Zitto, Lipumba na mkakati wa kuidhoofisha CHADEMA

Zitto anatumia style ya DON'T RUN FIGHT THEM! Hivyo naamini atajibu hoza za wakuu humu maana wanaokuchukia wanatafuta ulipo udhaifu wako hivyo huwezi kujua udhaifu wako kutoka kwa wanaokupenda
 
amua kuwa na sisi au kuwa na wao.

uhakika ni kuwa hatutegemei fikra zako wala za slaa, wala za mbowe, wala za Mzee Mtei, wala za Prof. Baregu kujua kuwa nchi hii ni ya kifisadi.

na wewe unarubunika kwa peremende. unashangaza.

mwanasiasa mahiri, lakini utapotezwa kama mrema,cheyo,mbatia na lipumba ambao anaonekana vituko kwa jamii.

LISEMWALO LIPO KAMA HALIPO LAJA.
Mtu unaonekana kila wakati kwa JK, mazungumzo yako ni kwa walinzi wa utawala wa JK (TISS). Huu ni unafiki mtupu. Huwezi kuwa POPO na ukabakia CDM. Una uhusiano gani na RA wewe!??Achia Ngazi tafadhali.
 
Niliwahi kueleza kwenye post nyingine jinsi CCM na intelijensia yao wanavyofanya mkakati wa kuidhoofisha CHADEMA. Mkatati huu unahusu kutoa rushwa kwa watu wenye ushawishi katika jamii kuishambulia CHADEMA kila mara kwa kudai kuwa chama hiki kinataka kumwaga damu, kuvuruga amani na umoja wa taifa.

Kwenye taarifa ya TBC1 leo asubuhi, wameweka habari ndefu ya Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, akitoa shutuma kali kwa CHADEMA. Habari hiyo ya Lipumba imepewa muda mrefu sana na kupambwa. Eti wameoneshwa baadhi ya wananchi (ingawa ni wachache) wa Tandahimba "wakishindwa kuzuia hisia zao na kusukuma gari la Lipumba." Katika hali isiyo kawaida kwa TBC1 kuripoti mikutano ya wapinzani, eti baadhi ya wananchi wakahojiwa na kusema wanampenda sana Lipumba na wamekuwa wanamsubiri kwa hamu. Likaoneshwa kundi dogo la wanafunzi wa primary kama 20 wanashangilia msafara wa CUF na mwandishi akasema eti kwenye kila njia Lipumba alilazimika kusimama kuongea na wananchi waliokuwa na hamasa kubwa ya kumuona.

Umati ulikuwa wa watu kama mia 2 tu, si maelfu ya wananchi ambao huendaga kwenye mikutano ya CHADEMA kumuona Dk. WILLIBROD SLAA. Lakini TBC1 wakataka kuonesha eti Lipumba na CUF ni maarufu sana.

Anyway, kikubwa ni hotuba ya Lipumba ambayo aliishambulia vikali CHADEMA. Bila kuitaja CHADEMA, alisema eti "Kuna baadhi ya chama cha kisiasa cha kaskazini ya Tanzania kinadhani kitatawala nchi nzima." Akaongeza kuwa eti wananchi wakatae vyama vya siasa vinavyotaka kuvuruga umoja na amani ya nchi.

Ni dhahiri kuwa Lipumba kwa kutumwa na CCM na intelijensia yao, anaendelea kuishambulia CHADEMA kwa propaganda za kutungwa kuwa eti ni chama cha Wachagga tu na kinataka kumwaga damu na kuleta udini.

Ukiacha CUF na Lipumba, CCM na intelijensia yao pia mara nyingi wamekuwa wanawatumia viongozi wengine wa vyama vya upinzani kuishambulia CHADEMA. Hawa ni pamoja na John Cheyo wa UDP, James Mbatia wa NCCR Mageuzi, Augustino Mrema wa TLP na viongozi wengine.

Pia hivi karibuni wamemtumia Mufti Simba wa BAKWATA kuishambulia CHADEMA lakini sisi Waislamu wengi tumempuuza Mufti huyu aliyekosa msimamo kwa kutumiwa na CCM.

