Zitto aongea na Power Breakfast ya Clouds FM


safi kabisa kuandika unachopenda kiwe. tusubiri tumwone 2010 huko mwandiga. duh, inaonesha ukimwona jamaa unaweza mmwagia tindikali maana machuk kibao
 
Kwa sababu maana halisi ya upinzani Tanzania ni ubinafsi na tamaa ya madaraka/kuhodhi mamlaka bila kujali maslahi ya taifa na wananchi wake! The most likely way to squeeze mafisa CCM out of the power is by opposition joining forces for the sake of national interests, but it's very unlikely that that would happen in today Tanzanian politics! I can't really see us doing a "Kenya" to treat that proven lethal CCM GLIOMA.
 

Kuiondoa CCM madarakani ndilo la msingi tu? Halafu baada ya hapo iweje?

Je, huu ndio utaratibu wa kuwaondoa ccm madarakani? Yaani tugawanyike kwanza ndipo tukusanye nguvu zetu pamoja; kweli hatutakuwa vichaa?

Hebu tusaidie, huu ushirikiano unakuwepo vipi bila kuwa na mkataba wa ushirikiano? Je, ni ushirikiano unapata nguvu zaidi pale unapovunja misingi iliyokuwa tayari imejengwa?

Tuanze tu ushirikiano kwa sababu kafulila kaenda nccr, ila kabla ya hapo sababu ya ushirkiano haikuwepo, kweli hatutakuwa vichaa?
 
Tuanze tu ushirikiano kwa sababu kafulila kaenda nccr, ila kabla ya hapo sababu ya ushirkiano haikuwepo, kweli hatutakuwa vichaa?

Acheni kudanganya umma. Zitto siku zote amekuwa akiamini katika ushirikiano wa wapinzani. Hata kabla ya uchaguzi wa 2005 yeye alikuwa mstari wa mbele kutika mikakati ya ushirikiano ambayo kama si umimi wa baadhi ya watu basi CUF, NCCR na CHADEMA wangeliweza kushirikiana na kusimamisha mgombea mmoja katika urais na kuachiana majimbo mengi tu.

Pia Zitto wakati wote amekuwa karibu na wanasiasa wengine hata wale wa CCM ambao hata kama alikuwa hakubaliani nao lakini pia haamini katika siasa za uadui. Waulize viongozi wa vyama vingine vya upinzani ni nani wanamuona muumini wa dhati wa ushirikiano ndani ya CHADEMA na watakutajia Zitto.

Hata wakati bado hajajitoa katika kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA moja ya ajenda yake kubwa aliyokuwa akitaja hata katika vyombo vya habari ni kujenga mazingira mazuri ya ushirikiano wa dhati wa vyama vya upinzani kuelekea uchaguzi ujao.

Tatizo katika upinzani bado wengi wao wamegubikwa na umimi, usisi, falsafa pinga na kujidanganya kuwa wanaweza pekee yao wakati realities says otherwise.

Wapo hata wanaofikia kudefine muingiliano wa Zitto na wanasiasa wa vyama vingine kuwa ni usaliti na sio mkakati chanya.

Tafuteni majungu mengine lakini katika hili Zitto ameonyesha muono mpana wa suala zima la maendeleo ya demokrasia nchini mwenu katika mtazamo wa mbali kuliko wanasiasa wengine.



omarilyas
 
Mag3 na Asha

Asanteni sana. Kubonyeza hakufai bila kuandika. Najua tunasafari ndefu but will get there.
 
Hivi jamani kauli ya Zitto kuhusu Kafulila inatufundisha nini?
 
Ukiwa na akili za kawaida utaelewa kwamba zitto yuko mbali kabisa na uongozi mzima wa chadema.maamuzi yote yatakayofanywa kinyume na mtazamo wake atawapinga wenzake kwenye vyombo vya habari ,sasa tusubiri muda siyo mrefu tutamjua zitto kwa rangi zake kamili.
 
Ndugu yangu Omar

 
Hivi jamani kauli ya Zitto kuhusu Kafulila inatufundisha nini?

Hivi Kabla ya Kafulila Kuondoka CHADEMA, hivi CHADEMA walikuwa na mpango gani kuhusu Kigioma Kusini? Je walikuwa na Mpango wa kuwaachia NCCR jimbo?
 

