Zitto Kabwe: Usiku wa kuamkia leo ulikuwa mgumu zaidi kwenye maisha yangu ya kisiasa

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Anaandika Mbunge Zitto Kabwe.
[HASHTAG]#HuuSiUtanzania[/HASHTAG]

Usiku wa kuamkia leo ulikuwa mgumu zaidi kwenye maisha yangu ya kisiasa.

Nimetumia muda mwingi nikitafakari na kumfikiria sana mwanasiasa mwenzangu, kaka yangu, mbunge mwenzangu na rafiki yangu Tundu Antiphas Lissu.

Siku zote, katika maisha yetu ya kisiasa, hata katika mambo tunayotofautiana na kupingana nimekuwa nikiamini kwa dhati kwamba tofauti hizo haziwezi zikatufanya tukashindwa kuvuka salama kama Nchi, Kama Taifa.

Kilichotokea na kumpata ndugu yetu Lissu jana, ni kitendo cha kihalifu na kisichoendana kabisa na utamaduni wetu wa ustahimilivu na undugu ambao nchi yetu imekuwa ikisimamia.

Kitendo kile cha kikatili kinakwenda kinyume kabisa na misingi ya utaifa wetu ambao tumekuwa tukiujenga kwa miaka 25 sasa kwa kuwa na taifa huru kidemokrasia.

Watanzania tunaolitakia mema taifa hili tuna kila sababu ya kulaani na kukataa kabisa utamaduni huu wa kimafia kuzoeleka katika taifa letu.

Tusimame kulaani kwani [HASHTAG]#HuuSiUtanzania[/HASHTAG]
 
Huu utamaduni wa kikatili, chuki na visasi ulianza rasmi October 2015.
 
MImi binafsi baada ya kumuona usiku Airport akipandishwa ndege akiwa kwenye machela huku ametundikiwa drip ya damu na kifaa nilichohisi kitakuwa labda ni life supporting machine, kwakweli usiku wa leo sikulala kabisa.

Wabunge na wananchi wengine tulikuwa kama tumepigwa ganzi kila mtu haamini macho yake.

Mbowe,Msigwa na mke wa Lissu ndio waliondoka na mgonjwa.

Kuona na kusikia ni vitu viwili tofauti kabisa.
 
Kilichotokea na kumpata ndugu yetu Lissu jana, ni kitendo cha kihalifu na kisichoendana kabisa na utamaduni wetu wa ustahimilivu na undugu ambao nchi yetu imekuwa ikisimamia.
Mwangosi aliuawa na nani na vipi? Ben Saa nane yupo wapi? Mawazo alikufaje na baada ya kifo chake kilifuata nini? Ulimboka, Kibanda hao ni wachache tu. Tuache porojo za kusema kisiwa cha amani wakati tunaishi kikondoo!!!! Unafiki ndo unatufanya tujidanganye eti kisiwa cha amani. Je, wangekuwa wanaruhusu kuandamana kupinga hivi vitendo, wangapi wangeingia barabarani leo? Walinzi wanasubiri mtu ajitokeze hapo ndo washa washa zinatoka mapangoni, na kila aina ya silaha.
 
zitto wewe ni oportunist, huna nia ya dhati na nchi hii. Mungu amsimamie lissu apone mapema arejee kwenye majukumu yake ya kila siku
 
Eti [HASHTAG]#huusiutanzania, [/HASHTAG]Zitto bwana, haka kajamaa sijuwi kama kanajitambua kwa kweli. Hivi Zitto ana uzalendo gani na nchi yake?
 
Hata kwangu huu usiku uliopita ulikuwa mgumu katika uzoefu wangu kama raia anayefuatilia maendelea ya kisiasa na kidemokrasia nchini. Hapakuwa na lolote nililoweza kufanya kando ya kuongozwa na roho ili kufanya maombi kwa Mungu; TAL apone kabisa na kurejea kwenye afya yake.

Hata mimi naingana na ZZK kulaani kwa nguvu zangu zote unyama aliofanyiwa TAL. Bila kuwa na maana ya kusonda kidole kwa yeyote, siamini kama raia wa kawaida anaweza kufanya shambulizi lile bila kuwa na motive ya kisiasa. Niwaase wenye chuki binafsi kumalizana na TAL mahakamani; na wenye chuki za kisiasa kwa kutofautiana na TAL kiitikadi kwa namna yoyote ile, wasijitafutie laana.

Nawaomba watanzania wote bila kujali itikadi zetu na kwa kuzingatia utu wa mtu, tumwombee TAL kwa Mola na pamoja nasi asukume maendeleo ya kisiasa na kidemokrasia.

Mungu ibariki Tanzania!

"The greatness of any nation lies in its fidelity to the constitution and strict adherence to the rule of law and above all respect to God" - CJ David Maraga
 
Anaandika Mbunge Zitto Kabwe.
[HASHTAG]#HuuSiUtanzania[/HASHTAG]

Usiku wa kuamkia leo ulikuwa mgumu zaidi kwenye maisha yangu ya kisiasa.

Nimetumia muda mwingi nikitafakari na kumfikiria sana mwanasiasa mwenzangu, kaka yangu, mbunge mwenzangu na rafiki yangu Tundu Antiphas Lissu.

Siku zote, katika maisha yetu ya kisiasa, hata katika mambo tunayotofautiana na kupingana nimekuwa nikiamini kwa dhati kwamba tofauti hizo haziwezi zikatufanya tukashindwa kuvuka salama kama Nchi, Kama Taifa.

Kilichotokea na kumpata ndugu yetu Lissu jana, ni kitendo cha kihalifu na kisichoendana kabisa na utamaduni wetu wa ustahimilivu na undugu ambao nchi yetu imekuwa ikisimamia.

Kitendo kile cha kikatili kinakwenda kinyume kabisa na misingi ya utaifa wetu ambao tumekuwa tukiujenga kwa miaka 25 sasa kwa kuwa na taifa huru kidemokrasia.

Watanzania tunaolitakia mema taifa hili tuna kila sababu ya kulaani na kukataa kabisa utamaduni huu wa kimafia kuzoeleka katika taifa letu.

Tusimame kulaani kwani [HASHTAG]#HuuSiUtanzania[/HASHTAG]
Kwa hiyo unahusisha tukio la kushambuliwa lissu na siasa? Kwa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom