Rais Magufuli, hapa Zitto kaongea ukweli kuhusu chanzo cha hizi tuhuma za upigaji wa fedha za elimu kuanzia hazina mpaka Serikali za Mitaa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Sifa kubwa ambayo Rais Magufuli amekuwa akipewa ni ile ya kupambana na rushwa. Lakini ushahidi unaonyesha kuwa rushwa Serikalini imeongezeka sana. Waziri Mkuu Majaliwa amethibitisha hilo ziarani Morogoro, hali hiyo ya Moro imesambaa mikoa yote nchini. Mchwa kila mahala

Nimefanya uchunguzi kwenye sekta ya Elimu eneo la Fedha zinazokwenda mashuleni ( capitation grants ) kutoka Hazina. Kuna mtandao wa ulaji wa Fedha hizi kuanzia Hazina mpaka kwenye LGAs. Billions zimepigwa. Nimepeleka hoja Bungeni kwa ajili ya Bunge la Novemba 2019.

Udhaifu wa vyombo vya usimamizi, vyama vya Siasa hasa vya upinzani (kutokana na kuminywa kufanya kazi za Siasa) na vyombo vya Habari ( kutokuwepo kwa habari za uchunguzi kama miaka ya nyuma) kumechangia sana juhudi za kupambana na rushwa kugonga mwamba. Usiri ni kiota cha rushwa.

Chanzo:Ukurasa wake wa twitter.
 
Huwezi pambana na rushwa kwa kuzuia vyama vya siasa kufanya kazi zake huku media nazo ukizibana.

Hata hii habari eti amerudisha nidhamu ya utumishi wa umma, ni nadharia nyepesi sana ya kisiasa isiyo na mashiko wala ukweli wowote.
 
Kapeleka hoja bungeni ya kutaka nini?
kutaka kuimalisha
-Uhuru wa kikatiba aliyoiapia Rais kuisimamia wa vyama vya siasa
-Uhuru wa vyombo vya habari Kufanya habari za kiuchunguzi
-Kuachana na kubana uhuru wa watu kujieleza
 
Kuna tatizo gani kwa hoja zako hapi juu?nbona zote zinatekelezwa tu
 
Wasiliana na waziri mkuu haraka ili watuhumiwa washughulikiwe mambo ya kupeleka hoja bungeni yamepitwa na wakati!
 
Huwezi pambana na rushwa kwa kuzuia vyama vya siasa kufanya kazi zake huku media nazo ukizibana.

Hata hii habari eti amerudisha nidhamu ya utumishi wa umma, ni nadharia nyepesi sana ya kisiasa isiyo na mashiko wala ukweli wowote.

Ukishaona mwanasiasa yoyote anahubiri kupambana na ufisadi lakini hataki uwazi, ujue hapo ni kama kuzuia risasi kwa debe.
 
Huwezi pambana na rushwa kwa kuzuia vyama vya siasa kufanya kazi zake huku media nazo ukizibana.

Hata hii habari eti amerudisha nidhamu ya utumishi wa umma, ni nadharia nyepesi sana ya kisiasa isiyo na mashiko wala ukweli wowote.
Unatuletea uzi alafu unakuwa wa kwanza ku comment " MERCENARIES AT WORK".

Hilo la ufujaji wa pesa za elimu, ulikuwepo kwa muda mrefu, na ni kweli yako kuwa system zilikuwa hazifanyi kazi kama inavyotakiwa, na hao matapeli kweny ngazi zote wako wafanyika,i wa kila chama, tatizo ni watu na wala sio serekali. Unfortunately waTanzania hatuko nationalistic.

Ila awamu hii tunaona waziri Mkuu akifuatilia na kuwakamata wahusika, na sio kupiga makelele majukwani. Pia wabunge wetu wote bila kuangalia chama, hayo ni moja ya majukumu yao, wanawajibika kufuatilia na kuyapigia kelele, hili jambo sio la awamu ya magufuli tuu, lilikuwepo tokea enzi ya mwalimu.

Zitto is liable on this issue, kwani hata jimboni kwake yanafanyika, mbona haendi kuwaumbua
 
Wasiliana na waziri mkuu haraka ili watuhumiwa washughulikiwe mambo ya kupeleka hoja bungeni yamepitwa na wakati!

Waziri mkuu ni chombo cha kupambana na rushwa? rushwa inapiganwa na mtu au mamlaka husika ndio zenye wajibu huo? Ukiona rushwa inapingwa na wanasiasa majukwaani jua huko ni kusaka sifa za kijinga. Nilimuangalia juzi waziri mkuu huko Morogoro akisaka point za mezani kuwa anapambana na rushwa nilicheka sana, pale ndio nilijua bado tuna viongozi wenye mbinu za karne iliyopita.
 
