Zitto kung’oka CHADEMA

Zitto kung’oka CHADEMA

Wooh, kumbe ZZK bado yupo na this time ame "make headline" katika Newsroom za baadhi ya vyombo vya habari!?

Lakini nakumbuka kuwahi kumsikia huyu bwana wakati flani akisema kuwa hawezi kuondoka CHADEMA mpaka kwanza hatima ya kesi yake mahakamani dhidi ya chama chake hiki "cha zamani" itakapokwisha (kwa yeye kushinda) ili kuhakikisha kuwa anajenga msingi (kwa mtazamamo wake) wa kuhakikisha watu wenye hulka na mitazamo kama ya kwake katika vyama vya siasa hawaonewi kwa misingi ya maamuzi kama yaliyochukuliwa na chama dhidi yake!!..

Kimetokea nini tena hata asiweze ku fulfill hii ambition yake? Au tayari ameambiwa kuwa hii ngoma ni nzito kwake na kwa hiyo aanzishe mapema kutafuta malisho mahali pengine.... ACT - TANZANIA?

I don't get it completely!!.......I mean, siiamini hii habari kwani ili aondoke CHADEMA huyu ni mpaka ashinde kesi yake aliyoifungua dhidi ya chama chake alichomo sasa!!!!

Na ki ukweli haya acha yafanyike katika vyama hivi tu, lakini ndani ya CCM ukifanya ujinga kama huu si tu kwamba watakupuga asubuhi tu, bali uhai wako ni halali yao!!
 
mwambieni aje chama chenu cha maauaji mpe uenyekiti ili chama chenu kizidi kung'aaa kwa wizi na rushwa, maana adui yako muombe njaaa, so kama ndiye alikipa umaarufu chadema na watu hawamthamini.. Sasa nyinyi mnaompenda bwana wenu mchukueni ili chadema kife,......, usilete siasa za maji taka hapa... Ameshindwa hata kuchimba visima jimboni kwake, hakuna maji anzia mwandiga yote, bitale, mkongoro hadi kalinzi njoo mpaka nyarubanda, hata umeme hayo maeneo hakuna... Sasa mtu akama alishindwa hataa kutumia mfuko wa jimbo tu kuchimba visima kwa miaka yoote hiyo bado ni wa maana huyo na maeneo yake hayo yana mito mingi tu, hata water table ipo karibu... Umefika jimbo lake?? Sasa niko huku.. So anaongea nacho kijua..... Mkuu usiongee tu kuonekana umechangia il;i nape mwandosya...akupe buku 7.. Ongea vitu harisi....

Zitto ameifanya Kigoma imekuwa Dubai ya Africa.. Hakika Zitto ni kiongozi shupavu
 
Kwangu Tanzania daima ni poor source of information kwa sababu liko biased kwa chadema.
 
M W A NA H A L I S I NOV 24,2010

MKUTANO wa kwanza wa Bunge la kumi uliomalizika Alhamisi iliyopita, mjini Dodoma, umeandika historia.

Ni kwa wabunge wa chama kikuu cha upinzani nchini – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kususia hotuba ya rais Jakaya Kikwete na kutoka nje ya ukumbi wa bunge.

Hilo ni tukio la kwanza kumkuta rais wa Jamhuri tangu taifa hili lipate uhuru, miaka 50 iliyopita.

Wengi wamezungumzia tukio hilo, lakini wengi wao, wamejikita katika kulaumu CHADEMA.

Bali, tukio lile lina sura nyingi za kujadiliwa. Kwa mfano, kuna rais anayesusiwa; aliyejibu ususaji kwa njia ya vijembe na kejeli; na kuna wabunge waliozomea badala ya kusikitika.

Kuna waziri mkuu anayelaumu na kulaani badala ya kuchukua hatua kabla ya tukio lenyewe kutokea; kuna serikali iliyoshindwa kuongea na viongozi wa CHADEMA ili kumuepusha mkuu wa nchi na aibu iliyompata.

Yupo spika “mwanafunzi” ambaye ameshindwa kufanya jitihada zozote za wazi kuepusha aibu iliyotokea na ambayo imemfunika yeye na historia yake aliyoiweka siku chache zilizopita.

