Zitto Kabwe: Taifa lina nyufa

Zitto Kabwe: Taifa lina nyufa

Akiwa mtu wa mwisho kuchangia katika hotuba ya wizara/mambo ya ndani bwana Zitto Kabwe alisema watanzania wanaishi kwa umoja na wanashirikiana katika kila jambo kwani wanashirikiana katika mambo mengi na wanaochochea udini ni viongozi hasa wanasiasa kwani mtu huzungumzia udini katika majukwaa ya siasa huku watu elfu tano wakiwa mbele yao na kama ilivo bungeni mtu anazungumzia suala la udini na anaona fahari kwa manufaa yake binafsi.

Akaongeza kuwa, serikali haipo tayari kuchukua hatua kwa yoyote anayesemwa anatumia udini kwa manufaa yake...huku wakiwa na uwezo huo.Pia akaiasa serikali kuchukua hatua sasa badala ya matamko tuu.

Kweli hili ni la kweli kabisa.
Zitto mdini namba moja ya BAKWATA NA JUMUIA YA WAISLAMU yanamhusu nn? Mdini na mgawanyaji wa watz namba moja.... Mdini huyo
 
Nadhani ZITTO bado anajaribu kuukumbatia mbuyu kwa kutokuusema ukweli...Udini Tanzania upo na umeasisiwa vizuri na PENGO na Vaticani yake uku ukielezwa vizuri na KILAINI hiyo 2006 walipowaaminisha watanzania kua JK/CCM ni chaguo la mungu kwa hiyo CDM/MBOWE CUF/LIPUMBA walikua ni machaguo ya shetani...ifike mahari ukweli usemwe apo ndo tatizo km kweli lipo na ninaamini lipo ndipo litakapoisha vinginevyo mnajiridhisha tu...wale wote walioupotosha umma wakina PENGO/KILAINI na wenzake washitakiwe kwa madhambi yao ya udini....
 
aliye leta nyufa ni kile kirusi cha pale makao makuu ya chadema,yule alivujisha barua ya zitto kwenda kwa kirusi.yule aliyesema nchi haitatawalika yule aliyesema mpaka kieleweke huku hataki kukitaja kitakacha eleweka.
 
“Mr. Speaker, after three years of my presidency, I can dare to modify the words of famous Zanzibar maestro Siti Binti Saada by saying, Tanzania is a good country, let one who wishes to come do so. God has showered blessings on our country. It is a country of unity, peace, love, rejoicing and exciding generosity. It is a country of people who love equality and justice. Our national unity brings from our firm believe in equality of human beings before God and before the Law. A Unity reinforced by correct policies of national building. Policies based on the principles of social justice, peace, harmony and development for all. A unity which is extra sensitive to policies, statements behavour and actions which may sore seeds discard hatred and suspicious among Tanzanias”

Mheshimiwa Mwenyekiti sitatafsiri. Lakini naomba kila Mbunge ajiulize leo iwapo Rais Mkapa tukimpa fursa ya kuja kuhutubia Bunge hili anaweza akayatumia maneno haya tena?
Sasa hapo Zitto nae anakosea.
Asipotafsiri kina Lusinde, Lukuvi na wenzao watajua nini inajadiliwa bungeni?
 
Zitto you are the great leader of this nation. Mungu akulinde kaka.
 
Mauaji ya mwembechai na Zanzibar ni waislamu dhidi ya nguvu za dola. hakuna kanisa limewahi kutuma waumini wake kwenda kuua waislamu. Hili limetokea kwa waislamu tu, kuwatuma waumini wake kwenda kuua padri, na kumwinda balozi wa papa! Na hata quran inapokojolewa, huwa mnaitoa wenyewe mkidai mkojoleaji atageuka kuku! Sasa vitoto vya kikristu ni vijiniasi na huwa vinawaaibisha na uongo wenu maana kama ingekuwa kweli vingeshageuka mijusi

Na yule kadinari wenu pengo alisema nini baada ya mauaji ya mwembechai usijidanganye wewe unaushahidi gani na ulichokieleza
 
Nina imani na Zito kabwe ila chama anachowakilisha hakiaminiki!
 
Na yule kadinari wenu pengo alisema nini baada ya mauaji ya mwembechai usijidanganye wewe unaushahidi gani na ulichokieleza

Kardinali hajawahi kumtuma mtu kwenda kuchoma msikiti, ni kinyume kabisa na mashehe wanowatuma waumini wa kiislamu kuandamana kumtoa ponda jela, kuchoma makanisa au kuua mapadri.
 
