Zitto Kabwe Jitafakari

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,523
4,991
Nilimsikiliza Zitto Kabwe, mmoja wa vigogo katika viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani hapa Tanzania, akitoa hotuba yake katika mkutano wa Baraza la Vyama vya siasa. Nilimsikia akimuomba Rais Samia, kwa unyenyekevu mkubwa, "asaidie" ili Mbowe awe huru.
Nilisikiliza pia majibu ya rais Samia.

Baadae nilisikiliza mtanange kati ya Zitto, kwa upande mmoja, na wanachama, wapenzi na viongozi wa CHADEMA , wakiongozwa na Tundu Lissu na Godbless Lema, kwa upande mwingine. Zitto akijitetea dhidi ya tuhuma kwamba amekidhalilisha chama cha CHADEMA na Mwenyekiti Mbowe, kwa kuomba msamaha kwa niaba ya Mbowe, ilhali Mbowe hajatiwa hatiani.

Zitto anasema yeye anaamini katika maridhiano. CHADEMA pia wamekuwa wakisema wapo tayari kwa maridhiano, toka enzi za Magufuli . Lakini inaonekana katika hiki kilichotokea kwenye Baraza la Vyama vya siasa, siyo majadiliano wala maridhiano, bali mitego mitupu na kuvikana vilemba vya ukoka.

Zitto mwenyewe amekiri kwamba alipigwa chenga. Mwanzo aliaminishwa kwamba atatoa neno la shukrani mwisho. Lakini ghafla akaarifiwa kwamba ataanza kuongea na rais ataongea mwisho. Hiyo ilikuwa chenga kubwa na yenye faida kubwa kwa CCM.

....inaendelea
 
Nilimsikiliza Zitto Kabwe, mmoja wa vigogo katika viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani hapa Tanzania, akitoa hotuba yake katika mkutano wa Baraza la Vyama vya siasa. Nilimsikia akimuomba rais Samia, kwa unyenyekevu mkubwa, "asaidie" ili Mbowe awe huru.
Nilisikiliza pia majibu ya rais Samia.

Baadae nilisikiliza mtanange kati ya Zitto, kwa upande mmoja, na wanachama, wapenzi na viongozi wa CHADEMA , wakiongozwa na Tundu Lissu na Godbless Lema, kwa upande mwingine. Zitto akijitetea dhidi ya tuhuma kwamba amekidhalilisha chama cha CHADEMA na Mwenyekiti Mbowe, kwa kuomba msamaha kwa niaba ya Mbowe, ilhali Mbowe hajatiwa hatiani.
Zitto anasema yeye anaamini katika maridhiano. CHADEMA pia wamekuwa wakisema wapo tayari kwa maridhiano, toka enzi za Magufuli . Lakini inaonekana katika hiki kilichotokea kwenye Baraza la Vyama vya siasa, siyo majadiliano wala maridhiano, bali mitego mitupu na kuvikana vilemba vya ukoka.

Zitto mwenyewe amekiri kwamba alipigwa chenga. Mwanzo aliaminishwa kwamba atatoa neno la shukrani mwisho. Lakini ghafla akaarifiwa kwamba ataanza kuongea na rais ataongea mwisho. Hiyo ilikuwa chenga kubwa na yenye faida kubwa kwa ccm.
....inaendelea
Kwahiyo ajitafakari kuhusu nini? 🙄
 
Back
Top Bottom