Kuna CHADEMA na uamuzi wa kutumia njia ya kususia badala ya kutumia nyingine kama kweli zilikuwepo. Vipo vyama vingine vya upinzani ambavyo badala ya kusikitika, viliinuka kuchukua viti vilivyoachwa wazi na CHADEMA.

Kwa ujumla, tukio lile lilikuwa na sura nyingi, lakini ushabiki wa baadhi ya waliojitosa kujadili, umewanyima wananchi wengi fursa ya kuchambua na kujadili sura hizo kwa faida ya vizazi vijavyo.

Makala hii, nayo haitajadili hayo. Badala yake, itajikita katika mjadala ulioibuliwa na mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), naibu katibu mkuu wa chama hicho na naibu kiongozi wa upinzani bungeni, Zitto Kabwe.

Yeye na baadhi ya wabunge wenzake wachache waliamua kutoingia bungeni kinyume na maelekezo ya chama chao.

Katika utetezi na ufafanuzi alioutoa kupitia televisheni ya taifa (TBC1), Zitto anadai pamoja na mengi, kuwa yeye na wenzake waliamua kutoingia ukumbini kuepuka kumwaibisha mkuu wa nchi ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu.

Kwamba, aliamua kufuata dhamiri na shinikizo la wapiga kura wake ili kuonyesha heshima kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye amefanya maendeleo makubwa mkoani Kigoma kuliko rais yeyote tangu uhuru.

Kwa Zitto, maendeleo mkoani Kigoma ni fadhila kutoka kwa rais na anajisikia deni mbele yake. Alihitimisha kwa kusema, “Rais ni alama ya umoja wa nchi na ni lazima aheshimiwe.”

Kabla ya utetezi wake, kulikuwa na taarifa kwamba Zitto alikuwa “anatumika” kushawishi wabunge wagawanyike katika suala la msimamo mmoja wa chama chao. Ilimlazimu kutumia hata udini ili kukamilisha adhima yake.

Kwa kuwa suala la udini alilizungumzia pia katika mahojiano yake na TBCI, nashawishika kuamini kuwa Zitto anayo ajenda ya udini katika kutimiza malengo yake ya kuigawa CHADEMA.

Iwe anayo yeye kama yeye, au anatumwa na wanaomtuma, kuna kila sababu ya kuamini kuwa Zitto ametekwa na fikra hizi mbaya za udini anaodai anaupinga.

Fikra hizi ni matusi kwa wananchi waliomchagua kutokana na kuamini kuwa ana uwezo wa kuongoza. Kumbe moyoni mwake anaamini kuwa alichaguliwa kwa misingi ya udini!

Kwa mwanasiasa kijana, msomi na aliyewahi kujijengea heshima siku za nyuma, hatua hii inawasaliti maelfu ya vijana waliokuwa na matumaini makubwa kwake, kwani wanaona kauli na vitendo vyake vinachonga jeneza lake na fikra zake.

Naendelea kumwamini hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyesema kuwa wanasiasa waliofilisika au wanaoelekea kufilisika, hujificha ndani ya kwapa la udini na ukabila.

Kwa hili, Zitto amefilisika mapema wakati biashara ya siasa ndiyo inaanza.
Siku mbili kabla ya tukio la bungeni, Zitto alikuwa na mazungumzo ya muda mrefu na alikuwa na mazungumzo ya ana kwa ana na waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na baadaye akafanya mazungumzo na Rais Kikwete kwa njia ya simu.

Habari hizi alizisema Zitto mwenyewe ili kuwashawishi wabunge wakubaliane naye katika “mpango” wake wa kukigawa chama chake.

Baadaye alikutana na “maofisa maalum” wa serikali aliodai kuwa walikuwa wanampa habari maalum za kusaidia kumaliza aibu ambayo ingetokea kwa kususia hotuba ya rais. Wanafahamika hata kwa majina.

Kwa ujumla, Zitto alionekana kumhurumia Kikwete kuliko hata Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenyewe kinavyomhurumia mwenyekiti wake.

Kwa mtu yeyote anayejali na kupenda kuimarisha siasa mbadala katika nchi, atasikitika kusikia na kuona haya yakifanywa na Zitto.

Hata kama upinzani si uadui, lakini upinzani unaojipendekeza kwa CCM kuliko hata wana-CCM wenyewe ni wa hatari; na wanachama wenyewe wa CCM hawautaki.

