Zitto, Lipumba na mkakati wa kuidhoofisha CHADEMA

Mheshimiwa Zitto Kabwe habari. Ni ukweli ambao kuna siku itabidi uukubali ingawa sasa utaona uzushi kama uzushi mwingine. Hawa watu (JF na Viongozi wa Chadema) hawakuamini kabisaaa! Mfano baadhi ya viongozi wenzako wanatumia magazeti yao kukuchafua kila uchao. Bila kuuma uma maneno hawan kuamnini kwa sababu ni MUISLAMU! Sina uhakika na uislamu wako ila hilo lina watia hofu sana. Umekuja mara nyingi hapa kujitetea lakini bado hawakuamini so long you are still a MUSLIM.

Ukitaka wakuamini, badili DINI uwe MKRISTO ikiwezekana MKATOLIKI kisha tafuta binti wa waasisi umuoe! Hapo utapewa uwenyekiti!

Usilete upumbavu wako wa dini hapa. Hakuna udini wowote hapa, hizi ni propaganda sumu zinazoendeshwa na CCM na intelijensia yao.

Huu moto mnaotaka kuuwasha wa chuki za kidini ukiwaka Tanzania kamwe hamtaweza kuuzima.
 
Nimefurahi kuona Zitto kajibu, nimekua nafuatilia kwa karibu sana mazungumzo ya shutuma za usaliti wa Zitto Kabwe, sitaki kuongeza chumvu lakini Zitto mdogo wangu wazungu wanasema katika hali hii jukumu ni lako kutushawishi kama bado ni mwenzetu.

Nakubali kwamba umetumia ujana wako, nguvu zako na fedha zako kutumikia chama, swala ni kukitumikia kwa faida ya nani kwanza? yako binafsi na sio ya watanzania wala chama.

Pili, tunafahamu sisi tuliokuana wewe shule moja mwaka mmoja kama wewe na Halima Mdee, mbona hatumzongi Halima? kumbuka pamoja na kudai kutumia rasilimali zako bado tunakumbuka jinis mbowe huyo unayemtukana leo alivyotumia rasilimali zake kwa chama chake na wewe kukutengeneza na kukujenga wakati ukiwa huna rasilimali zako kama leo hii mpaka una hammer na rasiliamali zisizoendana na kipato chako.

Sisi ya nyuma hatuangalii lakini kuwa na shukurani tu katika mwendeno wako, mungu hapendi kiburi, angalie yule mwehu mwingine pale habari aliyesaidiwa na mbowe wakati akitoe alikotokea akajengewa kijumba chenye vyumba vya milango inayofunguka yote mbele, akamtukana mbowe kwa naman ya ajabu kwa tamaa zake, leo hii tangu atoke kwa Mbowe hajabadilika chochote zaidi ya kupata freelander yenye engine ya rav 4 na kupoteza hata heshima ndogo aliyokua nayo zamani. Kapoteza vyote hawezi kurudi tena na hana allichokipata bora wewe wamekupa freelander na umenunua nyumba za garama, na itoshe
 
sina chuki na wewe kwa sababu hata mimi nina kwetu. ila unanisikitisha na huo ujeuri wako. kushiriki kujenga chama unakuwa jeuri namna hiyo, je ingekuwa umeshiriki kukianzisha? si kingekuwa kimeparaganyika kama vyama vya lyatonga?

Hana ujeuri wewe ndio umeona hivyo..wengine hatujaona hivyo. Ulitaka ajibuje sasa?? toa mfano wa jibu linaloonesha kuwa huyo mtu siyo jeuri.

Ahsante sana kwa ufafanuzi wako mzuri ndugu Zitto. Ninakuheshimu kwa kuwa muwazi kabisa kuwa una ambitions za kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku moja Inshallah. Ni viongozi wachache sana wenye ujasiri kama huo.

Ifikapo mwaka 2015 tutarejea kwenye kumbukumbu hii ya humu JF na kunukuu maneno yako haya mazito:

1. "Kumekuwa na juhudi za makusudi za watu kutaka nitoke CHADEMA, narudia tena siwezi kutoka."
2. "Kwamba nazungumza na NCCR ni uwongo, ni uzushi na propaganda yenye nia mbaya kwangu."

