Zitto mambo ya CCM hayakuhusu kaimarishe cdm yako na endelea kuibomoa NCCR
and then?
Zitto mambo ya CCM hayakuhusu kaimarishe cdm yako na endelea kuibomoa NCCR
Kabla hatujaanza kumpiga madongo Zitto, haujatuhakikishia chanzo cha habari yako ulipokitoa labda ni ya kwako wewe kama bourne.By.
Zitto Kabwe: Kwenye siasa ya nchi Kama zetu busara ya mapambano ni Jambo la msingi sana. Kama Nape wa CCM anaunga mkono hoja ya upinzani kuhusu posho, asibezwe wala kuzodolewa. Anapaswa kuungwa mono ili kuongeza Jeshi na kumkinga dhidi ya wapenda posho ndani ya chama chake. Akibezwa, siku nyingine Batak ga mono Jambo hata Kama ni jema kwa nchi. Hii ndio huitwa hekima za harakati. Nimesikitishwa sana na wanaobeza kauli ya Nape kuhusu posho za Wabunge
nimeipenda hii, kaka uko sahihi, nape katumwa tu baada ya hawa jamaa wa ccm kupima upepo, hakuna ubishi walomtuma ndo wapenda posho wakubwa, kwani malalamiko ya zito juu ya posho ni ya mda mrefu, uyo nape alikuwa wapi??? Nape muongo mkubwa uyozitto,ningependa ujue hapa hakuna anayembeza nape.sisi kama jamii ya wasomi, lazima tuangalie mambo from all directions.wote tunajua nape katumwa na ccm. Wote tunajua asilimia kubwa ya wabunge ni ccm na hawa wabunge ndio vinara wa kutetea hii posho.leo uje utuambie ccm inapinga posho? Big no. Ukiniambia hiyo ni kauli ya nape hapo nitamuunga mkono. Mimi nimekosa imani na misimamo ya ccm tangu ulipoanza msemo wa ''kuvua gamba'' this is just a very interesting comedy.
wasioelewa siasa ndo watakaombeza nape, lakini mpevu yeyote wa siasa (kama mimi) hawezi kumbeza nape hata kidogo, kwani nape anastahili kupongezwa yeye na chama chake kwa kuuuonesha umma wa watanzania juu ya msimamo wa chama hicho cha kijani na njano....!!
Katika binadamu, (mimi na wewe) nani amewahi kuyajua ya moyoni kwa mwenziwe? Sote twajadilia kitokacho kinywani! Tuhukumu kauli iliyotoka kinywani na si Roho ya Nape.
Nashindwa kuelewa, msimamo wa Nape ni wa Nape binafsi au NI msimamo wa CCM?Zitto,
Ningependa Ujue hapa Hakuna anayembeza Nape.
Sisi kama jamii ya wasomi, Lazima Tuangalie Mambo from all Directions.
Wote tunajua Nape katumwa na CCM. Wote tunajua asilimia kubwa ya Wabunge ni CCM na hawa wabunge ndio vinara wa kutetea hii Posho.
Leo uje utuambie CCM inapinga Posho? Big No. Ukiniambia hiyo ni Kauli ya Nape Hapo nitamuunga mkono.
Mimi nimekosa Imani na Misimamo ya CCM tangu ulipoanza msemo wa ''Kuvua gamba'' This is just a very interesting comedy.
Mheshimiwa Zitto hapa sintokubaliana na wewe hata kidogo... Nape ni MNAFIKI na hata siku moja huwezi kumpa sifa Mnafiki ambaye anayasema haya kwa malengo yake binafsi na anapokea posho vile vile, sawa na viongozi wa Chadema wanaopinga Posho lakini WANAZICHUKUA tena wengine wameisha pokea posho mpya.
Mimi naomba jivu kutoka Chadema hizo posho mnazopokea zinapelekwa wapi, chama kina mpango gani wa wabunge kuzirudisha kwa wananchi maana kusema tu wakati mnazitumbua haitoshi...Mimi ningependa sana kuelewa haswa matumizi ya Mbunge yamepigwa hesabu vipi.. 1. Mshahara umekadieiwa kutokana na nini? ikiwa anapewa posho ya Usafiri, mafuta, posho ya vikao vya bunge na sijui posho ya nini na nini...kiasi kwamba kila msomi leo anakimbilia siasa na Ubunge kwa sababu kuna ndiko kwa kutokea kimaisha. Na imefikia hadi watoto hawapendi Udaktari wala uinginia kwa sababu siasa za kupiga domotindi zinalipa..