Zitto Kabwe: Ni Mkulima tu Atatutoa Hapa Tulipo Kiuchumi

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Serikali ihangaike na Mkulima. Mkulima ndio Sura ya Umasikini wa Tanzania.

Sekta ya Kilimo inapaswa kukua kwa kasi ya 6-8% kwa Mwaka ili Pato la Taifa likue kwa 8-10% kwa Mwaka.

Tunahitaji kasi hiyo ya ukuaji wa Uchumi kwa Miaka 5 mfululizo ili kuwaondoa kwenye umasikini 60% ya Watu wetu. Tukishikilia ukuaji huo kwa Miaka 10 mfululizo tutafuta umasikini wa kutupwa ( abject poverty) kabisa.

57% ya mchango wa kilimo katika GDP ni sekta ya mazao. Hii ndio LOW HANGING FRUIT! Hapa ndipo pa kufanyia INTERVENTION na kuchochea WHOLE AGRICULTURAL SECTOR ECOSYSTEM.

Tuanze na TIJA! TIJA TIJA TIJA - Mkulima avune mazao mengi zaidi katika ardhi anayolima sasa.

Mchango wa shughuli ndogo za mazao katika Pato la Taifa (GDP) ni 15%. Shughuli za mazao zilikua kwa 2.7% tu Mwaka 2022. Shughuli hii ya Uchumi Ndio yenye Watanzania wengi zaidi na Ndio njia ya haraka kuwatoa Watu kwenye umasikini.

Watunga Sera waweke Mkakati wa kuongeza TIJA ( productivity) katika shughuli hii.

Kwa Mfano
  • Mkulima wa Mahindi azalishe gunia 10/ekari kutoka 4/ekari ilivyo sasa.
  • Mkulima wa Pamba azalishe kilo 800-1000/ekari kutoka kilo 150-200/ekari ilivyo sasa.
Kwenye kila zao tumwezeshe Mkulima kuongeza Tija katika kipande Chake cha ardhi anacholima hivi sasa. Hii peke yake itaongeza uzalishaji wa chakula mara 2 ya sasa, vile vile uzalishaji wa mazao ya Biashara mpaka mara 5 ya sasa na kuwezesha Nchi kupata Fedha nyingi za kigeni.

Tufanye nini

1. Serikali ifanye kazi kubwa ya mawasiliano na Wakulima ( Behaviour Change Communications ) hususan kuhusu mbinu za kuongeza tija na masoko. Turudi Enzi za vipindi vya ‘Mkulima wa Kisasa’ kwa kutumia njia za kisasa za mawasiliano. Mawasiliano! Mawasiliano! Mawasiliano!

2. Serikali itoe motisha kwa Wakulima wanaofanya vizuri kuanzia ngazi ya Kijiji mpaka Taifa. Mfano wakulima bora wa kila Kata nchini wakutane na Rais Kila Mwaka wakati wa wiki ya Wakulima na wapewe zawadi. Zoezi la Usajili wa Wakulima litasaidia sana hii kwani itakuwa rahisi kuwa na rekodi za uzalishaji wao.

3. Huduma za ugani kwa Wakulima ziimarishwe na maafisa ugani wanaofanya vizuri wapewe motisha na wanaofanya vibaya waadhibiwe. Tasnia ya uafisa ugani itazamwe namna inaweza kuwa huru yaani maafisa ugani Binafsi watambuliwe Rasmi.

4. NFRA iendelee kuongezewa uwezo wa kifedha na teknolojia ili itoe uhakika wa Soko la mazao ya chakula kwa Wakulima na vile vile uhakika wa ugavi wa chakula kwa walaji. Benchmark ya Hifadhi ya Chakula ya kutosha miezi 3 ( Mahindi tani 1.5M, Mchele tani 300,000, Maharage, Mtama, Uwele nk ) Itahakikisha kuwa angalau 25% ya chakula kinachozalishwa kinanunuliwa na NFRA.

