Zitto azuru kaburi la Amina Chifupa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto azuru kaburi la Amina Chifupa

Discussion in 'Jamii Photos' started by MaxShimba, May 25, 2011.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema jana alizuru kaburi la Mbunge wa zamani wa Viti Maalumu-Vijana wa CCM, marehemu Amina Chifupa, katika Kijiji cha Lupembe, Iyanjo, wilayani Njombe.

  Zitto alizuru kaburi hilo akiwa katika ziara ya mikutano ya hadhara ya Oparesheni Sangara na maandamano ya chama chake, ambayo sasa ipo katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ikiwa na lengo la kupinga ongezeko la gharama za maisha. Jana alikuwa akitembelea Jimbo la Njombe Kaskazini kufanya mikutano katika vijiji vya Lupembe, Kidegembye na Mtwango.


  Kabla ya kuanza mkutano wa kwanza katika Kijiji cha Lupembe, Zitto aliyeambatana na wabunge wa Viti Maalumu wa Chadema, Raya Ibrahim Khamis na Joyce Mukya waliamua kwenda kuzuru kaburi la marehemu Amina kwa ajili ya kumwombea dua.
  Amina alifariki dunia Juni 26, 2007 na kuzikwa Juni 28 mwaka huo kijijini hapo mkoani Njombe.

  Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lupembe, Zitto alisema: "Nashukuru sana kufika katika kijiji chenu kwani nimefarijika kufika mahali alipozikwa marehemu Amina Chifupa". "Amina alikuwa rafiki yangu sana, tulikuwa tukipambana katika Bunge la 9 la Jamhuri ya Muungano katika kutetea haki za vijana wa nchini."
  "Kwa bahati mbaya sikupata nafasi ya kushiriki katika mazishi yake, leo ndiyo mara yangu ya kwanza kufika kaburini kwake," alisema Zitto.

  Wakati wakiomba dua kaburini hapo, Mukya alishindwa kujizuia na kuanza kutokwa na machozi huku akisema: "Kwa kweli sitamsahau Amina kwa mambo matatu. Alikuwa mjasiri, mwenye upendo na alijitolea kuisaidia jamii pale alipotakiwa kufanya hivyo au kwa ridhaa yake mwenyewe."
  "Amina alikuwa mpambanaji bungeni japokuwa alikuwa na umri mdogo kuliko wabunge wote, aliweza kujitoa kupambana na wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya bila woga."

  Chanzo Habari: Mwananchi
   
 2. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  du!kumbe yule demu alikuwa mnyalukolo??aisee,sasa zitto na yule walikuwa na uhusiano gani??si alikuwa mke wa mtu yule au????
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  May 25, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu soma vizuri bandiko na sii kutazama picha tu!..
   
 4. P

  Popompo JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33

  kwani mtu akiolewa au kuoa hatakiwi kuwa na marafiki wa jinsia tofauti?ACHA MFUMO DUME NA UKALE!
   
 5. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  outdated
   
 6. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Mkuu unakumbukia nini?
   
Loading...