Zitto Kabwe aondolewe nafasi ya naibu katibu mkuu

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,899
3,390
Mkuu Zitto haya ni maoni yangu binafsi.

Umekuwa ukitofautioana na viongozi wa juu wa CHADEMA kwa mambo yasiyo ya lazima, (utoto). Nimeshindwa kukusoma wewe ni mtu wa aina gani haswa.

Nndugu yangu nataka ujue hii vita inayopiganwa ni ya kukomboa taifa kutoka mikono ya CCM waliotuharibia nchi yetu kwa miaka mingi, kuiondoa CCM ndio hatua ya kwanza kuelekea kwenye mabadiliko makubwa kabisa kutokea ndani ya nchi yetu, nataka ujue na kujifunza juu ya nini kinatakiwa kufanywa kwa wakati huu.

sasa tunasikia unataka kafulila arudi chadema,sasa ndugu yangu unataka kufanya mambo yako ya ubinafsi na sisi watanzania tunaowaunga mkono unashindwa kujua nia yetu,tunataka ccm waondoke,una tamaa sana wee jamaa,halafu mambo yako unafanya kijinga sana,umetupiwa shutuma juu ya kufulila na Nccr,tunataka uzijibu ili tuweze kwenda sawa,kama nia yako ni kuwa Rais nafikiri unakosea sana kwa sababu sisi watanzania hatupo tayari kukupa nafasi kama hiyo kwa vile hufai!

Vilevile kitendo cha wewe kulazimisha Shibuda ashike nafasi ndani ya chama kumbuka Shinyanga,,, kwa kwelii sina imani na wewe kabisa inaonekana wewe unafanya mambo ambayo huyaelewi na nafikiri kuna watu wanakutumia kwa siri, siupendi huu udhaifu wako, unanifanya niamini wanasiasa wa africa vi vigeugeu.

Naomba uongozi wa CHADEMA uangalie hili, ikiwezekana abakie kuwa mbunge ili asije kutuharibia mbele ya safari.
 

massai

JF-Expert Member
May 2, 2011
653
136
Kamanda zito ni wa ukweli,acha hizo immagination zako.huwezi taja mabadiliko bila kutaja kabwe.
 

Smile

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
15,360
11,568
Kitendo cha wewe kusafiri na kikwete kwenda sudan na kukaa naye kiti kimoja tunasikia kuna mazungumzo ya siri mliongea na siwezi kuamini kama ulitumwa na chama chako kufanya vile.
yaani huyu kijana anajipotezea dira yake kwa kukaa na wapotezaji CDM angekuwa ccm angefaidi zaidi ya hiyo red
 

Mzalendo

Senior Member
Mar 10, 2006
181
32
Mkuu Zitto haya ni maoni yangu binafsi.

Umekuwa ukitofautioana na viongozi wa juu wa CHADEMA kwa mambo yasiyo ya lazima, (utoto). Nimeshindwa kukusoma wewe ni mtu wa aina gani haswa.

Nndugu yangu nataka ujue hii vita inayopiganwa ni ya kukomboa taifa kutoka mikono ya CCM waliotuharibia nchi yetu kwa miaka mingi, kuiondoa CCM ndio hatua ya kwanza kuelekea kwenye mabadiliko makubwa kabisa kutokea ndani ya nchi yetu, nataka ujue na kujifunza juu ya nini kinatakiwa kufanywa kwa wakati huu.

Mkuu nataka ujue tuna kazi kubwa ya kuitoa CCM madarakani, sasa tukianza kutafuta makosa madogo madogo yanayofanywa kwa sababu ya udhaifu wa kibinaadam tutashindwa hii vita, kitendo cha wewe kusafiri na Kikwete kwenda Sudan na kukaa naye kiti kimoja tunasikia kuna mazungumzo ya siri mliongea na siwezi kuamini kama ulitumwa na chama chako kufanya vile.

