Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

Hayo ni mambo ya kusadikika tu, utakumbuka kauli ya juzi iliandikwa baada ya 5 days kupita, wapinzani wa CDM wako makini nao, walirusha hiyo ili kuwagombanisha lakini si uliona walikaa wakatulia, it is a game, mi naamini Zitto ni kiongozi mzuri hawa wengine wamekuja juzi tu, mfikirie Zitto kwa upana kidogo not just juu juu.

Dr. Slaa ni makini ndiyo maana yuko na Zitto hata kama wote wanataka urais. But Zitto is much better than hawa wanajichukulia umaarufu kwa kudai watu wale mchana Zanzibar.

Zitto is a leader, hata CCM wanamkubali, anatakiwa kiongozi kama huyu ili kuleta mahusiano mazuri ndani ya jamii ambayo sasa makundi yako wazi kabisa achilia mbali vyama, na udini pia umejaa, hata hapa JF habari ya Zitto kuna watu hawa ijadili hivihivi tu kuna mambo mengine nyuma ya pazia.
Tukubali tukatae zitto anatumika ku distabilise Chadema kumbuka wakati wa kampeini kule Arumeru watu wako kwenye battle field dakika za lalasalama nakumbuka zilikua zimebaki siku mbili tuu anaibuka na hoja ya kugombea uraisi ili ahamishe ajenda kuu ya kampeini thank God kwa busara ya Dr. Slaa alivo uliza juu ya kauli ile ya Zitto alisema hawezi kuzungumzia upuzi maana ajenda iliyopo ni Nasari kuingia bungeni. Ila kwa hili kapatikana na mengine yatafumuka hata mama yake mzazi aliwahi kukiri hadharani kwamba mwanae anatumiwa
 
Tunapokuwa si wa kweli wa dhati na dhamira zetu tunapatwa na aibu ya kufa. Kama dhamira ya Ziti Kabwe ni ya dhati bila shaka atapona na zahama hili vinginevyo ataipata fresh. Hii ni baraka kwa nchi yetu pendwa TANZANIA. Mungu anaingilia kati kwa jinsi ya ajabu kutuandalia utawala bora siku zijazo:flypig:
 
Kauli hii iko kwenye ukurasa wake wa twitter.

"Kwa masaa 3 nimejieleza mbele ya sekretariat ya chama kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu. Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa katibu Mkuu".

Amekiomba chama kifanye uchunguzi juu yake na kuchukua hatua akibainika.

Huu ndo mfumo wa kusaka haki... Na PCCB nao pia waende wakamhoji ili tupate ukweli na akibainika ni kweli afikishwe mahakamani na kama sio kweli Yule mbunge aliropoka jina lake bungeni achukuliwe hatua.
 
Nilivyoelezwa na rubani mmoja jinsi dogo anavyopiga misele ya hivyo vipepeo vya TANAPA nguvu zikaniishia kabisa. Dogo noma huyu, na Dhaifu ni mtu wake wa karibu sana na anawatumikia hao kwa nguvu nyingi sana !!

Aeleze na Ndege ya TANAPA yeye huwa anaitumia kama nani na kwa mamlaka yapi? Kama mwenyekiti Wa kamati ya Bunge ya Mahesabu ya mashirika ya umma ataweza kukagua TANAPA kwa haki? Zitto ni fisadi, aeleze Gari aliyopewa na Nimrod Mkono na huo mshahara anaolopwa na Rostam Azizi ni kwa kazi ipi.
 
Mpendwa Zitto,Sasa ni mapema mno kujihusisha hadharani na ambition yako ya kuwa Rais. Kwanza jenga Chama chako. Usikigawe katika makundi.

Ikiwezekana kubadilisha Katiba ya sasa ukakubalika kiumri, CDM wanaweza kukuteuwa upeperushe bendera yao. La sivyo Mwana CDM mwenye miaka 40 na zaidi awe Rais na umkampenie ili hatimae uweze kumrithi.

