Zitto chupuchupu kutimuliwa CHADEMA!

Zitto chupuchupu kutimuliwa CHADEMA!

Nashukuru kuwa mnafahamu kuwa ndani ya CDM kuna Ngano na Maguku hivyo kung'oa magugu kunahitaji umakini na busara kubwa maana inaweza kuwa balaa na hasara kubwa. Nashukuru kwa busara ya viongozi wa CDM.
 
Kamati kuu wamekaa watu wenye hekima na busara.................... tunataka haki, kila moja apewe anachostahili!
Kama Zitto ni Prezoo na shibuda ni PM7, tafuta uhusiano wa Zitto na Shibuda.

Hapa inabidi tutumie Quadratic Equation ili jibu liwe 0
Mkuu Mungi,hivi kiongozi ni mwenye kundi Chadema ni Zitto peke yake?
 
Chadema sasa imekuwa,INAJITOSHELEZA KUJIHUJUMU YENYEWE bila KUHITAJIKA MAMLUKI kutoka nje.TUKANANENI,KASHIFIANENI,VUANENI NGUO HUMU JF,HALAFU MJIDANGANYE KWAMBA NI VIJANA WA LUMUMBA,ENDELEENI KUFICHA UCHI,MUONE KAMA HAMJAZAA KONOKONO.
 
chama makini ni kile kinachowachukulia watu hatua bila kujali wadhifa, rangi au tabaka, na CHADEMA imekua makini katika kutekeleza hayo ispokua tu inapofika kwa Zitto. Je ni kweli kuwa hufahamu ni jinsi gani Zitto amekua akifanya mambo yake kinyume kabisa na misingi ya chama. Sasa kama chama kikianza kuwa na matabaka hasa katika kuchukua maamuzi hatutakua tofauti na CCM waliowafunga kima Farijala Hussein na kuwaacha KAGODA, au wanaposhinwa kuwashughulikia magamba aka mapacha watatu. Huoni kuwa misingi ya chama hapo itaanza kuwa ya kiupendeleo? hasa pale viongozi wa chini wanapowajibiswa kwa adhabu kali kali ikiwemo kufukuzwa uanachama, lakini huyu bwana haguswi? yeye ni nani?

kwa misingi hii ntarudisha kadi


Kaka umenena ukweli kbs...hata watu wenye akilizao walikua wanavutiwa na CDM na kui support hata bila kuwa wanachama au wanufaika lakini kwa swala hili wamejua kabisa kweli CDM ni chama cha kitabaka.
 
chadema hawana uwezo wa kumuondosha Zitto, Zitto ndiye pekee aliyeipaisha chadema, nani alikuwa anaijuwa chadema kabla ya Zitto? labda kwa kina Mbowe na wakweze tu.

Huu ni ukweli ambao unawauma Chadema, madai yanaletwa kila kukicha juu ya usaliti wa Zitto, hapa wapo kumtetea Mbowe hii habari siyo ya kweli na ni mtu wa kutochukua maamuzi ya pupa.

Wamesahau wiki chache zilizo pita walidai kuwa Zitto ni msaliti na atavuliwa uongozi sababu ni msaliti. Inakuwa kama vile hawajitambui katika hoja zao linapokuja suala la Zitto. Mie nina hamu afukuzwe nione nguvu ya Chadema katika maamuzi iko kiwango kipi.

Na asipofukuzwa ina maana hata habari na ushahidi ulioletwa na Ben Saanane wote ni magumashi siyo kweli na kuwa alikuwa anatafuta cheap popularity!
 
Ni makosa kuwazuia wanahabari wasiwepo ndio maana wanaweza kuandika namna hii. Hakukuwa na sababu ya msingi ya kuzuia waandishi wa habari kushuhudia ufanyaji kazi wa demokrasia...

Wewe mwanakijiji na wewe umezidi kujifanya mjuaji DEMOKRASIA pia ina mipaka yake yani watu wanapanga mipango yao na mikakati lazima waandishi wawepo kwani si watapewa taarifa na mikutano ya hadhara si ipo sikuungi mkono ata kidogo tatizo unaishi kwa kanuni za darasani sana.
 
Zitto ni zaidi ya superstar cdm,hakuna anayemuweza kwa kujenga na kusimamia hoja
 
ikifika december bado Zitto Kabwe hajafukuzwa ndani ya CHADEMA ntarudisha kadi yangu kwa hiari...nikiwa kama mwanachama wa kawaida sana, nasikitiswa sana na jinsi kijana huyu anavyohujumu mipango na mikakati ya chama, zito ni mbinafsi, msiri, mchochezi, mpika majungu na M-CCM pia...anamatukio ya ajabu ajabu sana..SHAME ON ZITTO ZUBERI KABWE.
Ni haki yako kurudisha kadi kama kusudio lako ni kupata raha na amani katika moyo wako. Hivi unadhani kipi chenye thamani ndani ya CDM kati ya kadi yako na ZZK??
 
Chadema hawana uwezi wa kumtimua Zitto ilo wanalijua wajaribu waone.

Sema kada , aka mtambo wa kupika majungu kwa mujibu wa Kinana , hili nalo ni jungu so unapuuzwa kwani weka mbali na Tembo ametufungua macho .......kuhusu makada wa CCM
 
Mtasema sana wana wa CDM lkn ukweli utabaki palepale jamii iliyowaheshimu kuwa mna nia ya kweli kukomboa taifa hili..,imejua kuwa hata nyie ni wababaishaji.....!Mziki wa gamba mlioutumia umewashinda nyie kuucheza. Na stop kujifanya mnaleta ukombozi kumbe mnapanga matabaka yenu na kuonea vijana wadogo kina Shoza na wenzake.