Wana-CCM makini hawapendi tabia ya Zitto kujipendekeza kwa viongozi wa juu na wakati mwingine kuwachonganisha kwa kuvujisha habari azipatazo kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine.

Tayari hatua ya Zitto ya kuchukua maneno ya huyu na kumpa yule, imechochea mgogoro wa chinichini ndani ya chama cha Kikwete.

Mgogoro huu unapata nguvu kutokana na utamaduni mpya wa mtendaji mkuu wa CCM, Yusuph Makamba kuthamini wapinzani mamluki wanaorejea CCM baada ya kuwa wameshakibomoa chama hicho kwa kukishushia lundo la shutuma.

Orodha ya wanaopewa kipaumbele na Makamba kuliko wanachama wengi wanaojitolea kujenga chama chao, inahusisha Steven Wasira, Tambwe Hizza, Mbarouk Msabaha, Dk. Amani Kaborou, Sahibu Akwilombe, Daniel Nsanzugwanko, Justine Sarakana na Thomas Ngawaiya.

Ndani ya chama cha Makamba na Kikwete, hawa ni wanachama wanaotoka daraja tofauti.

Naye Zitto anaelekea kupenda kujiunga na orodha hiyo kwa gharama mbili kubwa. Kwanza, kwa kuigawa CHADEMA (yenyewe kwa yenyewe) na pia CHADEMA na wapinzani wengine.

Pili, anaelekea kuanzisha migogoro ya ndani ya CCM kwa sababu anadai anayoyafanya ndani ya CCM anakuwa na ridhaa ya kiongozi mkuu wa chama – Makamba.

Wenye akili wanajua kuwa baadhi ya madai yake si ya kweli. Lakini hata yale machache yaliyo ya kweli, hayana dhamana ya chama hicho, bali utashi binafsi wa mmoja wa viongozi ndani ya chama hicho.

Katika suala la uadilifu kwa chama, CCM ikiwa taasisi, haina mwanachama aliye juu ya sheria hata kama wapo watu wengi nje ya chama hiki ambao wanaweza kupinga dai hili.

Kwa mfano, sidhani kama Zitto ana thamani kubwa ndani ya CCM kuliko Lowassa ambaye pamoja na mengi makubwa aliyokifanyia chama chake, bado wamegoma kumsafisha kutoka katika tuhuma zilizosababisha ateme kiti chake cha uwaziri mkuu.

Wala sidhani kama Zitto ni bora kuliko Samweli Sitta ambaye licha ya kuweka rekodi nzuri ya kusimamia bunge, ni CCM iliyosema Sitta hafai tena kuwa spika.

Ni Sitta na Lowassa waliofanikisha “kampeni za kisayansi” zilizomwingiza Kikwete madarakani mwaka 2005, lakini ni Kikwete huyohuyo aliyesema Sitta hafai na anaelezwa kila siku hadi asadiki kuwa Lowassa hasafishiki.

Mifano hii inatosha kumfundisha Zitto kuwa yuko hatarini pale anapojifanya na kudai kumheshimu mwenyekiti wa CCM kuliko anavyomheshimu mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

Usaliti ambao Zitto anaufanyia CHADEMA ni huohuo atakaoifanyia CCM endapo atajiunga na chama hicho.

Inavyoelekea si siku nyingi kutoka sasa Zitto atajisajili katika CCM ambayo anaitumikia sasa kwa mlango wa nyuma.

Nitakuwa wa mwisho kumkaribisha Zitto ndani ya CCM. Chama cha CCM kiko tayari kumtosa yeyote hata kama kwa kufanya hivyo kinapata hasara.

Zitto hajachelewa kuachana na utoto huu kwa kuheshimu chama chake ambacho, siyo tu kinaheshimiwa bali hata kuogopwa na wengi wakiwamo baadhi ya viongizi wakuu wa CCM.

Vinginevyo, Zitto awe tayari kuangamia.
 
Kigoma ni jiji linalokuwa kwa kasi kila siku, sio kama arusha jiji lililodumaa kimaendeleo
 
Mwanangu Zitto anatumiwa - Mama Zitto

M W A N A H A L I S I 18 November 2009

SHIDA Salum, mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Zitto Kabwe, ameibuka na kusema mwanaye anatumiwa kukivuruga chama chake.

