kanga
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 1,025
- 494
.Just thinking aloud!!
Hivi kama baba mwenye nyumba akialika wageni (bila kujali rangi au asili yao) waje nyumbani kwake kisha akawaruhusu waingie ndani ya nyumba yake na wawe huru kuchukua au kufanya kitu chochote watakachoona kina manufaa kwao ni halafu wale wageni wakaiba pesa na kubaka watoto ni nani wa kulaumiwa? Ni baba mwenye nyumba au ni wale wageni aliowaalika na kuwapa ruksa ya kuingia popote wanapotaka na kufanya chochote wanachoona kinafaa?
Hivi baba au mama mwenye nyumba akichukua raslimali ya nyumbani kwake akaipeleka nje (iwe kwa nyumba ndogo, kidumu au popote anapojua yeye) na kuiacha familia yake ikiwa maskini haina msaada ni nani wa kulaumiwa? Ni mwenye nyumba au wale wanaopelekewa mali ili watumie na zinazobaki waendeleze majumbani kwao?
Nadhani imefika wakati waafrika tukaacha kutafuta mchawi nje ya nchi na kuelewa ule msemo wa wahenga kuwa kikulacho ki nguoni mwako.
Kila dola inayoondolewa afrika ama ina baraka ya waafrika walioteuliwa kuwawakilisha wenzao kusimamia raslimali za nchi zao au inatoroshwa na hawa wawakilishi wenyewe na kupelekwa kwa wazungu, waarabu, wachina, etc. Tuache kupoteza muda wetu kutafuta wachawi ulaya, amerika na bara hindi wachawi wetu wapo humu humu nchini.
Eti hawa ndio viongozi tunaowategemea,wasomi wanaonyumbulisha na uelewa mkubwa.Ni ujinga mkubwa, Hivi leo hii Buzwagi,na Barick wanaovuna maelfu ya ton ya dhahabu kanda ya Ziwa wamelazimisha serikali ya Tanzania kulipa mrahaba wa 3%,na exemptions kibao?,how about Tanzanite One?,how about hoteliers?, ambao hata wapishi na wazibua vyupa wanaletwa toka philipines na China>,Ni sera zetu eti za Uwekezaji,huku misamaha ya kodi kibao,na tuna tegemea misaada kwa 42% ya bajeti na 80% ya bajeti ya maendeleo.75% ya development bajeti ni capacity building kulipana posho na kununua mashangingi ,V8 na Nissani ni ujinga Kabisa.Wazungu ndio wanatakiwa watushangae sisi kwa ujinga wetu.Tazama fedha za change ya Rada kama siyo wazungu wenyewe TZS 74bilion zingepotea tu.
Nchi ya Swiss yenyewe imeandaa sera ya namna hiyo ya kuvutia wawekazaji katika sekta ya fedha na ni kitu cha hospitality,honesty,secrecy, kama Tanzania nayo inaweza kufikia hatua ya namna hiyo ya kuaminiwa na nchi na watu duniani ni jambo jema.Otherwise MATATIZO MENGI YA AFRIKA/TANZANIA SULUHISHO NI WATANZANIA WENYEWE NA HAKUNA MCHAWI WA MATATIZO YA WAAFRIKA/WATZ.ALUTA CONTINUA, ALUTA CATABUU