Vilevile kitendo cha wewe kulazimisha Shibuda ashike nafasi ndani ya chama kumbuka Shinyanga,,, kwa kwelii sina imani na wewe kabisa inaonekana wewe unafanya mambo ambayo huyaelewi na nafikiri kuna watu wanakutumia kwa siri, siupendi huu udhaifu wako, unanifanya niamini wanasiasa wa africa vi vigeugeu.

Naomba uongozi wa CHADEMA uangalie hili, ikiwezekana abakie kuwa mbunge ili asije kutuharibia mbele ya safari.
Certified pumba, vipi umepona kisukari?
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
27,818
30,381
Kikwete angesafiri ndege moja na Kiongozi wa Upinzani ndani ya Bunge - mngesemaje? Yaani ukiwa mpinzani unazuiwa ku chat na wanasiasa wenzako wenye itikadi tofauti?

Ya Shibuda ni mengine kabisa, mbona unachanganya NSANSA na SWARU? (external service hiyo)
 

IGWE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
9,341
6,887
atafutwe mtu makini atakayeweza kazi mkuu

hata mimi nilianza kuhisi hilo mkuu,...na huu nafikiri ni ukweli ingawa wengi watakuja na hoja za kupinga ila ukweli ni kwamba huyu jamaa siku hizi ni kama ana ajenda fulan isiyoeleweka ndani ya chama,...nafikiri na huu ndio muda mwafaka wa kumtafuta mtu wa kum-replace zitto
 

ngwini

JF-Expert Member
Apr 5, 2011
482
89
Zitto watu walimsema weweee, yakapita na sasa wanaanza tena, DIRECTOR umesema wakiwa Sudan, Zitto na Jk walikaa kiti k1, is it possible for two people of the same gender ? May b...mh!
 

Nduka Original

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
1,000
794
Nisharushaka thread hapa nikasema wafuatao si wanachadema halisi

1. Shibuda
2. Marando
3. Zitto

CCM is investing massively to tear down CDM and some of their leaders have been murmuring that Zitto is not CDM any more.
 

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
5,703
1,877
Kweli mkuu Director1 Huyu Bwn Zitto haeleweki,

Kwanza uchaguzi wa Igunga kabla ya kuongea na wenzake yeye aliwahi kupost matokeo na kuomba watu wakubaliane kushindwa!!!!!!!! Kabla hatujakaa sawa akasisitiza kuwa tukubali matokeo kirahisi tuu, kama vile haikumpa taabu kushindwa uchaguzi!!!!! Tunajua yeye na Bwn Kafumu wanafahamiana coz walikuwa wote kwenye tume ya madini, zimwi likujualo--------!!!!!!!!

Sasa huyu Bwn vipi yuko so deep with the maghamba caucus, what do we expect!!! Kuna hints kibao za kona za huyu Bwn!!!!!!!! Kama kuna lengo la kuchukua dola, CDM chukua uamuzi mgumu mambo kabla hayajaharibika!!!
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
27,818
30,381
Kweli mkuu Director1 Huyu Bwn Zito haeleweki, kwanza uchaguzi wa Igunga kabla ya kuongea na wenzake yeye aliwahi kupost matokeo na kuomba watu wakubaliane kushindwa!!!!!!!!
ni vizuri kuwa na uhakika na uchaoongea, kukurupuka bila kufanya uchunguzi unaonekana kama umetoka kutibiwa kisukari sugu.
 

king'amuzi

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
615
225
huwezi kuwa na product 100% pure lazima kuwe na makape(impurity) zinazofanya kuonekana kwa pure so usiogope mambo yako fresh.uliowataja wote ni wapiganaji ambao wanatengenezewa sana temptation na wapinzani wetu.
 

WA-UKENYENGE

JF-Expert Member
Oct 1, 2011
2,920
1,226
Lets wait and see kama haya yatakuwa ni ya kweli, adhabu ya watu kama hao huwa ni kali ingawa wengi huwa hawaielewi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom