Zitto amburuza Kilewo polisi

Zitto amburuza Kilewo polisi

Status
Not open for further replies.
wamemwachia bila masharti na kesi ndiyo imeishia hapo hapo ! ninajipongeza sana kuikataa kazi ya polisi , kumbe huwa wanatumwa tu hata penye uzushi ?
 
kileo.jpg
Kamanda Kilewo akiwa mkono wa kulia na wakili wake aliyemuakilisha peter kibatala, wakili mussa mfinanga

KATIBU wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo, jana alihojiwa kwa muda na maofisa wa Jeshi la Polisi kutoka makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam, akihusishwa kutishiwa maisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA).

Kilewo aliwasili katika makao makuu ya jeshi hilo jana majira ya saa 06:03 mchana, akiwa ameongozana na wanasheria wawili pamoja na Diwani wa Ubungo, Boniface Jacob, huku waandishi wa habari waliopiga kambi katika eneo hilo la makao makuu ya Polisi kwa ajili ya kufuatilia kinachoendelea wakilazimishwa kuondoka.

Baada ya kuwasili, Kilewo na wanasheria wake walifika katika eneo la mapokezi na kujitambulisha, ambapo askari aliyekuwa na cheo cha sajenti aliwaelekeza idadi ya watu wanaoruhusiwa kuingia katika chumba cha mahojiano kuwa ni Kilewo mwenyewe na mwanasheria wake.
Hata hivyo maelekezo hayo ya polisi yalipingwa na wanasheria wa Kilewo, John Malya, ambaye alishinikiza waingie wote kwa ajili ya kusikiliza kile alichoitiwa mteja wao, hali iliyozua mabishano ya muda kabla ya baadhi ya maofisa wa polisi kuridhia matakwa ya wanasheria hao kuingia wote kwa ajili ya mahojiano.

Mara baada ya kuingia ndani, Kilewo na wanasheria wake walikaa kwa zaidi ya saa mbili kabla ya kutoka, ambapo mwanasheria wake, Malya, alizungumza na waandishi wa habari na kuelezea kile kilichosababisha mteja wake kufika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Malya alisema mteja wake alipata wito wa polisi kupitia simu ya kiganjani kuwa anahitajika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano huku akiwa hajafafanuliwa ni mahojiano ya namna gani na yanahusu jambo lipi.

Alisema baada ya wito huo wa njia ya simu walifika jana kuitikia wito, huku wakitaka kujua kilichosababisha mteja wao kuitwa.
"Kiutaratibu hawakufuata sheria, kwa kuwa hawakutoa hati ya wito au ya kukamatwa na zaidi hakuna mtu aliyefungua mashitaka dhidi ya mteja wangu," alisema.

Aliongeza kuwa walipofika polisi waligundua kuwa mtu aliyefungua malalamiko ya kutishiwa maisha na mteja wake kutakiwa kutoa maelezo katika fomu ya onyo ya Jeshi la Polisi ni Zitto Kabwe.
Alisema hali ya kutakiwa kuweka maelezo katika fomu ya onyo ilizua mjadala baada ya kutaka kujua kosa linalosababisha mteja wake kuhojiwa.

"Tuliwaambia wabadilishe fomu ya maelezo isiwe ya onyo, itumike ile ya ripoti nao wakakataa, tukakubaliana pale panapoandikwa kosa la mhusika papigwe mstari, kwa kuwa hawakutuambia mteja wetu anashitakiwa kwa kosa lipi," alisema Malya.
Alisema maelezo ya polisi waliyoyatoa kwao ni kuwa wanafanya uchunguzi juu ya taarifa zilizoandikwa katika gazeti la Majira juu ya Zitto Kabwe kutishiwa maisha na kwamba mteja wake alitoa maelezo na kisha kujidhamini mwenyewe.

Kilewo atoa kauli
Akizungumza baada ya kutoka katika mahojiano, Kilewo alisema Jeshi la Polisi linapaswa kubadilika na kufuatilia masuala ya msingi na liache kujiingiza kwenye masuala ya siasa.
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona polisi wanakuwa wa kwanza kuwafuata wanasiasa huku wakishindwa kuainisha hatua waliyofikia katika matukio ya kutekwa na kisha kujeruhiwa kwa mwandishi wa habari, Absalom Kibanda, tukio la kutekwa na kuteswa kwa Dk. Stephen Ulimboka na wengine.