Mimi binafsi kama Fareed naomba niweke wazi kuwa siko ndani ya CHADEMA, wala si mwanachama wa chama hiki. Ila wewe mwenyewe umekiri hapa kuwa unasikitishwa na baadhi ya viongozi wenzako ndani ya CHADEMA ambao wanaamini propaganda za "chuki, fitna, na WIVU!" dhidi yako.

Ukweli wa yote haya utathibitika tutakapokaribia uchaguzi wa 2015. Inshallah katiba itabadilishwa 2014 ili wewe na Watanzania wengine wote wenye umri wa chini ya miaka 40 waweze kugombea Urais. Ninavyojua ambitions zako, sitashangaa kama utachukua fomu kutaka uwe mgombea Urais wa CHADEMA mwaka 2015 iwapo katiba/sheria husika zitabadilishwa kuruhusu hiyo.

Kwa mujibu ya maoni ya watu kadhaa (me included), it is highly unlikely that CHADEMA will pick Zitto Kabwe as its presidential candidate in 2015 kutokana na mazingira halisi ya siasa za Tanzania na ndani ya chama hicho chenyewe. Sasa wewe na strong ambitions zako utafanyaje hapo? Ndiyo navyoona habari za wewe kuhamia NCCR na kuwa mgombea wake wa Urais 2015 zinaleta mantiki. Sidhani kama una subira kama aliyokuwa nayo Jakaya Kikwete kungoja miaka 10 kutoka 1995 mpaka 2005 alipofanikiwa kuteuliwa kuwa mgomea Urais wa CCM. Una sifa nyingi za uongozi, sijui kama patience is one of your virtues.

Lakini kwa kuwa umesema mwenyewe Zitto kuwa kamwe hutakihama CHADEMA. Hiyo ni habari njema, tusubiri matokeo ya kuelekea uchaguzi wa 2015 kama utakuwa mkweli kwenye ahadi yako hii.

Mkuu ulichofanya ni ku-connect dots kutokana na mazingira. Ungeandika post yako kwa mtindo wa kuuliza ingekuwa nzuri. Lakini umeandika kana kwamba una uthibitisho.
 
Kushiriki kikamilifu kujenga chama ni kigezo za JEURI YA CHADEMA! Wala sioni aibu kujivunia hilo. Kushiriki kwangu kujenga chama ndio kumewafanya wengi muingie CHADEMA. Nimekuwa mbunge miaka mitano na nimeshiriki kukipandisha sana chama. Lazima nijidai na huna mamlaka kunizuia kujidai. Kama una chuki saga nyembe umeze, sina cha kukusaidia

ZItto Hili ndo tatizo lako hacha kuwa na HASIRA JENGA HOJA USITUKANE MTU
 
Tumekusikia ukijibu hoja ndg ZITTO chamsingi ni kuaminisha watanzania kuwa wanachokisema si uzushi ili watanzania waendelee kukuamini kama ulivyokuwa mpinganaji juu ya dhuluma kwa watanzania,vinginevyo wataendelea kuangalia mwenendo wako ndani na nje ya chama ili kuamini kama upo nao katika kumpambana na wezi wanaodhulumu rasilimali za nchi hii kwa manufaa yao na familia zao.Watanzania wa leo sio wale wa miaka ya sabini wapo radhi kuhoji pale wanapoona hawatendewi haki.Na nyie kama viongozi mkubali kukosolewa ili kuwaletea watz maendeleo na muondoe dhana kuwa kiongozi ndie anayeelewa kila kitu na kufikiri mnaowaoongoza hawana uelewa juu ya masuala ya nchi hii.
 
