Zitto Kabwe: Usiku wa kuamkia leo ulikuwa mgumu zaidi kwenye maisha yangu ya kisiasa

Huu utamaduni wa kikatili, chuki na visasi ulianza rasmi October 2015.

wewe uliandika haya! unakumbuka maumivu aliyoyapata dr ukimboka? unakumbuka tukio alilofanyiwa kubenea la kumwagiwa tindikali na vifaa vyake kuchukuliwa? unakumbuka alichofanyiwa ablasoom kibanda kutobolewa macho? na mwisho kabisa, unakumbuka alichofanyiwa chacha wangwe??? leo yupo wapi?

unaposema matukio ya kikatili yalianza october 2015 unajitoa ufahamu au wewe ni mtoto wa miaka 2 haukuwepo enzi hizo????
 
  • Thanks
Reactions: SDG

Niwe na miaka miwili au mmoja it does not matter ila ninachojua ni kuwa huu utamaduni wa chuki, fitna visasi na ukatili ulianza rasmi October 2015.
 
[HASHTAG]#HuuSiUtanzania[/HASHTAG]

Usiku wa kuamkia leo ulikuwa mgumu zaidi kwenye maisha yangu ya kisiasa.

Nimetumia muda mwingi nikitafakari na kumfikiria sana mwanasiasa mwenzangu, kaka yangu, mbunge mwenzangu na rafiki yangu Tundu Antiphas Lissu.

Siku zote, katika maisha yetu ya kisiasa, hata katika mambo tunayotofautiana na kupingana nimekuwa nikiamini kwa dhati kwamba tofauti hizo haziwezi zikatufanya tukashindwa kuvuka salama kama Nchi, Kama Taifa.

Kilichotokea na kumpata ndugu yetu Lissu jana, ni kitendo cha kihalifu na kisichoendana kabisa na utamaduni wetu wa ustahimilivu na udugu ambao nchi yetu imekuwa ikisimamia.

Kitendo kile cha kikatili kinakwenda kinyume kabisa na misingi ya utaifa wetu ambao tumekuwa tukiujenga kwa miaka 25 sasa kwa kuwa na taifa huru kidemokrasia.

Wakati tukimuombea Lissu kupona kwa haraka, Watanzania tunaolitakia mema taifa hili tuna kila sababu ya kulaani na kukataa kabisa utamaduni huu wa kimafia kuzoeleka katika taifa letu.

Tusimame kulaani kwani [HASHTAG]#HuuSiUtanzania[/HASHTAG]

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Septemba 8, 2017

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaandika Mbunge Zitto Kabwe.
[HASHTAG]#HuuSiUtanzania[/HASHTAG]

Usiku wa kuamkia leo ulikuwa mgumu zaidi kwenye maisha yangu ya kisiasa.

Nimetumia muda mwingi nikitafakari na kumfikiria sana mwanasiasa mwenzangu, kaka yangu, mbunge mwenzangu na rafiki yangu Tundu Antiphas Lissu.

Siku zote, katika maisha yetu ya kisiasa, hata katika mambo tunayotofautiana na kupingana nimekuwa nikiamini kwa dhati kwamba tofauti hizo haziwezi zikatufanya tukashindwa kuvuka salama kama Nchi, Kama Taifa.

Kilichotokea na kumpata ndugu yetu Lissu jana, ni kitendo cha kihalifu na kisichoendana kabisa na utamaduni wetu wa ustahimilivu na undugu ambao nchi yetu imekuwa ikisimamia.

Kitendo kile cha kikatili kinakwenda kinyume kabisa na misingi ya utaifa wetu ambao tumekuwa tukiujenga kwa miaka 25 sasa kwa kuwa na taifa huru kidemokrasia.

Watanzania tunaolitakia mema taifa hili tuna kila sababu ya kulaani na kukataa kabisa utamaduni huu wa kimafia kuzoeleka katika taifa letu.

Tusimame kulaani kwani [HASHTAG]#HuuSiUtanzania[/HASHTAG]

Hakuna aliyelala kaka Zitto, hata watesi wa ndugu yetu Lissu nao hawakulala kwasababu mpango wao muovu ulifeli kwani Mwenyezi Mungu alisimama katikati na kuonyesha ukuu wake.
 
Huyu bwana mchiyemba ukimuangalia machoni anavyoongea....anajishtukia kabisaa...hana amani kabisa
 
Waislamu wanafundishwa kwamba sadaka inarefusha umri wa mwanadamu! Kilichomnusuru Lissu na kifo ni sadaka yake anayoitowa kwa wapenda haki kwa kutetea kwa nguvu zake zote kwa kutumia elimu na kipaji chake dhidi ya dhulma na uvunjwaji wa sheria. Bila ya kujali rangi, dini, kabila, au mrengo wa mty wa siasa.

Hiyo ni sadaka tosha kwake kumnusurisha kifo!
 
Aache unafiki, huwezi kula hela za mzungu ili umtetee then asikuue. Kinachotokea sasa inawezekana kuwa lissu na wenzake walikula hela za acacia ili wawatetee acacia bungeni na kwingine, na wakajitahidi na kununua baadhi ya media, na wakaona lisu ameweza kuwa mtumishi wao wa kweli na wazungu hao wanaona azima yao imeshindwa maana wanafungasha virago hao acacia basi wakaamu kulipiza kisasi kwa kumtwanga risasi. zzk aache kujipendekeza kwa wazungu, wazungu ni wauaji, hilo ni somo kwa wapinzani
kizuri ni kwamba kila nafsi itaionja mauti tofauti ni nyakati tu! na kama kweli hukumu ipo basi kila mmoja atajibia katika yale aliyo watenda wengine , mara nyingi mtu akisha patwa na baya huwa tunaanza na yule mbaya wake wa wazi na mbaya wa wazi kwa T.Lissu ni serikali hii , sikuwahi kusikia mgogoro wa lisu na hao acacia nadhan mpo kazini kujaribu kukiepusha kikombe hiki na serikali maana naona hoja zinazotoka upande wenu ni nyingi kwa hakika lakin mjue ya kuwa mwafanya kazi bure maana dunia nzina yajua adui wa T.Lissu ni yupi.na uzuri wanao huwa nao kuna wakati wao mungu atawaita pia maana wapo walio ua zaid na zaid na hawakuishi milele kamwe
 
kizuri ni kwamba kila nafsi itaionja mauti tofauti ni nyaka tu! na kama kweli hukumu ipo basi kila mmoja atajibia katika yale aliyo watenda wengine , mara nyingi mtu akisha patwa na baya huwa tunaanza na yule mbaya wake wa wazi na mbaya wa wazi kwa T.Lissu ni serikali hii , sikuwahi kusikia mgogoro wa lisu na hao acacia nadhan mpo kazini kujaribu kukiepusha kikombe hiki na serikali maana naona hoja zinazotoka upande wenu ni nyingi kwa hakika lakin mjue ya kuwa mwafanya kazi bure maana dunia nzina yajua adui wa T.Lissu ni yupi.
Serikali ina taratibu zake za kuua. Kwanza unapelekwa mahakamani, then kesi, ukipatikana na hatia kama ni kosa kubwa unahukumiwa kunyongwa, na rais hutia saini, basi hapo utanyongwa hadi kufa, kwa hiyo suala la lissu ni la wapinzani
 
Back
Top Bottom