Akizungumzia taarifa zinazoandikwa na baadhi ya magazeti kuhusu kinachoitwa mgogoro wa uongozi katika CHADEMA, kati ya Zitto na viongozi wenzake, Shida alisema, "hakuna mgogoro pale, kuna kikundi cha watu wanaotaka kumtumia mwanangu kufanikisha mambo yao."

Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar es Salaam, alidai kuna watu walio nje ya CHADEMA wanakula njama za kumgombanisha mwanawe na viongozi wenzake.

Alisisitiza, "kuna baadhi ya wanasiasa ndani ya CHADEMA wanaotumiwa na walio nje kugombanisha viongozi."

Akaongeza, "Mambo ya uchaguzi yalikwisha kitambo na Zitto kwa moyo mmoja alikubali kumaliza tofauti zake na Mbowe (Freeman Mbowe) ndiyo maana akamuacha Mbowe kuwa mgombee pekee wa uenyekiti."
Shida aliwatuhumu watu walio nje ya CHADEMA akisema ndio wanaopandikiza mbegu za chuki kwa lengo la kuwavuruga. Hata hivyo, hakuwataja.

Alisema kila mwenye akili timamu anajua kinachotafutwa, na nani mkweli na yupi anasingiziwa.
"Angalia wanaoandika haya. Kweli Zitto anaweza kutetewa na magazeti ya Habari Corporation yanayomilikiwa na Rostam Aziz halafu ukaamini kile kinachoandikwa?" alihoji.

Aliongeza, "Rostam yupi? Ni huyu tunayemjua au mwingine? Kwa wema upi alionao kwa chama chetu."
Wiki iliyopita magazeti ya Rai na Mtanzania yalinukuu taarifa zikidai kuwa zimetolewa na Shida, kwamba anataka mwanawe aondoke kwenye chama hicho kwa kile ilichoeleza kuwa "kumwepuesha na yaliyomkuta Chacha Wangwe."

Katika kujibu hilo, Shida anasema, "Mimi na Zitto tunajua katiba ya chama chetu. Tunafahamu taratibu za kuendesha chama. Yeye ni naibu katibu mkuu, mimi ni mjumbe wa Kamati Kuu. Tunajua nini maana ya uongozi, hivyo hatuwezi kukurupuka barabarani.

"Kwamba kama kuna malalamiko au tuhuma mathalani juu ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum, basi sote ni sehemu ya hicho kinacholalamikiwa. Kutokana na hali hiyo, hatuwezi kujifanya hatuhusiki na tukatuhumu kupitia vyombo vya habari, tena magazeti yanayomilikiwa na mwanachama wa CCM."

Shida alisema anajua kwa mapana chanzo cha yote yanayoandikwa na jitihada za kutaka kumgombanisha Zitto na viongozi wenzake, hasa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

"Yote haya tunafahamu chazo chake. Si uchaguzi wa ndani ya chama. Uchaguzi ulishakwisha na Zitto kwa moyo mmoja alikubali kumuachia Mbowe uenyekiti ili kulinda maslahi ya chama," alisema.
Alisema kuwa yeye kama mlezi, hawezi kuruhusu hali hiyo, hivyo atatumia nafasi yake ya mjumbe wa CC kuhakikisha kwamba tabia hiyo ya kugombanisha viongozi inakoma.

"Nikiwa mzazi, mlezi na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, siwezi kuruhusu Zitto kutumika kuingiza chama katika mgogoro. Nitasimama imara kuhakikisha kwamba CHADEMA inakuwa salama," alisema.
Wiki iliyopita, Dk. Slaa aliwaondoa katika nafasi za utendaji David Kafulila aliyekuwa Afisa Habari na Danda Juju aliyekuwa Afisa anayeshughulika na Halmashauri na Bunge kwa kile kinachoelezwa kuwa utovu wa nidhamu kwa chama na viongozi wake.

Kafulila alinukuliwa na baadhi ya magazeti kuwa alibeza kikao cha viongozi wa juu wa chama hicho kilichofanyika Dodoma ambapo Mbowe na Dk. Slaa walikutana katika kikao cha kawaida na wabunge wa chama hicho na baadhi ya wakurugenzi.