Huu ni utabiri kama wa tabiri nyingine tu na wasomaji wachukulie kama utabiri. Sina mazungumzo yeyote na chama chochote kuhusu kugombea Urais. Ni kweli nina ambition. Ambition zangu zimo ndani ya CHADEMA, chama ambacho nimeshiriki kukijenga.
Kumekuwa na juhudi za makusudi za watu kutaka nitoke CHADEMA, narudia tena siwezi kutoka. Narudia, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine choochote maishani mwangu tofauti na CHADEMA. Narudia, zaidi ya nusu ya umri wangu nimeutumia CHADEMA. Nimetumia nguvu zangu, akili zangu na rasilimaliu zangu kusaidiana na wenzangu kujenga CHADEMA.
Kwamba nazungumza na NCCR ni uwongo, ni uzushi na propaganda yenye nia mbaya kwangu.
Sizungumzi na mtu yeyote kuhusu kuhujumu chama changu. Nimeshasema yeyote mwenye ushahidi na jambo hili autoe. Gazeti la Mwanahalisi lilitoa muda na namba za simu za watu ninaozungumza nao. Nimewachallenge waseme nilikuwa nazungumza nini. Watoe content ya mazungumzo na kama itaonekana kwa namna yeyote ile nilihujumu chama changu nitawajibika.
Watanzania wamekuwa na tabia ya kuamini mambo kwa mkumbo.
Uzushi dhidi yangu umekuwa ukichukuliwa na watu kama ukweli tena ukweli mtupu. Watu kwa malengo yao wamekuwa wakitumia majina zaidi ya moja kwa mtu mmoja na kuingia JF kuandika uzushi (kama huu wa leo) ili kunichafua na kunigombanisha na wenzangu. Bahati mbaya sana baadhi ya viongozi wenzangu wa chama wanachukua chuki, fitna na uwongo unaoandikwa humu kama ukweli. Inasikitisha sana.
Ninapenda kuwafahamisha wasomaji wote wa JF kuwa sehemu ya habari iliyoandikwa hapa katika thread hii ni uwongo wa makusudi dhidi yangu. Ni imagination ya mtu ambaye anaumwa ugonjwa wa ZITTOPHOBIASIS! Ugonjwa ambao watu wengi wanaumwa na ninasikitika kuwa dawa ya ugonjwa huu hata kwa babu haupo maana ni ugonjwa unasambazwa na ugonjwa wa chuki, fitna, na WIVU!
Pole sana kijana mwenzangu, hao watu wenye Zittophobiasis(Ugonjwa wa wifu, chuki na fitina) watakuwa wanatajirika sana kwa kulipwa na hao wasiokitakia mema chama cha Chadema. Sasa ukitaka watu warudishe imani kwako nakushauri urudie enzi zile za Buzwagi, I mean ibua mabomu mazito mjengoni maana yapo mengi.
 
Baada ya kama miaka 10 kutoka sasa, ninaamini Zitto anaweza kuwa kiongozi mzuri sana. Lakini shurti apite kwanza kwenye hili tanuru la sasa.

Kwa sasa, he appears to be short of this and that which - to be fair - these need to be put right first.
He's not a kid but "a political virgin" could be a more appropriate tag - which means there's plenty of room for him to continue learning. Let him.

Nawapenda sana watu wanaom-challenge/criticise Zitto sasa hivi kwani wanampitisha kwenye tanuru la kumtengeneza kuwa kiongozi mzuri wa baadae. Akipita hapa, kiongozi tumepata.
 
Huu ni utabiri kama wa tabiri nyingine tu na wasomaji wachukulie kama utabiri. Sina mazungumzo yeyote na chama chochote kuhusu kugombea Urais. Ni kweli nina ambition. Ambition zangu zimo ndani ya CHADEMA, chama ambacho nimeshiriki kukijenga.
Kumekuwa na juhudi za makusudi za watu kutaka nitoke CHADEMA, narudia tena siwezi kutoka. Narudia, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine choochote maishani mwangu tofauti na CHADEMA. Narudia, zaidi ya nusu ya umri wangu nimeutumia CHADEMA. Nimetumia nguvu zangu, akili zangu na rasilimaliu zangu kusaidiana na wenzangu kujenga CHADEMA.
Kwamba nazungumza na NCCR ni uwongo, ni uzushi na propaganda yenye nia mbaya kwangu.
Sizungumzi na mtu yeyote kuhusu kuhujumu chama changu. Nimeshasema yeyote mwenye ushahidi na jambo hili autoe. Gazeti la Mwanahalisi lilitoa muda na namba za simu za watu ninaozungumza nao. Nimewachallenge waseme nilikuwa nazungumza nini. Watoe content ya mazungumzo na kama itaonekana kwa namna yeyote ile nilihujumu chama changu nitawajibika.
Watanzania wamekuwa na tabia ya kuamini mambo kwa mkumbo.
Uzushi dhidi yangu umekuwa ukichukuliwa na watu kama ukweli tena ukweli mtupu. Watu kwa malengo yao wamekuwa wakitumia majina zaidi ya moja kwa mtu mmoja na kuingia JF kuandika uzushi (kama huu wa leo) ili kunichafua na kunigombanisha na wenzangu. Bahati mbaya sana baadhi ya viongozi wenzangu wa chama wanachukua chuki, fitna na uwongo unaoandikwa humu kama ukweli. Inasikitisha sana.
Ninapenda kuwafahamisha wasomaji wote wa JF kuwa sehemu ya habari iliyoandikwa hapa katika thread hii ni uwongo wa makusudi dhidi yangu. Ni imagination ya mtu ambaye anaumwa ugonjwa wa ZITTOPHOBIASIS! Ugonjwa ambao watu wengi wanaumwa na ninasikitika kuwa dawa ya ugonjwa huu hata kwa babu haupo maana ni ugonjwa unasambazwa na ugonjwa wa chuki, fitna, na WIVU!