Ufahamu kwamba marafiki wako CCM wanakuponza ili udhoofishe CDM. Kamwe usitegemee ukiacha CDM na kujiunga nao, watakuteuwa kuwa mgombea wao. Labda hata Ubunge kwa tiketi yao watakunyima.
 
aeleze na ndege ya tanapa yeye huwa anaitumia kama nani na kwa mamlaka yapi? Kama mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mahesabu ya mashirika ya umma ataweza kukagua tanapa kwa haki? Zitto ni fisadi, aeleze gari aliyopewa na nimrod mkono na huo mshahara anaolopwa na rostam azizi ni kwa kazi ipi.
acha udaku wewe peleka hii comment kwenye udaku.com
 
Zitto is clean and smart, no discussion. Alafu kamanda tunakuomba husijiweke karibu na ma ccm kwa kigezo siasa sio huasama, we love you Zitto, sio marafiki wema hawo, then uwe makini na kauli unazotoa, wewe ni kiongozi mkubwa kamanda. Si unawaona Lissu, Dr Slaa, Mbowe na Mnyika wapo makini na kauli zao wanapozungumza mahala popote.
 
Kwa tabia yake ya undumila kuwili Zitto hawezi kuponyoka. Kama kweli anamilki Hummer na magari mengine kama ilivowahi kuripotiwa kuwa alimsadia magari Kafulila kwenye kampeni, Zitto ni fisadi hakuna shaka. Kinachofurahisha kwenye mchezo huu wa kuvuana nguo, hakuna fisi atayenusurika kutokana na ukweli kuwa hata hao wanaowashutumu wenzao hawafanyi hivyo kwa uzalendo bali visasi vya kuzuiwa kuliibia shirika la Umeme. Mhando si wa kwanza. Dr Idris Rashid aliiba sana ukiachia mbali familia na shemeji za Mkapa waliotumia Net Group Problems kulimaliza kabisa shirika letu.Bado serikali ambayo huwa halipii umeme inaotumia. Msururu ni mrefu kama uchunguzi wa kina utafanyika.
kamanda zitto ana marafiki wengi wakiwemo wale wajerumani waliotambulishwa mjengoni kuwa wanaanzisha mradi wa umeme wa jua,xo sioni tatizo yeye kumiliki magari ya kifahari coz kuna nchi zinajua umuhimu wake na zinamtumia kuandaa sera za madini katika nchi zao,hapa kwe2 c wanamdharau kisa ni CDM ingawa wanajua kuwa yeye ni miongoni mwa WACHUMI MADINI wanane tu ambao TZ tunao.
 
dr slaa ni mmoja wa wanaosemekana kuusaka urais 2015
je zitto ana imani dr slaa anaweza kuongoza sekretarieti? ukizingatia wanaomchafua zitto ni wabunge wapenda posho na wasaka urais kutoka vyama vyote, (hii ni kutokana na maelezo ya zitto mwenyewe)

Dr silaa hajawahi kutaka kugombea urais. bali aliombwa na wanacdm kukiwakirisha chama hicho baada ya kuonekana kuwa anafaa kukiwakirisha chama vizuri.
 
Nadhani huu ni uamuzi wa busara sana badala ya kusubiri maneno yazidi kukua ni vizuri kumaliza udhia mapema.
Nadhani sasa sekretariati imepata mengi kutoka kwake na hivyo kuinufaisha sana kamati kuu itakapokutana kwa ajili ya kutafakari tuhuma hizo dhidi yake.

Narudia tena kumshauri kamanda Zitto ajiepushe na tabia ya kupenda kuwa msemaji wa kila kitu kinachojitokeza mbele yake, afanye hivyo pale anapolazimika tu. Kama anajitambua kwamba yeye ni "presidential hopeful" lazima ajilinde kwa kauli na matendo yake. Hii vita baridi ccm wanayopigana nae yeye hajaijua kwakuwa wamekuwa wakimpamba na yeye akaanza kujisahau kumbe walikuwa wanamlia timing wammalize.
Unajua kama Nilivyowahi kusema ya Kwamba imeshaonekana Kuiangusha Chadema ni kupitia a weak link na ikaonekana ni Zitto baada ya Marehemu Chacha...Kwanza wakajaribu sana kumkosanisha na Mbowe, Ikashindikana ila kuharibu mahusiano yao wenyewe lakini haikukigawa chama.

