Ragamuffin
Senior Member
- May 2, 2009
- 160
- 6
Ndugu zangu. Nadhani ni hekima kujua Jambo kwa kina kabla ya kuanza kulitolea maneno na hukumu. Ninaomba kuelewa kifupi sana nini kilitokea huko twitter.
Kuna mama anaitwa Sarah. Mwingereza ambaye pamoja na mume wake waligombana na Benjamin Mengi kuhusu mashamba yanayoitwa sasa Silverdale Farms.
Ugomvi huu ulikuwa mkubwa na kuripotiwa mpaka katika Bunge la Uingereza. Huyu mama sasa hivi ameufanya Ugomvi ule binafsi na wa kibiashara kati yake na kina Mengi kuwa ni Ugomvi dhidi ya Watanzania wote. Amekuwa akiandika makala mbalimbali za kuichafua Tanzania. Amekuwa akitaka Serikali ya Tanzania imlipe yeye na mumewe fidia kwa makosa ya raia mmoja wa Tanzania anaitwa Benjamin Mengi.
Huyu mama na mumuewe hakuwahi kujiandikisha TIC ili kujua uwekezaji wake kwenye shamba na hata kupata protection ya kisheria. Sasa juzi kaandika makala kuhusu aid dependence ya Tanzania (Jambo ambalo ni la kweli) lakini akaweka takwimu nyingi sana za uwongo ambazo Watanzania wamezidaka na kuzizungumza Kama za kweli hivi. Baadhi yetu tukamwambia through twitter kwamba takwimu sake sio sahihi.
Pili tukamwambia alipaswa kusema Kama note katika makala yake kwamba yeye ana kesi na Serikali ya Tanzania. Kwamba yeye amekuwa akiilazimisha nchi yake ya Uingereza iinyime muswada Tanzania mpaka hapo Serikali ya Tanzania itakapomlipa fidia!
Mimi naongozwa na msimamo wa wazi kabisa kwamba 'right or wrong my country first' na hivyo siwezi kuruhusu mtu, tena mzungu anayejiita mwekezaji kuitukana nchi nchi yangu kwa sababu tu wamerushana na wafanyabiashara wenzake.
Hatuweziweka rehani kwa sababu ya magomvi ya watu binafsi.
Nimemwambia huyu mama na ninarudia kusema, muswada hii ni sehemu ya kurejesha Mali zilizonyonywa na ukoloni.
Nimemwambia huyu mama kwamba hata Waingereza wakitaka kuondoa misaada Yao waondoe na wala hatutakufa kwa kukosa misaada Yao. Nimemwambia hivyo na ninarudia hapa. That's me, what you see is what you get.
Huyu aliyeleta hii thread alete mtiririko wote wa mjadala na sio kipande kimoja tu cha mjadala na kuspin atakavyo yeye na wengi humu mmeingia katika mtego wake bila hata kuhoji.
Viongozi wanaotumia ukoloni kama kisingizio cha umaskini wetu ni wa kuwaogopa kama ukoma. Wengi wao hutumia excuse hiyo kutowajibika kwa wananchi, huku wakijilimbikizia mali ya umma, na hali ikiwa mbaya, hukimbilia huko huko kwa hao wakoloni ambako wameshajinunulia majumba ya kifahari, na kujiwekea akiba za mamilioni ya dollar. Zitto has to be very careful na kauli yake hii, kwani ni rahisi sana kuzidi kubomoa kuliko kujenga.
NI kweli kabisa, lazima tuwaogope sana. Jaribu kuangalia mambo aliyokuwa anafanya gavana na rais (gavana alikuwa fuska? mwizi? mwongo? mbabaishaji?) angalia mambo anayofanya leo RC, DC linganisha na yale alikuwa anafanya mtu wa namna hiyo mkoloni bado huwezi kufananisha hata kidogo. Unaona wazi kabisa kuwa tuliyenaye sasa ni mzugaji tu. It is very sad, very sad in deed, for a politician like Zito Kabwe to have that view, he should be there to tell us what is the way forward, sio kuanza kupiga politiki za kulialia.
Alisema kweli????
Impact ya colonisation ipo, hilo ni fact.Pamoja na ukweli kwamba UK was built in that way, we should not be fooled by politicians who use it as an excuse to justify their poor perfomance. Mkoloni aliondoka miaka 50 iliyopita, mbona hakuna kikubwa cha maana kilichofanyika? Kikubwa tulichofanya ni kuvuruga hata yale mazuri yaliyofanywa na wakoloni. Angalia shule alizoacha mkoloni uone hali yake ya sasa ikilinganishwa na mwaka 60, angalia hospitali, angalia barabara ovyo ovyo. Bado tunamlalamikia mwingereza?? Ukiangalia misaada iliyopata Tanzania toka kwa Uingereza, na nini kimefanyika na misaada hiyo unaweza kuonesha ni nini kimefanyika?
Si siri kuwa mkoloni alikuwa mwizi, lakini viongozi wetu wa sasa ni worse kuliko mkoloni, hawana haki ya kumlaumu mwingereza.
I hope it is part of a bigger sophisticated strategy coz kama aliropoka itatugharimu!Kweli!:lol:
Nini maana ya "your born"?
I hope it is part of a bigger sophisticated strategy coz kama aliropoka itatugharimu!
Viongozi wanaotumia ukoloni kama kisingizio cha umaskini wetu ni wa kuwaogopa kama ukoma. Wengi wao hutumia excuse hiyo kutowajibika kwa wananchi, huku wakijilimbikizia mali ya umma, na hali ikiwa mbaya, hukimbilia huko huko kwa hao wakoloni ambako wameshajinunulia majumba ya kifahari, na kujiwekea akiba za mamilioni ya dollar. Zitto has to be very careful na kauli yake hii, kwani ni rahisi sana kuzidi kubomoa kuliko kujenga.
This is nothing but a smoke screen.
Shameful!