Nimeona ni vema nitoe kauli yangu rasmi kuhusu
suala hili. Lengo ni kuweka rekodi sawa juu ya
azimio la Bunge na kwamba serikali inapaswa
kutekeleza azimio na sio kutoa kauli tata za kukata
tamaa,” alisema. Alisema kuwa suala la Serikali ya Uswisi kutaka
majina lilisemwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
wakati akichangia hoja yake binafsi aliyowasilisha
bungeni na pia wakati akileta maombi yake ya
kuiondoa hoja ambayo yalikataliwa na Bunge. “Kama sio sababu mpya ni kwanini imeibuka upya
na kwa kasi? Ni wazi serikali inajihami kwa kuona
kuwa itashindwa kutekeleza azimio la Bunge.
Watanzania wasikubali propaganda hii ya serikali,”
alisema Zitto. Alifafanua kuwa, Bunge limeagiza serikali kufanya
uchunguzi kwa kutumia njia za kiserikali au
wachunguzi binafsi wa kimataifa. Akahoji ni
kwanini serikali inaanza kubwabwaja ilhali wala
haijaanza kazi hiyo? Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa
CHADEMA, alihoji kuwa serikali inajaribu kuficha
nini na kwanini baada ya wiki iliyopita Benki Kuu
kufanya uchunguzi kwenye mabenki ya biashara
jijini Dar es Salaam wa namna fedha zimekuwa
zikipelekwa nje halafu leo serikali inakuja na kauli za kukakata tamaa. “Watanzania wajue kwamba taifa la Swiss
limejengwa na linajengwa kwa fedha hizi za wizi
ambazo watu mbalimbali duniani wanaiba au
kukwepa kodi kwenye nchi zao na kuzificha huko,”
aliongeza. Alifafanua kuwa Serikali ya Uswisi hata siku moja
haiwezi kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania
katika suala kama hili. Ndiyo maana azimio la
Bunge linataka wachunguzi binafsi ambao
hawatahitaji ushirikiano wa Serikali ya Uswisi. “Nawakumbusha kwamba mwaka 1997 mara
baada ya Rais Mobutu Seseseko kuangushwa na
Rais Laurent Kabila kule Kongo – Kinshasa, Serikali
ya Swiss iliitaka Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo kuonyesha ushahidi kuwa hela hizo za
Mobutu zilikuwa zimepatikana kwa njia haramu,” alisema. Kwamba Waswisi walitaka Kabila awahakikishie
kuwa fedha zile zaidi ya dola bilioni nane za
Kimarekani, Mobutu hakuzipata kihalali ndio
waweze kuzirejesha. Alisema kuwa majibu ya aina hii ni majibu
‘standard’ ambayo kila nchi inapewa. “Hata Marekani ilipokuwa inafuatilia wakwepa
kodi wao walijibiwa hivi hivi. Hatimaye Serikali ya
Marekani ikaamua kununua taarifa hizo na
kuwakamata wakwepaji kodi wao walioficha fedha
Uswisi. “Hao ndio Waswiss ambao Serikali ya Tanzania
inashabikia majibu yao. Bila aibu mawaziri wetu
wanayanukuu majibu ya Waswiss kama kasuku.
Tunasahau historia haraka sana. Tunakuwa kama
mazezeta,” alisema. Zitto alionya kuwa hatupaswi kuwa taifa la
mazezeta kwani mabwege na mazezeta huimba
kila wanachoambiwa kuimba. Kwamba sasa
Serikali ya Tanzania imekuwa msemaji wa Serikali
ya Uswisi badala ya kuchunguza utoroshaji wa
fedha haramu na kisha kutoa taarifa bungeni. Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC),
aliitaka serikali ianze uchunguzi mara moja kama
namna ilivyoelekezwa na Bunge. “Suala hilo sio la kisiasa, sasa ni Azimio la Bunge
ambalo linahitaji kutekelezwa kikamilifu. Suala hili
sio suala la Zitto Kabwe tena, ni suala la Bunge, ni
suala la wananchi. Wananchi hawataki uzezeta wa
watu waliopewa dhamana ya kutekeleza azimio
lao,” alionya. Alisisitiza kuwa, kama hawawezi wapishe watu
wenye uwezo wa kusimamia maslahi ya
Watanzania kwa kuchukua hatua stahili za
kuchunguza utoroshaji mkubwa wa fedha za
kigeni, ukwepaji mkubwa wa kodi na ufisadi
uliosababisha Watanzania kuficha mabilioni kwenye mabenki nje ya Tanzania. “Hatutakaa kimya mpaka tuone mwisho kamilifu
wa suala hili. Utekelezaji wa Azimio la Bunge
itakuwa ni salamu tosha kwa mafisadi na
watoroshaji wa fedha haramu kwamba hawana pa
kujificha na Tanzania sio taifa la kuchezeachezea.
Lazima tushinde vita hii. Anayeona hawezi kutuongoza kuishinda atupishe mapema,” alisema
Zitto.
Source:tanzania daima
 
Zitto tunaomba majina, mbona na wewe unatutia shaka?