5. Kwa kupitia Usajili wa Wakulima nchini, Skimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima inaweza kuanzishwa ili kuwezesha wakulima kuweka Akiba, kupata Fao la Bei na Bima ya Afya na uhakika wa Maisha ya uzeeni ( pensheni ).

6. Serikali iimarishe Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC) kwa kuiwezesha kushiriki katika Biashara ya kwanza usambazaji wa mbolea na baadaye uzalishaji wa mbolea. Kwa kutumia Usajili wa Wakulima, kila Mkulima apate mbolea kwa wakati na aina sahihi ya mbolea.

7. Serikali ibadili muundo wa Bodi za Mazao ili zitimize wajibu wao kwa ufanisi. Bodi za mazao zisiwe wanyonyaji wa wakulima bali wawezeshaji wa wakulima. Vyama vya wakulima viwe na Uwakilishi mkubwa kwenye Bodi za Mazao, Uwakilishi wa kupigiwa kura na wakulima wenyewe.

8. Tuimarishe sana ushirika. Vyama vya Msingi na Vyama Vikuu viwe vyombo vya Kidemokrasia na viendeshwe kwa matakwa ya wakulima wenyewe. Vyama vya Ushirika viwe vituo rejea vya Maendeleo ya wakulima. Serikali isiingilie uendeshaji wao na vile vile wakulima wasilazimishwe kujiunga. Ushirika ushindane na Sekta Binafsi ili kuongeza ufanisi. Wakulima wakiona matunda ya ushirika wataimarisha ushirika. Turudi nyuma kujifunza (rejea Ruvuma Development Association (RDA))

9. Rudia kusoma namba 1

10. Rudia kusoma namba 1

Marrakesh, Morocco
16/07/2023
 
Anaandika,

Ndug.Zitto Zuberi Kabwe

Serikali ihangaike na Mkulima. Mkulima ndio Sura ya Umasikini wa Tanzania.
Sekta ya Kilimo inapaswa kukua kwa kasi ya 6-8% kwa Mwaka ili Pato la Taifa likue kwa 8-10% kwa Mwaka. Tunahitaji kasi hiyo ya ukuaji wa Uchumi kwa Miaka 5 mfululizo ili kuwaondoa kwenye umasikini 60% ya Watu wetu. Tukishikilia ukuaji huo kwa Miaka 10 mfululizo tutafuta umasikini wa kutupwa ( abject poverty) kabisa.

57% ya mchango wa kilimo katika GDP ni sekta ya mazao. Hii ndio LOW HANGING FRUIT! Hapa ndipo pa kufanyia INTERVENTION na kuchochea WHOLE AGRICULTURAL SECTOR ECOSYSTEM.

Tuanze na TIJA! TIJA TIJA TIJA - Mkulima avune mazao mengi zaidi katika ardhi anayolima sasa.

Mchango wa shughuli ndogo za mazao katika Pato la Taifa (GDP) ni 15%. Shughuli za mazao zilikua kwa 2.7% tu Mwaka 2022. Shughuli hii ya Uchumi Ndio yenye Watanzania wengi zaidi na Ndio njia ya haraka kuwatoa Watu kwenye umasikini.

Watunga Sera waweke Mkakati wa kuongeza TIJA ( productivity) katika shughuli hii.

Kwa Mfano
  • Mkulima wa Mahindi azalishe gunia 10/ekari kutoka 4/ekari ilivyo sasa.
  • Mkulima wa Pamba azalishe kilo 800-1000/ekari kutoka kilo 150-200/ekari ilivyo sasa.
Kwenye kila zao tumwezeshe Mkulima kuongeza Tija katika kipande Chake cha ardhi anacholima hivi sasa. Hii peke yake itaongeza uzalishaji wa chakula mara 2 ya sasa, vile vile uzalishaji wa mazao ya Biashara mpaka mara 5 ya sasa na kuwezesha Nchi kupata Fedha nyingi za kigeni.

Tufanye nini

1. Serikali ifanye kazi kubwa ya mawasiliano na Wakulima ( Behaviour Change Communications ) hususan kuhusu mbinu za kuongeza tija na masoko. Turudi Enzi za vipindi vya ‘Mkulima wa Kisasa’ kwa kutumia njia za kisasa za mawasiliano. Mawasiliano! Mawasiliano! Mawasiliano!

2. Serikali itoe motisha kwa Wakulima wanaofanya vizuri kuanzia ngazi ya Kijiji mpaka Taifa. Mfano wakulima bora wa kila Kata nchini wakutane na Rais Kila Mwaka wakati wa wiki ya Wakulima na wapewe zawadi. Zoezi la Usajili wa Wakulima litasaidia sana hii kwani itakuwa rahisi kuwa na rekodi za uzalishaji wao.

3. Huduma za ugani kwa Wakulima ziimarishwe na maafisa ugani wanaofanya vizuri wapewe motisha na wanaofanya vibaya waadhibiwe. Tasnia ya uafisa ugani itazamwe namna inaweza kuwa huru yaani maafisa ugani Binafsi watambuliwe Rasmi.

4. NFRA iendelee kuongezewa uwezo wa kifedha na teknolojia ili itoe uhakika wa Soko la mazao ya chakula kwa Wakulima na vile vile uhakika wa ugavi wa chakula kwa walaji. Benchmark ya Hifadhi ya Chakula ya kutosha miezi 3 ( Mahindi tani 1.5M, Mchele tani 300,000, Maharage, Mtama, Uwele nk ) Itahakikisha kuwa angalau 25% ya chakula kinachozalishwa kinanunuliwa na NFRA.

5. Kwa kupitia Usajili wa Wakulima nchini, Skimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima inaweza kuanzishwa ili kuwezesha wakulima kuweka Akiba, kupata Fao la Bei na Bima ya Afya na uhakika wa Maisha ya uzeeni ( pensheni ).

6. Serikali iimarishe Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC) kwa kuiwezesha kushiriki katika Biashara ya kwanza usambazaji wa mbolea na baadaye uzalishaji wa mbolea. Kwa kutumia Usajili wa Wakulima, kila Mkulima apate mbolea kwa wakati na aina sahihi ya mbolea.

7. Serikali ibadili muundo wa Bodi za Mazao ili zitimize wajibu wao kwa ufanisi. Bodi za mazao zisiwe wanyonyaji wa wakulima bali wawezeshaji wa wakulima. Vyama vya wakulima viwe na Uwakilishi mkubwa kwenye Bodi za Mazao, Uwakilishi wa kupigiwa kura na wakulima wenyewe.

8. Tuimarishe sana ushirika. Vyama vya Msingi na Vyama Vikuu viwe vyombo vya Kidemokrasia na viendeshwe kwa matakwa ya wakulima wenyewe. Vyama vya Ushirika viwe vituo rejea vya Maendeleo ya wakulima. Serikali isiingilie uendeshaji wao na vile vile wakulima wasilazimishwe kujiunga. Ushirika ushindane na Sekta Binafsi ili kuongeza ufanisi. Wakulima wakiona matunda ya ushirika wataimarisha ushirika. Turudi nyuma kujifunza (rejea Ruvuma Development Association (RDA))!

9. Rudia kusoma namba 1
10. Rudia kusoma namba 1

Marrakesh, Morocco
16/07/2023
 
Serikali ihangaike na Mkulima. Mkulima ndio Sura ya Umasikini wa Tanzania.
Sekta ya Kilimo inapaswa kukua kwa kasi ya 6-8% kwa Mwaka ili Pato la Taifa likue kwa 8-10% kwa Mwaka. Tunahitaji kasi hiyo ya ukuaji wa Uchumi kwa Miaka 5 mfululizo ili kuwaondoa kwenye umasikini 60% ya Watu wetu. Tukishikilia ukuaji huo
HATA MKALIMA KAMA KUNA UPIGAJI ITAKUWA KAZI BURE. UNADHANI KILIMO KINAZIDI MAPATO YA BANDARINI IKISIMAMIWA VIZURI
 
Mimi I agree kilimo kitatutoa tuna large arable land, na pia workforce kubwa iko huko, ni basi tu kuna mahali tunakosea kilimo kiwe cha Faida kwa Watanzania
 
Kilimo pekee hakitoshi kututoa hapa tulipo.

