Zitto Kabwe: Taifa lina nyufa

Zitto Kabwe: Taifa lina nyufa

Akiwa mtu wa mwisho kuchangia katika hotuba ya wizara/mambo ya ndani bwana Zitto Kabwe alisema watanzania wanaishi kwa umoja na wanashirikiana katika kila jambo kwani wanashirikiana katika mambo mengi na wanaochochea udini ni viongozi hasa wanasiasa kwani mtu huzungumzia udini katika majukwaa ya siasa huku watu elfu tano wakiwa mbele yao na kama ilivo bungeni mtu anazungumzia suala la udini na anaona fahari kwa manufaa yake binafsi.

Akaongeza kuwa, serikali haipo tayari kuchukua hatua kwa yoyote anayesemwa anatumia udini kwa manufaa yake...huku wakiwa na uwezo huo.Pia akaiasa serikali kuchukua hatua sasa badala ya matamko tuu.

Kweli hili ni la kweli kabisa.

Msitufanye waTZ mazezeta, wanaohubiri udini tunawajua na tunawafahamu na wanaosmea ukweli tunawafahamu,vile vile wanaokemea udini tunawafamu msituchanganye akili hapa.

Padri kapigwa risasi kajeruhiwa na mwingine kauawa, nani ameshikwa na kuhukumiwa???, Wanajulikana Mashekh na Wachungaji wanaohubiri udini na chuk hapa TZ nani anawashughulikia, kwanini wameachwa???

Watu wanajua kuna vutuo vya watoto wa Primary na sekondary hadi Vyuo wanafundishwa Jihadi, na kupandikizizwa Chuki mbona hakuna Hatua zinazochukuliwa...

Mara Kibao inasemekana kuna kituo cha kufundisha ugaidi na jihadi Kiwalani mbona Kipo, cha kushangaza ni Magari mengi sana ya Serikali yanaenda sana pale kuchukua nini???

Au Ndiyo wakufunzi wa hizo Jihadi wanatumia Magari yenye Namba za Serikali??? Msitake kuwahadaa watu..

We know alot about this issues... Wala hamtudanganyi


Dhambi kubwa kuliko zote ni dhambi ya uwoga, Heri kufa kwa kutenda haki na kusimamia ukweli kuliko kuwa mnafiki.

ZZK lazima amtetee JK kwani wanatoka mbali na kamwahidi vitu kibao
 
Na kunisilimisha huwezi, na kulisilimisha taifa hamuwezi. Mtakaa kurusha viguruneti mnavyopewa na wasomali na vikiisha mtakuja kuomba kutibiwa kwenye hospitali za kanisa, hata elimu mtakuja kubembeleza, sasa hata mikopo mmeanza kuomba kwenye benki zetu, makafiri wakubwa!

Hapa unajenga una bomoa? Acha ujinga LUSIFA
 
Kafiri wewe habari za Yesu utazijulia wapi?????? Basi kumbe Yesu alilipua msikiti? Gaidi we!

kwa mara ya kwanza leo nakutana mlokole kiraza. Kwa taarifa yako. Huyo yesu ata kwenye vitabu vyetu nenda kamuhulize mchungaji wako. Huko baa gani mida hii unapiga monde
 
Utajaza, sauti yako si ya kigaidi saaaana, ila unaonekana kutaka kujipendekeza. Siogopi kafiri yoyote na kama wataendelea wataangamia kwa ghadhabu za Mungu anayejipigania mwenyewe. Ukweli wao magaidi lazima tuwape, uwawashe hadi ijumaa watakapoacha mafunzo ya kigaidi na kumrudia Mungu kwa toba

Naona huyu kichaa kakimbia na nguo zangu,sitakufukuza. Na mimi nitaonekana kichaa nitakapo kufukuza. Endelea kufanya kazi ya bwana yako LUSIFA.
 
