Ndugu Mukandara,
Hoja yako kuhusiana na maada hii ni ya msingi kabisa. Kama alivyoeleza Ndugu Soby, Tanganyika ilikuwa Mandated Territory. Hii inamaanisha Jamii ya Kimataifa (wakati huo League of Nations) iliipa Uingereza madaraka ya kisheria ya kuindesha Tanganyika kwa niaba yake hadi hapo Watanganyika wagelikuwa tayari kujitawala wenyewe.
Kwa hiyo, kama mtoa hoja hiyo alivyosisitiza, Waingereza walikuwa wakiripoti huko huko kwenye League of Nations, kuhusu maswala yote ya Tanganyika. Kadhalika, hii inaeleza kwa nini wakati wa kudai uhuru (kumradhi kwa wale wanaopendelea neno 'kupigania' uhuru) Mwalimu Nyerere alikwenda makao makuu ya League of Nations huko Marekani badala ya kwenda Uingereza kwa shughuli hiyo.
Swali sasa ni ilikuwaje miaka 50 baada ya kujitawala tunajikuta katika hali hii? Kwa miaka hii 50 taifa letu limekuwa likiishi (na linaendelea kuishi) kwa misaada kutoka mataifa ya nje wakati mataifa mengine ya Kiafrika kama vile Botswana na Mauritius yamefanikiwa kuinua hali za maisha ya raia wake; na muhimu zaidi, hayatembezi mabakuli yakiomba kutoka Stockholm hadi Pyongyng. Siyo hiyo tu bali Tanzania ina rasilimali nyingi mno kiasi kwamba ikitumia rasilimali hizo vizuri, inaweza kujitegemea katika kipindi kifupi cha miaka 10. Ilikuwaje?!
Je, Waingereza wangelikuwa wanapenda kujibu maada hii si wangelisema: 'Ehe! Nyie vipi, hamuoni pesa ambazo tumekuwa tukiwapeni kusapoti bajeti na miundo mibinu yenu, kwa miaka hiyo yote, ni zaidi ya reparation mnayo zungumzia hivi sasa?'; na pengine wangeliongeza: 'Hivi inakuwaje mnalaumu kunguru kwa kushuka nchini mwenu na kudonoa mzoga kabla ya kulaumu mazingira yaliyo sababisha mzoga kuwepo katika nafasi ya kwanza. Hamjui kuwa bila mzoga kuwepo, kunguru hashuki? Come on be fair! Sisi Waingereza tunaongoza nchi yetu kulingana na maslahi ya taifa letu, na siyo yenu, na wala sisi siyo Mother Tereza au charity organisation ya namna fulani. Sisi ni taifa, linalowajibika kwa mlipa kodi wa nchi hii na ambaye ni chanzo cha fedha ambazo tumekuwa tukikupeni miaka nenda-rudi. Hivi mlizitumiaje hela hizo? Mliendeleza a luta continua tu kwa gharama ya maendeleo ya taifa lenu au vipi? Tafadhali, msitulaumu kwa matumizi mabaya au udokozi wa fedha za misaada tuliyokupeni' wangelimaliza hoja yao.
Ninakili lkwamba kwa sababu za kidiplomasia na maslahi-tajwa, Waingereza wasingeliweza kusema hiivi bayana. Wao wanafahamu vizuri zaidi namna ya kudili na watawala mafisadi wa mataifa changa; mafisadi wanaotumia nyadhifa zao kujilimbikizia mali kwa gharama ya mnyonge. La zaidi, wanafahamu fika kwamba viongozi mafisadi wa Kiafrika hupenda sana kufanya yale wafadhili wanayopenda kwa imani kwamba, kwa kufanya hivi, wafadhili hawatawabana warejeshe kwa wananchi utajiri waliopata visivyo halali (na bila kujirudia walioupata kwa kutumia nyadhifa zao). Isitoshe, wanafahamu fika kuwa hiki ndicho chanzo cha siasa nchini Tanzania kuwa ni biashara kubwa na ya aina yake na wala siyo art, kama inavyopashwa kuwa. Kadhalika wanafahamu kuwa mali nyingi viongozi mafisadi waliyonayo, mara nyingi, huificha huko kwao.
Lakini mbali ya ufisadi, sababu nyingine zilizotufikisha hapa tulipo zinafahamika kwa wana JF, hakika. Je, hatukuelewa tangu mwanzo kwamba services sector iki exert pressure kwenye sekta ya kuzalisha tungeliweza kuwa na matatizo kama haya? Je, tulitumia muda mwingi kupambana na adui wetu, kinadharia, badala ya kutumia muda huo kujenga uchumi wenye nguvu kama njia pekee ya kupambana na ubeberu?