Wasiliana na waziri mkuu haraka ili watuhumiwa washughulikiwe mambo ya kupeleka hoja bungeni yamepitwa na wakati!
Haitasaidia kuwasiliana nae na wala hatachukua maamuzi ya haraka ,lazima nae afanye uchunguzi kwanza lakin itategemea atakavyolichukulia hilo jambo
 
Kiukweli katika uchambuzi kwa kutumia data, namkubali sana, Mhe. Zitto Zuberi Kabwe yuko vizuri sana.

P
 
Unatuletea uzi alafu unakuwa wa kwanza ku comment " MERCENARIES AT WORK".

Hilo la ufujaji wa pesa za elimu, ulikuwepo kwa muda mrefu, na ni kweli yako kuwa system zilikuwa hazifanyi kazi kama inavyotakiwa, na hao matapeli kweny ngazi zote wako wafanyika,i wa kila chama, tatizo ni watu na wala sio serekali. Unfortunately waTanzania hatuko nationalistic.

Ila awamu hii tunaona waziri Mkuu akifuatilia na kuwakamata wahusika, na sio kupiga makelele majukwani. Pia wabunge wetu wote bila kuangalia chama, hayo ni moja ya majukumu yao, wanawajibika kufuatilia na kuyapigia kelele, hili jambo sio la awamu ya magufuli tuu, lilikuwepo tokea enzi ya mwalimu.

Zitto is liable on this issue, kwani hata jimboni kwake yanafanyika, mbona haendi kuwaumbua
Awamu hii imezidi kwa sababu hata pesa zilizotengwa ni nyingi,lakin kumbuka awamu hii ndo inajinasibu kupambana na rushwa na ufisadi kupita awamu zote,sasa matarajio yetu tuone matukio hayo yanapungua badala ya kuwa kama ilivyo huko nyuma
 
Unatuletea uzi alafu unakuwa wa kwanza ku comment " MERCENARIES AT WORK".

Hilo la ufujaji wa pesa za elimu, ulikuwepo kwa muda mrefu, na ni kweli yako kuwa system zilikuwa hazifanyi kazi kama inavyotakiwa, na hao matapeli kweny ngazi zote wako wafanyika,i wa kila chama, tatizo ni watu na wala sio serekali. Unfortunately waTanzania hatuko nationalistic.

Ila awamu hii tunaona waziri Mkuu akifuatilia na kuwakamata wahusika, na sio kupiga makelele majukwani. Pia wabunge wetu wote bila kuangalia chama, hayo ni moja ya majukumu yao, wanawajibika kufuatilia na kuyapigia kelele, hili jambo sio la awamu ya magufuli tuu, lilikuwepo tokea enzi ya mwalimu.

Zitto is liable on this issue, kwani hata jimboni kwake yanafanyika, mbona haendi kuwaumbua
Hovyo kabisa wewe!!

Mimi kuleta hoja za Zitto hapa haimanisha sina haki ya kuchangia aliyosema Zitto.We kama umeguswa kuwa mpole na sio kuleta unafiki wako hapa!

Awamu hii inaweza kuja kuvunja rekodi ya ufisadi kwasababu hata tu kuandika habari za kiuchunguzi kuibua madudu ya serikali imekuwa ni jambo linalotaka moyo.

Kupambana na rushwa ndogo ndogo hakumanishi hakuna rushwa kubwa zinazofanywa na wenye mamlaka makubwa.

Subirini mtoke madarakani tuje tupitiea mikataba mlioingia na mambo mengine ndio tutajua kama awamu hii ilikuwa ni ya watu safi ama ni ya mafisadi kama zingine zilizopita.

Uongo hautuduma ipo siku ukweli utajulikana na usafi wenu ndio utapimwa na watanzania.

Ni swala la muda tu.
 
Huwezi pambana na rushwa kwa kuzuia vyama vya siasa kufanya kazi zake huku media nazo ukizibana.

Hata hii habari eti amerudisha nidhamu ya utumishi wa umma, ni nadharia nyepesi sana ya kisiasa isiyo na mashiko wala ukweli wowote.
Hela za kununulia wabunge waupinzani zinatoka wapi? Zile hela walizogawiwa wabunge wa CCM na kinana ili kupitisha mswaada zilitoka wapi? Zile hela alipokuwa anawapa Mnyeti madiwani wa chadema Arumeru zilitoka wapi?
 
Ni wajinga tu ndio wanaoamini eti awamu hii inapambana na rushwa!
 
Back
Top Bottom