Tuko mbele kwani huo ni uongo? Sasa nyie badala ya kuifuata njia ili mtufikie mnaamua kutupa mabomu kwa mbele. Tumestuka, sasa tumebadili njia. Mabomu yenu yatawateketeza nyinyi wenyewe. magaidi na makafiri wakubwa

ukimaliza kamwambie alokutuma uislamu wameushindwa fbi.c.i.a.na na hao wanaume wenu u.s.a sembuse wewe. Mfia dini walokutuma wametulia wanasubiri ukimaliza kujaza hapa uwapelekehe sadaka
 
Zitto alichotaka kukiongea hapo ni kuhusu BAKWATA (kama muislamu na ametumwa aongee hilo) basi hayo mengine yalikuwa kuomba attention tu, narudia Zitto ni mdini kama wadini wengine wa kiislamu, ambaye anachoamini na anachosema havina uhusiano hata kidogo, trust me...
 
Zitto alichotaka kukiongea hapo ni kuhusu BAKWATA (kama muislamu na ametumwa aongee hilo) basi hayo mengine yalikuwa kuomba attention tu, HILO LA TEC tumetoka wapi kama sio USHABIKI? narudia Zitto ni mdini kama wadini wengine wa kiislamu, ambaye anachoamini na anachosema havina uhusiano hata kidogo, trust me...
 
Akiwa mtu wa mwisho kuchangia katika hotuba ya wizara/mambo ya ndani bwana Zitto Kabwe alisema watanzania wanaishi kwa umoja na wanashirikiana katika kila jambo kwani wanashirikiana katika mambo mengi na wanaochochea udini ni viongozi hasa wanasiasa kwani mtu huzungumzia udini katika majukwaa ya siasa huku watu elfu tano wakiwa mbele yao na kama ilivo bungeni mtu anazungumzia suala la udini na anaona fahari kwa manufaa yake binafsi.

Akaongeza kuwa, serikali haipo tayari kuchukua hatua kwa yoyote anayesemwa anatumia udini kwa manufaa yake...huku wakiwa na uwezo huo.Pia akaiasa serikali kuchukua hatua sasa badala ya matamko tuu.

Kweli hili ni la kweli kabisa.

Huyo kijana ndio jembe pekee chadema ambalo linaaminiwa na watanzania wote hata wa ccm. huwa haongei upuzi kama kina fulani... yeye ni NCHI KWANZA then CHADEMA inafuata, wenzake wengine ni chadema na maandamano kwanza, halafu ndio TZ inafuata.ndio maana hawampendi...
 
Na kuwavumilia magaidi waislamu makafiri wanaolipua makanisa yetu kutatutia matatizoni zaidi..........bora tuwapasue jipu liwaume na muache ugaidi na mjifunze ustaarabu wa wakristu

Ingekuwa huyu jamaa ni muislam MODS wangeshampiga BAN.

Nadhani huko tuendako HAKI itapatikana tu. Upanga umegusa kwenye MFUPA. Ndio maana huyu jamaa anaropokaropoka tuu.
 
udini ulianzia pale yule mtoto mdogo alipokojolea msahafu bila kujua analofanya lina madhara gani-- reaction iliyotokea pale kwa waumini na shuluhisho la viongozi wetu; udini ukakua kuhusu sakata la uchinjaji kitoweo abapo mchungaji mmoja akapoteza maisha on the process suruhisho lililotolewa pale na viongozi wetu ndiyo tatizo. tusitafute mchawi, nyumba ikiteteleka basi lawama zote lazima ziende kwa wazazi hasa baba mwenye nyumba.

Udini ulianza na JK kabla ya Uchaguzi 2009.. Acheni kuwadanganya watu kuwa wakichana au kukojolea koran watakuwa vichaa vichaa. Watu wataamua kupove wrong, na nnyie kuamua kutumia ubabe kuchoma makanisa na kuua wakristo.
 
Ingekuwa huyu jamaa ni muislam MODS wangeshampiga BAN.

Nadhani huko tuendako HAKI itapatikana tu. Upanga umegusa kwenye MFUPA. Ndio maana huyu jamaa anaropokaropoka tuu.

