Zitto Kabwe: Nini kifanyike Tanzania?

Zitto Kabwe: Nini kifanyike Tanzania?

Nini kifanyike Tanzania?

Na Zitto Kabwe

Hali yetu ya sasa

Ni dhahiri kuwa hofu imetanda miongoni mwa Watanzania. Ingawa watawala na mashabiki wao hukanusha jambo hili, ukweli ni kuwa nina amini wao wenyewe ndani ya mioyo yao wanakiri kuwa nchi sasa inaendeshwa kwa hofu na wananchi wamejaa hofu kubwa.

Hivi sasa mwananchi akifanya jambo lolote linaloonekana kuwa kinyume na fikra za watawala, wenzake wanamtazama kwa jicho kuwa atakuwa mhanga wa vitisho, mateso, kutekwa, kupotea ama kubambikiwa kesi.

Hakika jamii iliyojaa hofu haiwezi kuwa jamii huru na kamwe haiwezi kupata maendeleo.

Hofu hii iliyotamalaki imekomazwa na matendo ya utawala kukandamiza uhuru wa watu kujieleza, kupata/kupasha habari, kukusanyika na kuhoji/kukosoa Serikali yao. Hizi ni haki za kikatiba ambazo wajibu wa Serikali ni kuzilinda.

Tumeshuhudia wananchi na haswa vijana wakishtakiwa mahakamani kwa makosa yatokanayo na haki yao ya kujieleza kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya vijana wamehukumiwa vifungo ama kulipa faini.

Mmiliki wa mtandao wa JamiiForums, mtandao wenye kutoa mawazo huru kwa wananchi na kwa muda uliochangia kwa kiasi kikubwa vita dhidi ya ufisadi nchini, Maxence Melo bado anaendelea na kesi zilizofunguliwa dhidi yake ikiwa sehemu ya vitisho vya dola ambavyo pamoja na shauri hilo amekuwa akilazimishwa kutoa majina ya wachangiaji wa mtandao huo.

Licha ya kwamba katiba yetu inaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na kujitangaza, kuandikisha wanachama, kukosoa sera za Serikali na hata kueneza sera mbadala, Serikali kupitia amri isiyo ya kikatiba wala kisheria ya Rais imezuia vyama kufanya shughuli zake hizo halali.

Matamko halali kabisa ya kisiasa ya wanasiasa sasa yanachukuliwa kama ni uchochezi na watoa matamko kushtakiwa kwa makosa ya jinai ikiwemo kwa kutumia sheria mpya kandamizi ya huduma za habari (The Media Services Act 2016 ).

Tumeshuhudia wabunge wakifungwa jela kwa makosa ya matamko ya kisiasa ambayo yangepaswa kujibiwa kisiasa tu kutoka upande wa pili ( watawala ).

Hivi sasa viongozi wakuu wa vyama vya upinzani wanakwenda mahakamani kila wiki kujibu tuhuma za kisiasa, lengo likiwa ni kuwapotezea muda na kuwajaza hofu washindwe kufanya shughuli zao ipasavyo.

Utawala umeweza kusambaza hofu kwa kugusa kila kundi katika jamii. Wanasiasa wanatishiwa na kesi za uchochezi, kutekwa au majaribio ya kuuawa kwa kupigwa risasi mchana kweupe ndani ya eneo lenye ulinzi mkubwa.

Waandishi wa Habari wanatishwa kwa ama vyombo vya habari kama magazeti kufungiwa au kutekwa na kutoonekana kabisa; Wakulima bei za mazao yao zimeporomoshwa makusudi kutokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali; Wavuvi wanachomewa nyavu zao na mitumbu yao kuchomwa moto; Wafugaji wanaondolewa kwenye maeneo yao ya malisho ili kuanzisha ranchi binafsi na wengine kuuwawa; Wafanyabiashara wanabambikiwa kesi ama kodi kubwa ili kuwakomesha na kuweka utii kwa dola; Wanawake wanatukanwa na kudhalilishwa ikiwemo kuwanyima fursa ya kujiendeleza kimasomo watoto wa kike wanaopata uja uzito mashuleni.

Viongozi wa dini wanaojaribu kuhoji watawala wanachunguzwa uraia wao; Wanaharakati wa asasi za kijamii wanaotoa mawazo yasiyopendeza watawala wanatangazwa sio raia wa Tanzania na asasi zao kutishiwa kufutwa kwa kutungiwa kanuni kandamizi za uendeshaji wa asasi hizo.

Wananchi kwa ujumla wanaumizwa na hali mbaya ya uchumi inayotokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo. Wananchi wa Zanzibar wamenyimwa haki ya kuongozwa na Serikali waliyoichagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hakuna kundi katika jamii ambalo limebakizwa, kila kundi limeguswa.

Tunataka nini?
Kwa maoni yangu Watanzania wengi wanapenda kuwa huru; Uhuru wa Mawazo, kujieleza, kukusanyika nk. Nadhani tunataka Tanzania yenye raia wenye uhuru kwa mujibu wa Katiba. Vyama vya siasa viwe huru kufanya shughuli zao bila bugudha na kwa mujibu wa sheria, Bunge la Wananchi liwe huru kuisimamia Serikali bila kuzongwazongwa na Watendaji, vyombo vya habari viwe huru kuandika/kutangaza habari bila woga wala upendeleo; Wananchi wawe huru kuikosoa serikali dhidi ya sera zake kandamizi zinazowasokomeza kwenye umasikini, Wazanzibari wapate haki yao ya uchaguzi (electoral justice) waliyoporwa Oktoba 2015 na viongozi wa dini na asasi za kiraia wawe huru kufanya kazi zao bila vitisho. Kiufupi tunataka nchi ya kidemokrasia ambayo asasi za kidemokrasia zinatimiza wajibu wao kwa uhuru.

Tufanye nini?

Sasa wakati umefika wa kujenga mshikamano kurejesha demokrasia tuliyokuwa nayo nchini na kujenga demokrasia madhubuti ambayo haitachezewa tena na yeyote. Haitoshi kila mtu kusema lake kwa wakati wake anapoguswa na matendo ya kidikteta, tunapaswa kuwa na sauti nyingi lakini zinazoratibiwa ili kuhakikisha kuwa tunalinda haki za watu na kuhami uchumi wa nchi wetu usiendelee kuporomoka. Tunapaswa kuwa na harakati za kutetea haki za kijamii (social justice), haki za kujieleza (freedom of speech) na Demokrasia. Tunapaswa kujenga vuguvugu pana la watu a broad based popular movement) ili kuleta mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Ili kujenga vuguvugu hili ni lazima kuweka mbele maslahi mapana ya Taifa letu na kuachana na maslahi binafsi ambayo yamekuwa yakitawala siasa za Tanzania kwa miongo miwili sasa bila mafanikio ya maana. Ni lazima kukubali ukweli kuwa, kwa hali ya nchi ilivyo sasa hakuna chama kimoja pekee ama kundi la jamii moja pekee linaweza kukabili utawala dhalimu wa kidikteta uliopo nchini na kushinda. Wasioweza kuukabili ubinafsi wao kwenye mambo haya tuwaombe basi wauweke kama akiba kisha tukimaliza kazi hii ya mabadiliko waendelee nao. Kila jambo tufanyalo lazima lijibu swali ‘ hili linatusaidia kutufikisha kwenye lengo la kuondoa utawala wa kidikteta nchini?’

Ni lazima tuwe na mshikamano katika kukabili dubwana tunalokabiliana nalo. Hatupaswi kuruhusu hata siku moja ya ziada baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 tukiwa na ‘regime’ hii tuliyonayo sasa.

Hili ni jambo linalowezekana iwapo tutakuwa na mshikamano madhubuti bila kujali vyama vyetu vya siasa.