Ya pili wakamtumia tena Zitto ktk Ukaskazini na Udini ikafanya kazi kubwa sana na lawama zikaanza kuingia vichwani mwa watu lakini ajabu chama ndio kikapata umaarufu zaidi ujio 2010..Baada ya kushindwa kote njia nyingine imejitokeza ambayo ni Zitto mwenyewe kuwa sababu achukiwe ndani na pengine kujitenga na chama hivyo kuwagawa ktk makundi mawili. Na hakika hii imeonekana inafanya kazi maana kweli Zitto anachukiwa na wanaChadema. Naye anaanza kuamini kama hana nafasi ndani ya Chadema na wanaChadema nao wanafunga uwezekano wa Zitto kufikia ambition yake.. In fact it's working japo very slow lakini inafanya kazi..

Halafu, Zitto hana makosa kujibu tuhuma hizi mbona Dr.Slaa alikuwa akizijibu nyingi tu hadi wakaenda personal na watu walikuwa nyuma yake hata kaa wanajua kweli tuhuma ni nzito...Kwa nini Zitto asijibu, isipokuwa kosa la Zitto ni kutojipanga nyuma ya chama ktk majibu yake. Kila kitu anachukulia personal kama wanavyotaka, badala ya kutumia kofia ya chama kujikinga. Niliwashtua both Zitto, Mbowe na Wanachamema hapa toka mwaka 2009 lakini watu hawaniamini.. Ninaujua mji wa Dar kama kiganja cha mkono na najua mengi yanayofanyika nyuma ya pazia japo niko nje ya nchi.

Hii tabia ya Zitto kujifanya independent (kwa sababu haamini mtu) wakati akitumia jukwaa la CDM ndio inayomweka bayana zaidi kisiasa. Anatakiwa kujifunza zaidi siasa, maana ndipo imani na uzalendo huanzia ili mawazo binafsi kuongoka. Let them say maadam mnaelewa malengo yao, nia zao haitawaumiza vichwa..
 
yaani hili jembe linavyozidi kujicontradict linaninyima amani kabisa,but why zzk,what is not happening?
 
nimesema humu kuwa jina la zitto halimo kwenye list bali kikao cha jana usiku ndicho kinataka kuhakikisha kuwa zitto anawekwa kwenye list na anatajwa na ilikuwa moja ya maazimio yaliyokwenda kw spika jana usiku...nilidokeza juu ya kikao hicho katika thread hii hapa chini.....na subirini hiyo kesho zitto akiongea na waandishi wa habari ndio mtaujua ukweli wa hili ninalosema

Hafla ya kupongezana juu ya kilichotokea jana huko Dodoma imekwisha na sasa kinachoendelea ni kikao cha hatua ya pili ya kukabiliana na mvutano uliopo bungeni miongoni mwa wabunge wenyewe na kuhakikisha baadhi ya wabunge wanadhibitiwa na hawapewi nafasi kusema kile kitakachoonekana kutibua na kuharibu hatua iliyofikiwa(ushindi wa jana) . Maagizo maalumu yametumwa Dodoma kwa spika wa bunge juu ya hatua za kuchukua kwa wabunge walioko katika kamati zinazotuhumiwa kupokea rushwa .

PUMA energy ni kampuni inayomilikiwa na kiongozi mmoja aliyeko serikalini (si kiongozi mdogo) akishirikiana na wenzake 3 wenye hisa katika kampuni hiyo. na si kweli kwamba Serikali ina hisa asilimia 50!!!.

Nitaishia hapa leo na nitasubiri iwapo spika makinda atayatekeleza maagizo yaliyokwenda kwake...
 
Aeleze na Ndege ya TANAPA yeye huwa anaitumia kama nani na kwa mamlaka yapi? Kama mwenyekiti Wa kamati ya Bunge ya Mahesabu ya mashirika ya umma ataweza kukagua TANAPA kwa haki? Zitto ni fisadi, aeleze Gari aliyopewa na Nimrod Mkono na huo mshahara anaolopwa na Rostam Azizi ni kwa kazi ipi.

