Zitto Kabwe: Nani anaongoza nchi yetu?

Zitto Kabwe: Nani anaongoza nchi yetu?

Waislam wengi ndio tabia zao wanajionaga dini yao ndio dini bora hapa duniani.
Kama dini yao ni bora Zitto Kabwe Muislamu anawapingaje waislamu wenzie Kassim Majaliwa aliyetoa tamko msikitini na kumpinga pia muislamu mwenzie Samia Suhuhu Hassan?

Tamko la Zitto linawapinga waislamu wenzie
 
Binadamu ni kinyonga.
Ukila dagaa atakusema umeishiwa,ukila nyama atakusema kuwa unaringa ☹️☹️
 
Zzb umeongea point tatizo liko kwa wadanganyika waliozea kunywa chai ya moto kwa mrija. Ni maumivu.
Watanzania wote wenye Akili timamu kabsa wanataka uwazi juu ya Afya ya magufuli, lakini watanzania wanufaika wa utawala wake hawataki uwazi kwani wanahofia kukutana na hasira za wote walioathirika na uonevu wake
 
Nyie ACT si ni sehemu ya serikali jamani au naota mpaka na mna makamo wa Rais! ina maana hata yeye Makamu wenu hajui Rais mwenzake alipo?
Angepotea wa znz wangejua
 
Bahati mbaya sana, suala hili limechukua sura ya kishabiki zaidi kuliko maslahi ya kitaifa. Hoja za Mhe. Zitto zina mantiki sana lakini tunajua hazitajibiwa kwani itakuwa sawa na kumpa ujiko.

Tumechagua kuwa taifa la usiri...usiri....usiri. Sijui tutafka wapi na mwendo huu, lakini kwa jumla hatuna hatma njema.
 
Bahati mbaya sana, suala hili limechukua sura ya kishabiki zaidi kuliko maslahi ya kitaifa. Hoja za Mhe. Zitto zina mantiki sana lakini tunajua hazitajibiwa kwani itakuwa sawa na kumpa ujiko.

Tumechagua kuwa taifa la usiri...usiri....usiri. Sijui tutafka wapi na mwendo huu, lakini kwa jumla hatuna hatma njema.
Usiri wa utawala huu ni Usiri usio na tija, kufanya Siri juu ya afya ya Rais ni Usiri wa ajabu huo
 
Kwa kutokujua nafasi yetu kama "RAIA" wa taifa hili, viongozi wamechagua kutufanya watakavyo. Hiyo ndiyo faida ya ujinga. Tungelijua nafasi yetu, suala la wahusika kutueleza aliko Rais lisingekuwa hisani, bali wajibu.

Bahati mbaya sana, wengi wetu tumempa Rais hadhi ya kuwa "naibu mungu" kiasi kwamba tunaona kuwa kuhoji chochote kuhusu hali yake na vitendo vyake ni sawa na dhambi ipasayo mauti.

INASIKITISHA SANA.
 
Namchungulia Mzee Lowasa anavyo tutazama tulivyo kuwa tunavyo mwambia Ikulu hakuna vitanda vya wagonjwa kweli kama ni haya Mdomo huumba tutumie vizuri ndimi zetu Kwaresma njema tuwaombee wagonjwa wote bila kubagua
Kuna mgonjwa aliwahi kusema mgonjwa mwenzie sijui kama atafika kesho alikuwa anakoroma Hana fahamu, Yule aliekuwa mzima alikufa usiku ule ule,hii story niliwahi kuishare wakati Lowassa anaambiwa kajinyea. Kila MTU ana siku yake ya kufa tuwe waangalifu Kwa kauli zetu na matendo. Ndio maana leo Lissu anadunda nae anapoza machungu maana si mnafiki.
 
