Zitto, Lipumba na mkakati wa kuidhoofisha CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto, Lipumba na mkakati wa kuidhoofisha CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fareed, Mar 29, 2011.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Niliwahi kueleza kwenye post nyingine jinsi CCM na intelijensia yao wanavyofanya mkakati wa kuidhoofisha CHADEMA. Mkatati huu unahusu kutoa rushwa kwa watu wenye ushawishi katika jamii kuishambulia CHADEMA kila mara kwa kudai kuwa chama hiki kinataka kumwaga damu, kuvuruga amani na umoja wa taifa.

  Kwenye taarifa ya TBC1 leo asubuhi, wameweka habari ndefu ya Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, akitoa shutuma kali kwa CHADEMA. Habari hiyo ya Lipumba imepewa muda mrefu sana na kupambwa. Eti wameoneshwa baadhi ya wananchi (ingawa ni wachache) wa Tandahimba "wakishindwa kuzuia hisia zao na kusukuma gari la Lipumba." Katika hali isiyo kawaida kwa TBC1 kuripoti mikutano ya wapinzani, eti baadhi ya wananchi wakahojiwa na kusema wanampenda sana Lipumba na wamekuwa wanamsubiri kwa hamu. Likaoneshwa kundi dogo la wanafunzi wa primary kama 20 wanashangilia msafara wa CUF na mwandishi akasema eti kwenye kila njia Lipumba alilazimika kusimama kuongea na wananchi waliokuwa na hamasa kubwa ya kumuona.

  Umati ulikuwa wa watu kama mia 2 tu, si maelfu ya wananchi ambao huendaga kwenye mikutano ya CHADEMA kumuona Dk. WILLIBROD SLAA. Lakini TBC1 wakataka kuonesha eti Lipumba na CUF ni maarufu sana.

  Anyway, kikubwa ni hotuba ya Lipumba ambayo aliishambulia vikali CHADEMA. Bila kuitaja CHADEMA, alisema eti "Kuna baadhi ya chama cha kisiasa cha kaskazini ya Tanzania kinadhani kitatawala nchi nzima." Akaongeza kuwa eti wananchi wakatae vyama vya siasa vinavyotaka kuvuruga umoja na amani ya nchi.

  Ni dhahiri kuwa Lipumba kwa kutumwa na CCM na intelijensia yao, anaendelea kuishambulia CHADEMA kwa propaganda za kutungwa kuwa eti ni chama cha Wachagga tu na kinataka kumwaga damu na kuleta udini.

  Ukiacha CUF na Lipumba, CCM na intelijensia yao pia mara nyingi wamekuwa wanawatumia viongozi wengine wa vyama vya upinzani kuishambulia CHADEMA. Hawa ni pamoja na John Cheyo wa UDP, James Mbatia wa NCCR Mageuzi, Augustino Mrema wa TLP na viongozi wengine.

  Pia hivi karibuni wamemtumia Mufti Simba wa BAKWATA kuishambulia CHADEMA lakini sisi Waislamu wengi tumempuuza Mufti huyu aliyekosa msimamo kwa kutumiwa na CCM.

  CCM wanacheza mchezo hatari sana wa kutumia dini kujaribu kupambana na CHADEMA kisiasa. Hii sumu ya udini itakuja kuwatafuna watawala wenyewe siku moja.

  Pia, baadhi ya vyombo vya habari vinaendelea kutumiwa kuishambulia CHADEMA, mfano TBC1, Mtanzania/RAI (Magazeti ya Rostam Aziz), Jambo Leo (Gazeti la Ridhwani Kikwete, Malegesi wa EPA), Channel Ten (TV ya Tanil Somaiya wa kashfa ya rada) na wengineo.

  Hata hivyo, mkakati mkubwa kuliko wote uliobaki wa kuidhoofisha CHADEMA ni kuhakikisha kuwa mabadiliko ya katiba wanayosema yatafanywa 2014, yatahakikisha kuwa umri wa kugombea Urais unashushwa kutoka miaka 40 mpaka 35 au 37.

