Zitto: Kwa ripoti ya CAG Serikali imepata hati chafu

Zitto: Kwa ripoti ya CAG Serikali imepata hati chafu

Watu mnawashwa kabisa!
Nchi inaliwa na vichaa wewe unapongeza?
Kumbe wenye akili za Makonda mpo wengi!
 
Kwa hali ya nchi za dunia ya tatu na hasa kusini mwa jangwa la sahara tumpongeze sana raisi tuliye naye.
Kwa ripoti hii au una lingine zaidi? Tafuta sympathy kwingine na bora ujipendekeze kwa shemeji akusongee ugali ule!
 
Zitto amekuwa mkalimani wa CAG anaenda kututafsiria.
 
Soma ukurasa wa 298 kwenye Ripoti ya Kiswahili
Mkuu bora umekuja hapa....umesema wazi kwenye awamu hii ya tano pesa zetu haziko salama kabisa...
Naomba utukumbushe ni kipindi na awamu gani wewe unaona pesa zetu zilikuwa salama?
Wewe ulikuwa kwenye kamati ya mahesabu katika mashirika ya Umma na mlikuwa mkiyakagua kila siku hebu tukumbushe nini kilitokea NSSF?
Ni kweli katika kipindi chako ukiwa mwenyekiti wa kama PAC pesa zetu zilikuwa salama sana kiasi kwamba kwa sasa haziko salama?
Hebu tukumbushe ni kipindi gani pesa zetu zilikuwa salama

Hebu tuambie wewe una kwenda kutafsiri nini kumshinda CAG?
Nini ambacho CAG hakusema unakwenda kusema?
 
Soma ukurasa wa 298 kwenye Ripoti ya Kiswahili
Kiongozi heshima kwako

Hakika wangalikuwapo wabunge wa ccm 5 tu km we walahi tungejaribu kuifikia tz ya viwanda

Mungu akulinde kwa kila jambo
 
Zitto kwa kutafuta "kiki" ni namba moja.

Zitto anawapata watu ambao ni wavivu wa kusoma makabrasha ya sheria na vitabu.

Mapitio ya hesabu jumuifu za taifa ni angalizo na ushauri unaotolewa na CAG kutokana na mahesabu yote serikalini ambapo alisema kwenye baadhi ya maeneo mahesabu hayaridhishi.

Eti fedha za umma haziko salama kwenye utawala wa awamu ya tano! Ni lini zilikuwa salama kwa sababu hata kwenye Jimbo lake linaloongozwa na ACT-Wazalendo limepata hati chafu. Au alidhani hizo siyo pesa za umma?

CAG ametuambia kuwa kwa ujumla kuwa mafanikio katika utunzaji wa pesa za umma ukilinganisha na miaka ya nyuma lakini hii haifuti ukweli kuwa baadhi ya taasisi za serikali zimepata hati chafu.

Hajui kuwa hayo majumuisho ni pamoja na Halmashauri ya Ujiji Kigoma ndio yanatoa ukweli wa kwa serikali katika utunzaji wa pesa.

Hizi "kiki" za Zitto zilikuja na zikapita!

Baada ya kufariki Mke wa Mandela alijitokeza haraka haraka na kudai ACT-Wazalendo itatuma jopo la viongozi wake kuhudhuria msiba. Hakuna aliyekwenda!

Alisema atafungua kesi mahakamani kupiga kuondolewa kwa katibu wa bunge. Hakufungua.

Alisema atafungua kesi mahakamani kwa sababu polisi wamemzuia kufanya kazi zake jimboni. Hakufungua.
Pamoja na ukweli kuwa Uko mstari wa mbele kuitetea Serikali Muhimu ni kwamba madudu yote haya yanatokea chini ya utawala wa COM. Wewe ukiwa mshauri au Vuvuzela
 
Kama Bunge litakosa kuwa na wivu na mamlaka na kazi zake za KUPITISHA BAJETI YA SERIKALI kwa mujibu wa Katiba ya JMT ibara ya 103, au kuishauri na kusimamia serikali, halina haja kabisa ya kuendelea kuwepo.
Kama matumizi ya billion 5 za kujenga UKUTU Meroreni hazikuwepo kwenye bajeti,
Kama kujenga uwanja wa Ndege CHATU hazikupitishwa na Bunge au
Fedha za kununulia BOMBADIER zetu 4 hazikupitishwa na Bunge, basi kukaa Dodoma kwa siku 70 hakuna maana yoyote, tumwache kiongozi wetu aamue matumizi kadri inavyopendeza,
Wawakilishi wetu waache kulalamika, wafanye kazi yao kwa mujibu wa Katiba ya NCHI.
Zitto na wenzake, waisimamie na kuishauri serikali, watende kwa mujibu wa sheria ya Bajeti ya 2014/2015 na kwa mujibu wa Katiba
 
Unachofanya Zitto ni sahihi kabisa na hata vyama vingine vinapaswa kufanya uchambuzi na kuueleza umma madudu yaliyoko katika ripoti ya CAG.

Bwana mkubwa anatumua sana nguvu ya media kuamisha yuko serious katika vita ya rushwa na ufisadi na kwamba eti ufisadi umepungua.

Ni wajibu wa vyama vya upinzani kutumia taarifa ya CAG kuwaeleza wananchi ukweli halisi na nyinyi mnapaswa kutumia media kama yeye afanyavyo.

Zitto nakuunga mkono kwa asilimia 100 na ningetamani na vyama vingine viige na si wanasiasa wa vyama hivI kuishia kufanya uchambuzi wa taarifa hii ya CAG mitandaoni tu.

Unachofanya Zitto ndio kazi hasa ya upinzani.
 
Na saivi kampekeka wizara ambayo sheria imeshapitiswa CAG hana mamlaka ya kuigusa wao wanakula tu na mhutu mwenzao hadi ukuta wamemjengea
 
Back
Top Bottom