Nishukuru kwa maelezo yako na kujaribu kujenga hoja. Kwa kifupi Mh Zitto ujuwe binafsi sina chuki na wewe na ni kiri ulikuwa mmoja wa wanasiasa niliowapenda sana hasa kipindi kile cha ulipofukuzwa bungeni imani yangu kwako ilikuwa kubwa. Tatizo nilionalo ni umebadilika ghafla hasa pale hoja ambazo tuliokuwa tunakufahamu usingeweza kuziunga mkono kwa mantiki ya kawaida siku hizi sivyo. Anzia ulivyo badiliaka kuhusu Dowans angalia matukio ya bungeni na taarifa nyingine nyingi tunazo zipata. Lakini pia nikiri kuwa sisi ni wanadamu tunamapungufu yetu kama wanadamu tusamehe pale kwa dhamira yako kabisa na Mungu akiwa shaidi kuwa tumekusingizia usivyo kweli hata mimi singefrahishwa. Lakini kama tuanayosema nia kweli itadhihirika tuu na imani yetu kwako itarudi tuu. Pia ujue kuwa Watanzania kwa sasa tumepigika kweli tunapoona tumepata chama kinachoweza kutuletea matumaini tunataka kukilinda kwa gharama yeyote ili mtu anayekwenda kinyume lazima tumlaani na laana ya watanzania wa sasa imemfikia mungu.
 
Huu ni utabiri kama wa tabiri nyingine tu na wasomaji wachukulie kama utabiri. Sina mazungumzo yeyote na chama chochote kuhusu kugombea Urais. Ni kweli nina ambition. Ambition zangu zimo ndani ya CHADEMA, chama ambacho nimeshiriki kukijenga.
Kumekuwa na juhudi za makusudi za watu kutaka nitoke CHADEMA, narudia tena siwezi kutoka. Narudia, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine choochote maishani mwangu tofauti na CHADEMA. Narudia, zaidi ya nusu ya umri wangu nimeutumia CHADEMA. Nimetumia nguvu zangu, akili zangu na rasilimaliu zangu kusaidiana na wenzangu kujenga CHADEMA.
Kwamba nazungumza na NCCR ni uwongo, ni uzushi na propaganda yenye nia mbaya kwangu.
Sizungumzi na mtu yeyote kuhusu kuhujumu chama changu. Nimeshasema yeyote
mwenye ushahidi na jambo hili autoe. Gazeti la Mwanahalisi lilitoa muda na namba

za simu za watu ninaozungumza nao. Nimewachallenge waseme nilikuwa nazungumza nini. Watoe content ya mazungumzo na kama itaonekana kwa namna yeyote ile nilihujumu chama changu nitawajibika.
Watanzania wamekuwa na tabia ya kuamini mambo kwa mkumbo.
Uzushi dhidi yangu umekuwa ukichukuliwa na watu kama ukweli tena ukweli mtupu. Watu kwa malengo yao wamekuwa wakitumia majina zaidi ya moja kwa mtu mmoja na kuingia JF kuandika uzushi (kama huu wa leo) ili kunichafua na kunigombanisha na wenzangu. Bahati mbaya sana baadhi ya viongozi wenzangu wa chama wanachukua chuki, fitna na uwongo unaoandikwa humu kama ukweli. Inasikitisha sana.
Ninapenda kuwafahamisha wasomaji wote wa JF kuwa sehemu ya habari iliyoandikwa hapa katika thread hii ni uwongo wa makusudi dhidi yangu. Ni imagination ya mtu ambaye anaumwa ugonjwa wa ZITTOPHOBIASIS! Ugonjwa ambao watu wengi wanaumwa na ninasikitika kuwa dawa ya ugonjwa huu hata kwa babu haupo maana ni ugonjwa unasambazwa na ugonjwa wa chuki, fitna, na WIVU!

