Ndugu wana JF,
Kumekuwa na mada nyingi sna humu ndani ambazo zinajaribu kuonyesha kuwa mimi ni mkosaji na kunipaka matope sana. Nimejdiliwa mno katika jf na hata kuzushiwa mambo mengi sana. Kuna wanaonisema kwa dhati y moyo wao kwamba nimekosea hapa na pale na kuna wanaoona huu ndio wakati wa kumwangusha Zitto na hivyo kuendeleza propaganda za kila namna.
Hii makala imetoka katika gazeti la Mwanahalisi la wiki iliyopita. Imeandikwa na Ansbert Ngurumo, Mhariri wa Tanzania Daima na Press Secretary wa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA. MwanaHalisi linamilikiwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA ndugu Antony Komu. MwanaHalisi limekuwa mstari wa mbele kunipaka matope na kutoa propaganda chafu dhidi yangu na sijui ni kwa faida ya nani.
Nadhani mmenijadili vya kutosha. Itoshe kusema nimesikia. Yale ambayo ni makosa nitajirekebisha maana mimi ni binaadamu. Yale ambayo ni uzushi, uwongo na propaganda nitayadharau.
Jambo moja nilisema na nimeshalisema huko nyuma ni kwamba, nimekuwa mwanachama wa CHADEMA toka nikiwa nina umri wa miaka 16 na sasa nina miaka 35, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote cha siasa. Sitegemei kuwa mwanachama wa chama kingine chochote cha siasa tofauti na CHADEMA. Sijawahi hata siku moja kusaliti chama changu na wala sitajaribu kufanya hivyo. Nina utii kwa Katiba ya chama changu na kwa chama kama Taasisi (Asasi). Pamoja na kutofautiana kimawazo na viongozi wenzangu (wote hatuwezi kufikiri sawasawa) sijawahi kukiuka maamuzi halali ya vikao vya chama kwa mujibu wa Katiba.
CHADEMA ni taasisi inayokua na hivyo changamoto zinaongezeka kila siku. Ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunazikabili changamoto hizi bila kuathiri kazi iliyombele yetu ya kujenga Tanzania yenye demokrasia ya kweli na yenye watu wenye fursa ya kuendeleza maisha yao.
Siasa za kupakana matope. Siasa za kumalizana. Siasa za maji taka, hazitasaidia nchi yetu wala chama chetu. Ifikapo mwaka 2015, wanachama wataamua nani atabeba bendera ya chama kwa njia za kidemokrasia. Hakuna sababu ya kuanza kumalizana sasa. Tukajenge chama wilayani na vijijini ili ifikapo uchaguzi ujao tuwe na mawakala kila kituo, walinde kura zetu na tuweze kushika Dola na kuongoza.
Watanzania mtusaidie katika jukumu hili. Jumamosi njema
Umewaudhi wapenda mageuzi, hata wapigakura wako, kwa tabia yako ya kuonekana kigeugeu, kwa kuwa umejitokeza, tunachokuomba uyafanye mambo kwa vitendo kuturudishia imani. Vile vile kama kuna tofauti kati yako na uongozi, take action to solve, tuendeleze CHADEMA yetu. Ndani ya CHADEMA hakuna udini, kama ulipitiwa siku unahojiwa TBC, ifute ile kauli yako humu. Asante sana kwani kidogo nimeanza kupata imani na wewe.
Sijafanya kikao chochote na Lowasa. Kulikuwa na kikao cha Lowasa na Mbowe ambacho mimi nilishiriki kama Naibu wa Mbowe Bungeni. Hata hivyo sijafanya kikao kingine chochote.
Makala hii imeandikwa kwa lengo baya na ndio maana mwandishi kaficha jina lake. Kama ana guts aweke jina lake wazi na aje na ushahidi wa haya aliyoyaandika.

Mmejadiliana nini na Lowassa ?
Hii makala imetoka katika gazeti la Mwanahalisi la wiki iliyopita. Imeandikwa na Ansbert Ngurumo, Mhariri wa Tanzania Daima na Press Secretary wa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA. MwanaHalisi linamilikiwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA ndugu Antony Komu. MwanaHalisi limekuwa mstari wa mbele kunipaka matope na kutoa propaganda chafu dhidi yangu na sijui ni kwa faida ya nani.
Kweli Chadema kumekucha.
Waswahili wanasema Nyani akimaliza miti huingia mwilini. Chadema imeamua kuvaana wenyewe kwa wenyewe?
achana nao hao zito,wanatumiwa na wachaga!
Kiranga mazee hii nikipindi kile kabla mzee manywele hajajiuzuru kwa manufaa ya wananchi ni vikao vya Bungeni tu
Mara Regia Mtema na Kitila (I swear I am not picking on her, mwenyewe kaja kutoa dukuduku hapa) mara Zitto na Komu, hayo ni ma beef yanayo leak hapa tu, huko ndani wenyewe wanaokujua sijui kukoje.
Sijafanya kikao chochote na Lowasa. Kulikuwa na kikao cha Lowasa na Mbowe ambacho mimi nilishiriki kama Naibu wa Mbowe Bungeni. Hata hivyo sijafanya kikao kingine chochote.
Makala hii imeandikwa kwa lengo baya na ndio maana mwandishi kaficha jina lake. Kama ana guts aweke jina lake wazi na aje na ushahidi wa haya aliyoyaandika.
Ile ilikuwa mbaya. Bora hata hii, mwandishi kaficha jina.
Wanaaibisha jina la chama tu.
Hivi mpaka Zitto aje ajitetee na kujaza information zote hizo kuwa linamilikiwa na nani na kuonyesha ugomvi ndani ya chama?
Angejitetea bila ya kutaja majina ya watu wa ndani ya chama angepungua wapi?
Sijawahi kusema mahala popote kuwa ndani ya CHADEMA kuna udini. Ninaomba clip ya TBC iwekwe hapa jamvini na mtu anionyeshe wapi nimesem kuwa ndai ya CHADEMA kuna udinni. Tafadhali usinywe sumu unazopewa.
Yaani jamaa wanaendesha chama cha kitaifa kama watoto wa shule fulani hivi.
Hiki ndicho chama mbadala kweli ? Prima donnas kibao.
Mara Regia Mtema na Kitila (I swear I am not picking on her, mwenyewe kaja kutoa dukuduku hapa) mara Zitto na Komu, hayo ni ma beef yanayo leak hapa tu, huko ndani wenyewe wanaokujua sijui kukoje.