CCM wanacheza mchezo hatari sana wa kutumia dini kujaribu kupambana na CHADEMA kisiasa. Hii sumu ya udini itakuja kuwatafuna watawala wenyewe siku moja.

Pia, baadhi ya vyombo vya habari vinaendelea kutumiwa kuishambulia CHADEMA, mfano TBC1, Mtanzania/RAI (Magazeti ya Rostam Aziz), Jambo Leo (Gazeti la Ridhwani Kikwete, Malegesi wa EPA), Channel Ten (TV ya Tanil Somaiya wa kashfa ya rada) na wengineo.

Hata hivyo, mkakati mkubwa kuliko wote uliobaki wa kuidhoofisha CHADEMA ni kuhakikisha kuwa mabadiliko ya katiba wanayosema yatafanywa 2014, yatahakikisha kuwa umri wa kugombea Urais unashushwa kutoka miaka 40 mpaka 35 au 37.

Lengo ni kumruhusu Zitto Kabwe wa CHADEMA agombee Urais mwaka 2015. CCM na intelijensia yao wanajua fika kuwa Zitto ana ambitions kubwa sana za kutaka kuwa Rais wa Tanzania. Zitto pia anajua kuwa bora agombee 2015 kuliko kusubiri 2020 kwani ni mbali na hawezi kuwa na uhakika kama atakuwa bado ana ushawishi kwani umaarufu wake umekuwa unaporomoka kwa kasi.

Zitto, CCM na intelijensia yao wanajua fika kuwa CHADEMA kamwe haiwezi kumteuwa Zitto kuwa mgombea wake wa Urais mwaka 2015 hata kama katiba ikibadilishwa kuruhusu yeye kugombea.

Hivyo basi, Zitto tayari ana makubaliano ya kimsingi na NCCR Mageuzi kuwa mgombea wa Urais wa chama hicho kwenye uchaguzi wa 2015. Jitihada zinafanywa ili Zitto aweze kuondoka na baadhi ya wabunge wa CHADEMA na viongozi wengine wakubwa wahamie NCCR mwaka 2015 ili kujaribu kuidhoofisha nguvu CHADEMA.

Mkakati ni to "neutralise" CHADEMA na kuidhoofisha ionekane kuwa chama hiki kinameguka na viongozi wake wanahamia NCCR Mageuzi.

Zitto amekuwa na mazungumzo ya siri ya mara kwa mara na CCM na intelijensia yao. Tayari imeripotiwa kuwa Zitto amekuwa akiwasiliana kwa karibu na Jakaya Kikwete, Rostam Aziz na baadhi ya viongozi wa intelijensia (usalama wa taifa) kutoka Tanzania Intelligence and Security Services (TISS) ambao eti wanadhani kuwa jukumu lao kubwa ni kuhakikisha kuwa CCM inaendelea kutawala milele.

CCM na intelijensia yao wamepanga kufanya wizi mkubwa wa kura kwenye uchaguzi wa 2015 kama walivyofanya 2010. Ila safari hii watachakachua zaidi kura za wagombea wote wa Urais wa vyama vya upinzani ili matokeo ya kupikwa ya uchaguzi wa 2015 yawe kama ifuatavyo:

1. CCM of course kushinda Urais na kuongoza kwa idadi ya wabunge
2. Zitto kuwa mshindi wa pili na NCCR iwe chama kikuu kipya cha upinzani
3. CUF iwe chama cha tatu kwa kura
4. CHADEMA itupiliwe mbali na kudaiwa eti ni chama cha 4 kwa umaarufu

Lengo ni kuhakikisha kuwa CCM na intelijensia yao wanaimaliza kabisa CHADEMA na wanakuwa wanamcontrol "kiongozi" mpya wa upinzani, Zitto Kabwe, na chama chake, NCCR Mageuzi.

Asalaam Aleykum.
Mkuu Fareed usemayo ni kweli kabisa, hizo ni hila SISIEM na vibaraka wao. Wanataka kuwatumia hao kina Lipumba na Kabwe kisha wawateme kama walivyo mtumia Mtikila.

Sasa hivi Mtikila hawezi kurudisha umaarufu kusukumwa na wana chuo kikuu kwenye gari lake. Hizo siasa za maji taka watu wameisha zistukia, hata ndani ya CHAMA tawala tayari kuna malumbano, tusitegemee kuwa upinzani uko nje pekee, hata ndani kuna moto unawaka.

KAZI YOTE HII INAFANYWA NA MAFISADI WEZI WA FEDHA NA RASILIMALI ZETU.

Wameweka vyombo vyao kuwapotosha wananchi kama Radio, TV, Magazeti lakini mwisho wasiku watu watatofautisha kati ya pumba na mchele. Adui wa ndani ni mbaya saana kama huyo Zito maana muelekeo wake haueleweki, anahitaji tiba ya haraka saana kabla hajaharibu chama chetu.

KAZI YA KUDAI KATIBA MPYA IANZE MAPEMA ILI TUWEZE KUPATA UKOMBOZI, MAANA BILA KUDAI HATUWEZI KUPEWA!!!!!!!!!!!
 
Huu ni utabiri kama wa tabiri nyingine tu na wasomaji wachukulie kama utabiri. Sina mazungumzo yeyote na chama chochote kuhusu kugombea Urais. Ni kweli nina ambition. Ambition zangu zimo ndani ya CHADEMA, chama ambacho nimeshiriki kukijenga.
Kumekuwa na juhudi za makusudi za watu kutaka nitoke CHADEMA, narudia tena siwezi kutoka. Narudia, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine choochote maishani mwangu tofauti na CHADEMA. Narudia, zaidi ya nusu ya umri wangu nimeutumia CHADEMA. Nimetumia nguvu zangu, akili zangu na rasilimaliu zangu kusaidiana na wenzangu kujenga CHADEMA.
Kwamba nazungumza na NCCR ni uwongo, ni uzushi na propaganda yenye nia mbaya kwangu.
Sizungumzi na mtu yeyote kuhusu kuhujumu chama changu. Nimeshasema yeyote mwenye ushahidi na jambo hili autoe. Gazeti la Mwanahalisi lilitoa muda na namba za simu za watu ninaozungumza nao. Nimewachallenge waseme nilikuwa nazungumza nini. Watoe content ya mazungumzo na kama itaonekana kwa namna yeyote ile nilihujumu chama changu nitawajibika.
Watanzania wamekuwa na tabia ya kuamini mambo kwa mkumbo.
Uzushi dhidi yangu umekuwa ukichukuliwa na watu kama ukweli tena ukweli mtupu. Watu kwa malengo yao wamekuwa wakitumia majina zaidi ya moja kwa mtu mmoja na kuingia JF kuandika uzushi (kama huu wa leo) ili kunichafua na kunigombanisha na wenzangu. Bahati mbaya sana baadhi ya viongozi wenzangu wa chama wanachukua chuki, fitna na uwongo unaoandikwa humu kama ukweli. Inasikitisha sana.
Ninapenda kuwafahamisha wasomaji wote wa JF kuwa sehemu ya habari iliyoandikwa hapa katika thread hii ni uwongo wa makusudi dhidi yangu. Ni imagination ya mtu ambaye anaumwa ugonjwa wa ZITTOPHOBIASIS! Ugonjwa ambao watu wengi wanaumwa na ninasikitika kuwa dawa ya ugonjwa huu hata kwa babu haupo maana ni ugonjwa unasambazwa na ugonjwa wa chuki, fitna, na WIVU!
Mheshimiwa pamoja na maelezo mazuri uliyotoa, binafsi bado nina shaka mbona unataka kuturudisha kwenye DOWANS na RICHIMOND wewe umetumwa na nani??????? Unamwelekeo kama vile una huruma na nchi hii lakini unajiingiza kwenye mkumbo wa mafisadi kina RA, hata ukisema ni rafiki zako lakini ngom'be mwizi akichungwa na mwenzake si wote wataiba tuu!!!!!!!! Tuna uchungu na mafisadi wewe ndio unafanya marafiki!!!!!!!Unataka tukuelewe je?????????
 