Watanzania wapo tayari, wanapaswa kuongozwa tu. Uongozi huu ni lazima uwe na watu wasiopenda yanayoendelea nchini ndani ya watawala, walio nje ya watawala, Wafanyakazi, Wakulima, Wavuvi, Wafugaji, Vjana, Wanawake, Wafanyabiashara, wana harakati na kila mtu anayetaka Tanzania na Zanzibar zilizo njema zenye Uhuru na Demokrasia.

Tunaweza tukiamua. Haya #twenzetu tukaunde vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini.

Dar Es Salaam
5/11/2018

Nini kifanyike Tanzania? Ni kuacha kuwa vibaraka wa nchi za Magharibi na kufanya siasa la ulaghai. Hebu onesha mfano kama kweli hauko kwenye payroll?
 
Tatizo nyie wapinzani mmekuwa wasaliti wa wananchi, bado hatujasahau wewe mh zitto na wenzako mlivyofanya harakati za kudhoofisha chadema .. na sasa unakuja na swali ati tufanyeje? acheni unafiki na ubinafsi , vinginevyo mtaendelea kukosa imani ya wananchi.. waacheni wananchi wapambane na hali zao sio kuwahadaa ...
Hayo baadaye, kwa sasa adui yetu yetu ni mmoja, tupambane naye kwanza kwa operation: "Magufuli out 2020" Udikteta mwisho Rwanda Urundi.
 
Neno "democracy " linapendwa na kila mtu... Lakn masharti yake hakuna ayapendaye... Unalala, ukiamka unatoa tamko la kisera bila kupitisha vikao. Kuna democracy hapo?

Je, hili n tamko "binafsi" la Zitto au n msimamo wa ACT-Wazanyeti?

Tuchoree picha ya Tanzania utajayotuletea baada ya kuondoa hii iliyopo... Je, unataka kusema kuwa Tanzania yako:
(1) kila MTu atasema lolote na atatukana yeyote=si kweli, kutukana mara nyingi inasabaishwa na hasira. Lakini ukiwa kiongozi wa umma, “those are things that comes with the territory” kama huna ngozi ngumu kwenye uongozi wa umma, ambapo unasimamia Taifa kwa niaba ya wananchi, lazima ukosolewe. Kutukana una exaggerate tu.

(2) hakuna kulipa kodi=nonsense! Hakuna serikali itakayoweza kuongoza bila kukusanya kodi.

(3) uvuvi Haram ruksa=nonsense

(4) Hakuna hifadhi za wanyama wala mapori yatakayohifadhiwa...tutachunga mifugo popote=nonsense

(5) bunge Hakuna kutunga sheria=how and why? Sijui hata sababu yako ya kuuliza haya maswali naona kama ya kitoto mkuu! Hili swali linajustify kitu gani? Kwasasa hivi bunge lenyewe si rubber stamp tu?

(6) nk... Au unamaanisha nini?

k

(1) kila MTu atasema lolote na atatukana yeyote=si kweli, kutukana mara nyingi inasabaishwa na hasira. Lakini ukiwa kiongozi wa umma, “those are things that comes with the territory”
(2) hakuna kulipa kodi=nonsense! Hakuna serikali itakayoweza kuongoza bila kukusanya kodi.
(3) uvuvi Haram ruksa=nonsense
(4) Hakuna hifadhi za wanyama wala mapori yatakayohifadhiwa...tutachunga mifugo popote=nonsense
(5) bunge Hakuna kutunga sheria=how and why? Sijui hata sababu yako ya kuuliza haya maswali naona kama ya kitoto mkuu! Hili swali linajustify kitu gani?
(6) nk... Au unamaanisha nini?=🤷🏾‍♂️
 
Wanasiasa walioko JF huwa hawajibu comments hata siku moja. Mtu anaanzisha mada halafu katika comments 200 hakuna yake hata moja. Hakuna tofauti na kusoma makala za kwenye magazeti kwa maana hakuna interaction kati ya Mtoa mada na wachangiaji.
 
