Zitto Kabwe, usipotoshe watu kuhusu Deni la Taifa

Unafananisha Japan na Tanzania?

Japan itaendeleea kukopeshwa, hata kama deni Lake ni sawa na uchumi wake,

Japan uchumi wake unajulikana, Japan ni nchi ya Viwanda..

Tanzania, nchi zinazotukopesha zitakatika tamaa, Tanzania uchumi wake haujulikani, sio nchi ya Viwanda wala kilimo,

Tanzania ni nchi tegemezi,inategemea mikopo ili kuendesha mambo yake..

Tuombe hawa wanaotupa mikopo wasije wakasusa kutukopesha..

God. Bless TZ
 
Zitto hapo hajafanya kosa lolote maana nyinyi wenyewe mlituambia tena kwa kujigamba kuwa hamna haja ya kukopa kwani ni matajiri sana na mna mapesa mengi.

Sasa leo hii tunaambiwa kuwa deni la taifa linakimbia kama na karibu tutaingia kwenye red line yaani kutokopesheka.

In God we Trust
Mzee anateseka na mikopo vibaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitu ambacho watu tunashindwa kujua no kuwa deni LA Japan au Marekani au nchi yoyote iliyoendelea wana madeni ya ndani, wakati sisi madeni tunayo ya ndani na ya nje. Deni LA ndani halina madhara makubwa kama deni LA nje.

Mfano serikali yetu ilikopa sana kwenye mashirika ya hifadhi,Pspf na kadhalika. Deni LA ndani hata lizidi 100% bado ni himilivu kwa maana hata ukilipa mzunguko Wa fedha unaongezeka nchini. Lakini deni LA nje unapolipa unahamisha fedha yote uliyokusanya kuwalipa mataufa nje na hapo unaua mzunguko Wa fedha nchini mwako.

Sasa tuchukue mfano mdogo Tanzania inakusanya 1300 bilioni kwa mwezi kodi ,lakini inalipa 700 bilioni. Ina maana kuwa zaidi ya nusu ya makusanyo yetu tunalipa kwenda kwa hao tunaowaita mabeberu, madhara yake uchumi unasinyaa.

sasa tufikirie kuwa deni tunaongeza Mara mbili ya Leo , maana yake makusanyo tutapeleka nje. Kwa hiyo hija sio ukubwa Wa deni , Bali in deni toka wapi. Ikifika mahali serikali inakopa ili ilipe mishahara, tujue deni likzidi ndio hapo nchi inakuwa rehani. Kuna MTU alishasikia Marekani na ujerumani au Japan inakpoa world bank au AfDB?

Wao ndio wanatoa hizo fedha tunazokopa WB na IMF. Halafu MTU mzima unajilinganisha na Mataifa wanaokopesha mashirika tunayokopa kwao ili tuendeshe mambo yetu. Tafadhali tusumbue akili yetu kabla ya kupost. Tafadhali kama hujui kitu acha kufurahisha soga. Hivi mnadhani Rais anapokiri Kazi ya urais no ngumu anamaanisha nini?

Ni pale matumizi ya serikali yanapozidi mapato na bado Kila taasisi inahitaji mgao. Mlishasikia bajeti hewa huko Japan? Sisi tunapangia wizara fedha kiasi Fulani halafu mwisho Wa mwaka zinapelekwa 27% fedha ya maendeleo . sababu tunakusanya kulipa mabeberu na mashirika yao.

TUSIJIFARIJI KWA KUJILINGANISHA NA NCHI WAFADHILI WA DUNIA. TUTAPOTOSHANA. MADENI YAO NA YETU NI TOFAUTI MNO. JUAN MANUEL,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nafasi uliyipewa ya kulamba miguu ya watu na kuwasafishia viatu,unafikili ungesemaje?lazima ugeuke kuwa msemaji wa Serikali ili kulinda tumbo lako,sasa hivi kila mtu ni msemaji wa Serikali.
 
Sasa upotoshaji wa Zito uko wapi? Mi nilidhani unakuja na data kuwa hatuna deni! Maan Zito kasema tunadaiwa, hakasema kama ni sisi tu ndiyo tunakopa.
Pengine zito katoa hizo data kwasababu serikali huwa inasema miradi yote inatekelezwa kwa fedha zetu, lakini kumbe huwa tunapigwa kamba, au ndiyo siasa yenyewe? Makambako1,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikutaka kushiriki huu mjadara nikijua kua mleta mada labda elimu ya Uchumi kwake ni ndogo.Lakini badae nikaenda mbali na kufuta kua ni msomi....Hizo nchi ulizotaja na kuringanisha na Tanzania katika ukopaji sijui kama umejiridhisha.

Japan, Canada,Marekani na Ujerumani ni kweli wanakopa...lakini pia wanazikopesha nchi nyingine, taasisi na zaidi wanatoa misaada.Sasa sijui unaringanisha nini hapo.

Ninadaiwa na Benki shililingi milioni 10 ila kuna watu ninaowadai jumla ya milioni 18 pia natoa msaada wa milioni moja kila mwezi.
Machali you're to low
 
Hivi angekata kakifungu kwenye kile kishika uchumba cha ACACIA si huu mkopo tungeona ni wazimu kuuomba?? Jamani viongozi, chungeni maneno mnayosema kwa watu mnaowaongoza. Ni hilo tu
 
Issue no kuelimishana sio upinzani dhidi ya watawala. Mtazamo finyu unaweza ukafubaza tafakuri. Nchi ikiingia zahama tunaathirika wore bila kujali itikadi yako. Tumo jahazi moja. Likizama tumeangamia haijalishi chama chako.
Wachangiaji wa hii mada toka upinzani wana hasira na mihemuko ya kisiasa na hawajaelewa mada. Ndio maana waliitwa nyumbu malofa na wapumbavu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom