Pia katika Taarifa hiyo ya habari japo kwa mwisho nimekuta Jaji Mkuu Agustine Ramadhani akimalizia kueleza kuwa; "Suala la mabadiliko ya Katiba linawezekana, kwani Tayari nchi nyingi zimefanya na kuzitaja Kenya na Uganda na kusema linazungumzika na lina namna yake ya kujadiliwa," Mtangazaji akauliza iwapo kitendo cha wabunge wa Chadema ni kosa Kisheria, Jaji mkuu anajibu "Siyo kosa kisheria, pengine lingeandaliwa katika kanuni za Bunge lakini pia anaamini kuwa hakuna kosa na ndiyo maana Spika hakusema lolote, lakini sana sana tunaweza kulielezea kama ni swala la maadili tu lakini si sheria".
Hii ni kwa Mujibu wa TBC 1 habari ya saa 2 usiku.
Jamani mbona saa mbili usiku haijafika !!