Zitto: Kwa ripoti ya CAG Serikali imepata hati chafu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,896
FB_IMG_1523723646867.jpg
7;
FB_IMG_1523723657129.jpg

Serikali Kuu ( Hesabu Jumuifu za Taifa ) imepata HATI CHAFU. Sababu za Hati Chafu kwenye Sura ya Nne na ya Tano ya Taarifa ya CAG zinatishia kabisa usalama wa Fedha za Umma.

Kesho nitazungumza na Waandishi wa Habari kuchambua Taarifa ya CAG ya mwaka 2016/17 na kufafanua hoja nzito sana alizotoa CAG kwenye ukaguzi wake kwa Serikali Kuu.

Kiufupi Fedha za Umma hazipo salama chini ya Utawala wa Awamu Tano iwapo wataendelea na mtindo wa Uongozi walio nao.

Kuanzia saa tano kamili asbh tutakuwa livestream pia kwenye akaunti hii
 
View attachment 744567 7; View attachment 744566 Serikali Kuu ( Hesabu Jumuifu za Taifa ) imepata HATI CHAFU. Sababu za Hati Chafu kwenye Sura ya Nne na ya Tano ya Taarifa ya CAG zinatishia kabisa usalama wa Fedha za Umma. Kesho nitazungumza na Waandishi wa Habari kuchambua Taarifa ya CAG ya mwaka 2016/17 na kufafanua hoja nzito sana alizotoa CAG kwenye ukaguzi wake kwa Serikali Kuu. Kiufupi Fedha za Umma hazipo salama chini ya Utawala wa Awamu Tano iwapo wataendelea na mtindo wa Uongozi walio nao. Kuanzia saa tano kamili asbh tutakuwa livestream pia kwenye akaunti hii
Zitto bhana sasa anataka kusema nini ambacho Prof Assad alisahau kutuambia!
 
Zitto kwa kutafuta "kiki" ni namba moja.

Zitto anawapata watu ambao ni wavivu wa kusoma makabrasha ya sheria na vitabu.

Mapitio ya hesabu jumuifu za taifa ni angalizo na ushauri unaotolewa na CAG kutokana na mahesabu yote serikalini kutoka taasisi na mashirika ambapo alisema kwenye baadhi ya maeneo mahesabu hayaridhishi.

Hii haina tofauti na kufanya hesabu ya 2x3x4x0=0

Hui ina maana kuwa kama kuna taasisi 1 kati ya 10 iliyopata hati isiyoridhisha ina maana hata kwenye hitimisho la hesabu jumuishi itakuwa hati isiyoridhisha.

Eti fedha za umma haziko salama kwenye utawala wa awamu ya tano! Ni lini zilikuwa salama kwa sababu hata kwenye Jimbo lake linaloongozwa na ACT-Wazalendo limepata hati chafu. Au alidhani hizo siyo pesa za umma?

Wakati Zitto akiwa Mwenyekiti wa PAC akipokea rushwa kutoka kwa wakuu wa NSSF kwenda kwenye kampuni fake ya LEKADUTIKITE hakuwahi kuona kuwa pesa za serikali haziko salama!

CAG ametuambia kuwa kwa ujumla kuna mafanikio katika utunzaji wa pesa za umma ukilinganisha na miaka ya nyuma lakini hii haifuti ukweli kuwa baadhi ya taasisi za serikali zimepata hati chafu.

Hajui kuwa hayo majumuisho ni pamoja na Halmashauri ya Ujiji Kigoma ndio yanatoa ukweli wa kwa serikali katika utunzaji wa pesa.

Hizi "kiki" za Zitto zilikuja na zikapita!

Baada ya kufariki Mke wa Mandela alijitokeza haraka haraka na kudai ACT-Wazalendo itatuma jopo la viongozi wake kuhudhuria msiba. Hakuna aliyekwenda!

Alisema atafungua kesi mahakamani kupiga kuondolewa kwa katibu wa bunge. Hakufungua.