Kafulila alisema mkutano huo wa viongozi haukuwa na maana; na alifika mbali zaidi kwa kuufananisha na vikao vya geto. Ni matamshi hayo na mengine yaliyomfanya Dk. Slaa kutumia mamlaka yake ya kikatiba kumuondoa Kafulila katika wadhifa huo.

Taarifa zinasema hoja ya kumuondoa Kafulila katika kikao ilitolewa na Msafiri Mtemelwa, mmoja wa viongozi wake na ambaye alikuwa meneja wa kampeni za Zitto wakati wa kuwania uenyekiti wa CHADEMA.
 
Hivi huyu jamaa alikuwa bado yuko cdm ? Au ndio anamsubiri Julius Malema aje azindue chama chake ?
 
“Kichwa changu sasa kinafikiria ni namna gani kitawasaidia Watanzania waikatae katiba inayopendekezwa ambayo imechakachukuliwa kwa ajili ya manufaa ya watu wachache”

Dr. Wilbroad Peter Slaa
 
Zitto ni mzushi – Kafulila


04/12/2009Na Irene Mark

DAVID Kafulila, mwanachama mpya wa NCCR-Mageuzi, ambaye amekuwa akitumia uhusiano wake binafsi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, kama kete ya kisiasa katika ugomvi wake na uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amesema Zitto ni mzushi.

Kafulila, ambaye alikuwa Ofisa Habari wa CHADEMA kabla hajavuliwa cheo hicho na kukimbilia NCCR-Mageuzi, alisema hayo jana Dar es Salaam, wakati akijibu taarifa kuwa mbunge huyo amekanusha kumsaidia magari matatu ya kufanyia harakati za kujijenga kisiasa mkoani Kigoma baada ya kujiunga na NCCR-Mageuzi.


Msukumo wa Kafulila kumshutumu Zitto umetokana na tetesi kwamba amekuwa anatumia barua pepe ya mbunge huyo kusambaza taarifa zinazoleta chokochoko katika CHADEMA, kwa kuwa anajua neno siri la anuani ya barua pepe ya mbunge huyo ambaye amekuwa anamtumia kama msaidizi wake katika masuala mengi walipokuwa CHADEMA.


Taarifa hizo zilitokana na mawasiliano ya Zitto na watu walio karibu naye ambao juzi waliliambia gazeti hili wanachokiita ukweli wa madai ya mbunge huyo kumuunga mkono Kafulila katika harakati zake mpya akiwa NCCR-Mageuzi, kiasi cha kumpatia magari matatu kwa ajili ya kuzunguka maeneo kadhaa ya Jimbo la Kigoma Kusini katika siku chache zijazo.


Jana Kafulila aliiambia Tanzania Daima kuwa kama ni hivyo, Zitto ni mzushi, kwani hajawahi kumpa neno la siri la kufungua anuani ya barua pepe yake, wala hafahamu lolote kuhusu anuani hiyo.


Katika toleo la jana, gazeti hili lilkuwa na habari kuwa Zitto alimkana Kafulila, na kwamba mbunge huyo amekiandikia barua chama chake (CHADEMA) kukijulisha msimamo wake binafsi, kwa maelezo kuwa wanaomhusisha na kauli za Kafulila wana nia ya kumchonganisha (Zitto) na uongozi wa CHADEMA.


Kauli kama hii ilitolewa na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto, katika mahojiano yake na gazeti la 'm w a n a h a l i s i' wiki mbili zilizopita, akisema mwanawe anatumiwa na watu wenye lengo la kuvuruga chama na kumgombanisha mwanawe na uongozi wa chama chao.


Katika kauli yake ya juzi, Zitto alinukuliwa akiwaeleza watu walio karibu naye kuwa hata taarifa zinazoandikwa na vyombo vya habari kuhusu yeye ‘kumbeba' Kafulila zinamnukuu bila kumhoji yeye.


Lakini jana Kafulila alisema: "Huo ni uzushi unaotengenezwa…password (neno siri) ni kitu muhimu, tena ni siri ya mhusika, sasa iweje Zitto anipe password yake? Hayo ni maneno ya uzushi."

Wakati huo huo, aliyevuliwa cheo cha Ofisa Mwandamizi wa Sera na Utafiti wa CHADEMA, Juju Danda, jana alitangaza rasmi kujiunga NCCR-Mageuzi kama Kafulila.

"Nimefukuzwa bila kufuata sheria. Sijaridhishwa kabisa na maamuzi yale, ndiyo maana nikaona nitafute tumaini jingine ambalo ni NCCR-Mageuzi," alisema.
 
Watasikika wakisema,

Who is Zitto!

Hana impact yoyote ndani na nje ya CHADEMA!

Hata huko Kigoma, hana Wabunge na Madiwani wa CHADEMA!

CHADEMA ndiyo imemfikisha hapo alipo!

Chama hakiwezi kuruhusu wasaliti ndani ya chama!

CHADEMA kwa sasa ni imara zaidi baada ya kumuondoa kwenye uongozi!

Etcetera, Etcetera...

Mkuu kaangalie tena katiba ya CCJ!
 
Aende akavune alichopanda! Atarajie usaliti mwingi zaidi katika uenyekiti wake!
 
Tuone je watakapotokea akina Zitto wengi kwenye uenyekiti wake atatumia mbinu zipi kuwashughulikia tofauti na zilizotumiwa kumshughulikia akiwa CHADEMA, imbazo inaelekea hakuzifurahia.

Time will tell!
 
zitto ameifanya kigoma imekuwa dubai ya africa.. Hakika zitto ni kiongozi shupavu

allah kumbe dubai wanatumia umeme wa mafuta kama kigoma, hawana maji, kilomita zaidi ya 300 nyakanazi mpaka kigoma town hakuna lami kumbe nako dubai ndivyo jinsi kulivyo, watu hawana maji, eti??? Basi zito ni jembe, na kwa kuwa ni jembe lazima liwekwe mpini ndiyo liweze kulima,
 
Kwani bado yupo cdm. Akamfuate ufo huko huko che che me
 
kinyesi.
yaani hii toilet paper ya DJ mntarajia iandike la maana kuhusu mbunge mahiri na mwelidi Zitto? again hichi ni kinyesi, period.

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), inadaiwa yupo katika hatua za mwisho kujiengua ndani ya chama hicho alichojijengea sifa kubwa

Kwa mujibu wa watu walio karibu na Zitto, wamelidokeza Tanzania Daima Jumapili, kuwa mbunge huyo alipanga kujiondoa ndani ya chama hicho mwezi uliopita lakini alishindwa kufanya hivyo kwasababu ambazo hazijawekwa wazi.

Inadaiwa Zitto, alipanga kuondoka CHADEMA sambamba na uzinduzi wa kitaifa wa chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) uliopangwa ufanyike mwezi uliopita.

Novemba 22, mwaka jana, Kamati Kuu ya CHADEMA iliamua kumvua nyadhifa za uongozi Zitto na wenzake wawili (Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba) kwa madai ya kukisaliti na kukihujumu chama.

Zitto alidaiwa kuwa kinara wa mkakati wa kuleta mabadiliko haramu ndani ya chama hicho, huku waasisi hao wakijipa majina ya MM, M1 na M2 ambao ndani yake anadaiwa kuwamo Dk. Kitila Mkumbo, mjumbe wa CC na NEC.

Hata hivyo Mkumbo na Mwigamba walivuliwa uanachama huku Zitto akikimbilia Mahakama Kuu kutaka CC isijadili unachama wake.

Katika hoja ya msingi iliyowasilishwa na Zitto kupitia wakili wake Albert Msando, aliiomba Mahakama Kuu kuwazuia washitakiwa kwa pamoja ambao ni Kamati Kuu ya CHADEMA au chombo chochote kwa makusudi, kujadili au kuamua suala la uanachama wake.

Maombi mengine ya Zitto ni kutaka apatiwe nakala za uamuzi wa Kamati Kuu iliyoamua kumvua uanachama ili aweze kukata rufaa kwa Baraza la Uongozi la CHADEMA.

Katika ombi la tatu, Zitto anaiomba mahakama iwazuie washitakiwa kuingilia kati wajibu na majukumu yake ikiwemo majukumu yake kama mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Mahakama Kuu ilikubali kwa muda kusitisha uamuzi wa CC ya CHADEMA kujadili uanachama wa Zitto mpaka itakapotoa uamuzi wa katika kesi ya msingi iliyofunguliwa na mbunge huyo.