Na kuogopa huku kufanya maamuzi fair inaonesha kabisa uongozi wa juu una madudu na umeoza kama alivyosema mchangiaji mmoja kwahiyo hamna uwezo wa kuongoza nchi reffer SITTA.
 
Wewe mwanakijiji na wewe umezidi kujifanya mjuaji DEMOKRASIA pia ina mipaka yake yani watu wanapanga mipango yao na mikakati lazima waandishi wawepo kwani si watapewa taarifa na mikutano ya hadhara si ipo sikuungi mkono ata kidogo tatizo unaishi kwa kanuni za darasani sana.
Hapo kwenye red nimecheka mpaka basi
 
Hili Gazeti ni la kidaku! Yaani mtu anawezaje kuibua hoja kama hiyo ya kufukuza mtu eti kwenye ajenda za mengineyo! Shame on you Mtanzania! Naona utulivu ulio ndani ya CHADEMA unawatia kichefuchefu, kajinyongeni basi!
 
Huu ni ukweli ambao unawauma Chadema, madai yanaletwa kila kukicha juu ya usaliti wa Zitto, hapa wapo kumtetea Mbowe hii habari siyo ya kweli na ni mtu wa kutochukua maamuzi ya pupa. Wamesahau wiki chache zilizo pita walidai kuwa Zitto ni msaliti na atavuliwa uongozi sababu ni msaliti. Inakuwa kama vile hawajitambui katika hoja zao linapokuja suala la Zitto. Mie nina hamu afukuzwe nione nguvu ya Chadema katika maamuzi iko kiwango kipi. Na asipofukuzwa ina maana hata habari na ushahidi ulioletwa na Ben Saanane wote ni magumashi siyo kweli na kuwa alikuwa anatafuta cheap popularity!

Mkuu,
Hilo huna hata ya msukumo kutaka kubainisha.

Huyo double agent anatumia nguvu nyingi za kimbea kutaka kuuaminisha umma kama Zitto ni adui number one wa maendeleo ya CDM bila kujua historia ya Zitto ndani ya chama. Yeye ndiye wa kuogopwa kama ukoma katika umaarufu wa kugonganisha viongozi kwa faida yake ya kisiasa.

What's really matter, ukweli ni ngao katika vita.

Fortunate, Aliingia ndani ya chama kwa mlango wa umbea na atatoka kwa mlango huo huo.

Time is in our side.
 
Ni haki yako kurudisha kadi kama kusudio lako ni kupata raha na amani katika moyo wako. Hivi unadhani kipi chenye thamani ndani ya CDM kati ya kadi yako na ZZK??

Watu wenye mawazo kama haya ni wavivu na wachovu kufikiri...we umuhimu wa mtu wako unaona ni kwenye magazeti au humu JF.

Ngoja nikusaidie kufikiri..

CDM inataka kuendesha nchi kwa hiyo kadi za wanachama kama SONGORO na wengine ni za umuhimu kuliko huyo mtu wako maana ndio waeneza sera na kushawishi watu pia ndio wapiga kura hao ...sasa wakitoka na wengi wanatoka baada ya kuona chama chenu pia kina fungato la umimi na wao.

Hii ni aibu na mmejiweka wazi kuwa mtu msafoi CDM ni mmoja Slaa. Hivyo wengine mnashindwa kuchukua maamuzi maana wote ni wachafu CDM kwaheri ndio mmeanza kuwa mahututi hivyo.
 
Wewe mwanakijiji na wewe umezidi kujifanya mjuaji DEMOKRASIA pia ina mipaka yake yani watu wanapanga mipango yao na mikakati lazima waandishi wawepo kwani si watapewa taarifa na mikutano ya hadhara si ipo sikuungi mkono ata kidogo tatizo unaishi kwa kanuni za darasani sana.
Mzee Mwanakijiji kama una mji wako najua huwa unawakaribisha wageni sebuleni, sidhani kama huwa unawakaribisha kwenye Bedroom yako! Vikao vya ndani ya chama si kwa ajili ya kila mtu! Ndo maana vyama vina watu wanaohusika na uhabarishaji wa shughuli za vikao vya ndani, chadema yuko John Mnyika na CCM yupo Nape Nnauye. Huu utaratibu uko dunia nzima kwenye taasisi kubwa!
 
Last edited by a moderator:
Binafsi nafikiri hakuna haja ya , Kama ikizibitishwa ana makosa apewe karipio, ni muda wa kufanya kazi pamoja dhidi ya adui wetu CCM.
 
Zitto ni zaidi ya superstar cdm,hakuna anayemuweza kwa kujenga na kusimamia hoja

Na pia katika msimamo ndani na nje ya chama.

Kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza. Chimera kama wangekuwa na hekima hata kidogo wangelijua hilo
 
Zitto ndio anachelewesha kifo cha Chadema.
 
Songoka jipime kwanza wewe na Zitto umuhimu wenu ndani ya Chadema.

hizi ni hoja tulizozoea kiziskia CCM..za fulani ni muhimu kuliko fulani..Mtaji wa chama ni wanachama nikiwemo mimi, Na si mimi pekeyangu mwenyekusikitishwa na jinsi zito anavyo achiwa achiwa kufanya anavyopenda ndani ya chama..je tukiacha watu wawili kupiga kura kwa chadema na zito mmoja akapiga nani atakua muhimu apo?? au chadema wakipungukuwa kura moja umuhimu wangu utakuaje apo??NGUVU YA CHAMA NI WANACHAMA NA HAKUNA WANACHAMA BILA MWANACHAMA NA MIMI NI MWANACHAMA... wewe utakuwa ccm kwani ndo wanaamini kiongozi ni bora kuliko wanachama.
 
Back
Top Bottom