Alisema atafungua kesi mahakamani kwa sababu polisi wamemzuia kufanya kazi zake jimboni. Hakufungua.
 
Zitto kwa kutafuta "kiki" ni namba moja.

Eti fedha za umma haziko salama kwenye utawala wa awamu ya tano! Ni lini zilikuwa salama kwa sababu hata kwenye Jimbo lake linaloingozwa na ACT-Wazalendo limepata hati chafu. Au alidhani hizo siyo pesa za umma?

Hajui kuwa hayo majumuisho ya hati chafu kama za Halmashauri ya Ujiji Kigoma ndio yanatoa hati chafu kwa serikali.

Baada ya kufariki Mke wa Mandela alijitikeza haraka haraka na kudai ACT-Wazalendo itatuma jopo la viongozi wake kuhudhuria msiba. Hakuna aliyekwenda!

Alisema atafungua kesi mahakamani kupiga kuondolewa kwa katibu wa bunge. Hakufungua.

Alisema atafunfua kesi mahakamani kwa sababu polisi wamemzuia kufanya kazi zake jimboni. Hakufungua.
Elimu ya uraia ifundishwe tenA, mtu kama huyu hajui Mkurugenzi ndio mwenye mamlaka ya fedha kwenye mkoa husika
 
Zitto kwa kutafuta "kiki" ni namba moja.

Eti fedha za umma haziko salama kwenye utawala wa awamu ya tano! Ni lini zilikuwa salama kwa sababu hata kwenye Jimbo lake linaloingozwa na ACT-Wazalendo limepata hati chafu. Au alidhani hizo siyo pesa za umma?

Hajui kuwa hayo majumuisho ya hati chafu kama za Halmashauri ya Ujiji Kigoma ndio yanatoa hati chafu kwa serikali.

Baada ya kufariki Mke wa Mandela alijitikeza haraka haraka na kudai ACT-Wazalendo itatuma jopo la viongozi wake kuhudhuria msiba. Hakuna aliyekwenda!

Alisema atafungua kesi mahakamani kupiga kuondolewa kwa katibu wa bunge. Hakufungua.

Alisema atafunfua kesi mahakamani kwa sababu polisi wamemzuia kufanya kazi zake jimboni. Hakufungua.
Uzuri ni kwamba unalipwa kwa kazi hii so utapita tu kama walivyopita akina MwanaDiwani Simiyu Yetu TandaleOne n.k

Unatumika kama mpira wa kinga
 
Zitto kwa kutafuta "kiki" ni namba moja.

Eti fedha za umma haziko salama kwenye utawala wa awamu ya tano! Ni lini zilikuwa salama kwa sababu hata kwenye Jimbo lake linaloingozwa na ACT-Wazalendo limepata hati chafu. Au alidhani hizo siyo pesa za umma?

Hajui kuwa hayo majumuisho ya hati chafu kama za Halmashauri ya Ujiji Kigoma ndio yanatoa hati chafu kwa serikali.

Baada ya kufariki Mke wa Mandela alijitikeza haraka haraka na kudai ACT-Wazalendo itatuma jopo la viongozi wake kuhudhuria msiba. Hakuna aliyekwenda!

Alisema atafungua kesi mahakamani kupiga kuondolewa kwa katibu wa bunge. Hakufungua.

Alisema atafunfua kesi mahakamani kwa sababu polisi wamemzuia kufanya kazi zake jimboni. Hakufungua.
CAG kawashika pa pabaya, mmevurugwa mkavurugika

Kwann unaanza kumshambulia Zito badala ya hoja yake?
 
Kwa hali ya nchi za dunia ya tatu na hasa kusini mwa jangwa la sahara tumpongeze sana raisi tuliye naye.
 
Ni wapi taarifa ya CAG imesema Serikali yote imepata hati chafu?
 
Zitto Mkuu unategemea Jiwe amsimamishe mtoto wa Dada Dotto James!? Haiwezekani kabisa hilo hata siku moja.

Back
Top Bottom