Zitto amemtuma ofisa wake kuisemea CHADEMA kuhusu Lowassa

Zitto amemtuma ofisa wake kuisemea CHADEMA kuhusu Lowassa

Asante mkuu Makene kwa kuliona hilo, kwani hawa jamaa na ACT yao wanazidi kujianika kwa Watanzania kuwa ingawa wanajifanya kuwapo huko waliko kimoyomoyo bado wanatamani kubaki Chadema, kwani kila kukicha ni kuitaja Chadema.
 
lowasa akienda act tunapiga bao la kisigino,ataenda na wafuasi wa ccm na vigogo,ccm wakigawanyika wengine ACT ukawa tunatoboa bila kwere chali angu

Mtaendelea kusubiria ndege stand ya msamvu badala ya uwanja wa ndege,na matokeo yake mtaambulia bus la mwisho
 
Ni jambo la kushangaza sana hawa wachaigiaji wanaomjibia Zitto, unlike them, Tumaini ni authority ya chama fulani, na hiki anchokifanya ndio hasa kinachofanywa na professional body ya communication ya chama chochote kile, si lazima kiwe chama kikubwa.

Watu waache matusi, communication siyo research ya kumtaka Tumaini atoe kidhibiti cha anachosema, kama umbea ni huo wa watu wa ACT kuongea mambo ya udhanifu, kwanza hawajamaliza kesi yao na Limbu na hivyo Lowassa hawezi kuwa mpumbavu wa kuingia chama cha uchocoroni kama hicho.

Acheni kutukana watu wanaofanya kazi zao kwa vile tu nyie hamjazoea kufanya kazi. Hii ni serious problem kwa vijana wa Kitanzania wanajifanya wajuaji sana ndio maana wengi wenu mnaoandika hayo mambo humu mko hoi. Tumaini ana kazi yake, ni professional, alichagua kuacha kazi Tanzania Daima ili kukitumikia chama chake, ana lipwa mshahara na anaishi maisha ya heshima ya kawaida ya Mtanzania.

Ninasema haya kwa kuwa wasemaji wengi wa aina hii tunawajua, mmechoka sana, kifedha, mikakati ya maisha na sasa mmefikia kuchoka fikra. Upumbavu ni roho kama Ukimwi, ikianza haisimami. Tumekuwa tukiwalaumu wasemaji wa kila chama hapa wanapochelewa kusafisha rumours, sasa huyu amefanya imekua tatizo, why?
 
Yaan mnatafuta kick tu baada ya kuona mipango yenu ya kumpata rais kutoka Kaskazini imekufa- inajulikana mlikuwa mnamsaidia Lowassa kuitishia CCM kuwa wasipo mpa nafasi atakuja CDM nasi ndio maaana hamkuwa tayari kufanya lolote na baada ya kuona jembe limepitishwa na yeye kugundua akihama bado atapigwa ameamua kutulia zake.

Sasa nyie mnaanza kusemana mara malaya ni fulan ndio mpenz wake mara hiv-ujinga mtupu, tunajua Chadema mmeumia baada ya kuona rais sasa hatoki kaskazini, maana angesimama Lowassa, bado mngependa maana mlichohitaj ni mtu wa kwenu tu no matter what
 
Zito ameachwa kwenye mataa na Lowasa,wako wapi wabunge 80 wakuhamia ACT hata baada ya bunge kuvunjwa.
 
Makene wewe ungeandika tu mambo ya UKAWA acha kusafiria nyota ya Zitto hajawahi kuwa level ya mtu yeyote ndani ya CDM.
kwani hapo kaandika nini,kukanusha kwamba Lowasa hajahamia Chadema sio mambo ya UKAWA?
 
Last edited by a moderator:
Asante mkuu makene kwa kuliona hilo kwani hawa jamaa na act,yao wanazidi kujianika kwa watanzania kuwa ingawa wanajifanya kuwapo huko waliko kimoyo bado wanatamani kubaki cdm,kwani kila kukicha ni kuitaja cdm.

CDM yenyewe ipo ICU km sio UKAWA ingeshakufa, sasa nan aitaman sema hamlalali baada ya kugundua wananchi sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye upinzani wa kweli ACT hawataki ulaghai na ghiliba za CDM (wizi na utapeli wa Mbowe na Slaa), sasa mnahangaika kutafuta umaarufu- hiyo ni aibu kubwa CDM
 
Ni jambo la kushangaza sana hawa wachaigiaji wanaomjibia Zitto, unlike them, Tumaini ni authority ya chama fulani, na hiki anchokifanya ndio hasa kinachofanywa na professional body ya communication ya chama chochote kile, si lazima kiwe chama kikubwa.

Watu waache matusi, communication siyo research ya kumtaka Tumaini atoe kidhibiti cha anachosema, kama umbea ni huo wa watu wa ACT kuongea mambo ya udhanifu, kwanza hawajamaliza kesi yao na Limbu na hivyo Lowassa hawezi kuwa mpumbavu wa kuingia chama cha uchocoroni kama hicho.

Acheni kutukana watu wanaofanya kazi zao kwa vile tu nyie hamjazoea kufanya kazi. Hii ni serious problem kwa vijana wa Kitanzania wanajifanya wajuaji sana ndio maana wengi wenu mnaoandika hayo mambo humu mko hoi. Tumaini ana kazi yake, ni professional, alichagua kuacha kazi Tanzania Daima ili kukitumikia chama chake, ana lipwa mshahara na anaishi maisha ya heshima ya kawaida ya Mtanzania.

