Zitto Kabwe awalipua wazungu!

Zitto Kabwe awalipua wazungu!

Habari kamili....





Zitto awalipua Wazungu

11th December 2012


*Ni uporaji wa
matrilioni


Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto
Kabwe, amewalipua Wazungu kuwa ni waporaji wakubwa wa rasilimali za
Afrika.

Pia ameitaja Uswisi moja kwa moja kwa moja kuwa inakumbatia sera
ambazo zinasaidia uporaji wa rasilimali hizo kwa kuweka vivutio vya kutokulipa
kodi na taratibu ngumu na zisizo wazi katika kufuatilia fedha zilizoporwa katika
mataifa ya Afrika.

Alisema uporaji huo kwa kiasi kikubwa unaziumiza zaidi
nchi nyingi za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara, kwa njia ya ukwepaji
kodi, rushwa na hila nyingine katika sekta ya uwekezaji.

Zitto ambaye ni
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni, alisema hayo wakati akihutubia mkutano wa masuala ya
ushirikiano wa uchumi kati ya Ujerumani na nchi za Afrika.

Mkutano huo wa
siku tatu mfululizo, kuanzia Desemba 9, mwaka huu, unafanyika mjini Berlin,
nchini Ujerumani.

Zitto anatoa kauli hiyo wakati kukiwa na harakati kubwa
nchini za kutaka Watanzania walioficha zaidi ya Dola bilioni 300 katika mabenki
ya Uswisi wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kurejeshwa kwa fedha hizo
nchini.

Miongoni mwa watu wanaodaiwa kuficha fedha hizo Uswisi ni pamoja
na watumishi wa umma na viongozi waandamizi.

Katika mkutano wa jana,
Zitto alisema kuwa nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikiporwa maliasili zake na
baadhi ya kampuni za kimataifa kupitia ukwepaji kodi pindi zinapokuja kuwekeza
barani humo.

Zitto alisema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mwaka 2012
katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (Unctad), jumla ya
uwekezaji wote uliofanyika duniani kwa mwaka jana ni trilioni 1.5 (Dola moja ni
sawa na Sh. 1,568) lakini kiasi cha fedha kilichotoroshwa kutoka nchi
zinazoendelea kwa mwaka ni wastani wa Dola za Marekani trilioni 0.84 kati yake
Dola trilioni 0.58 zilitoroshwa kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la
Sahara.

Kibaya zidi Zitto alisema wakati kiasi cha Dola za Marekani
bilioni 538 zinaibwa kutoka Afrika kwa nji za rushwa, ukwepaji wa kodi na mbinu
za kutokulipa kodi, ni kiasi cha Dola za Marekani bilioni 80 tu kinaingizwa
barani humo kama uwekezaji wa moja kwa moja na misaada.

"Kwa kila Dola
moja inayokuja Afrika, Dola nyingine saba zinatoroshwa kutoka Afrika kupitia
njia haramu! Hii haikubaliki," alisema Zitto katika mkutano huo unaozungmzia
pia jinsi kampuni zinavyowajibika kwa jamii kwa kurejesha kila
wanachochuma.

Alishauri kuwa uporaji huo ni lazima uzungumziwe kama moja
ya ajenda za ushirikiano wa maendeleo baina ya mataifa ya Afrika na
yaliyoendelea.

Alisema kwa mujibu wa taarifa kuhusu uadilifu wa matumizi
ya fedha duniani ya mwaka jana, kati ya mwaka 2000 hadi 2010, zaidi ya Shilingi
trilioni 1,331.8 (Dola za Marekani bilioni 844) ziliporwa kwa mwaka kutoka nchi
zinazoendelea kati yake ya fedha hizo, asilimia 69 zilichukuliwa kutoka nchi za
Afrika.

Kwa mfano, Zitto aliuambia mkutano huo nchi kama Uswisi na
nyinginezo zenye misamaha ya kodi, zinasaidia sera zake kufanikisha utoroshaji
wa fedha kutoka mataifa masikini ya Afrika na pia zinaweka taratibu ngumu za
uwazi juu ya fedha hizo hali aliyosema inasaidia kuongeza umasikini
Afrika.