  Lengo ni kumruhusu Zitto Kabwe wa CHADEMA agombee Urais mwaka 2015. CCM na intelijensia yao wanajua fika kuwa Zitto ana ambitions kubwa sana za kutaka kuwa Rais wa Tanzania. Zitto pia anajua kuwa bora agombee 2015 kuliko kusubiri 2020 kwani ni mbali na hawezi kuwa na uhakika kama atakuwa bado ana ushawishi kwani umaarufu wake umekuwa unaporomoka kwa kasi.

  Zitto, CCM na intelijensia yao wanajua fika kuwa CHADEMA kamwe haiwezi kumteuwa Zitto kuwa mgombea wake wa Urais mwaka 2015 hata kama katiba ikibadilishwa kuruhusu yeye kugombea.

  Hivyo basi, Zitto tayari ana makubaliano ya kimsingi na NCCR Mageuzi kuwa mgombea wa Urais wa chama hicho kwenye uchaguzi wa 2015. Jitihada zinafanywa ili Zitto aweze kuondoka na baadhi ya wabunge wa CHADEMA na viongozi wengine wakubwa wahamie NCCR mwaka 2015 ili kujaribu kuidhoofisha nguvu CHADEMA.

  Mkakati ni to "neutralise" CHADEMA na kuidhoofisha ionekane kuwa chama hiki kinameguka na viongozi wake wanahamia NCCR Mageuzi.

  Zitto amekuwa na mazungumzo ya siri ya mara kwa mara na CCM na intelijensia yao. Tayari imeripotiwa kuwa Zitto amekuwa akiwasiliana kwa karibu na Jakaya Kikwete, Rostam Aziz na baadhi ya viongozi wa intelijensia (usalama wa taifa) kutoka Tanzania Intelligence and Security Services (TISS) ambao eti wanadhani kuwa jukumu lao kubwa ni kuhakikisha kuwa CCM inaendelea kutawala milele.

  CCM na intelijensia yao wamepanga kufanya wizi mkubwa wa kura kwenye uchaguzi wa 2015 kama walivyofanya 2010. Ila safari hii watachakachua zaidi kura za wagombea wote wa Urais wa vyama vya upinzani ili matokeo ya kupikwa ya uchaguzi wa 2015 yawe kama ifuatavyo:

  1. CCM of course kushinda Urais na kuongoza kwa idadi ya wabunge
  2. Zitto kuwa mshindi wa pili na NCCR iwe chama kikuu kipya cha upinzani
  3. CUF iwe chama cha tatu kwa kura
  4. CHADEMA itupiliwe mbali na kudaiwa eti ni chama cha 4 kwa umaarufu

  Lengo ni kuhakikisha kuwa CCM na intelijensia yao wanaimaliza kabisa CHADEMA na wanakuwa wanamcontrol "kiongozi" mpya wa upinzani, Zitto Kabwe, na chama chake, NCCR Mageuzi.

  Asalaam Aleykum.
   
 2. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Asante sana, yote yanawezekana.

  Kama kweli Zitto ni mnafiki, basi atakuwa mchawi kama sio. Base qoute - Mrisho Gambo.

  Naipenda ile kauli ya wana-arusha. Bora kufa kwa risasi kuliko taifodi. Base qoute - Mrisho Gambo.

  Alhaj ANS
   
 3. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 80
  Mmmmh makubwa haya jamani.... tusubiri muda utatuambia!!!!
   
 4. J

  Jay-wa-Amani New Member

  #4
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni ngumu kuwadanganya watanzania wa sasa kwa mbinu hizo.....
   
 5. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  1.Kimsingi TBC kumshabikia Lipumba ni kuiua CCM, kuonyesha kuwa CCM imeanza kukataliwa na wananchi na ndio maana wanaishabikia CUF.
  2. Wananchi wa leo si wale wa kudanganywa, wanajua kuchagua kupembua na kuweka mbali liPUMBA na mchele.
  3. Zitto alibebwa kisiasa na CHADEMA, kwenda NCCR siyo kujipaisha bali kujimaliza.