Muungwana ni vitendo na tuupe muda nafasi,hii thread inaukweli kwenye mengi hasa kuhusu lipumba na ccm wanavyocheza karata zao,kuhusu zitto ni mengi tumesikia na pamoja na maamuzi yake mengi yasiyojenga chama chake ili kiwe mbadala wa ccm ambavyo yataendelea kuleta projections za uongo na kweli kuhusu zitto.

Viongozi wenzake kuingia mtegoni ndg yangu zitto usishangae,ni ukweli cdm inakubalika kuliko maelezo na mm nina mfano maana nimefanya kazi vijiji vingi na kujionea ukweli na hata huku mitaani,hivyo kwa sasa cdm imepaniwa mno hivyo kuwaweka viongozi ktk wakati mgumu kupambana ktk mazingira ya siasa za tz ambayo hata dola zinahakikisha ccm hawatoki madarakani,inapotokea mwenzao akawa mtata lazima wachukue tahadhari za msingi maana hata nccr wamekufa vivyo hivyo.rudisha imani kwa viongozi,wanachama na watanzania wote kuwa utapambana kama zitto tunaemjua maana zitto wa sasa ni zitto mpya.kelele zote hizi zitto ni sababu watu wamekupenda na kukuamini mno halafu ghafla ukaanza kutoa kauli tata.

Kwa angalizo tu ccm na mfumo wao kwa sasa hauwezi kubadili taifa hili zitto na naamini unajua hilo,tunachotaka ni utawala mpya na mifumo mipya na ccm hawatoki kwa kubembelezwa bila nguvu ya umma ingawa inahitajika mipango mizuri ili nguvu ya umma itumike vizuri bila madhara.kule bungeni mtapiga kelele sana haitasaidia labda majadiliano ya budget na mambo ya kisheria yasiyo na madhara kwao.

Zitto tunataka mikakati madhubuti kuiondoa ccm madarakani ili tujifunze kuwa na nidhamu kisiasa na hata cdm wakichemka wananchi wapate ujasiri wa kusema hapana.

CCM tumeichoka lakini mnaibeba bila kujua(pengine makusudi) na kudhoofisha cdm(maana hakuna upinzani mwingine).hebu naibu katibu mkuu wetu mfafanulie shehe mkuu nia ya cdm lakini pia waambie wapinzani wengine waache kejeli kwa cdm zisizojenga upinzani waambie naibu katibu mkuu wetu zitto maana najua inakuuma wanavyopaka chama chako matope wakati nusu ya umri wako umeshiriki mno kukijenga!
 
Cdm wangekuwa wanakubalika kihivo walau wangesimamisha mgombea ktk kila jimbo which they didn't. surprise surprise..

Teheh tehehe!! hueleweki.... wewe ni mpenzi/mshabiki/mshirika wa Mh Zitto ambaye ni mbunge/mwanachama/kiongozi na tena amechangia ktk kukiinua CHADEMA at the same time ni mchukia/adui/mpinzani wa CHADEMA!!!!!!!!!!!! Au ndo mnaompeleka kiongozi wetu Zitto kusiko???? umekuwa kinyonga wewe??????????:ballchain:
 
jamani hii ndiyo peoples power kushutumiana hivi. nakubaliana na kina lipumba and co. kuhusu kutumika kuidhoofisha chadema lakini si zitto. kila binadamu anakosea sasa isiwe kosa moja tu basi lawama zote tumtupie yeye. please let us change and help our chadema to prosper
 
Kushiriki kikamilifu kujenga chama ni kigezo za JEURI YA CHADEMA! Wala sioni aibu kujivunia hilo. Kushiriki kwangu kujenga chama ndio kumewafanya wengi muingie CHADEMA. Nimekuwa mbunge miaka mitano na nimeshiriki kukipandisha sana chama. Lazima nijidai na huna mamlaka kunizuia kujidai. Kama una chuki saga nyembe umeze, sina cha kukusaidia

Kumbe mhuni tu wewe. Sikufahamu.
 
.

Bahati mbaya sana baadhi ya viongozi wenzangu wa chama wanachukua chuki, fitna na uwongo unaoandikwa humu kama ukweli.

