Zitto amemtuma ofisa wake kuisemea CHADEMA kuhusu Lowassa

Zitto amemtuma ofisa wake kuisemea CHADEMA kuhusu Lowassa

Tumaini Makene,nampenda kukuambia kukujulisha kuwa UKAWA msipo weka mbali u binafsi wenu (hususani) CHADEMA pia msipoweka mbali tabia ya kusameheana na kusahau yaliyopita kamwe mwaka huu mtashindwa vibaya sana.

Chama chenu CHADEMA kina wasomi wengi na wanasheria wenye viwango vya huu sana lakini hawana hekima na moyo wa kusamehe mkiongozwa na Lissu. Lowassa asikudaganye mtu ndilo lilikuwa chaguo la Watanzania na kama sisi Wasukuma Magufuri tulikuwa hata hatufikirii kuwa raisi wa awamu hii na kila mmoja amepigwa na butwaa.

Sipendi nijikite kuongelea kuwa Wasukuma tunaelekea kupata raisi no mimi si muumini wa ukabila isipokuwa ni mhanga wa siasa na unyonyaji wa CCM pasipo kujali tabia njema za Magufuri. Mfumo wa CCM ni hatari kuliko mgombea hata kama angetokea Macca ama Vatican. Kamwe usitarajie huo umoja wenu utaing'oa CCM madarakani.
 
Msije jisahau piganieni mpate tume huru ya uchaguzi kabla ya kampeni hazijaanza bila hivyo hawa jamaa hawakawii kutumia goli la mkono.

Mkuu watakaozuia goli la mkono ni wananchi wala si NEC. Tuko Mazingira ya vitani tayari. Let us move mpiganaji.

Kama CCM wanadhani wataweza kushinda uchaguzi huu kwa kutumia goli la mkono baada ya kuona inazidi kuwa mbaya, watakutana na mikono elfu moja pale golini i.e Wananchi.
 
Sito acha kusema na nitaendelea kusema wewe ni mmoja ya wasemaji wenye uwezo mdogo kabisa wa kufikiri kama sio wakurupukaji ambao chadema imeshawai kuwa nao!
Tunajua wewe huwa una mchukia Zitto binafsi lakini katika hili unaendelea kudhihirisha chadema ni chama cha ovyo kabisa ambacho kinaongozwa na mihemko kabisa!
Hivi una ushahidi kuwa huyu mtu alitumwa na Zitto? Kama una ushahidi kwanini usimtaje hadharani muhusika na uoneshe jinsi Zitto alivyo mtuma?
Tumaini Makene umekurupuka na una sahau wewe ni msemaji wa chama ambacho kinadhani kinaweza kushika dola lakini cha kushangaza mnaongozwa na mihemko na hisia tuu!

Nilitegemea msemaji wa chama ambaye ni makini kutoka kwa watu ambao husema wao ni makini lazima angekuja na ushahidi wa Zitto kumtuma huyo kiongozi na ungemtaja muhusika hadharani na si kuandika mambo kama mtu ambaye hakusomea kabisa uandishi wa habari!

Pengine hii ilipaswa kuletwa na wakina Mungi Crashwise na wengine ambao si wasemaji wa chama lakini unapo ileta wewe na ina madhaifu namna hii ni wazi mnaendeshwa na mihemko tuu!
Dr.W.Slaa naomba nikuulize hivi hii habari na wewe uliafiki iletwe humu na wewe ulishiriki kumpa kazi makene? Na wewe unafikiri kabisa makene anajua anacho kifanya?

Nakudharaugi sana!
 
Tumaini Makene,nampenda kukuambia kukujulisha kuwa UKAWA msipo weka mbali u binafsi wenu (hususani) CHADEMA pia msipoweka mbali tabia ya kusameheana na kusahau yaliyopita kamwe mwaka huu mtashindwa vibaya sana.

Chama chenu CHADEMA kina wasomi wengi na wanasheria wenye viwango vya huu sana lakini hawana hekima na moyo wa kusamehe mkiongozwa na Lissu. Lowassa asikudaganye mtu ndilo lilikuwa chaguo la Watanzania na kama sisi Wasukuma Magufuri tulikuwa hata hatufikirii kuwa raisi wa awamu hii na kila mmoja amepigwa na butwaa.

