Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Kama Hatuna Uwezo Wa Kuijenga Wenyewe Ni Bora Tukaiacha Mpaka Tutakapokuwa Na Uwezo Wa Kufanya Hivyo Wenyewe
Na biashara itakuwa inatusubiri sisi mpaka tuje kupata uwezo au? utasema bahari tunayo sisi tu haya kama haikuja siku tunafuata mzigo Zanzibar.
 
Viwanda watanufaika vikijengwa kusema wachina wataleta watu wao ni sawa maana wanaweka pesa zao nyingi tu hata SGR tunakosema pesa zetu bado umesmskia CAG kuwa wafanyakazi wengi ni wageni tu. Wataweka watu na kampuni za ujenzi wanavyoona wao na ziko sheria za nchi katika mambo ya Labour.

Tanzania tunapenda kulalamika sana ujenzi wa barabara tu wanaiba mafuta mpaka basi na jusi Rais kasema wazi tu huwezi kumpangia mtu anayeweka pesa zake watu wa kuajiri katika baadhi ya position na nchi ina sheria za wazi namna ya kubalance ajira basi zifuatwe.

Rais kasema na lazima ifuatwe. kampuni ngapi za wawekezaji wamejaza wageni, nyingi tu maana sisi inawezekana tunaweza ila mkono tunao na hatuaminiki tunaibia mpaka mashirika yetu.
Achana. na Kicherembalga hakuna anachokijua
 
Na biashara itakuwa inatusubiri sisi mpaka tuje kupata uwezo au? utasema bahari tunayo sisi tu haya kama haikuja siku tunafuata mzigo Zanzibar.
Lakini si tuliambiwa meli za mizigo zimepungua Sana kuja kwenye bandari zetu!?..Ayo ma giant yataletwa na nini kinachozuia kuja SASA hivi kama sio kuingia bila kulipa Kodi!? Na je Dar es salaam na Tanga zimelemewa na mizigo?
 
Hivi hii nchi Tuko serious kweli..unawezaje kukabidhi mpaka wa nchi Kwa foreigners Kwa miaka 100..hii inatofauti gani na ule ukoroni wa awali?!
 
KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania

Kisha hizi meli tunazoziona zikileta mizigo Dar port ndio zitakuwa zinabeba miizigo kutoka Bagamoyo na kusambaza sehemu mbalimbali duniani amesisitiza Zitto

Tusiiache fursa hii jamani na siyo kweli kwamba kila mradi ulioanzishwa awamu ya Kikwete ulikuwa mbaya kwani hata reli ya SGR mradi uliasisiwa vizuri na serikali ya JK lakini serikali ya awamu ya tano imekuja kuutekeleza kwa namna tofauti, amemalizia Zitto.

Chanzo: Clouds 360
Anko nae ntu wa dili huyu sio wakumuamini
 
Huyu fala si ndio analalamika kila siku mambo yamekua magumu unyanyasaji mikataba ya hovyo sasa na yeye kaingia mkenge inamaana anaukubali mkataba ambao hata haujulikani ukweli ama uongo wake , wanasiasa uchwara hawa wana shida sana yaani ni kama kina mzee mdee tu
 
Tujenge kwa fedha za ndani hata ukikamilika miaka 70 ijayo poa kuliko kupumuliwa na mchinku.
 
Presentation yake ilikuwa nzuri sasa anachotaka ni kuona mkataba, hakuna.mahali aliposema bandari ijengwe kwa huo mkataba maana hajauona ndiyo maana anataka uwekwe wazi kila mtu auone kama ni mbaya basi itafutwe plan B ama renegotiation.

Pia kasema Oman imeingia mkataba na zanzibar kujenga bandari hivyo kujenga tena hiyo bandari bagamoyo itakuwa haimake sense unless waje na mpango ya jinsi hizo bandari mbili zinavyoweza kufanya kazi kwa pamoja.

Hivi Zitto anahitaji elimu ya kiwango cha PhD ili kutambua kwamba mkataba wa kibiashara sio public record? Ni nchi gani huanika mikataba ya kibiashara?