Mh. Zitto,

Kwa kuwa umekiri kwamba kuna baadhi ya viongozi wenzako ndani ya chama ambacho una haki ya kujivunia kwamba umeshiriki kukijenga hadi kimefika hapo kilipo, wanachukua chuki fitna na uongo unaoandikwa hapa jf na kuuamini kwamba ni ukweli, basi hapo una kazi mahsusi ya kufanya.

Unatakiwa kutafuta namna ama niite mbinu ya kuhakikisha kwamba hizo chuki na fitna za baadhi ya viongozi wenzako zinaondoka. Ni ukweli kwamba pamoja na wewe kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa chadema lakini ni ukweli pia kwamba kuna viongozi na wananchadema ambao wamechangia kukufikisha hapo ulipo, kwahiyo kama wewe umechangia ukuaji wa chama hilo ni jambo zuri na uliwajibika kuhakikisha chama kinakua.

Suala lingine, ni ukweli kwamba wengi wa watu wanaokupinga sasahivi, kuanzia jf hadi mitaani, hapo kabla walikuwa wakikuunga mkono sana, kwahiyo mabadiliko haya ni salamu tosha kwako kujitathmini na kuona ni wapi umekwenda kinyume na matarajio yao, ili ujirekebishe na uweze kupata uungwaji mkono kama kawaida. Mimi naamini kwamba hawa watu wanaokushambulia sio kwa sababu ya chuki ama fitna, hawa watu wanakupenda isipokuwa kuna mahali umekwenda kinyume na matarajio yao. Jiulize we mwenyewe kwanini ulipata ushindi wa kishindo mwaka 2005 kigoma kaskazini lakini mwaka 2010 ukapata ushindi wa kawaida!!?? au wapiga kura wako wa kigoma kaskazini nao wana chuki, fitna na husda!!??

Namalizia kwa kukushauri ujiepushe na maneno ya waimba taarabu, kumwambia mtu asage chupa anywe, ama maneno mengine yanayofanana na hayo, ni kauli tunazosikia kutoka kwa waimba taarabu, kwahiyo haitarajiwi kiongozi wa kitaifa kama wewe tena mwenye ambition za kuwa rais wa nchi hii ugeuke kuwa muimba taarabu katikati ya jukwaa la siasa.
 
Mh Zitto, binafsi nashukuru umejitokeza kukanusha hili suala. Nina maswali machache tu ambayo ukiyatolea majibu itatusaidia wengi kujua kuwa bado u pamoja nasi.
1. Kufuatia taarifa ya Mwanahalisi kuhusiana na zile simu ni UKWELI ulikuwa unawasiliana na mmoja wa viongozi waandamizi wa TISS. Ila ulitoa challenge walete content of communication kuprove kwamba uliuhujumu chama. Kwa sisi tuliobahatika kupata mafunzo ya kijeshi, mnapokuwa vitani halafu kamanda mwenzenu (anaongea na adui TISS mwenye Game Changing capabilities) kwa njia zake binafsi bila timu ya makamanda wenzio kujua, unajua hilo jambo likifahamika, utapelekwa kwenye court marshall na hukumu yake ni kifo kwa risasi. Hilo ni bila kujali ulikuwa unaongea naye nini. Sababu ni kuwa imani ikiondoka kushinda ni kazi au almost impossible. Wewe binafsi huoni kama lile lilikuwa ni kosa kubwa au bado unataka mpaka walete na maongezi?
2. Mawasiliano yako na mkuu wa nchi kwa njia binafsi huoni kuwazinazoofisha au kupunguza negotiating power kama chama?

Nijambo zuri kuona unajivunia kuwa umejenga Chadema kwa nusu ya umri wako. Sote tuliopitia System yetu ya Elimu tunafahamu kuwa Usalama wa Taifa umekuwa unarecruit vijana tokea wakiwa shule za Sekondari. Sasa unaweza kuwa umekulia Chadema ila matendo yako wakati mwingine yanasabisha maswali mengi ambayo majibu yake umekuwa ukiyajibu lightly. Utakubaliana nami kuwa Watanzania wa leo kiasi fulani wapo tofauti na wakipindi cha chuma. Kwa hiyo kama kiongozi usiwakatishe tamaa maana wewe ni role model wao.