Demokrasia anayozungumza Zitto ni demokrasia ya kufikirika. Ili kuweka kumbukumbu sawa, Zitto anaweza kusema ni kikao gani cha ACT- Wazalendo kilimchagua kama Kiongozi Mkuu wa Chama (Ruhollah Khomeini- Supreme Leader wa ACT)?
Ni rahisi sawa kusema kwa wengine.
 
huyu anacheza na akili za Watanzania muuliuze kwanza yeye ana nafasi gani ndani ya chama je ni mwenyekiti? katibu? au Mjumbe? huyu kila siku unasikia wanamwita Kiongozi so huyu ana nafasi zote je hiyo ndiyo demokrasia anayoipigania???
 
Nini kifanyike Tanzania?

Na Zitto Kabwe

Hali yetu ya sasa

Ni dhahiri kuwa hofu imetanda miongoni mwa Watanzania. Ingawa watawala na mashabiki wao hukanusha jambo hili, ukweli ni kuwa nina amini wao wenyewe ndani ya mioyo yao wanakiri kuwa nchi sasa inaendeshwa kwa hofu na wananchi wamejaa hofu kubwa.

Hivi sasa mwananchi akifanya jambo lolote linaloonekana kuwa kinyume na fikra za watawala, wenzake wanamtazama kwa jicho kuwa atakuwa mhanga wa vitisho, mateso, kutekwa, kupotea ama kubambikiwa kesi.

Hakika jamii iliyojaa hofu haiwezi kuwa jamii huru na kamwe haiwezi kupata maendeleo.

Hofu hii iliyotamalaki imekomazwa na matendo ya utawala kukandamiza uhuru wa watu kujieleza, kupata/kupasha habari, kukusanyika na kuhoji/kukosoa Serikali yao. Hizi ni haki za kikatiba ambazo wajibu wa Serikali ni kuzilinda.

Tumeshuhudia wananchi na haswa vijana wakishtakiwa mahakamani kwa makosa yatokanayo na haki yao ya kujieleza kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya vijana wamehukumiwa vifungo ama kulipa faini.

Mmiliki wa mtandao wa JamiiForums, mtandao wenye kutoa mawazo huru kwa wananchi na kwa muda uliochangia kwa kiasi kikubwa vita dhidi ya ufisadi nchini, Maxence Melo bado anaendelea na kesi zilizofunguliwa dhidi yake ikiwa sehemu ya vitisho vya dola ambavyo pamoja na shauri hilo amekuwa akilazimishwa kutoa majina ya wachangiaji wa mtandao huo.

Licha ya kwamba katiba yetu inaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na kujitangaza, kuandikisha wanachama, kukosoa sera za Serikali na hata kueneza sera mbadala, Serikali kupitia amri isiyo ya kikatiba wala kisheria ya Rais imezuia vyama kufanya shughuli zake hizo halali.

Matamko halali kabisa ya kisiasa ya wanasiasa sasa yanachukuliwa kama ni uchochezi na watoa matamko kushtakiwa kwa makosa ya jinai ikiwemo kwa kutumia sheria mpya kandamizi ya huduma za habari (The Media Services Act 2016 ).

Tumeshuhudia wabunge wakifungwa jela kwa makosa ya matamko ya kisiasa ambayo yangepaswa kujibiwa kisiasa tu kutoka upande wa pili ( watawala ).

Hivi sasa viongozi wakuu wa vyama vya upinzani wanakwenda mahakamani kila wiki kujibu tuhuma za kisiasa, lengo likiwa ni kuwapotezea muda na kuwajaza hofu washindwe kufanya shughuli zao ipasavyo.

Utawala umeweza kusambaza hofu kwa kugusa kila kundi katika jamii. Wanasiasa wanatishiwa na kesi za uchochezi, kutekwa au majaribio ya kuuawa kwa kupigwa risasi mchana kweupe ndani ya eneo lenye ulinzi mkubwa.