Mpaka kufikia 2015 watanzania waliofeli kidato cha nne( shule za kata) watakua mamilioni na watu ambao hawana kazi watakua mamilioni
Hawa ndo wataihukumu CCM. Watu walio katatamaa, wenye njaa ndo watakao linda kura za Chadema. Kuna hoja ambazo ukitoa mbele za watu wanakushangaa, watunga sera wa CCM hawaangaliii mbali. Hoja ya udini ni ya CCM na kila mtu mwenye masikio analijua hili( Rais, makamu wake, jaji mkuu, mkuu wa polisi nk). Hoja ya kuvuruga amani ni ya kuwatisha wazee, na c kwa vijana wanaotaka mabadiliko.

"Uwezi kuzuia mabadiliko labda utayachelewesha" Kama yaliyotokea Misri, Tunisia....
Jamani kwani Zitto ni nani kwa watanzania, mpaka watu msumbue bongo zenu kumjadili,
amewafanyia nini watanzania mpaka tumuamini, kwanza hana msimamo, ni viongozi uchwara wanatumia na nafasi ya ubunge kujikwamua kwenye umasikini ndo maana anawafuata akina Rostama. Zitto zadi ya ubunge na labda nafsi za kuteuliwa zaidi ya hapo nothing,hakuna anaemuamini mpaka tufikirie kumpa urais.
Kama kugombea hata Dovutua aligombea 2010.
Swala la ukabila, mimi natokea mara????
CCM hawana ujasiri wa kujibu hoja za Chadema so wanatafuta namna ya kuvuruga, ili watu wasahamu msingi ya mijadala
Wazee kwa vijana tukaze butu kuibua hoja nyinge zaidi
Tujipange, ningepenga kuona kila penye bendera za CCM basi na ya Chadema iweinapepea.
Kama kuna watu wana Tshirt,kofia, chupi basi na za CDM zipatikane(hata kwa kuuza, zitanunuliwa na chama kitapata mapato)
Nchi hii itakombolewa na vijana.
 
Niliwahi kueleza kwenye post nyingine jinsi CCM na intelijensia yao wanavyofanya mkakati wa kuidhoofisha CHADEMA. Mkatati huu unahusu kutoa rushwa kwa watu wenye ushawishi katika jamii kuishambulia CHADEMA kila mara kwa kudai kuwa chama hiki kinataka kumwaga damu, kuvuruga amani na umoja wa taifa.

Kwenye taarifa ya TBC1 leo asubuhi, wameweka habari ndefu ya Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, akitoa shutuma kali kwa CHADEMA. Habari hiyo ya Lipumba imepewa muda mrefu sana na kupambwa. Eti wameoneshwa baadhi ya wananchi (ingawa ni wachache) wa Tandahimba "wakishindwa kuzuia hisia zao na kusukuma gari la Lipumba." Katika hali isiyo kawaida kwa TBC1 kuripoti mikutano ya wapinzani, eti baadhi ya wananchi wakahojiwa na kusema wanampenda sana Lipumba na wamekuwa wanamsubiri kwa hamu. Likaoneshwa kundi dogo la wanafunzi wa primary kama 20 wanashangilia msafara wa CUF na mwandishi akasema eti kwenye kila njia Lipumba alilazimika kusimama kuongea na wananchi waliokuwa na hamasa kubwa ya kumuona.

Umati ulikuwa wa watu kama mia 2 tu, si maelfu ya wananchi ambao huendaga kwenye mikutano ya CHADEMA kumuona Dk. WILLIBROD SLAA. Lakini TBC1 wakataka kuonesha eti Lipumba na CUF ni maarufu sana.

Anyway, kikubwa ni hotuba ya Lipumba ambayo aliishambulia vikali CHADEMA. Bila kuitaja CHADEMA, alisema eti "Kuna baadhi ya chama cha kisiasa cha kaskazini ya Tanzania kinadhani kitatawala nchi nzima." Akaongeza kuwa eti wananchi wakatae vyama vya siasa vinavyotaka kuvuruga umoja na amani ya nchi.

Ni dhahiri kuwa Lipumba kwa kutumwa na CCM na intelijensia yao, anaendelea kuishambulia CHADEMA kwa propaganda za kutungwa kuwa eti ni chama cha Wachagga tu na kinataka kumwaga damu na kuleta udini.

Ukiacha CUF na Lipumba, CCM na intelijensia yao pia mara nyingi wamekuwa wanawatumia viongozi wengine wa vyama vya upinzani kuishambulia CHADEMA. Hawa ni pamoja na John Cheyo wa UDP, James Mbatia wa NCCR Mageuzi, Augustino Mrema wa TLP na viongozi wengine.

Pia hivi karibuni wamemtumia Mufti Simba wa BAKWATA kuishambulia CHADEMA lakini sisi Waislamu wengi tumempuuza Mufti huyu aliyekosa msimamo kwa kutumiwa na CCM.

CCM wanacheza mchezo hatari sana wa kutumia dini kujaribu kupambana na CHADEMA kisiasa. Hii sumu ya udini itakuja kuwatafuna watawala wenyewe siku moja.

Pia, baadhi ya vyombo vya habari vinaendelea kutumiwa kuishambulia CHADEMA, mfano TBC1, Mtanzania/RAI (Magazeti ya Rostam Aziz), Jambo Leo (Gazeti la Ridhwani Kikwete, Malegesi wa EPA), Channel Ten (TV ya Tanil Somaiya wa kashfa ya rada) na wengineo.

Hata hivyo, mkakati mkubwa kuliko wote uliobaki wa kuidhoofisha CHADEMA ni kuhakikisha kuwa mabadiliko ya katiba wanayosema yatafanywa 2014, yatahakikisha kuwa umri wa kugombea Urais unashushwa kutoka miaka 40 mpaka 35 au 37.

Lengo ni kumruhusu Zitto Kabwe wa CHADEMA agombee Urais mwaka 2015. CCM na intelijensia yao wanajua fika kuwa Zitto ana ambitions kubwa sana za kutaka kuwa Rais wa Tanzania. Zitto pia anajua kuwa bora agombee 2015 kuliko kusubiri 2020 kwani ni mbali na hawezi kuwa na uhakika kama atakuwa bado ana ushawishi kwani umaarufu wake umekuwa unaporomoka kwa kasi.

Zitto, CCM na intelijensia yao wanajua fika kuwa CHADEMA kamwe haiwezi kumteuwa Zitto kuwa mgombea wake wa Urais mwaka 2015 hata kama katiba ikibadilishwa kuruhusu yeye kugombea.

Hivyo basi, Zitto tayari ana makubaliano ya kimsingi na NCCR Mageuzi kuwa mgombea wa Urais wa chama hicho kwenye uchaguzi wa 2015. Jitihada zinafanywa ili Zitto aweze kuondoka na baadhi ya wabunge wa CHADEMA na viongozi wengine wakubwa wahamie NCCR mwaka 2015 ili kujaribu kuidhoofisha nguvu CHADEMA.

Mkakati ni to "neutralise" CHADEMA na kuidhoofisha ionekane kuwa chama hiki kinameguka na viongozi wake wanahamia NCCR Mageuzi.

Zitto amekuwa na mazungumzo ya siri ya mara kwa mara na CCM na intelijensia yao. Tayari imeripotiwa kuwa Zitto amekuwa akiwasiliana kwa karibu na Jakaya Kikwete, Rostam Aziz na baadhi ya viongozi wa intelijensia (usalama wa taifa) kutoka Tanzania Intelligence and Security Services (TISS) ambao eti wanadhani kuwa jukumu lao kubwa ni kuhakikisha kuwa CCM inaendelea kutawala milele.

CCM na intelijensia yao wamepanga kufanya wizi mkubwa wa kura kwenye uchaguzi wa 2015 kama walivyofanya 2010. Ila safari hii watachakachua zaidi kura za wagombea wote wa Urais wa vyama vya upinzani ili matokeo ya kupikwa ya uchaguzi wa 2015 yawe kama ifuatavyo:

1. CCM of course kushinda Urais na kuongoza kwa idadi ya wabunge
2. Zitto kuwa mshindi wa pili na NCCR iwe chama kikuu kipya cha upinzani
3. CUF iwe chama cha tatu kwa kura
4. CHADEMA itupiliwe mbali na kudaiwa eti ni chama cha 4 kwa umaarufu

Lengo ni kuhakikisha kuwa CCM na intelijensia yao wanaimaliza kabisa CHADEMA na wanakuwa wanamcontrol "kiongozi" mpya wa upinzani, Zitto Kabwe, na chama chake, NCCR Mageuzi.

