Zitto amburuza Kilewo polisi

Zitto amburuza Kilewo polisi

Status
Not open for further replies.
Zitto kwisha habari yako!!!!!!! Umekufa vibaya zitto kama nakuona vile unavotokwa na roho
 
anacho kifanya mh zito kwa ushauri wangu angetulia kwanza vuguvugu lipite kisha aendlee na huo utaratibu wake azma ya wanachadema wana dhamira njema katika kuleta mabadiliko ya kweli katika nchi hiii.na ni chama cha kwanza kufanya maamuzi mazito
 
Jukwaa la siasa si pahala pako, wewe saizi yako ni MMU. Jukwaa la siasa si sehemu ya mipasho kama hizi unazotoa kila leo, bali ni pahala pa kutoa hoja mahususi. Understand?!
naona wewe ndo umetoa point kwa uchakubimbi wako!!
 
WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikimwandikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe barua ya kumtaka ajieleze dhidi ya tuhuma zinazomkabili, yeye ameamua kukimbilia polisi akimshitaki mmoja wa viongozi wenzake.

Habari za kuaminika zimedai kuwa Zitto ambaye hivi karibuni alivuliwa cheo chake cha unaibu katibu mkuu wa CHADEMA, inadaiwa amefungua mashitaka polisi akimtuhumu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo kwa madai ya kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii.

Akithibitisha tukio hilo, wakili wa Kileo, Peter Kibatara, alisema kuwa mteja wake amemriwa kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumatano saa nane mchana na kuonana na mmoja wa maofisa wa juu wa jeshi hilo, aliyetajwa kwa jina moja tu la Mbutta, kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Zitto dhidi yake.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Kileo alikiri kuitwa polisi, ingawa alidai hajui ni waraka gani anaotuhumiwa kuusambaza unaomchafua Zitto.

“Kwa kweli sijui hata mimi ni waraka gani, ingawa hivi karibuni kulikuwa na waraka wa siri uliodaiwa kutoka CHADEMA, na ambao ulijaa tuhuma za usaliti. Lakini huo tuliishaukana siku nyingi. Labda kuna mwingine,” alisema Kileo.

Zitto kutwa nzima ya jana hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kufafanua mashitaka aliyofungua polisi. Simu zake zote za kiganjani zilikuwa zimezimwa.

-Tanzania daima.

Tanzania Daima?
 
Kabisa Mkuu naona huyu jamaa hakutegemea kabisa kwamba chama kinaweza kufanya maamuzi yaliyofanywa, sasa anaanza kutangatanga.

Mfa maji haachi kutapatapa. So my comrade Kilewo vuta subira na hakika kesi hii utashinda na hatimaye litakuwa pigo lingine tena kwa Zitto na hatimaye tutamsahau kabisa kisiasa. Walikutengenezea ya UGAIDI sembuse hii. Shame on them.
 
Mkuu niliwahi kutoa ufafanuzi hapa jf kwakuweka wazi wasifu wangu katika mjadala mmoja ulioitwa "uchochezi wa Mohamed Said"

nitanukuu tena hapa chini ili watu waone tena upi ukweli sio kuishi kwa hisia,




Maneno hayo uliyasema baada ya sisi kukubana na baada ya Andrew Nyerere kuja kukukana kwamba wewe si mwanafamilia ile,

Na hiyo ilitokea pale pale ulipokasema kwamba wewe "MWALIMU NYERERE NI BABA YAKO MZAZI""

Kwani haya tunakuzushia??

1.Kama huna undugu na Julius kambarage nyerere mbona ulikuja kifua mbele na kusema ni baba yako mzazi??

2.Kwanini usije kujiverify na jina lako halisi ya Yericko Yohanes Msambila??na uje kujiverify na yericko nyerere>??

3.Kipi kimekupa hali ya kujiamin kuja kujiverify na jina lisilo lako na hali ya kuwa mwenywe unasema kwamba "INASEMEKANA" BABU YAKO MZEE MSAMBILA ALIKUWA ANATOKA KASKAZIN MWA TANZANIA??

4.Na kwanin ukajipa majukumu ya kuja kuyasemea mambo ya nyerere humu jukwaani na kuonesha kwamba una ukaribu nae na hata butiama wanakufaham hadi ukafikia hatua ya kusababisha usumbufu kwa kina Andrew Nyerere kuja hapa jukwaani kukukana na kutolea ufafanuz kuwa hawakutambui??

5.Na je kwa sasa baada ya utapeli huo kufahamika,huoni sasa ni wakati muafaka wa kufuta jina hilo kwani janja yako na utapeli wako watanzania wameshakwisha ufaham??

NB;
BABA YAKO NA UKOO WAKO NDIYO ASILI YAKO,KUIKANA ASILI YAKO KWA MINAJILI YA UTAPELI NA KUTAFUTA UMAARUFU NI UTUMWA NA UNYONGE WA HALI YA JUU,

SHIME WATANZANIA TUKEMEE TABIA HII,NA TUWAPIGE VITA WATU WENYE HULKA KAMA HIZI MOJA KWA MOJA ILI IWE FUNDISHO KWA WENGINE

CC Ritz CHAMVIGA BOKOharam faiza foxy gombesugu MwanaDiwani kahtaan@faby and etc...

Mkuu unayosema ni kweli mpaka Andrew Nyerere alipokuja ndio akalegea na atalegea zaidi siku sio nyingi segerea ina muhusu huyu mwehu.
 
Last edited by a moderator:
Magamba yanamtetea ZZK baada ya mpango wao kubuma.
 
kaona ndio pa kuanzia
Atapanikana tu hana ujanja, tayari zimeshaonekana.
- email tracing
- IP address
- IP location
- Protocal route messages
- event viewer
- log analysis
- all information technology devices


 
Ukirejea waraka wa nyuma wa CHADEMA KUJITEKA NA KUMMWAGIA TINDIKALI KUBENEA, utagundua kwamba mtu kama ZITTO KABWE hakutakiwa kabisa kuwa CHADEMA. aina ya watu walioko katika chama hicho sio wa aina yake. Zitto ni mtu mwenye akili kubwa (kama alivyosema nchemba). Nadhani sasa anatakiwa atafute mwelekeo mpya ikibidi kujitoa kwenye siasa kwani anaweza kuisaidia nchi hii hata akiwa nje ya siasa au kuingia kwa wenzake wenye akili kubwa. Hawa wenye chama hicho watamsumbua sana.

Alikuwa anasubiri nini huyo msaliti? bora angejitoa mapema kukwepa aibu ya kufukuzwa.cdm haina uswahiba na wasaliti au wanafiki.wanafiki wamejaa ccm nadhani angeenda kujiunga nao.
 
Kwa mwendo wenu huu wa kishabiki chadema kinajidhalilisha na siasa za ukanda.
 
Wanasiasa wa Bongo bana....kutwa kulumbana tu!!!
 
Hivi huyu Kileo si alikuwa Magereza!! Ina maana alishatoka nje,? Ana kesi kubwa sana kule Igunga. Hii nchi nyepesi sana mtu ana kesi na bado anaachwa free tu!!
 
Who is Yericko by the way??watu wanalitumia jina la mwalimu vibaya sana
hivi kwani jina la Nyerere lina hati miliki? si ni jina kama jina jingine tu, Mussa, Hamad, Maulid, Peter,Obama, Bush ! inamaana nikizaa mtoto nikitaka kumuita Nyerere au mwenyewe nikiamua kubadilisha jina langu legally inabidi niombe ruhusa kutoka kwa Nyerere's family eeh ?? umburula ukizidi sana unabaki ukamasi tu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom