Zitto Kabwe awalipua wazungu!

Zitto Kabwe awalipua wazungu!

Kadogoo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2007
Posts
2,073
Reaction score
343
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe mbunge wa Kigoma Kusini na Waziri Kivuli wa CHADEMA amewalaani wazungu kwa utapeli na uporoji mkubwa wanaoufanya dhidi ya Waafrika! nadhani umefika wakati kwa Serikali yetu kuamka na kua macho na Wazungu wote wanaoingia nchini mwetu kwani hawana nia nzuri na nchi yetu!

habari zaidi kuhusu hoja za Zito gonga hapa: Home
 
Ile Buzwagi iliishia wapi? Wanaochimba pale ni wakazi wa Kahama? Mimi nafikiri tulinde maliasili zetu kwa wezi wote, weusi na weupe, watanzania na wasiokuwa watanzania. Hawa watu unaowaita wazungu hawaji moja kwa moja na kuvamia, wanatumia wanasiasa tuliowaamini kama yeye huyu kufanya uharamia. Zaidi ya hapo itakuwa ni racism.
robbing-africa.jpg
 
He nani huyu anaamka jioni??!! Nchi shauzwa nyie..
 
Nilivyoisoma habari hi toka IPP Media Zitto Zuberi Kabwe Mbunge kupitia Chadema amefanikiwa kufikisha ujumbe sahihi bila kigugumizi kwa mataifa haya ya nchi za magharibi wanaotumia werefu mkubwa kutuibia uchumi wetu kwa janja ya kuja kuwekeza huku wakichomoa zaidi ya wanachowekeza.

Uchambuzi wake katika mada iliyowakilisha imeonekana kutulia, ujumbe umewafikia, na huko kwenye vikao vyao vya umoja wa nchi za ulaya watayajadili.
 
Nchi ya Uswiss inanishangaza sana kutokana na kuwa na makao ya mojawapo ya Umoja wa Mataifa lakini hawao makini katika kulinda rasilimali za nchi maskini ila kufungua milango ya kupokea fedha haramu ziingizwe kwenye mzunguko wa uchumi wa nchi zao kwa njia ya mabenk.
 
Tatizo ni wageni,wala si wazungu pekee,kama alivyoainisha Zitto!je Mheshimiwa anataka kutuamini waarabu na waamerica ni watu safi na pia wanatupenda sana?
 
Wajibu wa kulinda rasilimali za Tanzania ni jukumu la watanzania wenyewe,endapo tutashindwa kutekeleza jukumu letu basi hakuna mtu anayeweza kutusaidia kwa hili!
 
Nchi ya Uswiss inanishangaza sana kutokana na kuwa na makao ya mojawapo ya Umoja wa Mataifa lakini hawao makini katika kulinda rasilimali za nchi maskini ila kufungua milango ya kupokea fedha haramu ziingizwe kwenye mzunguko wa uchumi wa nchi zao kwa njia ya mabenk.

Wewe nafikiri ni mgeni Dunia hii, unatokea sayari nyingine kabisa!
 
Tatizo ni wageni,wala si wazungu pekee,kama alivyoainisha Zitto!je Mheshimiwa anataka kutuamini waarabu na waamerica ni watu safi na pia wanatupenda sana?

Tatizo ni sie wenyewe, tunategemea tulindiwe rasilimali zetu badala ya kuchukua jukumu ya kuzilinda sisi wenyewe! Let's all get up be responsible individuals/citizens!
 
Tatizo ni sie wenyewe, tunategemea tulindiwe rasilimali zetu badala ya kuchukua jukumu ya kuzilinda sisi wenyewe! Let's all get up be responsible individuals/citizens!
Precisely mkuu!
 
Katika mijadala ya asubuhi ya kituo cha televisheni cha STARTV Jumapili iliyopita, wageni waalikwa katika mjadala ule walimulalamikia Mh.Zitto kwa kukurupusha hoja ambazo anashindwa kuzisimamia.Kudhibitisha hili ni kuwa katika bunge lililopita alisema atawataja walioficha pesa uswizi kama serikali haitawataja lakini wiki mbili zilizopita Mh. Zitto amesikika kupitia StarTv hiyohiyo kuwa hatawataja.

Hatujakaa sawa anaibuka na habari za kuwalaumu wazungu kwa wizi. Njia bora ilikuwa Mh. Zitto anahakikisha tunajisafisha sisi kwanza kwa kuwashughulikia wezi tunaowajua na kuziba mianya ya wizi kama Mh.Zitto alivyokuwa amenuia huko Bungeni ndipo sote kwa pamoja tuwageukie wazungu wezi.

Kitendo hiki cha Mh.Zitto kuwarukia wazungu wakati hili la kuwashughulikia wezi wa ndani kinatoa tafsiri mbaya sana juu yake juu nia aliyokuwa nayo kuhusu tuhuma alizozitoa bungeni za pesa za wizi zilizofichwa Uswisi, binafsi naona Zitto anataka kutumia mwanya huu wa kuwashambuliwa wazungu kufifisha suala zima alililojiapiza kushiriki kulikabili yaani suala la watanzania kuficha pesa za wizi Uswisi na kwingineko.

Zitto kuruka ruka na hoja ambazo azisimamii bado anazidi kudororesha imani ya raia wa Tanzania kuwaamini vijana katika shughuli za kuikwamua nchi yetu kutoka kwenye lindi la matatizo mengi ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kadhalika.

Kwa mara nyingine namtahadharisha Zitto aache mtindo wake huu wa kudidimiza nia ya watanzania ya kuwaamini vijana kuwa na uwezo wa kukwamua nchi yao kwani yeye bado anabeba taswira ya Mwanasiasa Kijana. kama hawezi kujirekebisha basi ajiuzulu masuala yote ya Siasa na aendelea na shughuli zake nyingine.

---MpigaKelele
 
Utawalaanije wazungu kwa ujinga wa Mwafrika?

Namsubiri Kiongozi wa Kwanza mwenye akili. Atakayehamasisha Watanzania wachange tusenti twao (wa alfu moja, mbili, tano, kumi, n.k) kuwa mtaji wa uwekazaji katika nyanja watakaichagua kuliko huu upumbafu wa kuandika kwenye karatasi/mitandao, kusoma kwenye Podium/iPad, kuwaponda wazungu majukwaani alafu ukishuka unakwenda kuwaomba misaada!
 
Back
Top Bottom