Waandishi wa Habari wanatishwa kwa ama vyombo vya habari kama magazeti kufungiwa au kutekwa na kutoonekana kabisa; Wakulima bei za mazao yao zimeporomoshwa makusudi kutokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali; Wavuvi wanachomewa nyavu zao na mitumbu yao kuchomwa moto; Wafugaji wanaondolewa kwenye maeneo yao ya malisho ili kuanzisha ranchi binafsi na wengine kuuwawa; Wafanyabiashara wanabambikiwa kesi ama kodi kubwa ili kuwakomesha na kuweka utii kwa dola; Wanawake wanatukanwa na kudhalilishwa ikiwemo kuwanyima fursa ya kujiendeleza kimasomo watoto wa kike wanaopata uja uzito mashuleni.

Viongozi wa dini wanaojaribu kuhoji watawala wanachunguzwa uraia wao; Wanaharakati wa asasi za kijamii wanaotoa mawazo yasiyopendeza watawala wanatangazwa sio raia wa Tanzania na asasi zao kutishiwa kufutwa kwa kutungiwa kanuni kandamizi za uendeshaji wa asasi hizo.

Wananchi kwa ujumla wanaumizwa na hali mbaya ya uchumi inayotokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo. Wananchi wa Zanzibar wamenyimwa haki ya kuongozwa na Serikali waliyoichagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hakuna kundi katika jamii ambalo limebakizwa, kila kundi limeguswa.

Tunataka nini?
Kwa maoni yangu Watanzania wengi wanapenda kuwa huru; Uhuru wa Mawazo, kujieleza, kukusanyika nk. Nadhani tunataka Tanzania yenye raia wenye uhuru kwa mujibu wa Katiba. Vyama vya siasa viwe huru kufanya shughuli zao bila bugudha na kwa mujibu wa sheria, Bunge la Wananchi liwe huru kuisimamia Serikali bila kuzongwazongwa na Watendaji, vyombo vya habari viwe huru kuandika/kutangaza habari bila woga wala upendeleo; Wananchi wawe huru kuikosoa serikali dhidi ya sera zake kandamizi zinazowasokomeza kwenye umasikini, Wazanzibari wapate haki yao ya uchaguzi (electoral justice) waliyoporwa Oktoba 2015 na viongozi wa dini na asasi za kiraia wawe huru kufanya kazi zao bila vitisho. Kiufupi tunataka nchi ya kidemokrasia ambayo asasi za kidemokrasia zinatimiza wajibu wao kwa uhuru.

Tufanye nini?

Sasa wakati umefika wa kujenga mshikamano kurejesha demokrasia tuliyokuwa nayo nchini na kujenga demokrasia madhubuti ambayo haitachezewa tena na yeyote. Haitoshi kila mtu kusema lake kwa wakati wake anapoguswa na matendo ya kidikteta, tunapaswa kuwa na sauti nyingi lakini zinazoratibiwa ili kuhakikisha kuwa tunalinda haki za watu na kuhami uchumi wa nchi wetu usiendelee kuporomoka. Tunapaswa kuwa na harakati za kutetea haki za kijamii (social justice), haki za kujieleza (freedom of speech) na Demokrasia. Tunapaswa kujenga vuguvugu pana la watu a broad based popular movement) ili kuleta mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Ili kujenga vuguvugu hili ni lazima kuweka mbele maslahi mapana ya Taifa letu na kuachana na maslahi binafsi ambayo yamekuwa yakitawala siasa za Tanzania kwa miongo miwili sasa bila mafanikio ya maana. Ni lazima kukubali ukweli kuwa, kwa hali ya nchi ilivyo sasa hakuna chama kimoja pekee ama kundi la jamii moja pekee linaweza kukabili utawala dhalimu wa kidikteta uliopo nchini na kushinda. Wasioweza kuukabili ubinafsi wao kwenye mambo haya tuwaombe basi wauweke kama akiba kisha tukimaliza kazi hii ya mabadiliko waendelee nao. Kila jambo tufanyalo lazima lijibu swali ‘ hili linatusaidia kutufikisha kwenye lengo la kuondoa utawala wa kidikteta nchini?’

Ni lazima tuwe na mshikamano katika kukabili dubwana tunalokabiliana nalo. Hatupaswi kuruhusu hata siku moja ya ziada baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 tukiwa na ‘regime’ hii tuliyonayo sasa.

Hili ni jambo linalowezekana iwapo tutakuwa na mshikamano madhubuti bila kujali vyama vyetu vya siasa.

Watanzania wapo tayari, wanapaswa kuongozwa tu. Uongozi huu ni lazima uwe na watu wasiopenda yanayoendelea nchini ndani ya watawala, walio nje ya watawala, Wafanyakazi, Wakulima, Wavuvi, Wafugaji, Vjana, Wanawake, Wafanyabiashara, wana harakati na kila mtu anayetaka Tanzania na Zanzibar zilizo njema zenye Uhuru na Demokrasia.

Tunaweza tukiamua. Haya #twenzetu tukaunde vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini.

Dar Es Salaam
5/11/2018
Eti mtu asiye huru anapata foram ya kutangaza civil strife bila hofu ya kukamatwa wala kuwajibishwa.
Huo ujinga unaouita demokrasia unafanyika kwa mujibu wa taratibu za nchi. Demokrasia si kama formula ya kutengeneza coca cola radha yake ifanane dunia nzima. Demokrasia lazima iakisi mila na tamaduni za Kitanzania.
 
Tunaweza tukiamua. Haya #twenzetu tukaunde vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini.

Mhitasari kamilifu kabisa wa matukio halisi ya mambo yaliyotokea ndani ya utawala huu. Matukio ambayo yanaifanya Tanzania kuwa nchi ya mifarakano badala ya maelewano na umoja.

Wanasiasa, ndani ya vyama vya upinzani na hata waliomo ndani ya chama tawala wasiopendezwa na hali hii ya nchi yetu, wajibu walio nao ni kuwafikia wananchi kwa njia zozote ziwezekanavyo ili kuelezea mabadiliko haya yanayotokea ndani ya nchi yetu.
Ni wananchi pekee ndio wana kauli ya mwisho kuhusu jambo hili, lakini wanahitaji kuwa na wasimamizi, waelimishaji., waratibu n.k.

Muda nao ndio huo unakwenda mbio sana. Kuzidi kuchelewa kuanza hii kazi ndio kuifanya iwe ngumu zaidi kwa sababu ufanisi wa utekelezaji utakuwa ni hafifu.
 
Hilo vuguvugu akalianzishie ACT na kisha kigoma ,akifanikiwa huko aje na huku.
 
Huyu mtu au dogo anaitwa Zitto sijui yukoje???!!! Kuna hofu gani TZ?? Kama iko hofu basi ni miongoni mwa wachache sana tena sana ambaosidhani wanafika hata watano ambao wao hawataki kutii mamlaka na wanadhani wanajua kila kitu kwa niaba ya Watanzania...hakuna democracy without restrictions...ikiwemo democracy ya aina hiyo basi hiyo ni chaos....Mimi naona yaliyomo kwenye hoja iliyowekwa hapa ni ya kuchochea vurugu....Kuandika eti "tunaweza tukiamua, haya twenzetu tukaunda vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini" ni maneno ya uchochezi ili kuleta vurugu katika nchi...kama maneno haya kweli ni ya zitto basi huyu dogo ana matatizo na ni sahihi kwa dola kumshughulikia....halafu kuandika kuwa eti "watanzania wapo tayari wanapaswa kuongozwa tu" kwa maana ya kuasi mamlaka ni uchochezi wa kiwango cha hali ya juu kabisa...huyu dogo kama kweli ameandika yeye ni vema afunzwe adabu..watanzania wa wapi hao ambao wapo tayari kuleta vurugu!!!???
Jamal Kashoggi na Saudi Kingdom !
 
Jamal Kashoggi na Saudi Kingdom ! Si vema kusukuma mamlaka kwa lugha za uchochezi namna hiyo...kushawishi uasi!
 
Tumekusikia kiongozi wetu wa upinzani ila nanyie mkutane muone namna ya kuunganisha nguvu ya kumuua nyoka 2020. Bila kuwa na umoja nyoka huyu atatusumbua sana
 
Back
Top Bottom