Zitto Kabwe 'amwaga Sumu' Kamati ya Mahesabu ya Mashirika ya Umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto Kabwe 'amwaga Sumu' Kamati ya Mahesabu ya Mashirika ya Umma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nice 2, Apr 18, 2012.

 1. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kupata taarifa kamili, fungua attachment,

  7.2 Mapendekezo ya Kamati Mheshimiwa Spika,kwa kuzingatia kanuni za kudumu za Bunge Toleo la mwaka 2007, Naomba kuwasilisha Mapendekezo ya Kamati kama ifuatavyo;

  7.2.1 Mheshimiwa Spika,
  kwa kuwa Kamati imebainisha kuwa Mashirika mengi ya Umma hayana mitaji ya kutosha kujiendesha, na kwa kuwa kutokuwepo kwa mitaji kunasababishwa zaidi na kutokuwepo kwa mfuko wa uwekezaji wa Umma ( Public Investment Fund), kwa hiyo Kamati inaendelea kupendekeza kuwa Mfuko wa uwekezaji wa Umma uanzishwe mara moja ili kwa utaratibu utakaoonekana unafaa baadhi ya Mashirika ya Umma yenye kupata faida yaanze kuweka fedha katika mfuko huo ili kusaidia Mashirika ya Umma yasiokuwa na mitaji ila ni strategic kwa Taifa letu.

  7.2.2 Mheshimiwa Spika,
  kwa kuwa Kamati imebaini viashiria vya Fedha za kufidia wakulima wa Pamba kutokana na anguko la uchumi duniani, kutowafikia walengwa kupitia kwenye Bodi ya Pamba Tanzania, na kwa kuwa viashiria hivyo vinatokana na ukaguzi wa Hesabu za Bodi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30,2010 ambao umeonyesha kuwa baadhi ya walengwa wa fedha za kunusuru bei ya Pamba wamekiri kutopewa fedha hizo na hivyo Mkaguzi kutoa hati yenye shaka kwa Bodi ya Pamba. Kwa hiyo Kamati inapendekeza kuwa, Kamati inapendekeza kuwa Bodi ya Pamba, iliyopo sasa hivi, ivunjwe na iundwe upya. Aidha Kamati inaitaka Serikali ifanye ukaguzi na uchunguzi maalumu ili kubaini iwapo fedha za kufidia anguko la bei ya Pamba ziliwafikia walengwa kama ilivyokusudiwa na kisha kuchukua hatua stahili kutokana na uchunguzi huo na Bunge lipewe Taarifa ya matokeo ya Uchunguzi huo.

  7.2.3 Mheshimiwa Spika,
  kwa kuwa katika tathmini yake ya viwanda vilivyobinafsishwa vya ubanguaji Korosho, imebainika kuwa baadhi ya wawekezaji wamekiuka kwa makusudi mikataba ya uendeshaji wa Viwanda hivyo, na kwa kuwa kwa kufanya hivyo wamesababisha Taifa kuendelea kusafirisha korosho ghafi kwenda Nje ya Nchi na hivyo kuondoa fursa ya wakulima kupata faida ya kutosha na kupunguza ajira Nchini, kwa hiyo Kamati inapendekeza kuwa Serikali ichukue uamuzi wa kuvirejesha viwanda vyote vya kubangua Korosho vilivyobinafsishwa na wawekezaji wake kushindwa kuviendeleza ili kuona namna bora ya kuwekeza kwenye ubanguaji wa korosho ikiwa na pamoja na Serikali kusisitiza umuhimu wa kuuza Korosho iliyobanguliwa Nje ya Nchi kwa kuwajengea uwezo wakulima wa kubangua Korosho.

  7.2.4 Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Kamati imebaini kuwa Bodi ya Madawa Tanzania (MSD) inatumia takribani siku 21 ili kukamilisha mchakato wa kuondoa dawa bandarini , na kwa kuwa ucheleweshaji huo una athiri usambazaji wa dawa hapa Nchini kwa wakati muafaka na muda mwingine kusababisha dawa kuharibika kabla ya kuwafikia walengwa na hivyo kusababisha Hoja kadhaa za Ukaguzi wa Hesabu, Kamati inapendekeza kuwa Bodi ya madawa ianze mchakato wa kuwa na ghala maalum (bonded ware house) ili kurahisisha utoaji wa dawa bandarini mapema iwezekanavyo na zikaguliwe huko na Mamlaka zinazodhibiti ubora kama Shirika la Viwango la Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA). Kamati inapendekeza kwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha na TRA kuharakisha jambo hili kabla mwaka wa fedha haujakamilika.