Mmh!!haya sasa!
 
kwani yeye zitto atake posho za nini wkt mafisadi wamemuwezesha?....tuulize sisi tunaomjua zitto in and out sio nyie mnaomuona mbele ya vyombo vya habari...zitto is a dangerous person bora hata kikwete

This is a very serious statement mkuu unaweza kusema zaidi maana u,emoshutua sama mkuu
 
nimesema humu kuwa jina la zitto halimo kwenye list bali kikao cha jana usiku ndicho kinataka kuhakikisha kuwa zitto anawekwa kwenye list na anatajwa na ilikuwa moja ya maazimio yaliyokwenda kw spika jana usiku...nilidokeza juu ya kikao hicho katika thread hii hapa chini.....na subirini hiyo kesho zitto akiongea na waandishi wa habari ndio mtaujua ukweli wa hili ninalosema
Zitto anajua kuwa anawindwa kila kona. Ningeshangaa kama angefanya kosa hili la kijinga.
 
mimi simhukumu Zitto ila napata tabu sana pale ninapopita huku JF nakuta karibu kila mtu hamsemi vizuri, ukienda mitaani bado hasemwi vizuri, ukienda kugida castle baridi pub.bar ama grocery ili tulipe kodi kupitia vinywaji ambavyo vimekuwa ni chanzo kikuu cha mapato ya taifa hili nako hasemwi vizuri, ukiazisha mada inayomuhusu zitto hata kwenye daladal nako hukosi watu wa kusema huyu haaminiki, mbaya zaidi hata ndani ya chama kwa kuwasikiliza wanachama wa CDM nako hawamwamini kwa matendo yake,watu wamebakiza maisha album kwamba Zitto ni yule wa enzi ya buzwagi aliekuwa amebeba maslahi ya watanzania wanyonge na huku angali kijana.

Nikifikia hapo ndipo nashawishika kwamba huenda kijana huyu anamatatizo ambayo yamepelekea jamii kubwa kumuona msaliti,kumuona siasa zale ni za kinafiki na sasa zmebeba ubinafsi,na kwa wale wanaotumainia abadiliko ndani ya taifa hili kupitia chama mbadala wanajenga chuki kwa kupoteza u-zitto wake wa awali,najiuliza kwa nini asingiziwe kwa muda mrefu consecutively?

Why Zitto most of the time if not frequently; napata shida sana, na kiukweli roho inaniuma sana kwani wakati namjua mwanasiasa huyu kijana nilimkubali sana na niliona taa yenye mwanga wa ukombozi imeanza kuwaka na inawashwa na vijana jasiri kama Zitto-leo nakosa amani moyoni kuona kwamba mtu niliemwani sana na nikajua anawasha mwanga wa ukombozi wa taifa hili kumbe anawasha mwanga wa kuwamulikia mafisadi wazione mali zote zilizosalia kwenye madini, kwenye nishati ya umeme, kwenye mashirika ya umma, kwenye fedha za wanyonge wa TZ wanaozipata wengine kwa kubeba zege, yaani anawamulikia mafisadi wazichukue mapema kisha cha moto tuendelee kukiona.

Hapa wakuu indipo ninapobaki kwenye diallema, kwamba Zitto huyu vipi? Ila nahisi alizidi sana kukaa jirani na mafisadi wa ccm kwa kisingizio kuwa hana siasa za chuki, sasa wengine wanadai ni mshirika mzuri wa Mkono, wengine wanadai anachukua posho kwa RA, mara hiki mara kile.

Zitto tuweke wazi, tena uwazi from the bottom of your heart, nakuonya kama utaendelea kuficha ficha wakati wengine wanujua ukweli wako watakuja kupaua jibu kipindi unataka kutimiza ndoto yako ya kwenda magogoni, siku hiyo utalia na kusaga meno, bado umri wako unakuruhusu,unaweza ukaomba msamaha na kisha watu watakuelewa hata kama ni siku zijazo kuliko kuficha kisha mambo yakaja kujulikana wakati ulishawahi kukanusha na kuwaambia watanzania kuwa huhusiki.mbona tunasikia mambo yako kibao?
 
Back
Top Bottom