Hakuna udini kwa mods!.. Baada ya mlipuko wa Arusha, wakristo wengi wakapandwa na jazba na kujibu ovyo.. wengi wakapigwa BAN!..
 
Nipigwe BAN kwa kosa gani? Nimekuiteni majina yaleyale mnayozoea kutuita. Nyinyi ni magaidi. Nyinyi ni makafiri! Kosa langu nini? MODs hawaendeshwi kwa ushawishi wa misikiti wala makanisa, bali hoja. Na leo nimekushikeni barabara, na siwaachii magaidi nyinyi

Shehe ILUNGA kwenye CD maarufu ya piga na kuua wakristo, alisema ... penye neno Gaidi weka dini yako!. sasa wao ni wajibu wao kusuka au kunyoa.
 
Redio imani imeanzishwa lini na kelele za waislam kunyanyaswa, kubaguliwa na kukandamizwa kumeanza lini? Toa mfano wa uchochezi au uzushi wake usikurupuke

hakuna cha kunyanyaswa hapa nendeni shule mmekalia kula futari hamjui dunia inakwendaje
mwisilamu gani aliyesoma ambaye amenyimwa haki yake , mbone wengi tu wenye elimu nzuri wako vizuri tu.
Shida yenu huwa hamsemi mnadai nini. Mmekalia mfumo kristu na ukatoliki
SEMA SHIDA YENU TUWAELEWE , SIO KULALAMA NA KUCHOMA MAKANISA , YOTE HAYO WIVU TU
 
miaka 50 ya uhuru tz inaishia kwenye vita vya udini.politicians are the source of religious conflicts for their own benefit.wanatz muda umefka wa kujtambua na kuepuka ku2miwa na wanasiasa kuleta vta vya kdn.Tanzanians together we can.GOD BLEC TZ.
 
Unajua kidini chenu cha ajabu sana. Sasa kama uislamu umewashinda FBI na CIA, ya nini kuwalipua wamasai wasio na makosa. Au kwa nini kumchinja padri mchaga. Makafiri nyinyi!

kumbe ushaidi unao peleka kwa I.G.P
 
udini ulianzia pale yule mtoto mdogo alipokojolea msahafu bila kujua analofanya lina madhara gani-- reaction iliyotokea pale kwa waumini na shuluhisho la viongozi wetu; udini ukakua kuhusu sakata la uchinjaji kitoweo abapo mchungaji mmoja akapoteza maisha on the process suruhisho lililotolewa pale na viongozi wetu ndiyo tatizo. tusitafute mchawi, nyumba ikiteteleka basi lawama zote lazima ziende kwa wazazi hasa baba mwenye nyumba.
si kweli,,,,,labda useme ulipamba moto,ila upo tangu na tangu,na 2010 ulianza kuonesha kustawi na kunawiri
 
Msomaji yeyote anaesoma ulichokiandika anajua nani kafiri kati yangu na ww.Matusi na kashfa ndio kimbilio la mkosa hoja na mtu asiyejijua hata yy mwenyewe.Chuki yako haikupi nafasi ya kufikiri japo kigogo.Ukristu wangu unaniambia nn ktk suala kama hili.Kwani mfuasi wa Belzebul ana muda wa kumpendeza Mungu?Ungekua unaijua Biblia yako na kuiheshimu usingethubutu kunitukana.Bahati mbaya sana kwako,sikio la kufa halisijii dawa.

Kafir maana yake ni mpingaji!.. Dini yako imetokea miaka 600 baada ya ukristo!.. story nyingi na manabii ni wale wale wa bible.. Hivyo story ya kweli ni ile iliyotangulia. Mpingaji daima ni yule anayefuata, si aliyetangulia.
 
hakuna cha kunyanyaswa hapa nendeni shule mmekalia kula futari hamjui dunia inakwendaje
mwisilamu gani aliyesoma ambaye amenyimwa haki yake , mbone wengi tu wenye elimu nzuri wako vizuri tu.
Shida yenu huwa hamsemi mnadai nini. Mmekalia mfumo kristu na ukatoliki
SEMA SHIDA YENU TUWAELEWE , SIO KULALAMA NA KUCHOMA MAKANISA , YOTE HAYO WIVU TU

shida yetu ni mfumo kristo
 
#NYUFA
TAIFA LINA NYUFA

NDUGU KABWE Z. ZITTO, MB – BUNGENI TAREHE 6 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia leo katika mjadala huu muhimu sana.

