Zitto kung’oka CHADEMA

Zitto kung’oka CHADEMA

kuna maelezo ambayo umeyatoa umekuwa kama unashutumu upande mmoja kwamba umemuonea zitto lakini ukweli huu unaousema uko sahihi kabisa mimi nilipata taarifa hii kwa aliyekuwa katibu wa cdm huku niliko ambae alikuwa ni kibaraka wa zitto kuwa atatoka kwenye chama soon ili kuja kukijenga act lakini ugumu kwa jamaa ana hofu na mapokeo ya chama chake yanakatisha tamaa anaona kama ataacha ujira wake wa ubunge na kama mwenyekiti pac kwa kazi ambayo haina maana
 
Zitto akifanya hivyo atakuwa ametenda kwa busara. Lakini pia akifika kule ACT awaelimishe kuwa adui yao si CHADEMA au CUF au NCCR bali malengo yao makuu ni kuleta mabadiliko yatakayoifanya nchi kaendelea kwa kuhakikisha CCM au chama chochote kinachoshika serikali hakipati 'absolute majority' na kufanya watakavyo bila woga.

Hata hivyo natabiri ACT kuwa kama TLP na UDP labda itokee miujiza. Mwaka mmoja hautoshi kujenga chama kikapata mafanikio makubwa.
 
Kwani bado yuko cdm huyo Zitto. Kama bado kila la heri tena amechelewa kutangaza kuondoka. Sisi tunajua si mwanachadema zaidi ya saliti wa chadema.
 
Kwani bado yuko cdm huyo Zitto. Kama bado kila la heri tena amechelewa kutangaza kuondoka. Sisi tunajua si mwanachadema zaidi ya saliti wa chadema.
Me pia nimeshanga sana mkuu kumsikia me nilikuwa ninajuwa labda alisha kuwa mvuvi amekuwa kama gwadu aliyetokea bahari kaja nchi kavu harudi hko huko aliko kuwa kainamishwa kichwa tunawaza jinsi ya kuwatokomenza mafisadi papa hatumuwanzi mpiga ramli zitto
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), inadaiwa yupo katika hatua za mwisho kujiengua ndani ya chama hicho alichojijengea sifa kubwa

Kwa mujibu wa watu walio karibu na Zitto, wamelidokeza Tanzania Daima Jumapili, kuwa mbunge huyo alipanga kujiondoa ndani ya chama hicho mwezi uliopita lakini alishindwa kufanya hivyo kwasababu ambazo hazijawekwa wazi.

Inadaiwa Zitto, alipanga kuondoka CHADEMA sambamba na uzinduzi wa kitaifa wa chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) uliopangwa ufanyike mwezi uliopita.

Novemba 22, mwaka jana, Kamati Kuu ya CHADEMA iliamua kumvua nyadhifa za uongozi Zitto na wenzake wawili (Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba) kwa madai ya kukisaliti na kukihujumu chama.

Zitto alidaiwa kuwa kinara wa mkakati wa kuleta mabadiliko haramu ndani ya chama hicho, huku waasisi hao wakijipa majina ya MM, M1 na M2 ambao ndani yake anadaiwa kuwamo Dk. Kitila Mkumbo, mjumbe wa CC na NEC.

Hata hivyo Mkumbo na Mwigamba walivuliwa uanachama huku Zitto akikimbilia Mahakama Kuu kutaka CC isijadili unachama wake.

Katika hoja ya msingi iliyowasilishwa na Zitto kupitia wakili wake Albert Msando, aliiomba Mahakama Kuu kuwazuia washitakiwa kwa pamoja ambao ni Kamati Kuu ya CHADEMA au chombo chochote kwa makusudi, kujadili au kuamua suala la uanachama wake.

Maombi mengine ya Zitto ni kutaka apatiwe nakala za uamuzi wa Kamati Kuu iliyoamua kumvua uanachama ili aweze kukata rufaa kwa Baraza la Uongozi la CHADEMA.