Nadhani ZITTO bado anajaribu kuukumbatia mbuyu kwa kutokuusema ukweli...Udini Tanzania upo na umeasisiwa vizuri na PENGO na Vaticani yake uku ukielezwa vizuri na KILAINI hiyo 2006 walipowaaminisha watanzania kua JK/CCM ni chaguo la mungu kwa hiyo CDM/MBOWE CUF/LIPUMBA walikua ni machaguo ya shetani...ifike mahari ukweli usemwe apo ndo tatizo km kweli lipo na ninaamini lipo ndipo litakapoisha vinginevyo mnajiridhisha tu...wale wote walioupotosha umma wakina PENGO/KILAINI na wenzake washitakiwe kwa madhambi yao ya udini....

Kilaini kasema JK chaguo la Mungu, sawa. Shehe wako kasema nenda kachinje padri! Kuna uwiano hapo?
 
Ninapenda kusema kuwa kama hatutakuwa na ujasiri kupambana na wote wanaoneza udini, ukabila na migawanyiko katika nchi yetu Tanzania itatumbukia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe. Ni lazima katika nchi yetu kupiga vita kwa nguvu zote bila kuona haya udini, ukabila na utenganisho. Ni wazi kuwa hivi sasa nchi yetu imegawanyika na kuwa waliotugawanya wamefanya hivyo kulinda masilahi yao binafsi.
Ni lazima kama Watanzania wenye kuitakia mema nchi yetu kuwa na miiko ya kitaifa ambayo yeyote yule anayeikiuka anakemewa na kuadabishwa pamoja na kuadhibiwa na sisi sote. Mwiko mkuu katika nchi yetu ni kutaka kuwagawa Watanzania kwa udini na ukabila. Mtu yeyote yule awe Raisi au kibarua, Askofu, Sheikh, Mchungaji, Maalim, Imam, Katekista, anayetugawa ni lazima ashughulikiwe kikamilifu. Ni muhimu kuwa Katiba yetu ni lazima imwikoshe/iharamishe udini na kuwa serikali ni lazima ijitoe kwa ukamilifu katika masuala yote ya kidini. Hii ni pamoja na kuwa vyombo vyote vya serikali ikiwa ni pamoja na taasisi zote za kiserikali kutokuwa na sura au taswira ya kidini. Narudia ni lazima vyombo vyote vya kiserikali viwe na muundo wa kisekula. Hakuna kurudi nyuma katika hilo.

Kama hatutaheshimu hilo si muda mrefu kutokana na mgawanyiko huu wa kijinga wa kidini ulioletwa na watu wenye nia mbaya na nchi yetu na wasio na sifa za kuongoza nchi yetu, Watanzania wa dini tofauti wataanza hata kupinga shida zao kutatuliwa na mtu wa dini ambayo si yake. Huko ndiko tunakokwenda ni lazima tuiokoe nchi yetu na tuwe Watanzania kwanza kabla ya udini, ukabila. Kusisitiza usekula na uzalendo na uaminifu kwa nchi yetu kwanza ni njia ya kweli ya kuliokoa taifa letu. Mwenye masikio asikie, mwenye macho aone, na mwenye upeo aangaze.
 
Mh ZZK unenena sawia, Udini unaletwa na viongozi wa aina zote wanaopenda cheap popularity kwa matamshi yao ya hovyo na wasiojiamini, mfano hao wanaosimama kwenye majukukwaa na kusema kwamba chama fulani ni cha dini fulani kwenye public, wakati sote tunajua sheria zetu ziko wazi kabisa kwamba kabla ya chama kuanzishwa moja ya mambo ya msingi yanayoangaliwa ni chama kutokuwa na mwelekeo wa udini, sasa hapa unategemea nini hapa unajenga hali ya watu kuanza kujadili dini badala ya hoja za msingi. Wananchi tunawajua wanaoleta udini katika nchi hii na lazima tuwaadhibu!
 
baadhi yetu nahisi tumeshindwa kujua kama hapo kuna speeches mbili tofauti na ni za watu tofauti.
 
aliye leta nyufa ni kile kirusi cha pale makao makuu ya chadema,yule alivujisha barua ya zitto kwenda kwa kirusi.yule aliyesema nchi haitatawalika yule aliyesema mpaka kieleweke huku hataki kukitaja kitakacha eleweka.
umesahau sheikh ilunga na mchungaji mtikila?
 
Imetulia hotuba ya mh. zito tunataka watu kama wew.ccm si wanatumia chombo chao BAKWATA kutawala ila yana mwisho.sis waislam ni yatima ktk taifa hili
 
Viongozi wanaotoa speech zenye kuwagawa wananchi kidini waondolewe madarakani
 
niwe muwazi udini umeanza pale chama tawala kilipoamua kurotate wagombea urais kwa kigezo cha udini nani asiyejua kuwa next election ni mkristo ndo anagombea kama nchi ni moja na tuko sawa kwanini wanatumia kigezo cha dini..magamba niwadini.
 
Back
Top Bottom