Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,363
- 145,024
Hayo mengine ya nyumbani kwake ana ma sofa ya kichina, na umemuona anaendesha Hummer, hayo I don't care a lick kujua mwanamme mwenzangu anaendesha gari gani, huo ni upashukuna. Twende kwenye hoja.
Zitto hajasema pasipo yeye hakuna kitu kingefanyika bungeni, ongea ukweli. Bali ametoa mifano mitatu ya kazi alizoongoza bungeni ambazo zimesababisha kuangushwa mara tatu kwa mawaziri wa C.C.M.
Swali lake: Iweje kibaraka wa C.C.M. awashinde wakereketwa wa CHADEMA katika kazi za kuiangusha C.C.M. bungeni?
I mean, that is the most poignant question ever posed in the history of intra party conflicts in the country.
Msaliti anaepeleka siri za upinzani C.C.M., kwa nini yeye ndio anaongoza kampeni zenye mafanikio za bungeni za kuparaganyisha serikali ya C.C.M ?????????????????????
Siasa ni mchezo mchafu!
Hizo habari za sijui yeye kuongoza kampeni zenye 'mafanikio' za bungeni za kuiparaganyisha CCM yaweza kuwa zuga tu ya kupoteza lengo na kuleta picha ya kwamba yeye ni mpinzani wa kweli ili kujenga imani kwa watu wasioiunga mkono CCM.
Kwa sababu, kwanza si kwamba hizo harakati au kazi zake ziliiangusha serikali nzima ya CCM. Ni watu wachache tu waliathirika na kusema ukweli hakuna la maana sana lililotokea zaidi ya mawaziri wawili watatu kujiuzulu.
Sasa zaidi ya wao kujiuzulu nini kimetokea? Chenge bado anapeta, Tibaijuka naye vivyo hivyo. Na waathirika wengineo nao sijaona la maana liliowatokea.
Na yawezekana kabisa kwamba kwa sababu yeye ni kibaraka wa CCM, hiyo ndo sababu kubwa ya yeye kuweza kuonekana kuongoza kampeni bungeni ambazo kwa wengine zina taswira ya mafanikio kwenye kuiparaganyisha CCM kwa kuwa alikuwa anapata taarifa toka CCM, ambao ndo serikali.