Ni kwa kiasi gani tulitazama mbele? Mathlan, hatukujua kwamba miundo mbinu tuliyoirithi wakati wa ukolloni, wakati idadi ya Watanzania ikiwa ndogo, isingelistahimili idadi kubwa ya watu inayoongezeka kila mwaka huko siku za mbeleni? Tulijiandaa vipi katika hilo? Je, hatukujua kwamba sisi kama wakulima wa pamba, wakubwa wakibuni synthetic, pamba yetu isingelikuwa na soko na kwa hiyo kuathiri uchumi wetu? Tuilidhani kama hali hii ingelitokea (kama ilivyotokea) pamba yetu tungeliifanyaje? Tuile?
Na teknolojia je? Hatukuelewa kwamba dunia inayotawaliwa na mifumo ya biashara na uzalishaji wa bidhaa ikivumbua vitu vipya kama Inernet, mathlan, itaua kwa kiasi kikubwa huduma za posta na watu wengu kupoteza ajira zao? Tulijiandaaje, kwa vitu vya namna hii kama taifa? Kwa maana wakubwa kule kwao, hawawezi kusitisha kukua kwa teknolojia yao kwa kuyafikiria mataifa ya wakulima na wafanyakazi kama yetu. Wajibu huo ni wa mataifa yetu na viongozi wake.
Na hili suala la Afrika kuzalisha isichotumia, na kutumia isichokizalisha, tulilishughulikiaje kama taifa? Maana kiongozi wa kitaifa kuwashauri wananchi ni nini cha kupanda na lini, peke yake hili halimalizi tatizo hili sugu. Na hili suala la rushwa tulidhani tutalimalizaje? Kuwapiga viboko watoao na kupokea rushwa ili waende waonyeshe wake zao? Je, tulipofanya hivyo kwa nini basi hatukufanikiwa kumaliza tatizo hili sugu?
Je, wazungu katika mataifa ya Magharibi ambapo kupigwa viboko mtu ni mwiko, mbona hawana rushwa kama sisi? New Zealand, Denmark, Norway, Iceland n.k kati ya mataifa yanayoongoza kutokuwa na rushwa, walifanikiwaje kutokuwa na wala rushwa katika jamii zao wakati kuwapiga watu viboko ni mwiko kwao?
Je, inawezekana waliopigwa viboko baadaye wakawapiga wengine mapanga; wanaopigwa mapanga kuwapiga wengine mashoka; wanaopigwa mashoka kuwapiga wenzao tindikali, na vitu kama hivyo? Ni kwa nini Wazungu hawapendi kuwapiga viboko raia wake na sisi tuifanye kama sera ya siasa? Kwa nini tunatofautiana katika mambo kama haya? Je, values za Wazungu; ambazo ndio msingi wa mataifa yao yalipojengwa; ndilo jambo mojawapo lililowafanya Wazungu wasonge mbele kijamii na kiuchumi kuliko sisi?
Vyuo vikuu ni ni chem-chem ya fikra mpya kwa taifa lolote; je, tunawatumia kiasi gani wataalamu wetu vijana katika kuushauri uongozi wa kisiasa katika maswala ya namna hii? Ukoloni unaweza kuwa umechangia kwa kiasi fulani katika hali yetu, kama watoa hoja wengine walivyoonyesha, lakini pengine ni vyema tutahadhari tusije kuwa watumwa wa historia yetu. Tukifikia hali hiyo, tunaweza kudhurika maradufu.
'Many people...want to punish you for speaking the truth, for being correct, for being you. Never apologise for being correct, or for being years ahead of your time. If you are right and you know it, speak your mind. Speak your mind even if you are a minority one. The truth is still the truth'-Mohandas Gandhi
All said ukweli utabakia kwamba hii misaada wanayoitoa ni aibu yao wenyewe kama reparation...Can't fool me! huwezi nambia Muingereza ana huruma saaana kutusaidia sisi wakati anatumia - When we were rulers they were better off! Hizi ndio story nazisikia sana kuhusu Oman na Zanzibar ati Zanzibar ilikuwa imeendelea sana chini ya Sultan na wajinga wanaamini wanataka kuvunja muungano bora warudi kwa Sultan. Hii misaada yote anayoahidi ni aibu ya kukoloni watu ati huruma!.
Siwezi kumsemea Zitto lakini size yake kuwaambia They can stick that shit in their ashakum!...huwezi kumsaidia mtu na matusi juu ukitegemea sisi tutakaa kimya kama tulivyotukanwa na Israel..