Solomon David
JF-Expert Member
- Mar 1, 2009
- 1,146
- 17
Kaka hizi details ulizotoa hapa zinanipa picha kuwa upo ndani unajua mengi kuliko hao unaobishana nao hapa. Tafadhali achana nao watu wanafrustrations zao za maisha ambao ili kujipa moyo kuwa maisha hayajawakalia vibaya basi njia rahisi ni kugeuza wengine wote kuwa ndio wenye matatizo....
Wengine ndio hivyo ni mabingwa wa kulia ukabila wakati wao ni wafaidika, waumini na waendekezaji wakubwa wa ukabila na udini wao. Unapoona mtu anamgeuzia mwezanke kuwa adui eti kwa kuwa aliquestion mantiki ya magazeti yanayomilkiwa na watu wa kabila moja kumshambulia wakati akiwa katika ushindani na mtu wa kabila lao basi ujue ni ukabila huohuo ndio unaoshape chuki zake hizo.
Mwenzao Zitto badala ya kukimbilia umaarufu kwa siasa za kikasuku amechagua kwenda kujielimisha zaidi kuhusu sekta ya madini na kujiongezea maarifa kwa upana zaidi katika upeo wa kimataifa na kufanya utafiti wa kisayansi ili aweze kutoa mchango madhubuti zaidi jinsi ya kuyashughulikia mapungufu yaliyopo katika sekta hiyo hapa kwetu.
Tatizo wengi wanamjua Zitto kwa muono wa buzwagi na mengineyo wanasahau kuwa uwezo wa kuthamini, kutafuta na kujielimisha kuhusu masuala aliyochagua kuyasimamia hata kabla ya buzwagi ndio imekuwa na inaendela kuwa nguvu yake kubwa kama kiongozi mahiri.
Hawa wao wanasubiri WAHANDISI WETU WA HABARI kutoka katika vyomboi vya havbari vilivyogubikwa na maslahi binafsi za wamiliki wake ndio wawapashe, wa-shape na kuongoza mitizamo yao katika mnasuala muhimu ya nchi.
Omar,
Mpaka pale Zitto atakavyofikia viwango vya elimu vya baadhi ya members hapa ambao wanampinga Zitto, nadhani ndipo utakuwa na audacity ya kutoa misifa kibao kwa elimu ya Zitto (ambayo bado anaitafuta na hakuna guarantee yoyote kuwa ataipata).
Msijione kuwa mnajua mambo mengi kuliko watanzania. Kuna watu kibao tu hapa wana elimu na uelewa zaidi ya Zitto. Tafadhali vijana, kama ndivyo mnataka uongozi wa nchi hii kwa maneno ya dharau na kashfa kama haya, basi mjue kuwa mna kazi kubwa sana mbele yenu.