Tanzania sio jamhuri ya twitter. Tuna mfumo wa political representation. Bunge ndiyo chombo ambacho tumekubaliana kikatiba kiwe macho, masikio na sauti yetu. Kamati ya kudumu ya Bunge inayohusika ikiomba kuona mkataba fulani itakuwa sawa. Haiwezekani mtu yeyote tu akiamua kudai document fulani anapewa. It doesn’t make any sense. After all, how is the decision going to be made? Je, tunataka kuendesha shughuli za Serikali kwa referendum?

Zitto anachotaka kuleta ni chaos; nothing else! Shida zake azipeleke kwa mbunge wake au wabunge wengine. Huo ndiyo utaratibu wa kikatiba tulionao.
 
Tatizo lenu hamtaki kusikiliza!

Mngekuwa mnasikiliza hoja na kizipima badala ya kupinga tu kwa kuwa mtoa hoja humpendi.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo,ulikuwa ujengwe kwa makubaliano ya uwekezaji wa pande tatu,Tanzania,Oman na China. Wawekezaji wangejenga miundo mbinu ya bandari na industrial parks kwa ajili ya viwanda zaidi ya 800 na kuchukua port charges kwa kipindi cha miaka 50. Serikali haikuyakiwa kutoa hata sumuni! Katika kipindi hicho serikali itachukua kodi zingine mbalimbali kama ushauri wa forodha kama kawaida. Baada ya miaka hiyo, bandari inakuwa mali ya serikali 100%

Utaratibu huu ndio unaotumika hata sasa kwenye bandari ya Dar. Wapo TICTS wanaendesha bandari hiyo.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo unamanufaa makubwa katika uchumi wa Tanzania. Pamoja na kuifanya Tanzania kuwa lango juu la bidhaa kwa zaidi ya nchi 8 za Afrika,unaifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda vya kisasa ambavyo vitahudumia soko la ndani na nchi nyingine za Afrika.

Mradi huu utazalisha ajira nyingi mno katika sekta mbalimbali kama mahoteli, usafirishaji nk.
Mkuu unamaanisha hayo ndo mashart yote ya mkataba?...

vip kuhusu ile kutokuingiliwa na serikali ili kujua kiasi cha pesa waliokusanya?...

na kuhusu kuongezeka KWA mda wa kuendesha bandari kama hawatarudisha pesa yao na kupata faida tajwa ILIHALI serikali haruhusiwi kukagua mapato yao?

Naomba majibu...
 
Tatizo lenu hamtaki kusikiliza!

Mngekuwa mnasikiliza hoja na kizipima badala ya kupinga tu kwa kuwa mtoa hoja humpendi.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo,ulikuwa ujengwe kwa makubaliano ya uwekezaji wa pande tatu,Tanzania,Oman na China. Wawekezaji wangejenga miundo mbinu ya bandari na industrial parks kwa ajili ya viwanda zaidi ya 800 na kuchukua port charges kwa kipindi cha miaka 50. Serikali haikuyakiwa kutoa hata sumuni! Katika kipindi hicho serikali itachukua kodi zingine mbalimbali kama ushauri wa forodha kama kawaida. Baada ya miaka hiyo, bandari inakuwa mali ya serikali 100%

Utaratibu huu ndio unaotumika hata sasa kwenye bandari ya Dar. Wapo TICTS wanaendesha bandari hiyo.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo unamanufaa makubwa katika uchumi wa Tanzania. Pamoja na kuifanya Tanzania kuwa lango juu la bidhaa kwa zaidi ya nchi 8 za Afrika,unaifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda vya kisasa ambavyo vitahudumia soko la ndani na nchi nyingine za Afrika.

Mradi huu utazalisha ajira nyingi mno katika sekta mbalimbali kama mahoteli, usafirishaji nk.
Kiukweli mtoa hoja sijawai kukutana nae namwona tu kwenye mitandao...pia huwa na heshimu na kuwapenda watu wote hata kama ni adui yangu..coz sina impact yeyote kwenye maisha yake

Afu nami nimeleta hoja hapo juu haina maana namchukia....
 
Kwamba hii Bagamoyo's project ipewe green light kwasababu tu ya kuyaona mameli makubwa ambayo hatujawahi kuyaona?..basi sawa!!!
Kweli sijaona upumbavu kama huu. Turuhusu mradi fisadi tuingie utumwani kwa sababu tunataka kuona mameli makubwa!. Foolish!.
 
Back
Top Bottom