Alitaka mataifa rafiki kama Ujerumani kusaidia mataifa ya Afrika
katika juhudi za kukataa uporaji unaofanywa na mataifa yenye sera kama za
Uswisi.

Zitto aliuambia mkutano huo kwamba Tanzania inaongoza kupokea
misaada kutoka nje baada ya Iraq na Afghanistan, lakini bado zaidi ya theluthi
moja ya watu wake wanataabika katika umasikini.

"Hali ni hiyo hiyo katika
nchi nyingi za Afrika. Mageuzi ya Ushirikiano wa Maendeleo ni yale ya
kuwawezesha watu kuamua hatima yao wenyewe," alisema.

Huku akiitaka
Ujerumani kuwa mdau na mshirika wa kusaidia mabadiliko ya kimahusiano ya
uwekezaji ili mataifa ya Afrika yaamue kuhusu hatma yake yenyewe, alimnukuu
hayati Mwalimu Julius Nyerere katika kitabu chake cha Uhuru na Maendeleo
akisema:

"Mtu ajiendeleze mwenyewe akikua au akipata kipato cha
kujitosheleza na kutunza familia yake. Atakuwa hajaendelea kama atapatiwa vitu
hivi na mtu mwingine."







CHANZO: NIPASHE
 
Wenyewe ni watu safi,maadui wetu sisi ni wazungu tu!!

Kweli TUKUTUKU, UMESEMA SAHIHI. WAZUNGU TU KWA KUWA NI WAZUNGU HAO NDIO ADUI ZETU. WAARABU WAJE NA MADAWA, USHOGA, UJINGA, UAMSHO, UCHUKUAJI ARDHI NA WANYAMA WETU WALE NI WATU SAAAAFI KABISA!!!!

MCHANA MWEMA.
 
Kweli TUKUTUKU, UMESEMA SAHIHI. WAZUNGU TU KWA KUWA NI WAZUNGU HAO NDIO ADUI ZETU. WAARABU WAJE NA MADAWA, USHOGA, UJINGA, UAMSHO, UCHUKUAJI ARDHI NA WANYAMA WETU WALE NI WATU SAAAAFI KABISA!!!!

MCHANA MWEMA.
Wanataka kutufanya wajinga,hii haikubaliki hata kidogo!
 
Kweli maji hufuata mkondo. Zito ananikumbusha Jakaya alivyokwenda South Africa akakurupuka eti wazungu watulipe kama fidia ya biashara ya utumwa. Jamaa akawa hata hajui ni sehemu gani ya Tanzania ambako wazungu walikuja kuchukua watumwa. Alionekana kama katoka pangoni. Kwa nini hawa watu wanakosa ujasiri wa kuhoji Waarabu waliojizolea watumwa lukuki Africa na kwenda kuwaua kikatili huko kwao?

Haki huokoa Taifa. Achieni upendeleo. Mzani wa haki humpendeza Mungu. Kuwadai wazungu na kuwaacha mataifa mengine kama waarabu na mafisadi wa ndani ni dalili za chuki binafsi dhidi ya Wazungu na kutokuwa na nia ya dhati ya kukomboa taifa.
 
Zitto amekuwa jasiri kuwaeleza wazungu maovu na hila wanazotumia kuzipata raslimali za Africa. Ni viongozi wangapi wenye ujasiri wa kufanya hivyo? Wengi wa viongozi wetu wamebaki ni vibaraka wa wazungu na husifia hata vile visivyikuwepo, na kusisitiza ushirikiano usio na tija, ushirikiano wakinyonyaji! Ushirikiano wa bwana na Mtwana nuawezekana? Hongera Zitto!
 
Just thinking aloud!!

Hivi kama baba mwenye nyumba akialika wageni (bila kujali rangi au asili yao) waje nyumbani kwake kisha akawaruhusu waingie ndani ya nyumba yake na wawe huru kuchukua au kufanya kitu chochote watakachoona kina manufaa kwao ni halafu wale wageni wakaiba pesa na kubaka watoto ni nani wa kulaumiwa? Ni baba mwenye nyumba au ni wale wageni aliowaalika na kuwapa ruksa ya kuingia popote wanapotaka na kufanya chochote wanachoona kinafaa?

Hivi baba au mama mwenye nyumba akichukua raslimali ya nyumbani kwake akaipeleka nje (iwe kwa nyumba ndogo, kidumu au popote anapojua yeye) na kuiacha familia yake ikiwa maskini haina msaada ni nani wa kulaumiwa? Ni mwenye nyumba au wale wanaopelekewa mali ili watumie na zinazobaki waendeleze majumbani kwao?

Nadhani imefika wakati waafrika tukaacha kutafuta mchawi nje ya nchi na kuelewa ule msemo wa wahenga kuwa kikulacho ki nguoni mwako.

Kila dola inayoondolewa afrika ama ina baraka ya waafrika walioteuliwa kuwawakilisha wenzao kusimamia raslimali za nchi zao au inatoroshwa na hawa wawakilishi wenyewe na kupelekwa kwa wazungu, waarabu, wachina, etc. Tuache kupoteza muda wetu kutafuta wachawi ulaya, amerika na bara hindi wachawi wetu wapo humu humu nchini.
 
Nilivyoisoma habari hi toka IPP Media Zitto Zuberi Kabwe Mbunge kupitia Chadema amefanikiwa kufikisha ujumbe sahihi bila kigugumizi kwa mataifa haya ya nchi za magharibi wanaotumia werefu mkubwa kutuibia uchumi wetu kwa janja ya kuja kuwekeza huku wakichomoa zaidi ya wanachowekeza.

Uchambuzi wake katika mada iliyowakilisha imeonekana kutulia, ujumbe umewafikia, na huko kwenye vikao vyao vya umoja wa nchi za ulaya watayajadili.

Prof Muhongo aliposema anataka kupitia mikataba Zitto alikuwa na mtazimo tofauti. Na kama mtu alifuatilia public discourse kipindi hicho kulitokea kelele nyingi sana (toka kwa watanzania) zikipingana na kauli ya Prof Muhongo. Na wengi walikuwa na hoja kwamba 'tutakimbiza wawekezaje". Hatimaye Prof Muhongo alilazimika (alilazimishwa - maoni yangu) kubadili kauli yake.

Hii ya kulaumu wazungu kwangu mimi ni kizunguzungu maana watetezi wakubwa wa hawa wazungu ni sisi sisi! Its pointless kulaumu wazungu wakati sisi ndio tumerahusu watubake! Pointless!
 
Tatizo ni letu wananchi.viongozi wanauza nchi tunawatazama tu.wageni wanaiba rasilimali zetu tunawatazama tu.Banda anataka kudhulumu eneo letu hamna hata maandamano.lakini ngoja watoto wakojolee nanihii..!hao ndio watz bwana!
 
Nahisi kachemka kwani wanaopeleka fedha na kuficha uzunguni ni viongozi wetu na wala si wazungu. tunaowasimamia katika uwekezaji wao hao wazungu ni sisi waafrika sasa kama si wenyewe ni wapumbavu tunashindwa kujisimamia kwenye rasilimali zetu wenyewe tunawalaumu vipi wazungu? Wahindi je walionunua viwanda vyetu na kuvibomoa na kupeleka machine zote india tunasemaje?
 
Nchi ya Uswiss inanishangaza sana kutokana na kuwa na makao ya mojawapo ya Umoja wa Mataifa lakini hawao makini katika kulinda rasilimali za nchi maskini ila kufungua milango ya kupokea fedha haramu ziingizwe kwenye mzunguko wa uchumi wa nchi zao kwa njia ya mabenk.

una akili ndogo sana, hii kitu huwezi kuijua dogo.
 
nadhani na wewe hapo umekurupuka, kama vile umetoka pangoni. zito hajazungumzia utumwa bali kaongelea uporaji wa mali au plunder. zzk kaongea kweli tupu na mimi namuunga mkono, wazungu ni watu wa hovyo sana, wabinafsi na wezi hayati sana. big up zzk, umeonesha uongozi. hawa ndo mk.e.re anaenda kuwapigia magoti akidhani ni watu kumbe ni wezi. Mugabe alisema hivi... "never trust a white man till he is in the coffin"
Kweli maji hufuata mkondo. Zito ananikumbusha Jakaya alivyokwenda South Africa akakurupuka eti wazungu watulipe kama fidia ya biashara ya utumwa. Jamaa akawa hata hajui ni sehemu gani ya Tanzania ambako wazungu walikuja kuchukua watumwa. Alionekana kama katoka pangoni. Kwa nini hawa watu wanakosa ujasiri wa kuhoji Waarabu waliojizolea watumwa lukuki Africa na kwenda kuwaua kikatili huko kwao?

Haki huokoa Taifa. Achieni upendeleo. Mzani wa haki humpendeza Mungu. Kuwadai wazungu na kuwaacha mataifa mengine kama waarabu na mafisadi wa ndani ni dalili za chuki binafsi dhidi ya Wazungu na kutokuwa na nia ya dhati ya kukomboa taifa.
 
Kweli maji hufuata mkondo. Zito ananikumbusha Jakaya alivyokwenda South Africa akakurupuka eti wazungu watulipe kama fidia ya biashara ya utumwa. Jamaa akawa hata hajui ni sehemu gani ya Tanzania ambako wazungu walikuja kuchukua watumwa. Alionekana kama katoka pangoni. Kwa nini hawa watu wanakosa ujasiri wa kuhoji Waarabu waliojizolea watumwa lukuki Africa na kwenda kuwaua kikatili huko kwao?

Haki huokoa Taifa. Achieni upendeleo. Mzani wa haki humpendeza Mungu. Kuwadai wazungu na kuwaacha mataifa mengine kama waarabu na mafisadi wa ndani ni dalili za chuki binafsi dhidi ya Wazungu na kutokuwa na nia ya dhati ya kukomboa taifa.

Nashindwa kukuelewa unapomtetea Mzungu aliekutawala kimabavu karne na karne na kukuibia maliasili yako! bila shaka una damu ya kizungu! huenda ama Mama ako ni Mzungu au Baba ndio mzungu!

Mimi simtetei Muarabu au Mzungu bali nazungumza kwa ushahidi kwamba kati ya Mzungu na Mwarabu ninani alietutawala Tanganyika? sasa Kama Zito Kabwe anawalaumu Wazungu kwa uthibitisho wa kutuibia mali zetu! wewe mbona unaigeuza issue hiyo kwa waarabu?
 
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe mbunge wa Kigoma Kusini na Waziri Kivuli wa CHADEMA amewalaani wazungu kwa utapeli na uporoji mkubwa wanaoufanya dhidi ya Waafrika! nadhani umefika wakati kwa Serikali yetu kuamka na kua macho na Wazungu wote wanaoingia nchini mwetu kwani hawana nia nzuri na nchi yetu!

habari zaidi kuhusu hoja za Zito gonga hapa: Home

Mbona hakuna alicholipua, hata masai wa ngorongoro anajua hilo na wana sema kila siku. Vipi kamaliza kazi ya Uswisi?Akishindwa wataja magamba watamaliaza kazi na yeye kisiasa.Watammaiza vizuri ili wasimlipe kwa kazi anayowafanyia ndani ya CDM.
 
Utawalaanije wazungu kwa ujinga wa Mwafrika?
Nadhani this presentation should be taken in its original context,
Or at least be aligned with the efforts he did bunge lililo pita.
He talks about tax evasion, corruption and development perspectives
Hayo mambo anaongelea huku, anaongelea na huko pia
What he says there is what can influence a positive change from outside,
but na huku he said what he thinks could influence change from inside
Sasa kama mtu anachukua just this presentation and ignore the other efforts
anaweza kusema kua he is starting from the wrong side, but he is not.
we should read it as part of a broader program that started zamani.
 
Kama unatafuta ugonvi na wamasai basi nenda huko kwao uwaseme waarabu kuwa ni wabaya ,utakiona kilichomfanya twiga awe na shingo refu :boink:

fazza3tanzanya308.jpeg
 
I salute you Zitto Zuberi Kabwe!! My worry is what impacts will it have thereafter!! Do they real listened to you??
 
Back
Top Bottom