Hapa Afrika kulikuwa kuna nchi, na bado ipo, inaitwa Ivory Coast. Ilikuwa ni nchi ambayo inasifika sana kwa amani na utulivu; na ilikuwa ni nchi ya kupigiwa mfano. Leo hii Ivory Coast imegawanyika vipande vipande. Ukienda leo Ivory Coast unakuta wanaoitwa Ivorite na wanaoitwa wageni ambao wazazi wao walienda Ivory Coast kufanya kazi miaka mingi sana. Lakini pili katika mgawanyiko huo kuna mgawanyiko mkubwa sana wa kidini kati ya watu wa Ivory Coast wanaotokea Kaskazini na watu wa Ivory Coast wanaotokea Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa tuna Sierra Leone nchi ambayo wageni walikuwa wanakirimiwa katika hali ambayo haijawahi kutokea hapa duniani. Lakini leo Sierra Leone ina rekodi kubwa sana ya watu wenye ulemavu kwa sababu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Naomba nichukue nafasi hii kufuatia matukio ambayo yametokea hivi karibuni na hasa jana na siku zilizopita ninanukuu hotuba ambayo Rais wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa aliitoa katika Bunge hili tarehe 4 Novemba, 1998. Alisema:

“Mr. Speaker, after three years of my presidency, I can dare to modify the words of famous Zanzibar maestro Siti Binti Saada by saying, Tanzania is a good country, let one who wishes to come do so. God has showered blessings on our country. It is a country of unity, peace, love, rejoicing and exciding generosity. It is a country of people who love equality and justice. Our national unity brings from our firm believe in equality of human beings before God and before the Law. A Unity reinforced by correct policies of national building. Policies based on the principles of social justice, peace, harmony and development for all. A unity which is extra sensitive to policies, statements behavour and actions which may sore seeds discard hatred and suspicious among Tanzanias”

Mheshimiwa Mwenyekiti sitatafsiri. Lakini naomba kila Mbunge ajiulize leo iwapo Rais Mkapa tukimpa fursa ya kuja kuhutubia Bunge hili anaweza akayatumia maneno haya tena? Hakuna mtanzania yoyote anayeweza kuthubutu leo kutumia maneno haya tena kwa sababu nchi yetu ina nyufa. Ina nyufa ambazo kwa kujua au kwa kutokujua sisi kama watu ambao tumepewa wajibi na wananchi wa kuitunza nchi hii na kuipeleka pamoja tumejikuta tukiingia katika kutoa kauli, maneno na vitendo ambavyo ni “irresponsible” vinavyopelekea kugawanya nchi; na yanayotokea sasa ni matumizi ya nyufa hizo.