  7.2.5 Mheshimiwa Spika
  , kwa kuwa Kamati imebaini na kuthibitisha ukosefu wa mitaji ya kutosha na uwekezaji mdogo wa serikali katika baadhi ya Mashirika ya Umma ili yatekeleze mipango mikakati muhimu kwa manufaa ya Umma na baadhi ya Mashirika hayo ya Umma ni yale ambayo ni chachu ya maendeleo ya Taifa (strategic parastatals) , na kwa kuwa ukosefu wa fedha na mitaji unazorotesha juhudi za Taifa letu kupata maendeleo, kwa hiyo Kamati inapendekeza kuwa Serikali itoe bajeti ya kutosha kwa Mashirika yafuatayo, Baraza la Taifa la uwezeshaji kiuchumi ( NEEC) ambalo linahitaji kiasi cha shilingi bilioni 25.5 kutekeleza majukumu yake ya kisheria, Shirika la Tija la Taifa (NIP) na Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) ili Mashirika haya yaweze kutekeleza mipango yake ipasavyo ambayo mingi imelenga kuinua Maisha ya Watanzania wa kawaida waweze kushiriki shughuli za kiuchumi ipasavyo.

  7.2.6 Mheshimiwa Spika,
  kwa kuwa Taifa linakabiliwa na Changamoto kubwa zinazohusiana na shughuli za usimamizi wa Nishati ya Gesi asilia na Mafuta na hasa uchimbaji na usimamizi wa mapato yatokanayo na gesi asilia, na kwa kuwa tunalo Shirika la Umma la Mafuta na Petroli (TPDC) ambalo ndilo lenye jukumu la kuendeleza Sekta hiyo hapa Nchini, na kwa kuwa Shirika hilo linakabiliwa na changamoto kubwa ikiwamo kutojiendesha kwa mujibu wa Amri ya Uanzishwaji wake (establishment order) na hivyo kukwama kutekeleza majukumu yake ipasavyo, kwa hiyo basi Kamati inapendekeza kuanzia sasa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) lijiendeshe kwa mujibu wa Amri (order) ya uanzishwaji wake[1] ( TPDC Establishment Order of 1969 na pia Public Corporation Act of 1992) ikiwa ni pamoja na kubaki na fedha zote inazokusanya kama Mashirika mengine (retention) badala ya kurudishwa Wizara ya Nishati na Madini. Aidha Kamati inasisitiza kuwa, Wizara ya Nishati na Madini isiingilie utendaji kazi wa kila siku wa TPDC, ili Shirika hili lifanye kazi kwa ufanisi, kwa uhuru na kwa misingi ya uanzishwaji wake.

  7.2.7
  Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kumedhihirika wazi ukosefu wa ufanisi katika uendeshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kulikosababishwa na matatizo ya Menejimenti iliyokuwepo na mikataba mibovu (mfano ukodishwaji wa ndege ya Air bus), Kamati inapendekeza hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote waliohusika na uingiaji wa mikataba hiyo, lakini pia kamati inapendekeza Serikali ifikirie uundwaji upya wa Shirika la Ndege la Taifa.

  7.2.8 Mheshimiwa Spika,
  kwa kuwa tathmini ya ubinafsishaji wa Mashamba ya Mkonge imedhihirisha kuwa, Hali ya mashamba mengi siyo nzuri. Kati ya mashamba yote yaliyobinafsishwa, ni mashamba mawili tu ya Mkambara na Mwelya yanayoridhisha kwa namna yanavyohudumiwa. Kamati inashauri serikali ifuatilie kwa ukaribu uendelezaji wa mashamba ili sera ya ubinafsishaji iwe na matunda yaliyokusudiwa. Aidha ili kuepuka migogoro na Wananchi, Maeneo ya mashamba yaliyovamiwa na wananchi yaachiwe kwa wananchi hao na mipaka ya mashamba ilindwe ipasavyo, na kwa wawekezaji walioshindwa kuendeleza mashamba ya Mkonge, Serikali iyarudishe na kuyagawa upya ikiwezekana hata kwa Wakulima wadogo. Fikra kwamba Mkonge lazima ulimwe na Wakulima wakubwa imepitwa na Wakati, Serikali iwawezeshe Wakulima wadogo kupitia Taasisi za fedha walime Mkonge katika Mashamba hayo.

  7.2.9 Mheshimiwa Spika, Kutokana na ongezeko la riba inayotokana na Mkopo ambao Serikali imechukua kutoka kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii kugharimia ujenzi wa Chuo Kikuu Dodoma, Kamati inatoa pendekezo mahsusi kwa Serikali kutia saini Makubaliano ya Mkopo baina yake na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini kwa fedha walizotoa kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma. Ni vema ikafahamika kuwa Fedha hizi ni mali ya Wanachama na hivyo ni lazima zilindwe ipasavyo. Itakumbukwa kuwa pendekezo hili limetolewa kwa mara ya tatu mfululizo na Kamati kwenda Serikalini na hadi sasa halijatekelezwa; Kamati inataka kupata maelezo ya Serikali juu ya jambo hili, kwa hiyo Kamati inaliomba Bunge liazimie sasa, na kuitaka Serikali kutia saini makubaliano hayo ili madeni ya Mifuko ya Jamii yawe salama kwa mujibu wa Sheria ya Dhamana, mikopo na ruzuku. Kamati inasisitiza kuwa madeni ambayo hayana Mashaka yaanze kulipwa mara moja.