Ninasema haya kwa kuwa wasemaji wengi wa aina hii tunawajua, mmechoka sana, kifedha, mikakati ya maisha na sasa mmefikia kuchoka fikra. Upumbavu ni roho kama Ukimwi, ikianza haisimami. Tumekuwa tukiwalaumu wasemaji wa kila chama hapa wanapochelewa kusafisha rumours, sasa huyu amefanya imekua tatizo, why?

Vitu vingine ni vidogo sana kuvisema yeye, kumbuka Makene anawakilisha taasisi ambayo wengi ni mbadala ya chama Kikubwa na mama CCM. Kusema Zitto anamtuma afisa wake bila kuweka jina, habari hiyo ya kutumwa ni kama majungu tu. Mimi ni Chadema, tena damu, lakini siyo baba na mama yangu, kwahiyo mnapokosea lazima niseme tu yaani hamna wa kunizuia.

Chama mbadala lazima kiwe great thinker beyond wale wa chama tawala. Wabunge wetu wa Chadema wanafanya kazi nzuri sana, tatizo ni sisi vijana. Kuwashambulia watu wenye wafuasi kwenye jamii bila strong reasons ni upuuzi wa kukemea.

Mfano mdogo tu, Lowassa alikuwa na wafuasi kibao, hata kama aliwanunua au hakuwanunua, kwa hiyo kumponda Lowassa waziwazi kipindi kama hiki tunazikosa kura ambazo wengi wangepiga kwa hasira ya kuwakomoa CCM kwa kumkata Lowassa. Sijasema mumpe uanachama Lowassa. Taasisi kama Chadema inabidi iwe na qualified and well trained skilled personel.

Viva Chadema.
 
CDM yenyewe ipo ICU km sio UKAWA ingeshakufa, sasa nan aitaman sema hamlalali baada ya kugundua wananchi sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye upinzani wa kweli ACT hawataki ulaghai na ghiliba za CDM (wizi na utapeli wa Mbowe na Slaa), sasa mnahangaika kutafuta umaarufu- hiyo ni aibu kubwa CDM

Kijana your wrong kabisa.. Chadema ipo na itaendelea kuwepo. ACT ni chama cha siasa bado kichanga sana.
 
Asante mkuu Tumaini Makene

Ila ninapenda kushauri, Kama Edward Ngoyai Lowasa Mwamba wa Kaskazini atakubali kutubu dakika za mwisho naomba Chadema isimwacha kwani jamaa ni kiungo mzuri tu tatizo ni chama alichokuwa nacho.

Mf:
Kuna wachungaji, Mashehe, Maaskofu na Mapadri wazuri sana na wanafanya kazi ya Mungu kwa uaminifu mkubwa sana ila kipindi cha Nyuma walikuwa majambazi, makahaba, na hata wachawi wakubwa.

Pia tukumbuke kuwa ata katika kitabu cha Mungu (BIBLIA TAKATIFU) Sauli, alimuudhi sana Mungu kwa kuwatesa na kuwauwa watumishi wa Mungu lakini alipogeuka na kumgeukia Mungu alipendwa sana na kufanya kazi ya Mungu kwa Uaminifu.

Pia Ikumbukwe Bwana Yesu alipokuwa Msalabani Mnyang'anyi Mmoja alityubu pale msalabani alisamehewa na kukaribishwa kwenye ufalme wa Mungu.

Hivyo Basi, ni busara ya Hali ya juu kwa Raisi wetu wa awamu ya tano Mh. Dr. W. Slaa kumkumbuka Mh. Edward Lowasa katika ufalme wake.

Asante
 
Lowasa anaweza kuwasaidia ukawa kwa kupata wabunge wengi kwenye uchaguzi huu na kupunguza kura za uraisi
 
Makene unaiangusha sana CHADEMA, uko very personal. Kusema kweli CHADEMA ni chama kikubwa sana sasa hivi tunahitaji mtu mwenye uwezo mkubwa sana kwenye nafasi hii. Hakukuwa na haja ya kumpa Zitto airtime namna hiyo. Inatosha tu kukanusha taarifa basi.
 
Je Chadema wako tayari mpokea Lowasa endapo atajiunga nanyi?
 
Makene, wewe ni msemaji wa chama, tena taasisi kubwa sana. Wakati mwingine unaiaibisha CHADEMA. Usikurupuke kijana, sio lazima kila kitu kujibu, yaani wewe unajibu kila kitu. Mi nadhani viatu ulivyopewa vimekupwaya. CHADEMA ni taasisi kubwa, mnatuangusha na siasa za kitoto kama hizi. Mungu bariki CHADEMA

Uongo ukiachwa usemwe muda mrefu hugeuka kuwa ukweli
 
Habari nyepesi sana hizi kutolewa maelezo ya kukanusha..vitu vingine mnapotezea tu.!
 
Mkuu, kwa sasa vita vipigwe kwa CCM tu hebu ipotezeeni ACT, sio kila afanyalo mliseme. Wapuuzwe tu, kwani kuwataja taja mnawapa nafasi na mnakosa nguvu ya kupambana na adui ccm ambae nae amejipanga hasa kwa bwana Magufuli
 
Back
Top Bottom