Ben Saanane,
Ulikuja jukwaani ukamshutumu ZZK kuwa alikuwa kiongozi wa kundi la wasaliti wa CDM ambalo wewe mwenyewe ulikuwa mshiriki. Ukaliambia jukwaa la JF kuwa una ushahidi wa mambo yote uliyokuwa umeyasema juu shutuma ulizotoa.
Mwenyekiti wa BAVICHA katika taarifa yake kwa ya vyombo vya habari baada ya kikao kilicho fukuza "masalia" alise wewe Ben Saanane umesamehewa kwa sababu umekiri makosa na umeomba msamaha kwa kumchafua kiongozi mwandamizi wa CDM (hakutajwa jina ila kila anaefuatilia JF anamjua ni nani, walisoma post zako). Siku ya pili ukaja ukapinga hapa JF kwa kutaja jina kuwa hujawahi wala hutawahi kumuomba msamaha ZZK kwa sabab huna kosa lolote ulimfanyia ZZK, jambo linaloonesha kimisingia ni kweli ulikuwa na ushahidia wa kutosha katika shutuma zako kwa ZZK.
Yaliyojiri juzi yamejiri na wana JF wameyasikia, kila mmoja moyoni anajiuliza hivi hili suala la ZZK na ushahidi wa Ben Saanane ulipolekwa CDM limeishia vipi? Inawezeka kukawa na ushahidi wa uhakika(kiasi cha kupingana na mwenyekiti wako wa BAVICHA juu ya wewe kuomba msamaha) wa sauti na video wa ndugu ZZK akisaliti chama halafu CDM wakamuacha hivi hivi tu?
Hebu tufanunulie au nifafanulie hili jambo limekuaje ndugu Saanane!
Je, hivi ni kweli ulipeleka ushahidi wako wa uhakika ndani ya chama?
Je, CDM kimetupilia mbali au kudharau ushahidi wako?
Je, kuna mchakato wowote unaendelea ndani ya chama kuhusu shutuma zako hizi kubwa kubwa kwa ndugu ZZK?
Je, bado uko katika msimamo ule ule kuwa ZZK ni msaliti na alikuwa kiongozi wako katika usaliti?
Je, kwa nini usiuweke ushahidi hapa JF kama ulivyo weka shutuma hasa ukizingatia kuwa chama hakija chukua hata hatua ya kumjadili mtuhumiwa ZZK?
Je, wewe kama mwana CDM unaemini katika mabadiliko ya kweli unalionaje hili suala ya ndugu ZZK kubaki ndani ya CDM ilihali wewe una ushahidi usio na mashaka kuwa anakisaliti chama?
Ben,
Ulikuja hapa JF ukayaanzisha na ukatueleza haya mambo, hebu yamalize basi. La sivyo picha inageuka, tena inageuka sana. Wewe unakuwa ndio msaliti(tena usaliti wa aina mbaya kabisa) na ZZK anachukua ushujaa na pongezi zote wana JF walizokupa hapa jukwaani.
Zitto,
Ndugu naomba nikuulize swali. Kama yote aliyosema Ben Saanane juu yako si ya kweli na amekusingizia shutuma zote, na msingi wa kusamehewa kwake BAVICHA ni kuomba msamaha kwa makosa yake yote ikiwemo kukushutumu wewe, na ndugu Saanane amepinga hapa JF kuwa hajawahi kuomba wala hatawahi kukuomba msamaha juu ya suala la kukushutumu kuwa kiongozi wa masalia, mbona huyu kijana hajachukuliwa hatua yoyote na chama? mbona vijana wenzake walio toa shutuma dhidi ya viongozi wengine wamechukuliwa hatua na chama?
Hebu tufafanulieni hili jambo, mmoja kati yenu hatakiwi aendelee kuwepo CMD, ila nyote bado mpo CDM!! Kuna jambo haliko sawa hapo.
Huu ufa tuuzibe leo, kabla hujamuangukia mtu halafu ukatulazimu tujenge ukuta.