  Zidumu fikra zao zilizopitwa na wakati:boom:
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  aende na Mwanza wakamsukume. Professor kilaza asiye na akili wala mke.
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  wametumia mbinu ya kuhakikisha Zitto Kabwela hashiriki harakati za Chadema, wamefulia.

  Slaa anapendwa kuliko huyo kibaraka wenu Zitto. Anaushawishi Kigoma tu.
   
 8. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wote wanaopanga mambo ya 2015 kwa hila na dhuluma dhidi ya watanzania wajue kuwa kesho si yao kuitaka, ni Mungu kuwajalia.
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi wanadhani watanzania ni wajinga kiasi hicho?
   
 10. J

  Joblube JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huu ni ukweli kabisa na hali hii inafahamika mipango hii ipo lakini ni wakati wa watanzania kuwa macho na kupambana hadi tone la mwisho kwa hali ilivyosasa CCM wamefanya madhambi makubwa sana kiasi wanaogopa kutoka madarakani kwa kuwa mambo yatafumuka. Msishangae mkaona wale waandishi wenye ushawishi kwenye jamii wakaanza kuishambulia CHADEMA. Hawa majambazi wapo tayari kutumia mbinu zote kupambana wasitoke madarakani lakini mwisho wao umekeribia hakuna uovu usio na mwisho. Chamsingi nilishaeleza tangu mwanzo CHADEMA wawe makini na Zitto Kabwe huyu yupo ndani adui wa ndani na hatari zaidi kuliko adui wa nje waendelee kumpuzaa ili ajimalize mwenyewe wasishughulike naye wala kushirikisha katika mikakati ya kuindoa CCM madarakani hafai kabisa huyu.
   
 11. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hayo ni kweli,ila msimamo ni wa watanzania waone hila zote hizi na wachukue hatua,sasa kunawatu wameshajiona wao ndio watawala wa nchi hii,TBC wanachachawa ila wajue hakuna lililo na mwanzo halina mwisho,walimfukuza Tido mzalendo,wakaweka vibaraka wao,ila watambue iposiku kipofu ataona
   
 12. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #12
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Huu ni utabiri kama wa tabiri nyingine tu na wasomaji wachukulie kama utabiri. Sina mazungumzo yeyote na chama chochote kuhusu kugombea Urais. Ni kweli nina ambition. Ambition zangu zimo ndani ya CHADEMA, chama ambacho nimeshiriki kukijenga.
  Kumekuwa na juhudi za makusudi za watu kutaka nitoke CHADEMA, narudia tena siwezi kutoka. Narudia, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine choochote maishani mwangu tofauti na CHADEMA. Narudia, zaidi ya nusu ya umri wangu nimeutumia CHADEMA. Nimetumia nguvu zangu, akili zangu na rasilimaliu zangu kusaidiana na wenzangu kujenga CHADEMA.
  Kwamba nazungumza na NCCR ni uwongo, ni uzushi na propaganda yenye nia mbaya kwangu.
  Sizungumzi na mtu yeyote kuhusu kuhujumu chama changu. Nimeshasema yeyote mwenye ushahidi na jambo hili autoe. Gazeti la Mwanahalisi lilitoa muda na namba za simu za watu ninaozungumza nao. Nimewachallenge waseme nilikuwa nazungumza nini. Watoe content ya mazungumzo na kama itaonekana kwa namna yeyote ile nilihujumu chama changu nitawajibika.
  Watanzania wamekuwa na tabia ya kuamini mambo kwa mkumbo.
  Uzushi dhidi yangu umekuwa ukichukuliwa na watu kama ukweli tena ukweli mtupu. Watu kwa malengo yao wamekuwa wakitumia majina zaidi ya moja kwa mtu mmoja na kuingia JF kuandika uzushi (kama huu wa leo) ili kunichafua na kunigombanisha na wenzangu. Bahati mbaya sana baadhi ya viongozi wenzangu wa chama wanachukua chuki, fitna na uwongo unaoandikwa humu kama ukweli. Inasikitisha sana.
  Ninapenda kuwafahamisha wasomaji wote wa JF kuwa sehemu ya habari iliyoandikwa hapa katika thread hii ni uwongo wa makusudi dhidi yangu. Ni imagination ya mtu ambaye anaumwa ugonjwa wa ZITTOPHOBIASIS! Ugonjwa ambao watu wengi wanaumwa na ninasikitika kuwa dawa ya ugonjwa huu hata kwa babu haupo maana ni ugonjwa unasambazwa na ugonjwa wa chuki, fitna, na WIVU!
   
 13. F

  FUSO JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,878
  Likes Received: 2,343
  Trophy Points: 280
  asante... ingawa mzee kuna hoja nyingi sana inabidi utupe ufafanuzi ukipata muda ili tuwe sawa.
   
 14. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #14
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Tafadhali thibitisha ukweli wa haya maana unasema ni kweli!
   
 15. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  amua kuwa na sisi au kuwa na wao.

  uhakika ni kuwa hatutegemei fikra zako wala za slaa, wala za mbowe, wala za Mzee Mtei, wala za Prof. Baregu kujua kuwa nchi hii ni ya kifisadi.

  na wewe unarubunika kwa peremende. unashangaza.

  mwanasiasa mahiri, lakini utapotezwa kama mrema,cheyo,mbatia na lipumba ambao anaonekana vituko kwa jamii.
   
 16. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #16
  Mar 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Waalimu wetu walikuwa na kazi sana........................
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Wasanii wanalumbana..
   
 18. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #18
  Mar 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Heshima yako mkuu,

  Japo mimi ni mgeni hapa jamvini lakini kuna kitu nimekishuhudia si mara moja wala mara mbili! Watu huwa wanakaa na kuja na hoja zinazokuhusu na wengi wa wachangiaji huwa wanakupinga dhahiri hii haina maana kuwa hukubaliki lahasha! Wananchi wa jimboni kwako wana imani na wewe na wanakuhitaji ndio maana wamekuchagua tena kuwawakilisha.

  My take.

  Hawa wanaokushutumu wanafanya hivyo kwa kusukumwa na chuki zao binafsi zilizojaa choyo! Usife moyo watumikie wananchi waliokuchagua na ambao hawakukupa kura jimboni kwako na watanzania kwa ujumla. Vyama vinapita Tanzania na Watanzania wataendelea kuwepo.

  Shukran.
   
 19. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #19
  Mar 29, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Zitto wanafiki wako ni wachache na watashindwa kwani Mungu anakulinda zaidi, wanafanya hivi ili kujaribu kuupunguza uwezo wako wa kiutendaji lakini wamenoa. Chapa kazi mkuu, na usisite kuwaelimisha kwani hao wanaokuchukia hawana nia ya dhati kwa maendeleo ya taifa.Kata ya mahembe tuko pamoja nawe. wanafiki watashindwa tu.
   
 20. k

  kiche JF-Expert Member

  #20
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Asante kwa upelelezi wako,ila naomba umma uelewe kuwa miaka hii siyo ya 80,kwa mkakati huu sidhani kama watafanikiwa mambo yamebadilika sana kama ni kweli wametumia mikakati iliyopitwa na wakati mno,pia zitto hana nguvu kiasi hicho cha kuigawa cdm na kamwe asijidanganye kama kweli mawazo hayo yapo licha ya kuwa ameshakanusha,zitto umesema umekuwa ukienezewa uongo ambao mpaka baadhi ya viongozi wenzako wamekuwa wakiamini!unachotakiwa ni wewe binafsi kujiondoa katika hizo dhana,mwisho naomba kukuuliza ni kwanini ujihusishi na maandamano ya chadema?huoni kwa kutofanya hivyo ndiyo miongoni mwa sababu ya watu kukuhisi kwamba ni msaliti?,tafakari chukua hatua.
   
Loading...