Hao "wananchi" anaowasemea ni wangapi, alikutana nao lini, na ni kweli kama walimpa hoja hizo alizozijadili, au ni ubunifu wake binafsi au unawakilisha foreign interests za watu wa nje wanaomtumia?
Kama dhamira zake/zao zinawatuma kuamini kama anaumwa, basi uwasilishaji wa hoja zake zinakiuka uungwana, utamaduni na malezi ya Watanzania. Nilitarajia aonyeshe angalau chembe ya huruma na simamzi, badala yake kinachojionyesha ni kibri, kukosa utu na kufurahia madhira ya wengine!
Utamaduni huu ni mgeni kwetu na wale tusiufumbate! Na kwa vile chama chake kina wabunge...awatumie kupata taarifa sahihi kwa kile anachokitilia shaka!
Kunyamaza pia ni uungwana!
 
Zitto ungejaribu kuwa na subira,umeambiwa mzee wetu yuko ofisini anachapa kazi zake kama kawaida,sasa shida yako mini


Labda ungefuata ushauri wa mama Samia jana wa kuwa nchi iko salama kabisa na tunachotakiwa kufanya sasa
wana wa nchi ni kushikamana tu kama ilivyokuws kabla ya wahuni kuibua huu uvumi

Yaani mzee wetu kutokwenda kanisani jumapili moja tu mmefanya kuwa tukio kubwa na la ajaaaaaaaaabu
 
Ujinga ujinga tuu, kama ni mzima si atokee aseme , kama ni mugonjwa si mtwambie , kama amekufa si mseme ( kwenye kifo tutawashangaa sababu mlikaa kimya kipindi akipigania uhai kitandani) ....hii dunia ya Mungu watu wanapita na kuiacha , baada ya miaka 100 ijayo wote tunaocomment na kusoma news humu + waliozaliwa leo sote tutakuwa kaburini ....... Kama mtu yupo mahututi semeni ili akifa tusishangae ,..., wenye kulia tutalia na wenye kucheka watacheka..hata hvyo maisha lazima yaendeleee tuu
 
Na wewe zitto ni walewale lengo lao kuleta hali ya wasiwasi na mfarakano nchini kwa njia ya uzushi. Huu uzi wako wala haukua na ulazima ila unaendeleza tu malengo ya wapinga maendeleo. Viongozi wakuu wa nchi wameeleza rais yuko kazini ila vibaraka wanataka rais eti ajitokeza hadharani ili kuonesha sio mgonjwa. Huu ni uchokozi wa kusudi kwa dola ya wananchi kwa sababu hakuna sababu yoyote kuhisi rais ni mgonjwa. Itafika mahali wananchi tutataka wazushi na wale wenye kuwaunga mkono wachukuliwe hatua kabambe maana sheria za kuwawajibisha zipo.
Kuuliza rais yupo wapi ni kupinga maendeleo?!
 
Sasa kama waziri mkuu keshatoa hilo tamko ina maana Zitto hajui anayeongoza nchi nani? Ni Dk Magufuli aliyeongea na Waziri Mkuu
Tamko la waziri lina siku zaidi kadhaa sasa hivyo tamko la waziri mkuu linahitaji kutizamwa kwa jicho la 3
 
Zzb umeongea point tatizo liko kwa wadanganyika waliozea kunywa chai ya moto kwa mrija. Ni maumivu.
Wanufaika wa uonevu unyanyasaji uovu kwa watanzania ndiyo wenye pressure kubwa, lakini watenda haki wapo wametulia wanasoma upepo
 
Mkitaka kujua Rais yu wapi hakuna haja ya kutumia nguvu kubwa😂🤣😀
Ombeni ugeni mkubwa wa Rais eg India, chancellor ujerumani ama waziri mkuu wingereza au hata Baba mtakatifu aje Tanzania tuone ni protocol ipi itazingatiwa kumkaribisha Kati ya mgeni wetu pendwa noted
Najaribu kuwaza kwa sauti🤣🤣🤣😂😅😅
Waziri kabudi atawazuia wasije juu kwa juu, labda uombe Rais wa ulimwengu Baiden atue hapo bongo ghafra akiwa njiani kuelekea Nchi ingine
 
Back
Top Bottom