Pili ushauri wa bure, ni kwamba kamwe watu waliopo madarakani hata siku moja hawatoki/hawaachi madaraka kwa hiari yao ila tu kama kuna katiba imara inayowaamuru watoke na wananchi (including waliopo kwenye security organs)watakapokuwa wanauelewa mzuri wa civics. Hivyo basi kwa mazingira yetu bila collective power kamwe hatutaweza kuwaondoa kina future CCM ya kina Ridhiwani and Co. Sidhani kama utapenda kuona watoto wako wanaongozwa na kiongozi kama tuliyenaye leo(aliyeonyesha mapungufu lukuki) ambaye wewe binafsi unamfagilia.
Kweli mkuu,na watu wanatumia hoja nyepesi kuwa siasa sio chuki ila kwa aina ya siasa zetu ukaribu wa aina hii na tena ambao hakuwepo zamani ni kupunguza makali ya hoja za msingi ni bora akane kuzungumza nao kuliko kusema tumezungumza nini! Hìi ni sawa na kukuta unaongea na mtoto wangu under 16 kwenye mazingira hatarishi alafu uniambie leta ushahidi nini tulikuwa tunaongea! Nitakufirigisa mbaya!
 
na hii umeandika wewe? au kuna watu wanakusemea?

au waberoya kaamua kukuchafua?

Bahati mbaya sana baadhi ya viongozi wenzangu wa chama wanachukua chuki, fitna na uwongo unaoandikwa humu kama ukweli.
 
Mh Zitto, binafsi nashukuru umejitokeza kukanusha hili suala. Nina maswali machache tu ambayo ukiyatolea majibu itatusaidia wengi kujua kuwa bado u pamoja nasi.
1. Kufuatia taarifa ya Mwanahalisi kuhusiana na zile simu ni UKWELI ulikuwa unawasiliana na mmoja wa viongozi waandamizi wa TISS. Ila ulitoa challenge walete content of communication kuprove kwamba uliuhujumu chama. Kwa sisi tuliobahatika kupata mafunzo ya kijeshi, mnapokuwa vitani halafu kamanda mwenzenu (anaongea na adui TISS mwenye Game Changing capabilities) kwa njia zake binafsi bila timu ya makamanda wenzio kujua, unajua hilo jambo likifahamika, utapelekwa kwenye court marshall na hukumu yake ni kifo kwa risasi. Hilo ni bila kujali ulikuwa unaongea naye nini. Sababu ni kuwa imani ikiondoka kushinda ni kazi au almost impossible. Wewe binafsi huoni kama lile lilikuwa ni kosa kubwa au bado unataka mpaka walete na maongezi?
2. Mawasiliano yako na mkuu wa nchi kwa njia binafsi huoni kuwazinazoofisha au kupunguza negotiating power kama chama?

Nijambo zuri kuona unajivunia kuwa umejenga Chadema kwa nusu ya umri wako. Sote tuliopitia System yetu ya Elimu tunafahamu kuwa Usalama wa Taifa umekuwa unarecruit vijana tokea wakiwa shule za Sekondari. Sasa unaweza kuwa umekulia Chadema ila matendo yako wakati mwingine yanasabisha maswali mengi ambayo majibu yake umekuwa ukiyajibu lightly. Utakubaliana nami kuwa Watanzania wa leo kiasi fulani wapo tofauti na wakipindi cha chuma. Kwa hiyo kama kiongozi usiwakatishe tamaa maana wewe ni role model wao.

Pili ushauri wa bure, ni kwamba kamwe watu waliopo madarakani hata siku moja hawatoki/hawaachi madaraka kwa hiari yao ila tu kama kuna katiba imara inayowaamuru watoke na wananchi (including waliopo kwenye security organs)watakapokuwa wanauelewa mzuri wa civics. Hivyo basi kwa mazingira yetu bila collective power kamwe hatutaweza kuwaondoa kina future CCM ya kina Ridhiwani and Co. Sidhani kama utapenda kuona watoto wako wanaongozwa na kiongozi kama tuliyenaye leo(aliyeonyesha mapungufu lukuki) ambaye wewe binafsi unamfagilia.

Very wise of you mkuu,salute
 
Kiukweli habari hizi hasi kumuhusu Zitto huwa zinatuumiza sana roho vijana wengi. Zitto tulikuamini na kukupenda sana, ila hauoneshi kwa vitendo kama mengi yanayosemwa humu si ya kweli.
 
Back
Top Bottom