Stephen Buloya
Member
- Aug 1, 2007
- 38
- 13
Kuna tatizo kubwa la utekelezaji. Kamati inatoa mapendekezo, serikali haitekelezi. Akizungumza kuhusu NSSF na chuo kikuu cha dodoma "Itakumbukwa kuwa pendekezo hili limetolewa kwa mara ya tatu mfululizo na Kamati kwenda Serikalini na hadi sasa halijatekelezwa". CAG naye kila mwaka anatoa ripoti za malipo kwa wafanyakazi hewa na mapendekezo ya kuweka performance contracts kwa wakurugenzi wa halmashauri na kutokuwepo kwa wabunge katika bodi za wakugurugenzi kwenye taasisi na mashirika ya umma. Lakini hakuna utekelezaji. Mimi nahdani imefika wakati wabunge, hasa wabunge wa upinzani wabuni njia mbadala ya kushinikiza serikali ifanya mabadiliko yanayo pendekezwa na wataalamu. Hizi ripoti na mapendekezo wamezizoea. Process ina fanyika, ripoti inatolewa, wahusika wana sikiliza, hakuna utekelezaji. It is like a cycle that keeps repeating itself.