Zitto amtembelea Lema gerezani baada ya kunyimwa dhamana

Zitto amtembelea Lema gerezani baada ya kunyimwa dhamana

Amemuomba "MUNGU" kwa kumpa "MKE" jasiri ambae ndio "NGOME" yake kwa sasa....
Hapo nilitarajia angesema:-
Amemuomba "MUNGU" kwa kumpa "CHAMA" jasiri ambacho ndio "NGOME" yake kwa sasa
Kwenye maisha family ndo ya muhimu kwanza
 
Viongozi aina ya Zitto bado tunawaitaji asante kwa kumtembelea lema roho inauma kuona sheria za nchi hazifuatwi
 
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kwa mara nyingine leo (jana) amenyimwa dhamana na imeamriwa na mahakama kuwa akae mahabusu mpaka Februari mwakani kesi yake itakapotajwa tena.

Mahakama imetoa uamuzi huo baada ya kuridhishwa na vigezo vya kisheria ambavyo vilitolewa na mawakili wa Jamhuri ambao waliweka pingamizi Lema asipewe dhamana.

Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), alimtembelea Lema gerezani leo na haya ndiyo ameyaandika kuhusu Lema, kesi yake na hali ya kunyimwa dhamana.

ZITTO KABWE:

Leo (jana) Ijumaa Desemba 2/2016 nimepata fursa ya kumsalimu ndg. G Lema, mbunge wa Arusha Mjini Katika Gereza la Kuvu la Arusha. Nimemtembelea Kama mbunge mwenzangu na kumhakikishia solidarity katika harakati za kutafuta na kulinda haki.

Lema ana ari kubwa ya mapambano. Anasikitishwa sana na ukiukwaji mkubwa wa haki na mahakama kuonekana kuendeshwa na Serikali. Yeye ameona ni bora akae ndani mpaka hapo dola itakapopenda kumpa dhamana. Kosa lake lina dhamana na hakimu alimpa dhamana.

Ameomba tutazame mahabusu wengi wanaokaa ndani miaka mingi bila kesi zao kuendelea. Tuwatetee.

Amemshukuru Mungu Kwa kumpa mke jasiri anayempa moyo na ndio ngome yake kwa sasa.

Nimemwomba Lema aone kuwa hii struggle sio yake peke yake bali anawakilisha watu wengi wanaotaka haki kutendeka katika uendeshaji wa nchi yetu. Siku zote haki hushinda.

CHANZO: Maandishi Genius
Haki imetendeka kwa Lema kurudishwa mahabusu na kunyimwa dhamani.
Lema anatakiwa apigwe kifungo hata cha miezi 6.
 
Huwa najifunza mengi sana kwa zitto kabwe ni mtu mstaarabu na pia mvumilivu na ni mwanasiasa wa kweli aisekuwa na lepe la unafki
Ni wachache sana wanaweza kuwa na moyo kama wake.
 
Acha unafiki. Toka mwanzo wa hili sakata la Lema msimamo wako umekuwa hasi sana juu yake.
Sasa hivi umeona kiongozi wa chama chako ameenda kumjulia hali nawe unajifanya muungwana.
Mbona unafiki wako kwa Lowassa tumeunyamazia??....BTW Lema anatakiwa kubadili mbinu....otherwise ataozea huko lupango
 
Nilipomsikia mtu mmoja anasema eti kuna mhimili mmoja umechimbiwa chini zaidi nilishangaa sana!

Nadhani maana yake ndio hii sasa!
Ulishanga nini kwani hujui kusoma, kasome vizuri katiba badala kusomewa na DJ wenu.
 
Ulishanga nini kwani hujui kusoma, kasome vizuri katiba badala kusomewa na DJ wenu.
Unazungumzia katiba ipi hiyo unayotaka nikaisome leo?
Akili zile zile za "kuna mhimili mmoja umeenda chini zaidi" alafu unanitaka nikasome katiba..
 
Zitto tulikuheshimu sana lakini kwa hili la Lema,kaa mbali nasi.
 
Hujiulizi ni kwa nini Mandela alipotoka Gerezani alipokelewa na Winnie Mandela na siyo kina Oliver Thambo. Vitu rahisi namna hii kueleweka vinapokuwa vigumu kwenu ndiyo inayotufanya tujue ni kwa nini mnawashabikia wale jamaa!!
lumumba wabovu wa kufikiri kweli,, sasa ategemee chama kwani lema alioa chama? Familia kwanza
 
Huwa inatokeaje wajinga wakawa watawala wa dunia huku werevu wakiwaangalia?
 
Back
Top Bottom