"Nchi inakabiliwa na mambo makubwa, kuna uhalifu unaotishia maisha ya Watanzania, badala ya polisi kuhangaika na hivyo wao wanageuka kuwa wanasiasa," alisema Kilewo.

Kwa upande wake Msemaji wa Jeshi la Polisi, SSP Advera Senso, alikanusha kuwa wito wa katibu huyo wa CHADEMA hautokani na malalamiko ya Zitto, bali ni utaratibu wa kawaida kwao kumuita mtu yeyote na kuongea naye pale wanapoona kuna haja ya kufanya hivyo.
Kuhusu waandishi kufukuzwa katika eneo la polisi, Senso alisema polisi haikuwa na haja ya kuita vyombo vya habari katika tukio hilo, na kama mhusika aliviita, waandishi wa habari walipaswa waende katika ofisi yake.

Tanzania daima ya leo tarehe 29/11/2013

Taratibu atatulia na kuacha kiherehere na kuungana na makamanda wenzake wakafanye ukombozi tunaouona kwa karibu sana.
 
Kwa kamanda Kilewo, achana na mambo haya kama ulivyosema nenda Mwanga kaendelee kumwaga sumu ya ukombozi mkuu, tunakuhitaji mwanga achana na hao walikwisha jijenga nawe kajijenge kwako, naamini unaweza sana.
 
washaanza kutengeneza kesi zao hao policcm,..
 
Polisi wapo fasta sana kwenye ishu zinazomuhusu mwanachama wa Chama pinzani au mtu yeyote anayehatarisha uwepo wa CCM madarakani, Hivi suala la Kapuya vp? wamemuita japo kumhoji tu?
 
kweli naamini zitto ni mtu wa system maana ccm wote macho yamewatoka na serikali nzima macho yamewatoka. kama chadema ni chama cha upinzani nilidhani hii ingekuwa sherehe kwao.
 
Kapuya anapasua anga tu. Leo kuna kijana kahukumiwa kifungo cha maisha kwa makosa kama ya Kapuya.
 
bado zamu ya mzee slaa,yericko na ben wote lazima wafike polisi kujitubu tuhuma zao.
 
View attachment 123864
Kamanda Kilewo akiwa mkono wa kulia na wakili wake aliyemuakilisha peter kibatala, wakili mussa mfinanga

KATIBU wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo, jana alihojiwa kwa muda na maofisa wa Jeshi la Polisi kutoka makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam, akihusishwa kutishiwa maisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA).

Kilewo aliwasili katika makao makuu ya jeshi hilo jana majira ya saa 06:03 mchana, akiwa ameongozana na wanasheria wawili pamoja na Diwani wa Ubungo, Boniface Jacob, huku waandishi wa habari waliopiga kambi katika eneo hilo la makao makuu ya Polisi kwa ajili ya kufuatilia kinachoendelea wakilazimishwa kuondoka.

Baada ya kuwasili, Kilewo na wanasheria wake walifika katika eneo la mapokezi na kujitambulisha, ambapo askari aliyekuwa na cheo cha sajenti aliwaelekeza idadi ya watu wanaoruhusiwa kuingia katika chumba cha mahojiano kuwa ni Kilewo mwenyewe na mwanasheria wake.
Hata hivyo maelekezo hayo ya polisi yalipingwa na wanasheria wa Kilewo, John Malya, ambaye alishinikiza waingie wote kwa ajili ya kusikiliza kile alichoitiwa mteja wao, hali iliyozua mabishano ya muda kabla ya baadhi ya maofisa wa polisi kuridhia matakwa ya wanasheria hao kuingia wote kwa ajili ya mahojiano.

Mara baada ya kuingia ndani, Kilewo na wanasheria wake walikaa kwa zaidi ya saa mbili kabla ya kutoka, ambapo mwanasheria wake, Malya, alizungumza na waandishi wa habari na kuelezea kile kilichosababisha mteja wake kufika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Malya alisema mteja wake alipata wito wa polisi kupitia simu ya kiganjani kuwa anahitajika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano huku akiwa hajafafanuliwa ni mahojiano ya namna gani na yanahusu jambo lipi.

Alisema baada ya wito huo wa njia ya simu walifika jana kuitikia wito, huku wakitaka kujua kilichosababisha mteja wao kuitwa.
“Kiutaratibu hawakufuata sheria, kwa kuwa hawakutoa hati ya wito au ya kukamatwa na zaidi hakuna mtu aliyefungua mashitaka dhidi ya mteja wangu,” alisema.

Aliongeza kuwa walipofika polisi waligundua kuwa mtu aliyefungua malalamiko ya kutishiwa maisha na mteja wake kutakiwa kutoa maelezo katika fomu ya onyo ya Jeshi la Polisi ni Zitto Kabwe.
Alisema hali ya kutakiwa kuweka maelezo katika fomu ya onyo ilizua mjadala baada ya kutaka kujua kosa linalosababisha mteja wake kuhojiwa.

“Tuliwaambia wabadilishe fomu ya maelezo isiwe ya onyo, itumike ile ya ripoti nao wakakataa, tukakubaliana pale panapoandikwa kosa la mhusika papigwe mstari, kwa kuwa hawakutuambia mteja wetu anashitakiwa kwa kosa lipi,” alisema Malya.
Alisema maelezo ya polisi waliyoyatoa kwao ni kuwa wanafanya uchunguzi juu ya taarifa zilizoandikwa katika gazeti la Majira juu ya Zitto Kabwe kutishiwa maisha na kwamba mteja wake alitoa maelezo na kisha kujidhamini mwenyewe.

Kilewo atoa kauli
Akizungumza baada ya kutoka katika mahojiano, Kilewo alisema Jeshi la Polisi linapaswa kubadilika na kufuatilia masuala ya msingi na liache kujiingiza kwenye masuala ya siasa.
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona polisi wanakuwa wa kwanza kuwafuata wanasiasa huku wakishindwa kuainisha hatua waliyofikia katika matukio ya kutekwa na kisha kujeruhiwa kwa mwandishi wa habari, Absalom Kibanda, tukio la kutekwa na kuteswa kwa Dk. Stephen Ulimboka na wengine.

“Nchi inakabiliwa na mambo makubwa, kuna uhalifu unaotishia maisha ya Watanzania, badala ya polisi kuhangaika na hivyo wao wanageuka kuwa wanasiasa,” alisema Kilewo.

Kwa upande wake Msemaji wa Jeshi la Polisi, SSP Advera Senso, alikanusha kuwa wito wa katibu huyo wa CHADEMA hautokani na malalamiko ya Zitto, bali ni utaratibu wa kawaida kwao kumuita mtu yeyote na kuongea naye pale wanapoona kuna haja ya kufanya hivyo.
Kuhusu waandishi kufukuzwa katika eneo la polisi, Senso alisema polisi haikuwa na haja ya kuita vyombo vya habari katika tukio hilo, na kama mhusika aliviita, waandishi wa habari walipaswa waende katika ofisi yake.

Tanzania daima ya leo tarehe 29/11/2013

sasa mi nadhani ifike muda tukubaliane waungwana haya mambo ya zitto tuweke kapuni tuangalie mambo yanayo lisumbua taifa kwa sasa kama kama kupanda kwa umeme na kuahirishwa kwa mara nyingine kwa wiki 2 kutolewa kwa rasim ya pili ya katiba
 
Polisi wapo fasta sana kwenye ishu zinazomuhusu mwanachama wa Chama pinzani au mtu yeyote anayehatarisha uwepo wa CCM madarakani, Hivi suala la Kapuya vp? wamemuita japo kumhoji tu?

kapuya nasikia alishahojiwa akashinda kesi haikuwa na mashiko ila ya lema ya kubaka wingereza ndiyo imekaa vibaya.
 
Zitto asipofukuzwa chadema atatuvuruga sana, afukweuzwe aende zake CCM anakotaka kwenda, tunamuda mfupi sana kuingia katika uchaguzi mkuu tunachotakiwa kufanya ni kujipanga mapema ni jinsi gani tutajipatia ushindi na sio kuzozana na huyo msaliti. Chadema bila Zitto inawezekana afukuzwe tu aondoke zake.
UHAI WA CHADEMA NI ZITTO NA WENZAKE WOTE KUFUKUZWA KUNDINI.
 
Mhe. Zitto na Kamanda kilewo, Siyo kila anayewapatia ushauri wanasikitika kwa mambo yanayoendelea ndani ya Chadema na wanahuzuni na ninyi na Chama chenu. Wengine wanawasengenya na wanapenda kuwaona siku moja mnakosa muelekeo wa kisiasa. Nawasihi muwe wavumilivu wa siasa. nyie ni viongozi na mtabaki kuwa viongozi Daima. Jambo la msingi ni kumaliza tofauti zenu kama zipo ili msonge mbele pamoja kwa kuaminiana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom