Ndugu Watanzania,
Napenda kuchukua nafasi hii kuwaasa kuwa walioko Igunga watumie busara kubwa katika kutafuta kura. Chadema msikubali kuchafua CV yenu kwwa sababu za watu wachache wajinga wanaowatia vishawishi. Nawapongeza kwa kumkamata DC, kazi yenu kubwa iwe kukamata bila kupiga wala kukwaruza mahali. Kamata, piga picha, chukua movie, pelekea polisi kwa taratibu zingine japo najua zimwi likujualo....
Lakini nimesikitishwa sana na baadhi ya kauli za viongozi wetu. Imenisitikisha zaidi hasa kwa huyu anayeitwa sijui Kiravu sijui nani. Lugha aliyotumia yeye kujibu tuhuma za Chadema yeye ndo anaonekana MHUNI zaidi kuliko Chadema. Chadema hawakuwa na jinsi, lazima kilichotokea kingetokea tu maana wao wako kazini na wanajua utaratibu wa kampeni unasema nini wakati mikutano ya hadhara inaendelea. Lazima vijana wapate jazba kutokana na historia ya CCM. Sisi tuseme wao kule Igunga walikuwa na hasira lakini kiravu kwenye majibu yake alikuwa kwenye kiti chake.
Kiravu katika lugha ya maadili amekosa adabu, hana staha, amekosa heshima na kauli yake ya kuwaita Chadema wahuni asifikiri anamwita mtu mmoja au chama ajue anawaita watanzania zaidi ya milioni 2 na nusu waliokipa Chadema kura na rais wake. Viiongozi walioko serikalini wajifunze yanatokea Libya. Ghaddafi hakujua kama atatoka kwenye siagi-Kiravu acha jazba, yatakuja kukutokea puani. Kiravu na wenzako jitahidi kusoma alama za nyakati-mwisho wako unakuja, CCM haitaongoza milele, wala Rais Kikwete hatarudi tena kuwa Rais.
Namwambia Kiravu kuwa vijana waliomkata DC siyo wahuni, ni wasomi wana Degree zao tena siyo moja mbili na wengine zaidi, wamepigika na wanajua wanachokifanya. Asidharau dharua tu akifikiri serikali itamlinda, ajifunze yanayowatokea kina Chenge, Lowassa, Rostam, Ballal, Karamagi, Msabaha, na wengineo. Kiravu acha kiburi kwenye kiti ulichokalia, TENDA HAKI Mungu atakupigania. CCM siyo ALFA na OMEGA, mwisho wake unaweza kufika saa na wakati usiojua, siyo lazima 2015, hata kesho watanzania wakiamua wote mtaenda mafichoni.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU TUBARIKI SOTE TUNAOPIGANIA HAKI ZA WANYONGE.
Asanteni sana kwa kunisoma!