Asalaam Aleykum.

shauri zao watahangaika sana ila CDM itasimama daima
 
Nakubaliana nawe kwa sehemu, ila jamii ya wana mageuzi watakubaliana nami kwamba bado una mambo ya kujibu na kufafanua ili kutoa madukuduku yetu, mfano ni hapo unapolitaja gazeti la Mwanahalisi, kimsingi japo hujaainisha unakubaliana na kilichoandikwa tatizo ni content ya mazungumzo! sasa mh. Zitto kama umezungumza na adui yetu (maana tunaamini kwamba usala wa taifa unasaidia ccm) ni wewe ndiwe mwenye jukumu la kutujuza content ilikuwa nini ili kutoa dukuduku zetu na ikiwezekana turejeshea imani yetu.

Gazeti la Mwanahalisi lilitoa muda na namba za simu za watu ninaozungumza nao. Nimewachallenge waseme nilikuwa nazungumza nini. Watoe content ya mazungumzo na kama itaonekana kwa namna yeyote ile nilihujumu chama changu nitawajibika.
 
Teheh tehehe!! hueleweki.... wewe ni mpenzi/mshabiki/mshirika wa Mh Zitto ambaye ni mbunge/mwanachama/kiongozi na tena amechangia ktk kukiinua CHADEMA at the same time ni mchukia/adui/mpinzani wa CHADEMA!!!!!!!!!!!! Au ndo mnaompeleka kiongozi wetu Zitto kusiko???? umekuwa kinyonga wewe??????????:ballchain:

Umenisoma vibaya.

Kaka mie ni nyiutro observer tu nipo hapa kuona sanaa inavoendelea , ultimately siezi kuamini ktk siasa wala mwanasiasa maana sijawahi skia mwanasiasa kuvumbua walau nailcutter au kutatua tatizo lolote.
 
Ndugu zito ninakuomba sana uzidi kuwa makini katika mapambano yako kwani wapo watakaojidai wanakupinga kumbe wapo upande wako na wapo watakaojidai wanakuunga mkono kumbe malengo yao uharibikiwe. Pole ninajua unapitia kipindi kigumu ambacho kitaamua hatima yako ya kisiasa sisi wakristo tuansema majaribu ni mtaji. Ukiutumia vizuri unafanikiwa na ukiutumia vibaya unaanguka
 
"Hoja za kisiasa hujibiwa kisiasa" kama uhuni basi hakuna uhuni kama siasa............

Mzee wa Tanga ohh sorry Lushoto, umeivisha mapeasi??

Back to the topic, The man in question yupo kundi gani kati ya haya mawili; "Our country has too many politicians and too few statesmen. While the statesmen are concerned with the next generation, the politicians are terribly concerned with the next elections".
 
Huu ni ukweli kabisa na hali hii inafahamika mipango hii ipo lakini ni wakati wa watanzania kuwa macho na kupambana hadi tone la mwisho kwa hali ilivyosasa CCM wamefanya madhambi makubwa sana kiasi wanaogopa kutoka madarakani kwa kuwa mambo yatafumuka. Msishangae mkaona wale waandishi wenye ushawishi kwenye jamii wakaanza kuishambulia CHADEMA. Hawa majambazi wapo tayari kutumia mbinu zote kupambana wasitoke madarakani lakini mwisho wao umekeribia hakuna uovu usio na mwisho. Chamsingi nilishaeleza tangu mwanzo CHADEMA wawe makini na Zitto Kabwe huyu yupo ndani adui wa ndani na hatari zaidi kuliko adui wa nje waendelee kumpuzaa ili ajimalize mwenyewe wasishughulike naye wala kushirikisha katika mikakati ya kuindoa CCM madarakani hafai kabisa huyu.

Hakuna ukweli wowote hapa, acheni majungu. Hapa CHADEMA inajihami tu
 
wanatwanga maji kwenye kinu huyo zitto alishashtukiwa na kufika mwaka 2015 atakuwa kesha ondolewa kwenye chama. Afterall zitto hana impact yoyote kwa sasa keshafulia kisiasa.
 