Nguvu kubwa ielekezwe kwenye kuendeleza rasilimali watu, sayansi na technology.
Zito hajamaanisha kilimo kama kilimo, anachomaanisha ni kuwa hata hizo ahadi za DPw kuleta neema Tanzania ni ndoto za abunwasi. Kwa vile analamba sukari akaamua kutumia tafsida ya kuwa "kilimo pekee" ili kufikisha ujumbe kuwa tusihadaike na mbwembwe za Dpw
 
Yaaani kuna wengine sijui mnakuaga wanafiki au wachawi? Yaani karne ya 21 unahimiza watu walime na tumeona technology inavobadilika kwa kasi hivi! Tuunde mifumo uzalishaji inayotokana na ubunifu na vipaji tutatoka mapema ila sio hizo idea za agri revolution 🚮🚮
 
Mimi I agree kilimo kitatutoa tuna large arable land, na pia workforce kubwa iko huko, ni basi tu kuna mahali tunakosea kilimo kiwe cha Faida kwa Watanzania
Utawekezaje katika kilimo ilhali hujui kama DPw ataitaka ardhi yako au la? Na iwapo akiitaka hata kama umewekeza mamilioni basi itabidi umpishe kaka mwarabu. sasa hapo usalama wa mitaji utakuwaje?
 
Hongera Zitto kabwe,hakika kilimo ni uti wa mganga wa Taifa,Cha ajabu waganga Njaa wamekomaa na siasa uchwara tuh, mfano muulize Wilbroad Slaa anazo hata Hela mbili za mahindi?Hana,Kisha anajifanyq ana uchungu na wananchi.
 
Mkuu Una utani wa ngumi 🤣🤣🤣
Sio utani huo ndo uhalisia. Mkataba kwa jinsi ulivyo ni hatari kwa mzawa kuwekeza popote ambapo ni economic strategic area, kuanzia kwenye trade center kama Kariakoo hadi kwenye kilimo (strategic zones) kama bonde la ihefu huko Mbarali. Mfano waarabu wakianza operation wakaitaka Kariakoo na wakasema hawataki kuona mapembelo (mkinga) yeyote pale Kariakoo basi serikali italazimika kumuondoa mkinga mmoja mmoja hadi Kariakoo ibaki bila encumbrance yoyote ya mapembelo.
Sasa kwa hali hiyo ni nani mwenye akili atawekeza tena ili aje alipwe fidia kiduchu?
 
Wenyewe wanasema hawadeal na siasa za matukio bali za masuala. Ndio hapo wanaongea mambo yasiyowafikia hata hao walengwa, na wala huko serikalini hawana muda wa kuyatekeleza maana hayana pressure kwao.
Matukio ni nini na masuala ni nini?
Mtu anachukua bandari zote, trade centers zote kama Kariakoo na miji mikubwa, logistic centers, export procossing zones , ardhi nzuri na miundombinu strategic infrustratuctures kama SGR, DART mwendokasi n.k hayo siyo matukio bali ni masuala.
Licha ya hayo nimependa ulivyomjibu Zitto kupitia signature yako.
 
Mfuatilie vizuri Zito na chama chake, wao huwa wanasema hawajihusishi na siasa za matukio, bali siasa za masuala. Mfano halisi, kwa sasa umesikia popote Zito na ACT wakiongelea hili suala la bandari hasa kinyume cha mtazamo wa serikali?
 
Serikali ihangaike na Mkulima. Mkulima ndio Sura ya Umasikini wa Tanzania.
Sekta ya Kilimo inapaswa kukua kwa kasi ya 6-8% kwa Mwaka ili Pato la Taifa likue kwa 8-10% kwa Mwaka. Tunahitaji kasi

Marrakesh, Morocco
16/07/2023
Sawa kwa hiyo zito anataka kututoa kwenye rel ya DP
 
Back
Top Bottom