Duh! Rafiki yangu - nawe umekuwa kasuku wa Waswisi? Ni jukumu la Serikali yetu kuifanyia kazi taarifa ya Uswisi kuwabaini walioweka pesa huko kwao kwa lengo la kuwakamata huku. Ni kazi ya serikali na vyombo vyake husika vya dola. Si kazi yangu, wewe, Zitto au mwingine yeyote.

Kujiuma uma kwa serikali ni dalili kwamba haina nia kulifuatilia suala hili kwa dhati na sababu yake hata mtoto wangu wa miaka 12 anafahamu.


Utawala huu wa JK ni hovyo kupindukia!! Kuna mwingine sasa hivi atasema Zitto anatafuta umaarufu wa kisiasa!!!
 

Duh! Rafiki yangu - nawe umekuwa kasuku wa Waswisi? Ni jukumu la Serikali yetu kuifanyia kazi taarifa ya Uswisi kuwabaini walioweka pesa huko kwao kwa lengo la kuwakamata huku. Ni kazi ya serikali na vyombo vyake husika vya dola. Si kazi yangu, wewe, Zitto au mwingine yeyote.

Kujiuma uma kwa serikali ni dalili kwamba haina nia kulifuatilia suala hili kwa dhati na sababu yake hata mtoto wangu wa miaka 12 anafahamu.


Utawala huu wa JK ni hovyo kupindukia!! Kuna mwingine sasa hivi atasema Zitto anatafuta umaarufu wa kisiasa!!!

Asemayo Zitto ni kweli kabisa. mamlaka ya Benki Kuu ya uswisi zimetoa taarifa za kuwepo kwa mapesa ambayo Watz wakiwemo wanasiasa wameyaweka huko. sasa Mkuchika anataka Watanzania ndiyo wapeleke majina na details za hizo accounti/ SHHHIIT!!!

Hiyo ni kazi ya serikali, fullstop. Itakuwa ni aibu kwa serikali hii ya Kikwete baadaye kusema imeshindwa kuwabaini watu hao kwa sababu wananchi Watz wameshindwa kutoa ushirikiano!!!

Again nasema hii itakuwa BULLSHIIIT!
 
Bunge lina-track record ya kukingia mafisadi vifua. Huu uchunguzi anaoutaka ZZK hapa ndo ulitumika kwenye Richmond. Je ulisaidia nini?

ZZK, acha kutafuta cheap popularity kwa kujifanya una uchungu na nchi, kwanza ushawahi sema unayo majina, kwanini usiweke mambo hadharani?

Pili, ni suala la kiutaratibu kwa benki za Uswiss kutaka PEP( names of politically exposed persons) ili itoe ushirikiano. Nimetoa link hapa chini. Kila linaloongelewa hapo chini linaonesha jinsi gani benki za ki-swiss zipo tayari kutoa ushirikiano tofauti na ZZK anavyozipaka matope.

ZZK tumwogope kama ukoma. Ana kikosi chake cha propaganda kinachofanikiwa kulaghai watu wengi

How a New Swiss Law Can Help Egypt Get Its Money Back - TIME
 
Maswali ambayo hao wenye mabilioni wanatakiwa waulizwe:

1. Waonyeshe vyanzo vyao vya mapato vilivyowawezesha kuwa na pesa nyingi kiasi hicho na rekodi za kuonyesha kila walipokwenda kudeposit pesa hizo ikiwemo receipts toka bank na passport ambazo zitaonyesha tarehe ambazo waliingia Switzerland kuweka pesa hizo.

2. Watanzania hawaruhusiwi kuwa na bank accounts nchi za nje, kama sikosei hii sheria bado ipo mpaka kesho. Wahusika waonyeshe ni nani aliyewapa kibali kule BoT cha kufungua bank accounts nchi za nje.

3.Viongozi hujaza forms za kuonyesha mali mbali mbali walizonazo. Hili kama sikosei hufanywa kila baada ya muda fulani. Je, hao viongozi wahusika waliwahi kuyaorodhesha mabilioni hayo katika form hizo?

Wapewe muda wa mwezi mmoja tu kukamilisha hayo na wakishindwa kufanya hivyo basi wapandishwe kizimbani kama wahujumu uchumi na wafilisiwe mali zao.
 
Tanzania inabidi tufike mahala tuwe na vyombo vya uchunguzi huru ambavyo havina mkono wa serikali lakini unachukua kesi ya mkapa unampelekea mkuchika halafu unasubiri maajabu mimi sana sana nakushangaa wewe kumshangaa mbabaishaji mkuchika.
 
