Mkuu Zitto haya ni maoni yangu binafsi.
Umekuwa ukitofautioana na viongozi wa juu wa CHADEMA kwa mambo yasiyo ya lazima, (utoto). Nimeshindwa kukusoma wewe ni mtu wa aina gani haswa.
Nndugu yangu nataka ujue hii vita inayopiganwa ni ya kukomboa taifa kutoka mikono ya CCM waliotuharibia nchi yetu kwa miaka mingi, kuiondoa CCM ndio hatua ya kwanza kuelekea kwenye mabadiliko makubwa kabisa kutokea ndani ya nchi yetu, nataka ujue na kujifunza juu ya nini kinatakiwa kufanywa kwa wakati huu.
Mkuu nataka ujue tuna kazi kubwa ya kuitoa CCM madarakani, sasa tukianza kutafuta makosa madogo madogo yanayofanywa kwa sababu ya udhaifu wa kibinaadam tutashindwa hii vita, kitendo cha wewe kusafiri na Kikwete kwenda Sudan na kukaa naye kiti kimoja tunasikia kuna mazungumzo ya siri mliongea na siwezi kuamini kama ulitumwa na chama chako kufanya vile.
Vilevile kitendo cha wewe kulazimisha Shibuda ashike nafasi ndani ya chama kumbuka Shinyanga,,, kwa kwelii sina imani na wewe kabisa inaonekana wewe unafanya mambo ambayo huyaelewi na nafikiri kuna watu wanakutumia kwa siri, siupendi huu udhaifu wako, unanifanya niamini wanasiasa wa africa vi vigeugeu.
Naomba uongozi wa CHADEMA uangalie hili, ikiwezekana abakie kuwa mbunge ili asije kutuharibia mbele ya safari.