Sipendi nijikite kuongelea kuwa Wasukuma tunaelekea kupata raisi no mimi si muumini wa ukabila isipokuwa ni mhanga wa siasa na unyonyaji wa CCM pasipo kujali tabia njema za Magufuri. Mfumo wa CCM ni hatari kuliko mgombea hata kama angetokea Macca ama Vatican. Kamwe usitarajie huo umoja wenu utaing'oa CCM madarakani.

Pole. Wananchi kushinda Uchaguzi wa Mwaka huu si lazima waungane na wanaoamini katika kusaliti mapambano. Uchaguzi watakaoshinda ni Watanzania dhidi ya CCM.

Mimi pia siamini katika ukabila. Huwa hata nasahau kabila langu many times except during jokes au rituals if need be...lakini nasikitika na kushangaa ninyi namna mnavyowadanganya watu kuwa Magufuli ni msukuma. Kwanini mnadanganya? Ili kupata kura? Mnaanza kuvutia ukabila? Alas!
 
Mkuu watakaozuia goli la mkono ni wananchi wala si NEC. Tuko Mazingira ya vitani tayari. Let us move mpiganaji.

Kama CCM wanadhani wataweza kushinda uchaguzi huu kwa kutumia goli la mkono baada ya kuona inazidi kuwa mbaya, watakutana na mikono elfu moja pale golini i.e Wananchi.

Ok sasa tumaini kuna hili lililojitokeza la watu wasio raiya wa tanzania kujiandikisha je mna mkakati gani wa kujua hivyo vitambulisho walivyokwisha jiandikisha kama havitatumika kwenye kujazia maeneo walishikwa? Na pili ile computer ya kuandikia wananchi iliyoibwa mna taarifa nayo na sisi wananchi tunaomba muwe na wataalamu waaminifu wa I.T ili hawa jamaa wasijezichezea manake wana mbinu nyingi kamanda tupo pamoja mwaka huu ccm rangi zote wataziona.
 
mdetichia kwa kweli umesema neno na nategemea hili Tumaini Makene atakuja na jibu murua!!!
 
Last edited by a moderator:
Pole. Wananchi kushinda Uchaguzi wa Mwaka huu si lazima waungane na wanaoamini katika kusaliti mapambano. Uchaguzi watakaoshinda ni Watanzania dhidi ya CCM.

Pole sana Makene kwa kuendelea kuhadaa umma uliokatishwa tamaa za maendeleo duni ya mkoloni mweusi CCM. Kupata viti kadhaa vya uenyekiti serikali za mitaa kumewafanya kuvimba vichwa. Mimi sitabishana sana na wewe msomi mimi ni STD VII tu niliyebobea kwenye siasa za vijijini.
 
lowasa akienda act tunapiga bao la kisigino,ataenda na wafuasi wa ccm na vigogo,ccm wakigawanyika wengine ACT ukawa tunatoboa bila kwere chali angu

Ogopa sana huo utabiri wako ndugu Viol. Lowassa akienda ACT ndipo atawapa nafasi zaidi CCM ya kushinda kwani itabidi UKAWA wapambane na maadui 2 ACT na CCM. Ni bora Lowassa akatulia Nyumbani kwake ama ajiunge UKAWA. Samahani kama takuwa nimekukera.
 
Lowassa anakwenda ACT. Huyu mzee sijuwi Ni nani anamshauri huu upuuzi.naona bado hajajifunza kupitia kwa zitto.
 
lowasa akienda act tunapiga bao la kisigino,ataenda na wafuasi wa ccm na vigogo,ccm wakigawanyika wengine ACT ukawa tunatoboa bila kwere chali angu

je anakaribishwa UKAWA?
 