Kama kweli zito anamachungu na nchi yake kwanin asiyataje hayo majina tukajua??
Zito akifariki leo na hizi dana dana za mafisadi za kuteteana wanazopiga kweli tutafanikiwa kuyatambua majina ya hao wezi na wahujumu uchumi wetu??
 
Bunge lina-track record ya kukingia mafisadi vifua. Huu uchunguzi anaoutaka ZZK hapa ndo ulitumika kwenye Richmond. Je ulisaidia nini?

ZZK, acha kutafuta cheap popularity kwa kujifanya una uchungu na nchi, kwanza ushawahi sema unayo majina, kwanini usiweke mambo hadharani?

Pili, ni suala la kiutaratibu kwa benki za Uswiss kutaka PEP( names of politically exposed persons) ili itoe ushirikiano. Nimetoa link hapa chini. Kila linaloongelewa hapo chini linaonesha jinsi gani benki za ki-swiss zipo tayari kutoa ushirikiano tofauti na ZZK anavyozipaka matope.

ZZK tumwogope kama ukoma. Ana kikosi chake cha propaganda kinachofanikiwa kulaghai watu wengi

How a New Swiss Law Can Help Egypt Get Its Money Back - TIME

mkuu kwenye hii link wanaonekana ni viongozi tena marais huoni hao tayari kwa title zao huitaji kuwataja Hossin Mubaraka (Egypt) Charles Tailor(liberia) Mobutu SeSeseko (zaire) tatizo kwetu wao wamesema kuna hela sisi serikari yetu iseme watu hao ni fulani na furani ili waproove na kuwafilisi. pia fahamu hata Membe alisema anawajua mbona kaka kimya na lalitangaza bungeni. anawajua. Tusimwonee Zitto serikari imepata taarifa ichunguze si kama mahakamani ukibaka si polisi wanachunguza kama kweli umebaka anaetakiwa kuchunguza ni yule anaeleta mashtaka au.
 
tatizo kwetu wao wamesema kuna hela sisi serikari yetu iseme watu hao ni fulani na furani ili waproove na kuwafilisi. pia fahamu hata Membe alisema anawajua mbona kaka kimya na lalitangaza bungeni. anawajua. Tusimwonee Zitto serikari imepata taarifa ichunguze

Nachosema mimi ni kwamba ZZK kwa hili la kurecover pesa za Uswiss to this end he hasn't played any useful part. Therefore he should stop barking like a toothless dog

If CCM leaders won't bell the cat, why can't ZZK jump at the chance and gladly do it? According to his report, in the last parliamentary session, he has proof of how these POLITICALLY EXPOSED PERSONS got kick backs through oil&gas contracts.

That kind of evidence is all he needs. It's not only required in the RESTITUTION OF ILLICIT ASSETS ACT but also in the initial procedures of INTERNATIONAL MUTUAL LEGAL ASSISTANCE

You definitely need a dedicated person or government with a will to do it. I can't see that in Membe. Actually I can't see that in the whole corrupt government of CCM
 
Akili ndogo kutawala akili kubwa ndo madhara yake haya..
Majibu rahisi kwa maswali magumu (sifa za mazezeta na mabwege aka majuha)
Nachukia sana nionapo mzee kama yule Mkuchika nashadidia upuuzi katika vikao vya Bunge na kutoa kauli ambazo haziendani na hadhi ya umri hata na kazi yake ya awali (Afisa wa Jeshi Mstaafu). Watoto wetu wanajifunza nini kupitia yeye na wenzie wenye umri na sifa kama zake?
Ama hakika, kizazi hiki hakina cha kujifunza kutoka kizazi kilichopita zaidi ya UFISADI na UONGO uliopitiliza.
Wanastahili kupigwa mawe.
 
angalia baadhi ya kauli za moto ...

“Watanzania wajue kwamba taifa la Swiss limejengwa na linajengwa kwa fedha hizi za wizi ambazo watu mbalimbali duniani wanaiba au kukwepa kodi kwenye nchi zao na kuzificha huko.....

Suala hilo sio la kisiasa, sasa ni Azimio la Bunge ambalo linahitaji kutekelezwa kikamilifu. Suala hili sio suala la Zitto Kabwe tena, ni suala la Bunge, ni suala la wananchi. Wananchi hawataki uzezeta wa watu waliopewa dhamana ya kutekeleza azimio lao,” alionya Zitto.

Alisisitiza kuwa, Hatutakaa kimya mpaka tuone mwisho kamilifu wa suala hili. Utekelezaji wa Azimio la Bunge itakuwa ni salamu tosha kwa mafisadi na watoroshaji wa fedha haramu kwamba hawana pa kujificha na Tanzania sio taifa la kuchezeachezea. Lazima tushinde vita hii. Anayeona hawezi kutuongoza kuishinda atupishe mapema,” alisema Zitto.
  • :israel:
 
Back
Top Bottom