Katika ombi la tatu, Zitto anaiomba mahakama iwazuie washitakiwa kuingilia kati wajibu na majukumu yake ikiwemo majukumu yake kama mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Mahakama Kuu ilikubali kwa muda kusitisha uamuzi wa CC ya CHADEMA kujadili uanachama wa Zitto mpaka itakapotoa uamuzi wa katika kesi ya msingi iliyofunguliwa na mbunge huyo.

Katika amri hiyo, Jaji John Utamwa alisema kwa kuzingatia masilahi ya pande zote mbili ni vema walalamikiwa wakasitisha uamuzi wowote wa kujadili uanachama wa Zitto mpaka shauri hilo litakapotolewa uamuzi na mahakama.

Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa Zitto, anatarajia kwenda ACT-Tanzania kushikilia wadhifa wa Mwenyekiti wa chama hicho ambacho makada wenzake Mkumbo na Mwigamba wamekimbilia.

Harakati hizo za Zitto, zinadaiwa kushamiri zaidi hivi sasa baada ya CHADEMA kumaliza uchaguzi wake wa kitaifa na nafasi aliyokuwa akiishikilia imejazwa na John Mnyika

Kumalizika kwa uchaguzi wa CHADEMA, uliofanyika kwa utulivu hivi karibuni kunatajwa sababu ya Zitto kukata tamaa ya kurejea madarakani hivyo anaona njia pekee ya kujinusuru kisiasa ni kuhama CHADEMA.

Mbunge huyo kabla ya kukimbilia mahakamani alitaka kiitishwe kikao cha Baraza la Uongozi ili apewe fursa ya kujitetea ambako aliamini atapata uungwaji mkono
Hata hivyo tangu Zitto atoe ombi hilo Baraza hilo limeketi mara mbili bila kuwepo ajenda inayomuhusu kujadiliwa jambo lililoashiria hakukuwa na uungwaji mkono
Zitto afunguka

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, juu ya taarifa za kujitoa CHADEMA, Zitto alisema kwa muda mrefu kumekuwa na taarifa potofu dhidi yake.

Alisema baadhi ya taarifa zina lengo la kumchonganisha na kumharibia sifa yake mbele ya jamii na makada wenzake.

Zitto alisema jambo lolote linalomhusu hatosita kulizungumzia mwenyewe kama alivyowahi kufanya katika masuala mbalimbali.

Alisema kwa muda mrefu kumekuwa na mambo yanayovumishwa dhidi yake ambayo hayana ukweli
Zitto, alibainisha kuwa ikiwa ataondoka au ataendelea kubaki CHADEMA jambo hilo analijua mwenyewe.

"Watu wasema mambo kwa kuhisia hisia, mimi ndiye ninajua ninachokifanya……Hizo nyingine ni hisia za watu siwezi kuzizuia" alisema

"Nawaomba watu wajiepushe na maneno maneno ya mitaani, nina uwezo mkubwa wa kuzungumzia masuala yanayonihusu" alisema.

Dk. Slaa anena

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa, amesema ni haki ya kikatiba na ruhusa kwa mwanachadema yoyote kuhamia chama chochote cha siasa anachoona kinamfaa.

Dk. Slaa, alisema fununu za aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe, kutaka kujiunga na chama kipya cha ACT Tanzania, anazisikia na hawezi kumzuia kuhamia huko.

Alisema haoni kama anayo sababu yoyote ya kumjadili Zitto katika uamuzi wake wa kutoka CHADEMA na kuhamia chama kingine.

"S mimi Dk. Slaa wala CHADEMA, wanayo sababu yoyote ya kumjadili mtu na uamuzi wake mwenyewe …anayo haki ya kuhamia chama chochote ambacho ataona ana manufaa nacho, hana haja ya kupata kibali cha mtu"

"Zitto hatokuwa mwana- CHADEMA wa kwanza kuhama cha hiki na wala hatakuwa wa mwisho ….wengi watahama na wengi watahamia hivyo sioni kama kuna dhambi yoyote hapo" alisema
Katibu Mkuu huyo alisema kwa sasa hayuko tayari kuzungumzia mwanachama anayehama na kuhamia, bali yuko tayari kujadili maslahi ya Watanzania na nchi hasa suala la katiba iliyopendekezwa.