  7.2.10 Mheshimiwa Spika,
  kwa kuwa Mkataba baina ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Star Times International Communication una mapungufu kadhaa ya kisheria na ambayo yamebainishwa na Mkaguzi wa Hesabu wa TBC baada ya kuchambua Mkataba na Taarifa ya Hoja za Ukaguzi,na kwa kuwa mapungufu hayo yanaweza kuwa na athari katika utendaji wa TBC kwa siku zijazo , kwa hiyo basi Kamati inapendekeza kuwa, Serikali iupitie upya Mkataba huo ili kuainisha maeneo ya maboresho, aidha Serikali ifanye utaratibu wa kuangalia namna nzuri ya kutoa fedha kwa uendeshaji wa TBC ili kiwe chombo cha utangazaji wa Umma chenye kujiendesha kwa uhuru na kwa maslahi ya Umma.

  7.2.11 Mheshimiwa Spika, kwa kuwa suala zima la ubinafshaji wa yaliokuwa Mashirika ya Umma limekuwa na changamoto kubwa, zaidi kutokana na baadhi ya mali za Mashirika kuuzwa kwa bei isiyolingana na thamani , pia Mikataba mingi ya ubinafsishwaji kukiukwa na wawekezaji, na kwa kuwa kwa kiasi kikubwa zoezi hili halikufanikiwa katika maeneo mengi, na kwa kuwa Bunge kama mwakilishi wa Wananchi lingependa kufahamu faida na changamoto ya zoezi zima la ubinafsishaji ili Waheshimiwa Wabunge wapate nafasi ya kujadili zoezi hilo kwa uwazi, hivyo, Kamati inapendekeza Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuendesha Uchunguzi Maalum (inquiry on Privatisation Policy in Tanzania ) kwa kushirikiana na Shirika Hodhi la yaliyokuwa Mashirika ya Umma ( CHC) , Taarifa ya uchunguzi huo iwasilishwe na kujadiliwa ndani ya Bunge mapema iwezekanavyo. Kamati inaazimia kufanyika kwa " public inquiry" katika zoezi la ubinafsishaji, uchunguzi huu utakuwa wazi na Taarifa yake itajadiliwa Bungeni na kuwa wazi kwa Wananchi.

  7.2.12 Mheshimiwa Spika,
  kwa kuwa changamoto zinazolikabili Taifa katika Sekta ya mafuta na gesi ni kubwa na hivyo kuhitaji Mkakati wa Makusudi wa muda mrefu wa kukabiliana nazo, na kwa kuwa Mashirika ya Umma ikiwa ni pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli( TPDC) ndio wadau wakubwa wa kuhakikisha Nchi inanufaika ipasavyo na Sekta ya gesi na Mafuta, na kwa kuwa Makampuni yanayotafuta mafuta na gesi hapa Nchini yamekuwa yakipeleka fedha TPDC ili ziweze kutoa mafunzo kwa watumishi ili kuongeza uelewa katika Sekta hiyo, kwa hiyo Kamati inapendekeza kuwa, kuanzishwe Mfuko Maalumu (Trust Fund) ili fedha zote za Mafunzo ziwekwe humo ili kupanua wigo kwa watanzania wote ambao wangependa kusomea fani za gesi na mafuta waombe ufadhili katika Mfuko huo wapate mafunzo badala ya fedha za mafunzo kutumika kwa watumishi wachache wa TPDC na Wizara ya Nishati na Madini na muda mwingine kutumika kwa shughuli zisizo za Mafunzo kama ilivyobainishwa na Kamati ya Nishati na Madini.

  7.2.13 Mheshimiwa Spika,
  kwa kuwa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) linakabiliwa na hali mbaya ya kifedha unaotokana na gharama kubwa za kununua umeme kutoka kwenye makampuni binafsi (kwa mfano IPTL pekee wanalipwa shilingi bilioni 64.2 kwa mwaka), na kwa kuwa gharama za ununuzi wa umeme ndio zinasababisha TANESCO iendelee kupata hasara kila mwaka (kwa mfano hasara ya shilingi bilioni 47.3 kwa mwaka 2009/2010) na hata kuongeza gharama za umeme kwa Wananchi, Kamati inapendekeza kuwa, katika muda mfupi baada ya mtambo wa TANESCO wa (jacobsen) kuanza kazi waachane na kununua umeme wa gharama kubwa kama ule wa IPTL, na katika muda mrefu Kamati inasisitiza kufanyike uwekezaji wa kutosha katika kuzalisha umeme. Miradi ya Umeme inayopendekezwa kufanywa na Mshirika ya Umma ipewe kipaumbele sana ili kuwepo na mchanganyiko sawia (right balance) kati ya uwekezaji binafsi na ule wa Umma.

  7.2.14 Mheshimiwa Spika,
  kwa kuwa Taarifa za uchunguzi kuhusiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) uliofanywa na Kamati Ndogo ya POAC ulikamilika na Taarifa kuwasilishwa kwako, na kwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali pia amekamilisha uchunguzi kuhusu TBS na utekelezaji wa majukumu yake ya kisheria, Kamati inapendekeza sasa Serikali ilete Taarifa ya utekelezaji na majibu ya Hoja za Taarifa hizo mbili ili Bunge liweze kupata nafasi ya kuzijadili kwa kina.

  [HR][/HR][1] TPDC Establishment Order of 1969 and Public Corporation Act, 1992

  [​IMG]
  Zitto akiwasilisha ripoti
   

  Attached Files:

 2. T

  Triple DDD Senior Member

  #2
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hongera bwana zito, tuko nyumba yako.
  Kipaji chako ni kikwazo kwa wengine na jinsi unavyoona mbali huwakwaza watu.

  Mafikira yako ni sahihi ila washirikishe wengine kasi zako ili muende pamoja
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hakika vijana wa CDM wanafanya kazi bora kutokana na uongozi uliotukuka wa Mbowe na Slaa.
   
 4. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Naona mkuu umeathiriwa sana jambo fulani.
  The guy is good Independently, give him his credit mzee.
   
 5. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Zitto kaiva jamani lakini tusiwasahau slaa na mbowe ndo wanaomlea kijana.Big up zitto
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu
   
 7. i

  interprevist Member

  #7
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  huwezi kutenganisha mafanikio yake na viongozi wake
   
 8. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,215
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280
  Good job. Ukiacha mapendekezo ya kamati ya Zitto, Nimependa pia ripoti ya kamati ya Mrema pamoja na mapendekezo yake. Iwapo magamba wana lengo la kunyanyuka na kurudisha imani yao kwa wananchi, basi hawana budi kuwawajibisha waliopendekezwa kuwajibishwa na kamati hizi.
   
 9. m

  mob JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  shida moja tuliyonayo tuna maneno mazuri ila hawayafanyii kazi
   
 10. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Dr Mrema kamati yake inafanya kazi nzuri, imetoa mapendekezo mazuri. Kama Serikali ingekuwa inafanyia kazi haya mapendekezo hakika tungepata mafanikio
   
 11. U

  Uswe JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  huyu bwana hata kama angekua chini y uongozi wa mwenyekiti wa ccm bado angeng'ara tu
   
 12. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tatizo wanasiasa wanaibua maovu ya watendaji mwisho wa siku wanaishia kupewa rushwa na watendaji,imekuwa kama sehemu ya kupatia riziki.business as usual.
   
 13. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sasa hapo anasema tuache kununua umeme wa IPTL kwani mkataba wetu na IPTL unasemaje kwanza? yasije kuwa yale yale ya Dowans!
   
 14. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280

  hakuna cha mkataba wala nini , umeme wa IPTL ni bei sana tena mafuta tunanunua sisi na bado umeme tunalipia
   
 15. e

  ephrem Member

  #15
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  According Albert Einstein "You cannot solve the problem by using the thinking that created it". Kwahiyo hoja kwamba Bwana Zitto angekuwa chini ya uongozi wa ccm angengara tu ni dhaifu sana!
   
 16. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Always mapendekezo huwa hayafanyiw kaz!
   
 17. Judi wa Kishua

  Judi wa Kishua JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 525
  Trophy Points: 180
  zitto njia nyeupe ya urais,hakuna wa kukuzuia.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Binafsi bado niko kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na hasa kama NSSF ambao ndio mfuko mkubwa. Nikisoma ripoti ya CAG na taarifa ya Zitto najiuliza inakuwaje NSSF na mifuko mingine ikakubali kutoa fedha za wanachama kwenda kwenye miradi ya serikali bila makubaliano yenye kueleweka na serikali hiyo? Binafsi ningependa viongozi wa mifuko hii wa wajibishwe!! Iweje sasa baada ya miaka kupita na madeni kutolipwa ndio watu waingie mikataba?
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Baada ya miaka miwili shirika hili la NSSF linaweza kuwa taabani kifedha maana watu wanakimbiza pesa zao wanajitoa.
   
 20. b

  busar JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  mwanakijiji, nakubaliana nawe, lkn sheria na sera zetu ndo shida, mifuko imefanya kazi ya ukarim na "kujenga heshima bar"
   
Loading...