Makambako1
Member
- Jan 17, 2020
- 25
- 38
Na Moses Machali
Nimepitia tweet yako inayo circulate mitandaoni Mhe Zitto Kabwe kuhusu deni la taifa ukijaribu kuamisha watu kuwa huenda ni Tanzania pekee inayokopa duniani. Kwa ufupi sana hali ya madeni kwa baadhi ya nchi ikihusianishwa na ukubwa wa uchumi wao kwa mujibu wa
tovuti ya:
www.worldpopulationreview.com/countries/countries-by-national-debt/
ni kama ifuatavyo:
Japan ndiyo taifa lenye deni kubwa ikilinganishwa na ukubwa wa uchumi wake (yaani Debt to GDP Ratio of the country). Nchi hii ina deni la Dola za marekani 9.087 trilion sawa na 234.18% ya uchumi wake.
Tanzania tuna deni la 36.5% ya GDP yetu. Sasa usishangae Tanzania kukopa na kufanya mambo makubwa kama inavyoonekana chini ya serikali hii ya awamu ya tano.
Nchi nyingine wana madeni makubwa kama ifuatavyo:
Canada inadaiwa Dola 925 billion sawa na 83.81% ya DGP ya nchi hiyo.
Ujerumani ina deni la Dola za Kimarekani 2.527 billion sawa na 59.81%.
Kwa hiyo upotoshaji mwingine haufai kwa sababu tu mtu ana chuki na kiongozi wa Fulani wa nchi. Siyo ajabu nchi au mtu au Kampuni kukopa bali suala au hoja ya msingi ni je, nchi au mtu au Kampuni inakopa kwa ajili ya kufanya nini?
Serikali kwa niaba ya taifa ikikopa na kujenga miundombinu ya Msingi kama inavyofanya hivi sana serikali siyo dhambi. Kwa hiyo Zitto uache kujaribu kupotosha kuwa deni la taifa ni kana kwamba halina manufaa kwa nchi yetu. Rudi kwenye msitari.
Pengine tueleze iwapo deni la taifa limefanya mambo makubwa au halijfanya mambo makubwa katika nyanja mbalimbali?
Wanakopa nchi Tajiri duniani sembuse sisi Tanzania? Canada wanakopa, Marekani, Ujerumani, Uingereza, Ubeligiji, China, nk wanakopa. Hata jirani zetu wa Kenya wana deni la 55.50% ya Ukubwa wa uchumi wao huku Tanzania tukiwa na deni la 36.5% ya ukubwa uchumi wetu.
Muwe na siku njema
Moses J. Machali
15/02/2020
Soma: Mkopo wa SGR wa tril 3.3 kwa riba ya 9% kwa miaka 20 tutalipa jumla ya zaidi ya Tshs Tril 7.36 huku riba ikiwa tril 4.06