Zitto Kabwe: Rushwa imeongezeka nchini, ushahidi upo

Zitto Kabwe: Rushwa imeongezeka nchini, ushahidi upo

Asalaam Aleykhum warahmatullah wabarakattul....!

Ndugu wadau, Mheshimiwa Zitto Zubeir Kabwe katika Account yake ya twitter amepost kuwa, Ingawa Rais John Pombe Magufuli anasifiwa kwa kuweza kuzuia rushwa nchini....Ushahidi unaonesha kuwa rushwa imeongezeka kila kona.

Mchwa wapo kibao wanaokula rushwa.

Ametoa mrejesho wa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa alipoenda Morogoro na kubaini hilo.

Je Rais ameshafanikiwa wapi mpaka sasa?
Kuna ukweli. Traffic wamekuwa wanyang’anyi kabisa.
 
Zitto ni kichaa! Nasema ni kichaa kwa sababu anadhani waTanzania ni waninga na hawaoni wala hawasikii. Magufuli ndiyo mpango mzima.
 
Ndugu Zitto japokuwa mara nyingi ninazipenda data na ushauri wake kwenye mambo ya economy, lakini hili rushwa kwenye awamu hii haliko kama lilivyokuweko awamu zilizopita, lazima tufurahie namna hii serekali inavyoweka wazi wanapogundua uharibifu ama rushwa. PM anastahili pongezi kwa kazi nzuri.

Ndugu Zitto this is Political tantrums at their best,

Sasa hivi sio kwamba hamna rushwa, bali vyombo vya habari vinaoogopa kutangaza habari za rushwa, maana serikali haitaki habari hizo kusikika ili ihadae umma kwamba rushwa imedhibitiwa. Matokeo yake rushwa inayotangazwa ni ile iliyotajwa na viongozi wa serikali tu ili serikali ipate sifa, lakini kiukweli rushwa bado ipo sana.
 
Zitto ni kichaa! Nasema ni kichaa kwa sababu anadhani waTanzania ni waninga na hawaoni wala hawasikii. Magufuli ndiyo mpango mzima.

Watanzania wanaona na wanasikia ila hakuna anayethubutu kuongea ukweli kwa kuogopa kutekwa au kupigwa risasi. Sasa hivi kuweka mambo ya rushwa hadharani inachukuliwa ni kama kuichafua serikali. Kuongoza taifa kwa propaganda hakuondoi ukweli wa tatizo. Kwa mfano sasa hivi kila siku tunasikia serekali ikisema mahospitalini kuna dawa, hebu nenda kisha ulete mrejesho hapa jukwaani.
 
Ingawa Rais John Pombe Magufuli anasifiwa kwa kuweza kuzuia rushwa nchini....Ushahidi unaonesha kuwa rushwa imeongezeka kila kona

Mnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake, ingependeza aseme anafanya vizuri/anajitahidi ili kumtia moyo, kiuhalisia the man is strggling to get things in place ila anakwamishwa na watu design ya Kebwe
 
Rushwa ipo sana, mfano kwenye passport hawapokei maombi ya passport bila rushwa. Wala rushwa awamu hii ni werevu mno.
Tunapigwa kimya kimya kila sehemu awamu hii ya5.
Kama unajua rushwa bado ipo wewe binafsi umechukua hatua gani kuhakikisha kwamba unadhibiti hayo maovu kwa kushirikiana na vyombo au taasisi za kuzuia na kupambana na rushwa? Au unataka Magufuli atoke ikulu apite kila ofisi kukamata wala na watoa rushwa? Tuache kulalamika na sisi wananchi tutimize wajibu wetu. Pia kumbuka hakuna nchi ambayo hakuna kabisa rushwa ila nchi nyingi hasa zilizoendelea zinajitahidi kwa kiasi kikubwa kupunguza vitendo vya rushwa. USIULIZE NCHI YANGU ITANIFANYIA NINI BALI NITAIFANYIA NINI NCHI YANGU!
 
Ina maana yeye Mh.Mbunge hakuwahi kutoa au kupokea rushwa?
Hili kutokomeza rushwa ni wajibu wa kila mtu kujitathimini ni namna gani alipata Mali zake kwanza.
Ili kama alifanya hivyo ni wajibu wake sasa kurejesha Mali zote kwa hiari.
Huo ndio utakuwa Uzalendo wa kweli.
Mzalendo wa kweli ni yule tu anayeweza kujipima na kuwajibika kwa maslahi ya wengine.
 
Unapopambana na rushwa ndio unazidi kugundua maeneo mengi ilikojificha......kinachoongezeka awamu hii ya Magufuli siyo rushwa bali kasi ya kuyaibua machimbo ya rushwa!
Wapi trilioni 1.5 na 2.4?ukijibu hilo ntakua kweli mnapambana na ufisadi,usilete ngonjera.
 