Katika amri hiyo, Jaji John Utamwa alisema kwa kuzingatia masilahi ya pande zote mbili ni vema walalamikiwa wakasitisha uamuzi wowote wa kujadili uanachama wa Zitto mpaka shauri hilo litakapotolewa uamuzi na mahakama.

Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa Zitto, anatarajia kwenda ACT-Tanzania kushikilia wadhifa wa Mwenyekiti wa chama hicho ambacho makada wenzake Mkumbo na Mwigamba wamekimbilia.

Harakati hizo za Zitto, zinadaiwa kushamiri zaidi hivi sasa baada ya CHADEMA kumaliza uchaguzi wake wa kitaifa na nafasi aliyokuwa akiishikilia imejazwa na John Mnyika

Kumalizika kwa uchaguzi wa CHADEMA, uliofanyika kwa utulivu hivi karibuni kunatajwa sababu ya Zitto kukata tamaa ya kurejea madarakani hivyo anaona njia pekee ya kujinusuru kisiasa ni kuhama CHADEMA.

Mbunge huyo kabla ya kukimbilia mahakamani alitaka kiitishwe kikao cha Baraza la Uongozi ili apewe fursa ya kujitetea ambako aliamini atapata uungwaji mkono

Hata hivyo tangu Zitto atoe ombi hilo Baraza hilo limeketi mara mbili bila kuwepo ajenda inayomuhusu kujadiliwa jambo lililoashiria hakukuwa na uungwaji mkono

Zitto afunguka

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, juu ya taarifa za kujitoa CHADEMA, Zitto alisema kwa muda mrefu kumekuwa na taarifa potofu dhidi yake.

Alisema baadhi ya taarifa zina lengo la kumchonganisha na kumharibia sifa yake mbele ya jamii na makada wenzake.

Zitto alisema jambo lolote linalomhusu hatosita kulizungumzia mwenyewe kama alivyowahi kufanya katika masuala mbalimbali.

Alisema kwa muda mrefu kumekuwa na mambo yanayovumishwa dhidi yake ambayo hayana ukweli

Zitto, alibainisha kuwa ikiwa ataondoka au ataendelea kubaki CHADEMA jambo hilo analijua mwenyewe.

“Watu wasema mambo kwa kuhisia hisia, mimi ndiye ninajua ninachokifanya……Hizo nyingine ni hisia za watu siwezi kuzizuia” alisema

“Nawaomba watu wajiepushe na maneno maneno ya mitaani, nina uwezo mkubwa wa kuzungumzia masuala yanayonihusu” alisema.

Dk. Slaa anena

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa, amesema ni haki ya kikatiba na ruhusa kwa mwanachadema yoyote kuhamia chama chochote cha siasa anachoona kinamfaa.

Dk. Slaa, alisema fununu za aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe, kutaka kujiunga na chama kipya cha ACT Tanzania, anazisikia na hawezi kumzuia kuhamia huko.

Alisema haoni kama anayo sababu yoyote ya kumjadili Zitto katika uamuzi wake wa kutoka CHADEMA na kuhamia chama kingine.

“S mimi Dk. Slaa wala CHADEMA, wanayo sababu yoyote ya kumjadili mtu na uamuzi wake mwenyewe …anayo haki ya kuhamia chama chochote ambacho ataona ana manufaa nacho, hana haja ya kupata kibali cha mtu”

“Zitto hatokuwa mwana- CHADEMA wa kwanza kuhama cha hiki na wala hatakuwa wa mwisho ….wengi watahama na wengi watahamia hivyo sioni kama kuna dhambi yoyote hapo” alisema

Katibu Mkuu huyo alisema kwa sasa hayuko tayari kuzungumzia mwanachama anayehama na kuhamia, bali yuko tayari kujadili maslahi ya Watanzania na nchi hasa suala la katiba iliyopendekezwa.

“Kichwa changu sasa kinafikiria ni namna gani kitawasaidia Watanzania waikatae katiba inayopendekezwa ambayo imechakachukuliwa kwa ajili ya manufaa ya watu wachache” alisema.


Chanzo: Tanzania Daima
 
Acha habari zako za kipuuzi... Chadema iko TZ nzima ona kusini tunashain. Lkn yawezekana we ni mwanae Kinainai
 
Back
Top Bottom