This is FUndamental Hoja, je Kabla ya Kafulila kwenda NCCR-Mageuzi Chadema walikuwa na Mpango gani na Kigoma Kusini?
 

Serayamajimbo
 
This is FUndamental Hoja, je Kabla ya Kafulila kwenda NCCR-Mageuzi Chadema walikuwa na Mpango gani na Kigoma Kusini?

kwa kuwa NCCR walipinga CHADEMA na CHADEMA ipinge NCCR? Visasi visasi visasi. Wapinzania walipoteza majimbo mangapi mwaka 2005 kwa kugawana kura?
Watanzania wanachosha kabisa
 

Hai CCM wamepa 92% ya vijiji, unasema CHADEMA waiachie CCM?

Huyo Zito alitoa ushahidi wa NCCR kufadhiliwa na pesa za kagoda? Maana nasikia CHADEMA nao walipata mgawo huo kupitia kwa mwenyekiti wao ambaye alikuwa mgombea Urais. Zito mwanasiasa tu kama wengine leo tukimuuliza ushahidi hana na hapa hamkumuuliza ushahidi.

Kwani huyo Muslim alipata kura ngapi huko Kigoma Kusini?
 
Katika kipindi cha power breakfast Zitto alonga live nakusema hato ondoka chadema wala atarajii kuondoka Chadema.

Kwani kusema ndio kutenda?nakumbuka hata kina Tambwe Hizza walisema hivyo hivyo tena Tambwe alisema kama akienda CCM labda akamfufue mama yake na kulala naye but yuko CCM sasa bila aibu. Wengi huwa wanasema lakini mambo yanapowawia magumu hufanya tofauti na maneno yao.chama cha siasa sio baba wala mama mzazi kusema kwamba lazima ufe nacho.
 
Katika kipindi cha power breakfast Zitto alonga live nakusema hato ondoka chadema wala atarajii kuondoka Chadema.

According to Wagagagigikoko News Network, the damage has already been done and Chadema will NEVER be the same again!!!!
Let's hope for the best for Chadema for the 2010 elections!
 

1. Akaogopa wazee akajitoa!
2. Wangapi wamekua wenyeviti wa kamati? Nothing special here!
3. Hapo ndi anaonyesha udhaifu haswaaaa, hajui definition ya political party?
4. Tena PM, aliyoyafanya tuliokua nae naomba tu tunyamaze...aibu...na watanzania wangeua wala wasingemwamini hivyo!
5. Hapo ndipo nilipodhibitisha everyone has a price...uliona wapi umegombana na mtu afu unamshauri mwanao akaoe palepale? kesi badi iko mahakamani akataka tununue mitambo yao...
 
Hivi Kabla ya Kafulila Kuondoka CHADEMA, hivi CHADEMA walikuwa na mpango gani kuhusu Kigioma Kusini? Je walikuwa na Mpango wa kuwaachia NCCR jimbo?

Swali zuri...naomba wanamsapoti Zitto wasilikimbie walijibu tu vizuriiii.

Na ndio hicho nnachosema mimi, kumsapoti mtu wa chama kingine sio vibaya, ila Zitto anamsapoti Kafulila coz ni mfuasi wake au kwa ajili ya kuimarisha upinzani?

Utamsapoti vipi mtu wa chama kingine wakati hujui chama chako kitamsimamisha nani katika jimbo hilo?

Nyerere alimsapoti yule wa upinzani baada ya kuona wa CCM hafai, sasa Zitto anamsapoti kafulila bila kujua chama chake kinamsimamisha nani, does that make sense?

UBINAFSI tu ndio umemjaa kijana huyu, na kujiona yeye yuko juu ya chama!
 

Hakuwa PM alikuwa Katibu Mkuu. Serikali aliyoongoza DARUSO pamoja na Waziri wao wa fedha Makundi ndio serikali ya kwanza kuita wakaguzi kukagua hesabu za DARUSO. Nilikuwa chuo miaka yake na kijana huyu alikuwa imara na hakuwa na mchezo na haki za wanafunzi. Kama huna CHUKI, basi wewe ni mwongo tu. Sifagilii siasa zake, lakini kwenye uadilifu huyu kijana rekodi yake ni safi sana.
 

CHUKI tu zimekujaa. Hebu eleza huo ubinafsi wake kwa mifano maana inawezekena tujadili hewa. bamiza mtu kwa facts sio hisia zinazotokana na inferiority complex
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…