Ripoti ya CAG ya mwisho imeshashughulikiwa???speaker vipi,ameshafikishwa mbele ya sheria kuhusu ubadhirifu wa mamilioni kwenye matibabu??rushwa ipo tuu,sema sasa hivi ni kimya kimya.
 
Mwanri amewaambia wananchi waandike kwa siri majina ya majambazi

Sasa kwanini isitumike hiyo pia kuandika wanaokula rushwa?
Jina likiandikwa na watu wengi ale kichwa
 
Hata yeye zito bado anachukuanrushwa
Asalaam Aleykhum warahmatullah wabarakattul....!

Ndugu wadau, Mheshimiwa Zitto Zubeir Kabwe katika Account yake ya twitter amepost kuwa, Ingawa Rais John Pombe Magufuli anasifiwa kwa kuweza kuzuia rushwa nchini....Ushahidi unaonesha kuwa rushwa imeongezeka kila kona.

Mchwa wapo kibao wanaokula rushwa.

Ametoa mrejesho wa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa alipoenda Morogoro na kubaini hilo.

Je Rais ameshafanikiwa wapi mpaka sasa?
 
Ndugu Zitto japokuwa mara nyingi ninazipenda data na ushauri wake kwenye mambo ya economy, lakini hili rushwa kwenye awamu hii haliko kama lilivyokuweko awamu zilizopita, lazima tufurahie namna hii serekali inavyoweka wazi wanapogundua uharibifu ama rushwa. PM anastahili pongezi kwa kazi nzuri.

Ndugu Zitto this is Political tantrums at their best,
imepungua rushwa ya wazi wazi ile (takrima) ila sasa kuna rushwa kubwa zaidi alicho fanya jpm sio kurudisha nidhamu makazini bali kutupa cheo wapumbavu na kujihisi tuna haki matokeo yake tunapewa huduma mbovu na inatulazimu kutoa rushwa bila kupenda

rushwa ipo ya chini chini,tena kubwa kuliko ya mwanzo
 
Naona NIDA na Uhamiaji wanalamikiwa sana.hapo panaitani marekabisho
 
Asalaam Aleykhum warahmatullah wabarakattul....!

Ndugu wadau, Mheshimiwa Zitto Zubeir Kabwe katika Account yake ya twitter amepost kuwa, Ingawa Rais John Pombe Magufuli anasifiwa kwa kuweza kuzuia rushwa nchini....Ushahidi unaonesha kuwa rushwa imeongezeka kila kona.

Mchwa wapo kibao wanaokula rushwa.

Ametoa mrejesho wa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa alipoenda Morogoro na kubaini hilo.

Je Rais ameshafanikiwa wapi mpaka sasa?

Tatizo waliojenga mfumo wa 'misuse of public fund' ni ccm.

Itakuwa ajabu sana hao hao wakijitutumua kuumaliza.

It is imposssible.
 
Niliweka uzi hapa kuwa Magufuli ni anti corruption hero kwa africa,
Jamaa wameuunganisha kwenye pongezi za magufuli.
anti corruption hero wa wapi? Huyu anayewapandisha vyeo akina Mnyeti na Ole Sabaya?
 
Unapopambana na rushwa ndio unazidi kugundua maeneo mengi ilikojificha......kinachoongezeka awamu hii ya Magufuli siyo rushwa bali kasi ya kuyaibua machimbo ya rushwa!
Rushwa haiwezi isha au kuondoka bongo

Ova
 
Hebu nyie watoto mkuwe sasa. Taifa gani Duniani lisilokuwa na ubadhirifu au rushwa? Kinachoangaliwa ni jitihada za kuizuia na wanaobainika kufanya vitendo hivyo hatua kali huchukuliwa dhidi yao.
Nani alimwambia zito kuwa rushwa Tanzania imekwisha? Hakuna ubishi serikali hii inawatisha walarushwa wazembe na wabadhirifu
Hata wakati wa baba wa Taifa, rushwa ilikuwepo... Ila alipambana, kwa kupambana huko TUNAMSIFIA NYERERE. Utaipata wapi nch isiyo na rushwa?
 
Hata wakati wa baba wa Taifa, rushwa ilikuwepo... Ila alipambana, kwa kupambana huko TUNAMSIFIA NYERERE. Utaipata wapi nch isiyo na rushwa?
Vijana wanatafuta turufu ya kuingilia kwenye uchaguzi. Document za CAG zimebuma sasa hivi zito hana pa kushika
 
Back
Top Bottom