Yaan msemaji wa Cdm unampigia kampen Zitto hivi ni lini utaanza kujfunza siasa nzur?... Achen hizo mambo kuna mengi kutoka ukawa wananchi wanapaswa kuyajua syo kutuandikia tetesi na maneno yasyo eleweka
 
Tumaini Makene

ni wakati wa UKAWA kubadili strategy sasa...mwekeni mtu makini ambaye hajawahi kugombea...na kwa upande wangu mtu huyo ni Tundu Lissu pekee....ndie anaweza kupambana vema na kina Magufuli ...na aliwahi pia kupambana nao bunge la katiba na taifa zima likamwona.....Dr. Slaa akagombee ubunge na pia kumnadi Lissu..wakipita wote they will make a good team in the government..Time for UKAWA to change strategy ni sasa...Mkichelewa mtazisoma namba za ccm....Ngosha nawaambia.....
 
Last edited by a moderator:

Taarifa kutoka vyanzo vyangu zinasema kuwa Lowassa atafanya mkutano na waandishi wa habari kesho saa 3 huko Dodoma. Atakachozungumza anakijua vizuri yeye labda na watu wake pia.

Makene

Kwa intelegensia yangu ya kichwani kama mkutano ni Dodoma jamaa tayari wamemwagiza kufanya hivyo na hili linamaanisha tayari kamwaga manyanga na kunyoosha mikono juu.Wapambe walionyuma yake wajipange kama alivyofanya Nchimbi.

Staili hii inafaa kuwekwa kwenye vitabu vya kumbukumbu .
 
Mkuu, mtaje jina huyo basi, halafu weka uhusika wa Zitto katika hilo. Uwe mwangalifu maana ukiandika chuki huwa unajidharaulisha, nadhani wewe ni shahidi. Anaweza kuwa ACT anaweza kuwa ameandika, ila uhusika wa Zitto unatupa mashaka, sidhani na wewe mr. Makene kila post humu inakuwa approved na Mbowe na Slaa!

Unajulikana kuwa unamchukia Zitto, mmejishusha so low! Zitto katawala akili zako hauangalii kuwa adui yako ni CCM na wameishasimamisha mtu wao ambao hata Chadema wanamkubali! This is a blow. You have wasted energy and time to fight against Zitto and not the ruling party! Inapokuja blow kama hii ya Magufuli, hauna namna zaidi ya kuendelea vita yako na Zitto.

Zitto kwa tunaomjua, he will be there na atashine, maana ana brain na anafikiria , anaijua siasa na yuko matured. Utamsema sana ila ameishaondoka Chadema na yuko huko na maisha yake! Ona aibu kwa hili.

Think big!
Makene ni msemaji wa chama wa ovyo kabisa namsubiri aoneshe uhusika wa Zitto kwenye hayo anayo yasema!

Hakika chuki hupofusha na kupumbaza kabisa!
 
Last edited by a moderator:
Chama chetu unataka nani tena. We achaaaaa!! Sisi ndo tunajua jinsi ya kukiendesha.
Tumaini Makene

ni wakati wa UKAWA kubadili strategy sasa...mwekeni mtu makini ambaye hajawahi kugombea...na kwa upande wangu mtu huyo ni Tundu Lissu pekee....ndie anaweza kupambana vema na kina Magufuli ...na aliwahi pia kupambana nao bunge la katiba na taifa zima likamwona.....Dr. Slaa akagombee ubunge na pia kumnadi Lissu..wakipita wote they will make a good team in the government..Time for UKAWA to change strategy ni sasa...Mkichelewa mtazisoma namba za ccm....Ngosha nawaambia.....
 
Last edited by a moderator:

Itakumbukwa juzi mara baada tu ya majina 5 ya makada wa CCM yaliyokuwa yamepitishwa kwenye CC ya chama hicho kuwa yamejulikana (kwa kadri ya utaratibu wao), kiongozi mkuu wa ACT, Zitto, haraka haraka kama ilivyo kawaida yake akakimbilia mtandaoni kuandika kuwa Edward Lowassa anajiunga na ACT na atakabidhiwa kadi.