Ndugu yangu waTZ hawadanganyiki kirahisi tena, Zito hawezi kuwa nafasi ya pili, walijitahidi sana mwaka huu kwa lipumba wakashindwa unafikiri kwa Zito itawezekana?

Nani ataratibu huo mpango? maana CCM wenyewe sasa kumechimbika kila mtu anatafuta pa kutokea.

2015 itakuwa kama ubungo ya 2010, Dr Slaa akiulizwa kwenye kampeni amejifunza nini kwenye uchaguzi wa 2010? Atajibu kulinda KURA.

peoples power.
 
kushiriki kukijenga isiwe kigezo cha kuwa jeuri na mkaidi.

Mnataka Zitto awalambe miguu ndio mfurahi? Tukisema kuna uchaga chadema mnakataaa! Mwacheni Zitto he has a lot to do! Yani watanzania hatuachi roho mbaya na wivu hata kama uwe Critical Thinker bado umbea upo pale pale! Mwacheni Zitto!
 
Huu ni utabiri kama wa tabiri nyingine tu na wasomaji wachukulie kama utabiri. Sina mazungumzo yeyote na chama chochote kuhusu kugombea Urais. Ni kweli nina ambition. Ambition zangu zimo ndani ya CHADEMA, chama ambacho nimeshiriki kukijenga.
Kumekuwa na juhudi za makusudi za watu kutaka nitoke CHADEMA, narudia tena siwezi kutoka. Narudia, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine choochote maishani mwangu tofauti na CHADEMA. Narudia, zaidi ya nusu ya umri wangu nimeutumia CHADEMA. Nimetumia nguvu zangu, akili zangu na rasilimaliu zangu kusaidiana na wenzangu kujenga CHADEMA.
Kwamba nazungumza na NCCR ni uwongo, ni uzushi na propaganda yenye nia mbaya kwangu.
Sizungumzi na mtu yeyote kuhusu kuhujumu chama changu. Nimeshasema yeyote mwenye ushahidi na jambo hili autoe. Gazeti la Mwanahalisi lilitoa muda na namba za simu za watu ninaozungumza nao. Nimewachallenge waseme nilikuwa nazungumza nini. Watoe content ya mazungumzo na kama itaonekana kwa namna yeyote ile nilihujumu chama changu nitawajibika.
Watanzania wamekuwa na tabia ya kuamini mambo kwa mkumbo.
Uzushi dhidi yangu umekuwa ukichukuliwa na watu kama ukweli tena ukweli mtupu. Watu kwa malengo yao wamekuwa wakitumia majina zaidi ya moja kwa mtu mmoja na kuingia JF kuandika uzushi (kama huu wa leo) ili kunichafua na kunigombanisha na wenzangu. Bahati mbaya sana baadhi ya viongozi wenzangu wa chama wanachukua chuki, fitna na uwongo unaoandikwa humu kama ukweli. Inasikitisha sana.
Ninapenda kuwafahamisha wasomaji wote wa JF kuwa sehemu ya habari iliyoandikwa hapa katika thread hii ni uwongo wa makusudi dhidi yangu. Ni imagination ya mtu ambaye anaumwa ugonjwa wa ZITTOPHOBIASIS! Ugonjwa ambao watu wengi wanaumwa na ninasikitika kuwa dawa ya ugonjwa huu hata kwa babu haupo maana ni ugonjwa unasambazwa na ugonjwa wa chuki, fitna, na WIVU!

Umejitetea vizuri. Ila kuna mambo fulani ambayo watu wanatilia mashaka ambayo wewe kama kiongozi mmojawapo wa kitaifa unatakiwa uonyeshe ukomavu na kujiamini badala ya kutafuta visingizio vya kukwepa kwepa majukumu ya pamoja.

Umejitahidi kujirekebisha tabia ya kukimbilia vyombo vya habari, lakini hujajisahihisha kushiriki kikutano na maandamano ambayo viongozi na wabunge wenzako wanashiriki. Siwezi kuamini kwamba mara zote unakuwa na dharura kuliko viongozi na wabunge wengi wa Chadema. Jitahidi kujenga msingi wa kujiamini ndani ya Chama chako badala ya kuwa popo ili uonekane mzuri kote kote mwisho utachokwa kote kote.
 
Back
Top Bottom