"Kichwa changu sasa kinafikiria ni namna gani kitawasaidia Watanzania waikatae katiba inayopendekezwa ambayo imechakachukuliwa kwa ajili ya manufaa ya watu wachache" alisema.
 
zzk ameshndwa kusaidia jthada za kupata maji kgma kaskazn wanawake wanahangaika kusafir umbal mref kuyafuata maj ila leo mnamwta mtu maarufu?

Katumia muda mwingi kukijenga chama, shukurani yenu ikawa kumuwinda kama Swala.....shame on you.
 
Zitto ndio aliipa umaarufu Chadema. Bila zitto chadema ni sifuri
 
Chadema wanajua Zitto ndio ameshikilia uhai wa Chama..
 
Atoke tu, tunamtakia kila rakheri na wasaliti wenzake
 
Jina la Zitto likitajwa mtaa wa Lumumba huwa unaamka usingizini!

kaka c mtaa wa Lumumba peke ake hata mtaa wa Ufipa wana jamba kinoma.

kwan zitto akiondoka chadema kuna dhambi gani?..kwan hao wanao mwita msaliti c walitoka CCM?

Au usaliti ni kutoka chadema kwenda vyama vingine na si kutoka vyama vingine kuingia chadema?

komaeni basi kisiasa mbona hambadiliki kimawazo?
 
Mnajifariji..zitto amekimegua chadema kimebaki mapande mapande..

Alaah kumbe bado chadema kimebaki kinapumua , niliamini kimekufa kama ambavyo mzee wako wa gombe na gaidi mwizi wa vyeti vya watu mwigulu alivyowaaminisha wapuuzi wenzake wa sisiemu kuwa wampe cheo eti aiue chadema kabla ya 2013.. Poleni sana

zitto angekuwa na akili mwandiga kwake angeshindwa hata kutumia fedha za mfuko wa jimbo kuchimba visima , mwandinga, mkongoro, hadi kalinzi yote maji ni shida watu wanatumia maji ya mto, unalijua jimbo lake?? au unabwata tu hapa... labda anaakili kukuzidi wewe....
 
zitto ndio aliipa umaarufu chadema. Bila zitto chadema ni sifuri

mwambieni aje chama chenu cha maauaji mpe uenyekiti ili chama chenu kizidi kung'aaa kwa wizi na rushwa, maana adui yako muombe njaaa, so kama ndiye alikipa umaarufu chadema na watu hawamthamini.. Sasa nyinyi mnaompenda bwana wenu mchukueni ili chadema kife,......, usilete siasa za maji taka hapa... Ameshindwa hata kuchimba visima jimboni kwake, hakuna maji anzia mwandiga yote, bitale, mkongoro hadi kalinzi njoo mpaka nyarubanda, hata umeme hayo maeneo hakuna... Sasa mtu akama alishindwa hataa kutumia mfuko wa jimbo tu kuchimba visima kwa miaka yoote hiyo bado ni wa maana huyo na maeneo yake hayo yana mito mingi tu, hata water table ipo karibu... Umefika jimbo lake?? Sasa niko huku.. So anaongea nacho kijua..... Mkuu usiongee tu kuonekana umechangia il;i nape mwandosya...akupe buku 7.. Ongea vitu harisi....
 
Until when mtazunguzia suala hili? Mnataka kuendelea kumpunguzia Umaarufu? Msimtajetaje...

Sio chochote kwenye Siasa ya NCHI ya TANGANYIKA labda kwa SIASA za kulazimisha ubaguzi za KIGOMA...

Our Country POLITICS is tired na Greedy POLITICIANS!!!!!!!!!

Hamna watu nilipata kuwaamini humu kama wewe, kumbe nawe unahubiri siasa za ukabila, amekosa mtu sio Kigoma, na kama kigoma ndio mwathirika wa siasa za usariti basi mjitazame upya, kwanini kila siku ninyi, nilipata kuongoza seriksli moja ya wanafunzi chuo kikuu, msaidizi wangu alikuwa dada wa kigoma baada ya mgomo akaniruka hatua 100, hili nalo tusiseme, kuna tatizo Kigoma jamani kwenye misimamo. Sorry kama ntamkwaza mtu
 
Back
Top Bottom