How can you lie about something that anyone can prove it is a lie and expect to be taken seriously? Did he really post that kwenye mitandao? NO. May be he only posted to you. But the big question is, what are you doing following up on what Zitto is up to? CDM and UKAWA are in a position that no other opposition side has ever been blessed with and you are busy responding to something that some nameless ACT officer (alleged) has said, completely showing your obsession with Zitto while giving no link whatsoever between your story and him.

Grow up man, its time for big things.

SAD!
 
Ofisa mmoja wa chama kiitwacho ACT ambaye mara kadhaa amenukuliwa akiwa ni msemaji wa chama hicho, ameandika na kueneza habari mtandaoni kuwa kada mwandamizi wa CCM Edward Lowassa anahamia CHADEMA!

Inashangaza kidogo! Ama ni kwamba wahusika wa chama hicho hawana uratibu wa mawasiliano kiasi kwamba kila mtu anaweza kujiandikia tu au wanaendelea kukubuhu katika siasa nyepesi.

Itakumbukwa juzi mara baada tu ya majina 5 ya makada wa CCM yaliyokuwa yamepitishwa kwenye CC ya chama hicho kuwa yamejulikana (kwa kadri ya utaratibu wao), kiongozi mkuu wa ACT, Zitto, haraka haraka kama ilivyo kawaida yake akakimbilia mtandaoni kuandika kuwa Edward Lowassa anajiunga na ACT na atakabidhiwa kadi.

Wafuasi wa Zitto kwa kuendekeza siasa nyepesi za umaarufu wa mtu, wakakimbilia nao mitandaoni kusema kuwa tayari Lowassa ameshajiunga na ACT na kwamba ni Mgombea urais na 'taswira na nuru' ya chama tayari kapewa cheo cha Uwaziri Mkuu, alas!

Hawakuishia hapo. Wakaenda mbali hata kughushi nembo ya moja ya mashirika makubwa ya habari duniani kisha wakaandika mambo yanayokidhi matamanio yao, kwamba Lowassa kahamia ACT na Zitto kamkabidhi kadi.

Sasa haijajulikana hiyo kauli ya Zitto imeishia wapi ndani ya masaa 48 tu ghafla ofisa wake amekwenda mitandaoni akijigeuza kuwa msemaji wa taasisi isiyomhusu kuwa Lowassa amehamia CHADEMA.

Tumsaidie Zitto asiendelee kufanya siasa nyepesi. Alikuwa mtu wa kwanza kumkaribisha Lowassa kwenye chama chake mapema kabla hata hajachukua fomu ndani ya CCM. Sasa awaambie watu wake vizuri hilo 'deal' limeishia wapi?

Taarifa kutoka vyanzo vyangu zinasema kuwa Lowassa atafanya mkutano na waandishi wa habari kesho saa 3 huko Dodoma. Atakachozungumza anakijua vizuri yeye labda na watu wake pia.

Habari hizo kwamba Lowassa amehamia CHADEMA hazina ukweli wowote. Zinatengezwa na kupikwa na hao 'vijana' kwa maslahi wanayoyajua wao.

Kwa kushirikiana na vyama washirika wenza katika UKAWA, tunaendelea na maandalizi ya kwenda kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kushika dola na kuongoza serikali kuwatumikia Watanzania. Kila kitu kinakwenda sawa. Maandalizi karibu yote yamekamilika...ni #UKAWA Julai 14.

Hilo ndilo suala la msingi kwa sasa. Baada ya giza totoro la siasa za ghiliba, rushwa na hila huko Dodoma kwa takriban mwezi mzima, wananchi wanasubiri nuru ionekane Julai 14 kupitia UKAWA. Yamebakia masaa mchache kuuona mwanga unaosubiriwa na Watanzania wote wapenda mabadiliko ya kimfumo na kiutawala, si mabadiliko ya majina na sura za watu kutoka mfumo ule ule uliotukwamisha hapa tulipo.

Makene

ujio anaotaka kuja nao lowasa ndani ya cdm unatofauti gani na dr slaaa?

mbona makene unaibisha heshima yako japo hapo kabla uliisha haribu taluma yako kwa kumnyenyekea mnyika kumbebea begi mnyika sasa unaharibu kwa mandishi ya hovyo
 
Back
Top Bottom