NDUGU KABWE Z. ZITTO

Asubuhi hapa Mheshimiwa Lissu amesema, ametoa rekodi ya namna ambavyo wanasiasa wa chama kinachoongoza (CCM) wamekuwa wakitoa kauli dhidi ya vyama vya upinzani kuhusiana na masuala haya ya kidini. Wametoa mfano kuhusu chama cha CUF kilipoitwa chama cha waislam, wamekitolea mfano kuhusu CHADEMA kinavyoitwa mpaka sasa chama cha wakristo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inawezekana ikawa ni rahisi sana tuka-“point fingers” kwa wenzetu nyie, ni rahisi sana; lakini CUF wakati wanaitwa ni chama cha waislam ambao walikuwa hawaitwi ni chama cha waislam hawakunyoosha mkono kupinga. Wakati CHADEMA kinaitwa cha cha Kikristo ambao hawaitwi hivyo hawakunyoosha mkono. Matokeo yakeni nini? Tumejenga hofu kubwa sana katika Taifa na hii ni lawama kwa wote. Wote kama nchi ili tuseme kwamba hapa tumekosea na tuanze upya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, adui anapokuja kwenye nyumba anaangalia ni wapi ambapo ni rahisi kamba kukatika. Tumeji-“expose” , tumejiweka wazi. Leo mtu anayetaka kuishughulikia Tanzania ata-deal na udini tu. Kwa sababu anajua watanzania hivi sasa wamegawanyika katika misingi hiyo. Jana limetokea tukio Arusha, angalia kwenye mitandao ya kijamii mara moja watanzania wenyewe kwa wenyewe na ukiangalia majina ya watu wanaojadiliana wanaanza kusemana kwa dini zao. Ndiyo hatari ambayo tumeifikia; na ndio anachokitaka adui. Ni hicho. Atakuja, wanaitwa “Agent Provacateur”, watapiga, mtabaki mnagombana ninyi. Tukiruhusu NYUFA hizi ziendelee hatutakuwa taifa. Ni lazima sote kwa pamoja tusimame imara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, waislam na wakristo nchi hii hawana chuki kwa sababu wanaishi pamoja, ni marafiki, ni ndugu na kama ingekuwa kwa mfano waislam wanawachukia wakristo waislam wangevunja makanisa au wangechoma makanisa au wangewalipua wakristo. Wakati wa tukio la Mwembechai ndipo ambapo Polisi waliingia mskitini wakaua watu, wanawake wakateswa kwenye magereza na kadhalika, watu wakakaa miezi mitano gerezani bila kushtakiwa lakini hapakuwa na mtukio yoyote ya namna hii. Waislam na wakristo wa nchi hii ni wamoja. Wananchi wetu ni wa moja lakini sisi viongozi kwa kutoa kauli ambazo ni “very irresponsible” tunawagawa watu wetu na ni lazima tukatae hali hii. Tunafanya nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima twende mbele. Kwanza ni lazima sasa Serikali ijenge utamaduni wa kufuatilia “grievances” zote ambazo wananchi wanazo bila kujali dini zao. Pili turuhusu watu kuwa huru kusema. Nimesikia hapa watu wanasema kwamba maandamano ni tatizo nakadhalika. Maandamano si tatizo, ukimzuia mtu kuandamana akiweka hasira zake kesho atafanya nini? Atatoka na bomu. Turuhusu “honest discussions” miongoni mwetu kama wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu ni lazima sasa tuseme ya kwamba ni marufuku kuwa na kauli za chuki “hate speeches”. Kama hatuna vipengele vya kisheria tutunge sheria kwa sababu kumekuwa na “hate speeches” nyingi sana katika hii nchi na hakuna hatua ambazo zinachukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, state, dola, ihakikishe inajiondoa kwenye shughuli za uendeshaji wa mambo ya kidini. Ijiondoe kabisa. Kwa mfano kuna lawama ya muda mrefu sana ya waislam kuhusu BAKWATA, Waislamu miaka mingi toka mwaka 1969 wakati Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika. Leo hii Serikali ikitaka kuzungumza na waislam inafanya nini? Inaenda kuwaita BAKWATA. Hawana legitimacy ya waislam, hamtaweza ku-addres masuala ya waislam lakini ni rahisi sana kuweza kuongea na CCT kwa sababu CCT ni chombo ambacho kina uhuru wake. Kwa hiyo Serikali ijiondoe kwenye uendesheji wa shughuli za kidini. Hapa ndipo tutakapoweza kuhakikisha kwamba tunakuwa na nchi moja nchi ambayo ina amani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namaliza kwa kusema nchi hii si ya waislam peke yake, nchi hii si ya wakristo peke yake. Nchi hii si ya CCM au ya CHADEMA, CUF au ya NCCR-Mageuzi au TLP na kadhalika. Nchi hii ni moja, nchi hii ni ya Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania. Lazima wote tusimame kuhakikisha tunailinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru sana asante

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom