Zitto, Kwenye hili tayari umeshinda!

Zitto, Kwenye hili tayari umeshinda!

My young brother comrade Mchange! kwanza nimefurahi kukuona online, you have guts, thaz great!

katika maisha yangu usha wahi kufanya nitoe machozi mala mbili, moja, walipokichakachua uchguzi, nilitoa machozi, pili, niliposikia upo kwenye kindi la wasiojitambua,akina Mwampamba, nilitoa machozi! why? niloshakshuhudia wakati huo na niliku rate juu saana, niksshangaa na kutoa machozi.

Naona, ingalau you can write something that will make one understand! ila, bahati nzuri you are a moslem, ungekuwa mkristo ningekuuliza, je unafahamu yaliyo mpata Yuda Iskarioti? Maandiko yanasema baada ya kugundua usaliti wake alijinyonga, so, what next baada ya usaliti is kujinyonga tuu, it stands like that!

And, hayo mambo ni kweli, you are still young, badala ya kuhalalisha mambo maovu uliyotenda, omba msamaha and kama unataka kuhama, uhame huku usha rekebisha kila kitu, take courage and do that my young brother nafasi bado ipo comrade!
 
Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na mtindo wa kurushwa kwa shutuma mbali mbali kutoka kwa viongozi wajuu wa CHADEMA wakitumia majina bandia kumuelekezea ndugu zitto kabwe.

Kwa makusudi kabisa viongozi hao wakiongozwa na mwenyekiti, katibu mkuu na wakurugenzi kadhaa wamekuwa wakirusha kila aina ya shutuma humu mtandaoni lakini kwa hofu kubwa ndio maana wanajificha kwa kutumia akaunti bandia.

Jana na juzi nimepokea sms, emails na simu nyingi sana kuhusu hiki kinachoitwa ripoti ya siri ya SLAA, MBOWE NA WAGAZA WENGINE dhidi ya ZITTO zikisema namie nimetajwa humo kuwa ninashirikiana na Zitto kukihujumu CHADEMA.

Bahati mbaya sana, hakuna ripoti ama shutuma zozote anazopelekewa Zitto kutoka kwa hawa majamaa ambazo hazinitaji, na kwentye hii nayo nimeshuhudia nikitajwa mara nyingi kupokea pesa kutoka kwa Zitto kukihujumu chama.

Bahati mbaya zaidi ni kwamba wafadhili wa mkakati huu ''OPERESHENI ONDOA ZITTO KWENYE HOJA ZENYE MASLAHI YA TAIFA'' wamekosa njia sahihi ya kutumia, wamekuwa wakiwatumia watu wale wale ambao kwa zaidi ya miaka na miaka tumekuwa tukikitetea chama kuwa si cha namna hiyo.

kitendo cha MBOWE na SLAA kuwatumia JOSHUA NASSARY, GODBLESS LEMA, MAMUYA na wengine, kinauthibitishia umma wa watanzania kuwa sio kweli kwamba zitto ni tatizo kwenye CDM, kitendo hiki cha kuwatumia watu wanaolalamikiwa kuwa wanabebana kimisingi ya ASILI ya wanakotokea kinatuthibitishia watanzania kwamba CHADEMA ni chama cha watu wa eneo hilo.

lakini wamefeli zaidi kumtumia LEMA kuwa eti ni KAMANDA mwenye uchungu na CHADEMA kuliko ZITTO, hiki pia ni kielelezo cha upeo mdogo wa kufikiri kwa watu hawa.

ZITTO ni mjenzi wa NYUMBA inayoitwa CHADEMA, Zitto ameshiriki mpaka kuijenga CHADEMA tangu ikiwa nyumba ya nyasi, mpaka ikawa ya udongo, ikaja ikawa ya tofali za kuchoma na sasa CHADEMA ni nyumba ya VIGAE,

LEMA ni mpangaji tu kwenye hii nyumba CHADEMA, hakuna jinsi yoyote mpangaji akawa na uchungu na nyumba kuliko mwenye nyumba, hakuna na haitaka itokee.

LEMA ni mpita njia tu kwenye CHADEMA, Kamwe hawezi kuwa na uhalali wa kumsema na kumtukana mtu aliyekijenga chama kilichomsaidia kumfikisha hapo alipo.

Nani humu jukwaani alikuwa anamfahamu LEMA mwaka 2006, NANI?. nani alikuwa anafahamu lolote kuhusu lema 2007,2008,2009 mpaka 2010 kabla ya uchaguzi mkuu?.

Nani anayemfahamu Lema kipindi hicho kwenye CHADEMA?. LEMA ni TUNDA LA KAZI NZURI YA KISIASA ILIYOFANYWA NA ZITTO KABWE.

Wakati Zitto anahangaika kushirikiana na viongozi wenzake kuijenga CHADEMA, LEMA alikuwa ni KIBARAKA wa MZEE AUGUSTINO MREMA wa TLP.

Wakati Zitto anaibua hoja za msingi zenye maslahi kwa Taifa kama BUZWAGI na nyinginezo, LEMA bado alikuwa hata hajui chaguo lake la kisiasa katika nchi hii, yaani lema hakuwa akijua aende chama gani cha siasa.

Wanaokumbuka na wenye akili timamu watakubaliana nami kuwa ni zitto aliyekwenda Arusha kumnadi mgombea wa TLP wa udiwani wakati wa uchaguzi wa marudio 2008 huku lema akiwa mpiganaji kibaraka wa augustino mrema wa TLP.

wanachadema wanafahamu kuwa wakati tunafanya uchaguzi wa ndani ya chama mwaka 2009 LEMA ndio kwanza alikuwa ana siku 4 za uanachama wake ndani ya CHADEMA.

LEMA anapita tu njia CHADEMA kwa kuwa yeye ni msaka tonge tu kama wasaka tonge wengine, ndio maana alipita NCCR, ILIPOKUFA AKAKIMBIA, AKAPITA TLP ilipokufa akakimbia na sasa yupo CHADEMA nayo ikiyumba sidhani kama hataacha kukimbia. LEMA hana hadhi ya kukubali kutumiwa na kina MBOWE na GENGE lake kumshambulia ZITTO, hana hiyo moral authority. mpangaji hawezi kuwa na uchungu sawa na mwenye nyumba,

Leo CHADEMA ikipasuka, leo CHADEMA ikiyumba, ikitetereka atakayeumia ni ZITTO aliyeijenga na si LEMA aliyeidandia.

Nasisitiza hapa kuwa Hakuna namna yoyote ile inayoweza kumshusha Zitto kwenye heshima yake aliyojijengea kwa kusambaza uwongo wa namna hii, hakuna na hitakaa itokee.

Hakuna namna yoyote ile ya kumshusha zitto kwenye orodha ya wanasiasa bora na makini kwa kuwatumia watu kama kina lema na nassary ambao wakati wanaomba kura waliomba wakisema WATUMWE WAENDE BUNGENI WAKAWE KAMA ZITTO.

Again, ni rahisi sana kumshusha zitto kama kuna lolote baya amelifanya lisilo na maslahi kwa umma wa watanzania. ni Rahisi sana kumshusha na kumchafua zitto kama njia anazopita sio sahihi, LAKINI SIO KWA UWONGO WA KIPUUZI NAMNA HII.

Pamoja na kukiri kuwa Zitto ndiye mwanasiasa ninayemuamini na anayenivutia kuliko mwanasiasa yoyote Tanzania, na pamoja na ukweli kwamba zitto sio rafiki kwangu bali ni kaka yangu. Lakini sijawahi hata siku moja kupokea pesa kutoka kwake ama kwa MPESA au kwa TIGO PESA tangu nimefahamiana nae mpaka leo.

Ndio maana ninawapa pole MBOWE na vijakazi wake wanaotunga uwongo wa namna hii bila hata kujifikiria mara mbili mbili.

Uchaguzi mkuu wa ndani ya chama unawatia homa kundi la Mbowe na wagaza wenzake, uchaguzi huo unawafanya waweweseke kutwa kucha, mchana usiku.

Hakuna sababu ya kuhangaika na Zitto, wanachadema wapo na wataamua kwa yale mliyoyafanya, Zitto yeye ameshawaacha mile 2000 kwenye siasa zenye tija kwa Taifa.

Nimelazimika kuandika maneno haya baada ya kuona kuna huu ujinga unaofumbiwa macho na viongozi wa CDM kwa makusudi kabisa.
iliwahi kuandikwa humu mtandaoni kuwa ''Zitto ni maporomoko ya Nile, hayazuiliki kwa kifusi'' amewashinda na anaendelea kuwashinda.

Narudia tena kusema KWENYE HILI TAYARI ZITTO AMESHASHINDA.

1. Aliwashinda kwenye uwongo wenu mliokuwa mkiusambaza wa kupokea rushwa TANESCO lilipobumbuluka wakina mnyika, lissu na nassary wote waliufyata.

2. Aliwashinda mlipounda tume ya kumchunguza kuasisi migogoro ndani ya chama.

3. Alishinda kwenye hoja ya Buzwagi

4. Alishinda kwenye hoja ya kuwatimua mawaziri vilaza kwa kutoa hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu

5. Amewashinda kwenye hoja ya kuficha mali nje ya nchi (kama mabilioni ya uswisi) leo mnatapa tapa kwa kuwa bossi wenu anamiliki mali uarabuni.

Naomba niwakumbushe kuwa zitto ndiye mwanasiasa pekee wa upinzania anayeweza kuilazimisha serikali ikafanya maamuzi kutokana na hoja yake hata kama haipendi kufanya hivyo kwa wakati huo. Mfano ni hiyo hapo juu.

Naomba nihitimishe kwa kusema, ni kweli kwamba uwongo unapanda ghorofa kwa kutumia klifti, lakini hauwezi kubadilisha ukweli wa mambo daima dumu. uwongo utabaki kuwa uwongo tu na utaendelea kupuuzwa milele na milele.

Ndimi,
Habibu mchange
0762178678
mchangehabibu@yahoo.com

Ndg. Mchange,

Kwanza nikiri kuwa sikufahamu kabisa, wala sijawahi kukusikia kwenye medani za kisiasa, sisemi hivyo kwa maana kuwa wewe si lolote katika medani za siasa, hasa ndani ya CDM, lah! Bali labda kutoka na aina ya mihangaiko yangu ya kila siku, nashindwa kuwajua wapiganaji!

Kwa mujibu ya maandiko yako hapo juu, wewe una nafasi ndani ya CDM, sasa huoni hayo uliyoondika kama yatazidi kuleta mpasuko?

Ndani ya CDM hakuna pakusemea haya, mpaka kwenye social media?

Je, ukiambiwa uthibitishi jinsi MBOWE, anavyomtumia Lema, Nassary na wangine unaowajua wewe kumchafua ZITTO unaweza?

Je, unadhani hayo uliyoandika yanajenga chama au yanaboa, huoni kuwa wewe ni muumini wa ukabila, ndio maana unagusia hizo chembe kwenye maandiko yako?

Je, kwa upeo wako, unadhani leo ZITTO akipewe nafasi ya kuongoza CDM , akiwa Mwenyekiti, chama kita-stawi au kitadumaa!

Wewe unaamini kuwa ZITTO ndio mzalendo wa kweli, je uliwahi kumuuliza chochote juu hizo shutuma zinazoelekzwa kwake!

Naomba hayo majibu!

VIVA CDM
 
Awe makini na uhai wake tu. Cc Ben Saanane, Yericko Nyerere, Ritz, chama.
· Swala la Bomu Arusha ulishiriki na lengo ilikuwa ni kumuua mwenyekiti wa Chadema pamoja na
Ndg. Lema. Hii kitu ulipanga, wewe, mwigulu na vyombo vya usalama ·Zitto, rais Kikwete alipoenda Sudan ya Kusini uliambatana naye. Unakumbuka sababu ya wewe kuitwa? Nikukumbushie kwamba ilikuwa zawadi kwako ya kuihujumu chadema. CCM hawakupendi, bali wanapenda hujuma zako ndio maana walikudanganya kwamba watakusaidia kupata uenyekiti CDM ikiwepo kumuua Mbowe na kumdhoofisha Dr. Slaa

theo mutahaba..
 
Kwanini watu wanaongelea makundi CHADEMA badala ya kukazia kwenye kutofautiana kwa Zitto na Lema kwenye suala ya Posho? sasa CHADEMA yahusika vipi?

Team Zitto acheni kupotosha, msipoteze lengo ni POSHO
 
· Swala la Bomu Arusha ulishiriki na lengo ilikuwa ni kumuua mwenyekiti wa Chadema pamoja na
Ndg. Lema. Hii kitu ulipanga, wewe, mwigulu na vyombo vya usalama ·Zitto, rais Kikwete alipoenda Sudan ya Kusini uliambatana naye. Unakumbuka sababu ya wewe kuitwa? Nikukumbushie kwamba ilikuwa zawadi kwako ya kuihujumu chadema. CCM hawakupendi, bali wanapenda hujuma zako ndio maana walikudanganya kwamba watakusaidia kupata uenyekiti CDM ikiwepo kumuua Mbowe na kumdhoofisha Dr. Slaa

theo mutahaba..

Msipende kuwa waganga wa kienyeji.
 
5. Amewashinda kwenye hoja ya kuficha mali nje ya nchi (kama mabilioni ya uswisi) leo mnatapa tapa kwa kuwa bossi wenu anamiliki mali uarabuni.


Ndimi,
Habibu mchange
0762178678
mchangehabibu@yahoo.com

Sina nia ya kulumbana lakini hapa utakuwa umemtoa Zitto kwenye lengo la kufatilia mabilioni ya Uswiss. Lengo ni mafisadi hasa vigogo wanaoficha fedha za umma nje.

Mbowe ametoa taarifa juu ya mali zake nje na amesema ameorodhesha zote kwenye tume ya maadili kama sikosei wanakotaja mali za viongozi.

Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Ndo mtu ambaye ametaja mali zake nje na kama sikosei kwa umri nilionao sikuwahi kumsikia kwamba alikuwa serikalini.
 
Ahsante bwana Mchange. Hakika umenena ya moyoni na yaliyo ya kweli

Masalia Mchange huu utumbo wako utasomwa na vilaza kama hawa wa magamba ila nashukuru pamoja na kusoma kwa kuruka ruka nimeona mahali unapotambua Chadema ni nyumba ya vigae kwa sasa na imara kamwe hamtaweza kuiyumbisha na vibaraka wa Lb7 project hata mzikiri uchi kupitia kwa huyo kibaraka wenu prezoo...
 
Last edited by a moderator:
Nakujua tangu udom,siasa zako za kuabudu watu(zito)hujaacha tu,nimewahi kukushauri juu ya siasa zako,naona hushauriki bwanamdogo
 
Yani CHADEMA hii vita ya ndani sababu kuu ya kuileta public hasa ni nini?
Kama CHADEMA wanadhani kua wakisambaa hivi watakaobaki wana nafasi 2015 ni kujidanganya, CHADEMA ikisambaratika hivi 2015 hakuna atakayewaheshimu tena wote wataonekana wao ovyo tu... Once again magamba watachukua, jipangeni upya kwa 2020 labda... na hapo kati wakijipanga fresh mnaweza mkashangaa wanafululiza miaka yote
 
Huu mnyukano unafurahisha maana kila mmoja anataka aonekane ndio mkweli, uzuri wa ukweli ni kuwa hujionyesha mwishoni mwa yote lakini kuna ambao hata pale ukishaonekana huwa wanaukana japo hiyo haiubadilishi.
Huu mjadala mpya naona umeufunika ule wa 'majumba ya Mh. Mbowe'!
Tuseme tusemayo ukweli ni kwamba ndani ya cdm kuna wasaliti; Mwenyekiti kikili, Katibu mkuu kakili na hata Naibu Katibu mkuu kaweka wazi juu ya 'virusi'. Ni Mh. Lema aliyeenda hatua moja mbele kwa kutaja majina ambapo angalau kuna kukubali au kukanusha.
 
Mchange hizo nondo ni hatari,Jamaa wanaweweseka,Zitto hajawahi kushindana akashindwa,hata wakaanga sumu wanalijua hilo. Fitna alizofanyiwa Jamal Malinzi TFF ndizo anazofanyiwa Zitto na Mkumbo Chadema,naamino watashinda kama ilovyokuwa Kwa Malinzi,na siku zitto akiwa mwenyekiti wa chama Taifa ndipo wanafiki watadhalilika kama wanavyodhalilika wanafiki wa TFF.
 
Kuna mtu anasema thibitisha kuwa ulikuwa hupewi fedha. hebu naomba tusaidiane kidogo kwenye hili hivi mtu unathibitishaje kuwa ulikuwa hupewi fedha? Sio kwamba anayesema ulipewa ndiye anayetakiwa kuthibitisha hivyo? Au inakuwaje hapa wadau wa hili sakata maana naona bado bichi sana.
 
Yani CHADEMA hii vita ya ndani sababu kuu ya kuileta public hasa ni nini?
Kama CHADEMA wanadhani kua wakisambaa hivi watakaobaki wana nafasi 2015 ni kujidanganya, CHADEMA ikisambaratika hivi 2015 hakuna atakayewaheshimu tena wote wataonekana wao ovyo tu... Once again magamba watachukua, jipangeni upya kwa 2020 labda... na hapo kati wakijipanga fresh mnaweza mkashangaa wanafululiza miaka yote
Viongozi wa serikali/ccm walishatamka hadharani kuwa cdm itakufa baada ya mwaka ambao kimsingi ulikuwa ukiishia mwaka jana kama sikosei. Rejea mambo mengi na mengine ya kutisha kama ugaidi na bomu la Soweto-Arusha, kama hivi vyote vimepita bila chama kufa basi na hili ambalo labda lilikuwa 'pigo la mwisho' litapita tu.
Cha muhimu zaidi ni bora ccm wakashinda uchaguzi 2015 kwa hila kama hizi za kuvivuruga kinafiki vyama halali kwa mujibu wa sheria kuliko cdm kutoweka kabla ya mwisho 2012 kama 'ilivyopangwa'. CDM endelevu ndiyo italikomboa taifa hili badala ya kuwa na chama kilichojaa wasaliti kama wale waliomdanganya Mwalimu kuwa ni wajamaa kumbe mjamaa ni yeye na Mzee Kawawa tu.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom